CHADEMA yawapa raha watanzania: Taifa Lazizima

CHADEMA yawapa raha watanzania: Taifa Lazizima

Nina pata wasiwasi na uwezo na upeo wako wa kufikiri. Ungeliangalia bunge leo wakati wanapitisha muswada huu , wazi kuwa CDM walikuwa wanaomba huruma ya CCM , kwa Lissu mishipa ilikuwa inamtoka mpaka Jaji Werema alikuwa anamwonea huruma. Na kama umesoma waraka wa Kafulila juu ya suala hili ni wazi kuwa CDM wamelamba garasa badala ya dume. Kwa taarifa yako ni mapendekezo yasiyozidi 5% ndio yamefanyiwa kazi, sasa hapo mtu amepata 5% unampa pongezi ya nn badala yakumsikitikia?

leo zamu yako au umepangwa kwenye uzi huu maana siwaoni wenzano kwenye huu ila kwa hili la 5% unadhilhilisha jinsi shule za kata zilivyo kupa elimu duni pole mkuu ila wana ruhusu kureseat utaratibu wa mwaka huu ni mgumu sijui utafanyaje dah !!!
 
Ndio maana huwa mimi nadhani mashabiki wote wa chadema wamerukwa na akili na kama si hvyo basi ni kwamba mnajifanya wajuaji saaana tu mpaka mnakuwa kama wajinga.kwanini swala la katiba mnalifanya kam lenu na kujigamba eti nyie ndio source?acheni masifa bwana it wl cost u!

Mkuu unaruhusiwa kubisha kwa kadiri unavyowez lakini huyo mkuu wa kaya a.k.a. baba Mwanaasha amelikubali hilo ndo maana akaleta mabadilliko ya sheria ambayo tokea ameisign, hauijatumika na inafanyiwa marekebisho. CCM A na CCM B mlipitisha, sasa sijui mnataka kujiteteta kwa lipi.
 
Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba umepitishwa huku CHADEMA wakiwa hawana cha maana walichokiambulia. Bado Marais ndiyo wanaoteua Tume. Bado Mawaziri wa Katiba na Sheria ndiyo wanaoteua Sekretarieti ya Tume. Bado Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wamebaki kama walivyokuwakatika Mswada wa awali. Bado Rais wa Zanzibar ana nguvu zile zile katika kusimamia maslahi ya Zanzibar kwenye mchakato huu. Bado Zanzibar ina nafasi zake zote zilizoingizwa awali katika kusimamia maslahi yake. Bado kura ya maoni itasimamiwa na kuendeshwa na Tume za Uchaguzi zilizopo. Bado ni kosa la jinai kuingilia au kuizuia Tume ya Katiba kufanya kazi zake. Sasa kununa na kususa kwa CHADEMA kumeleta mabadiliko yepi yamaana? Waende kwa CUF WAKAFUNZWE SIASA!
 
Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba umepitishwa huku CHADEMA wakiwa hawana cha maana walichokiambulia. Bado Marais ndiyo wanaoteua Tume. Bado Mawaziri wa Katiba na Sheria ndiyo wanaoteua Sekretarieti ya Tume. Bado Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wamebaki kama walivyokuwa katika Mswada wa awali. Bado Rais wa Zanzibar ana nguvu zile zile katika kusimamia maslahi ya Zanzibar kwenye mchakato huu. Bado Zanzibar ina nafasi zake zote zilizoingizwa awali katika kusimamia maslahi yake. Bado kura ya maoni itasimamiwa na kuendeshwa na Tume za Uchaguzi zilizopo. Bado ni kosa la jinai kuingilia au kuizuia Tume ya Katiba kufanya kazi zake. Sasa kununa na kususa kwa CHADEMA kumeleta mabadiliko yepi yamaana? Waende kwa CUF WAKAFUNZWE SIASA
 
hongera chadema na wana chadema .big up .people's power .
 
katika uzi huu nashangaa Ritz Barubaru FF na wengine wamekimbia kabisa.
 
Wapo pia akina Kafulila wa NCCR ambao walikuwa sambamba na Makamanda wa CDM katika hili, nakumbuka walizomewa sana walipokuwa wanatoka bungeni. Bila shaka wabunge wa ccm wamejifunza kuweka ushabiki pembeni na kutanguliza maslahi ya Taifa.

Asante kutukumbusha mkuu
 
Excellent analysis.Huu ndio ukweli mtupu.Mungu azidi kuwaongoza CDM.Hakika umenifurahisha na Heading yako-CDM yatupa raha watanzania

Asante.Pamoja tujenge Taifa.
 
Na juu ya yote, watanzania wanastahili pongezi sana kwa kuonyesha moyo wa imani kwa chadema.

Tangu suala la shgeria ya katiba mpya lilipoanza, na hasa pale wabunge wa chadema walipotoka nje kupinga muswada ule, wananchi wa kada mbali mbali na kutoka kila kona ya nchi walionekana kuwaunga mkono, na hatimaye sasa angalau yale mapungufu mengi ya msingi katika sheria ile yameweza kurekebishwa kwa maslahi ya watanzania wote ili hatimaye tupate katiba ya watanzania wenyewe.

Bila shaka chadema itaendelea kusimamia na kuongoza utoaji wa elimu kwa wananchi ili waweze kushiriki vizuri na kikamilifu katika kutoa maoni yao juu ya katiba mpya.

Viva Chadema, Viva Watanzania.

Mwita asante sana kwa kuongezea.Ukiwa kama kiongozi wa CDM na wewe unastahili pongezi.
 
Pongezi zangu zawaendea WAZEE WETU WA HESHIMA SANA ndani ya nchi Wazee Joseph Sinde Warioba na Salim Ahmed Salim kwa kufanikisha hili.

Aidha pongezi za pekee ziwaendee vijana kote nchini pamoja na JF kwa kusimama kidete muda wote katika hili. Hata hivo vijana tusilale bado mapambano.

Kwa mara ya kwanza nawapongeza pia Rais Kikwete, Dr Kashillila, Kichaa wetu Ndugai pamoja na wabunge wa CCM kwa kuonyesha uzalendo katika hili na kubwa zaidi ni kule kutambua kwamba yote juu ya yote, TAIFA KWANZA!!!!!!!

Mkuu umekumbusha jambo la msingi.Tuwaenzi pia wazee hawa
 
fmpiganaji,

Bravo. Huo ni ukweli na ukweli mtupu. CHADEMA wanastahili pongezi za dhati kabisa. Frankly speaking CHADEMA ndiyo kioo cha Uongozi katika Taifa hili mabalo kwa sasa limepoteza mwelekeo kutokana na uongozi MBOVU wa Chama cha *******.
Kwa heshima na Taadhima napenda nami kuwapa pongezi nyingi Viongozi waandamizi wa CDM,Wabunge,Wanachama na Wapenzi wa CDM.

Sitakuwa nimetenda haki pasipo kumtaja Marehemu, dada yetu mpenzi Bi Regia Mtema(RIP) kwa mchango na mawazo yake kwenye mchakato huu kabla hajatutoka mapema mwezi uliopita.

Mkuu Makoye Hakika uliyosema.RIP Regia
 
Hongera mleta Mada,ni analysis nzuri yenye sura ya uhalisia wa mchakato mzima hadi leo,kweli ulikuwa ni mpambano mkali sana na hata wabunge mashabiki wa CCM NA CUF mara nyingi huwa wanashabikia vitu tu.
cha msingi tuungane pamoja kueneza elimu ya uraia na watu wenye mapenzi mema tushirikiane kukijenga chama kwa moyo mmoja na tuwe kitu kimoja hadi tujikomboe

Nashukuru mkuu wangu.Pamoja sana
 
Pomoja na CDM; pia natambua uwepo wa:-

MOSI: (Narudia) Natambua uwepo wa Mkuu wa kaya kuungana na sisi wanyonge; akaamua kuiweka CCM yake kando na kuuva uzalendo wa Tanzania na kusema YATOSHA wana CCM wenzangu, Ya kaisali basi mpeni kaisali ...Hongera Mkuu wa kaya kwa usikivu wako: kwa kitendo hili cha kizalendo kwa niamba ya CDM POKEA TANO:

PILI: Hata JF inabidi tujipongeze wenyewe , kuna watu wamechangia hoja nzito sana humu kuhusu katiba, na hilo lilisaidia kufungua maskio kwa baadhi ya wabunge na wana CCM ambao walifikiri bado tunaandika katiba ya CCM kumbe sisi tunaandika katiba ya Tanzania ambayo inahitaji makundi yote kushirikiswa asilimia mia. hongera wana JF -- Makofi kwenu Tafadhali.. kwa kitendo hiki na nyie POKEENI TANO:

TATU: Wapenzi na wanachama wa CDM; tupo pamoja kuimalizia hii project yetu ili 2015 tuikabidhi nchi hii kwa wenyewe ambao ndiyo sisi walala hoi, kwa uvumilivu wenu wa ajabu tangu kupokea matokeo ya uchaguzi mpaka sasa na nyie kwa kitendo hiki POKEENI TANO:

NNE: na mwsho inakuja kwako wewe mleta hoja, kweli ulijipanga vilivyo -- kwa kitendo hiki na wewe POKEA TANO:

Hakika umenikumbusha jambo.WanaJF ni moto wa kuotea mbali.Hata mbinu mbalimbali za kukabiliana na jambo hili kwa kiasa kikubwa wanaJF tulishiriki.
 
utaifa kwanza vyama baadaye. Watanzania msio na vyama pazeni sauti zenu msiogope hakuna chama cha kuwafukuza. Lazima tuwe na mchakato ambao hautahodhiwa na chama kama CCM wanavyokomaa na ma dc wakati wanajua kabisa kwamba ni mawakala wa CCM wilayani na wanatumia nguvu kuliko akili. Wakurugenzi ni wataalamu hawapo pale kwa sababu ya vyama. Pia ikumbukwe kila mtu anaweza kuwa mkuu wa wilaya lakini si kila mtu anaweza kuwa mkurugenzi.
 
Back
Top Bottom