CHADEMA yawapa raha watanzania: Taifa Lazizima

CHADEMA yawapa raha watanzania: Taifa Lazizima

Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba umepitishwa huku CHADEMA wakiwa hawana cha maana walichokiambulia. Bado Marais ndiyo wanaoteua Tume. Bado Mawaziri wa Katiba na Sheria ndiyo wanaoteua Sekretarieti ya Tume. Bado Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wamebaki kama walivyokuwakatika Mswada wa awali. Bado Rais wa Zanzibar ana nguvu zile zile katika kusimamia maslahi ya Zanzibar kwenye mchakato huu. Bado Zanzibar ina nafasi zake zote zilizoingizwa awali katika kusimamia maslahi yake. Bado kura ya maoni itasimamiwa na kuendeshwa na Tume za Uchaguzi zilizopo. Bado ni kosa la jinai kuingilia au kuizuia Tume ya Katiba kufanya kazi zake. Sasa kununa na kususa kwa CHADEMA kumeleta mabadiliko yepi yamaana? Waende kwa CUF WAKAFUNZWE SIASA!

Mkuu wangu pamoja na maoni yako lakini nadhani ni wakati sasa wa kusimama kama watanzania na kutengeneza katiba itakayotumika miaka 100 ijayo.Hizi porojo za vyama hazitatusaidia chochote
 
Hongera zangu kwa viongozi na wapenzi wote wa CHADEMA.
 
hongera sana chadema tunawapongeza kwa kazi nzuri ya kuliamsha taifa na kutupatia sheria ambayo kwa kiasi kikubwa inakidhi matakwa ya watanzania wengi kuwa na katiba itakayo tokana na wananchi nas siyo inayotokana na chama fulani
 
Wanastahili mkuu.Mungu azidi kuwaongoza
 
pongezi za pekee zimuendee mh Beatrice shelukindo kwa kujipambanua wazi kuwa ni mpiganaji wa aina gani. Mpaka kumtishia mzee wa kaya kumpuga. Hongera mrembo tambua katiba ni ya watanzania wote sio yenu

Eti huyu mama naye anajiita mpiganaji wa vita dhidi ya ufisadi.Hakika tuna safari ndefu
 
Ni kweli CDM wanastaili pongezi kubwa kwa mambo ambayo wanatufanyia watanzania mungu awabariki waendelee kuwa na afya njema ikiwezekana waje waongoze nchi 2015 haya ndiyo mabadiliko ya kweli tunayotaka watanzania ahsanteni sana CDM
 
Hakikisheni mnaweka mikakati madhubuti
Ni kweli kabisa inatakiwa mikakati makini na madhubuti mapema, na wapenda nchi wote wahakikishe pia ktk u
chaguzi ujao, wanajiandikisha mapema ktk daftari la wapiga kura,isijekuwa ni ushabiki wa JF tu. kura zetu ni muhimu kuliko ushabiki wetu
VIVA CHADEMA
 
Ewe Mwenyezi Mungu mtukufu,twakushukuru kwa wema na upendo wako kwa kuilinda na kuiongoza CDM ili iwe mwanga wakati wa giza,maji wakati wa kiu,mana wakati wa njaa,ngome imara wakati wa dhoruba,kimbilio wakati wa unyanyasaji,faraja wakati wa uonevu,kinga wakati wa hatari na zaidi ya yote sauti na nguvu ya umma ya watu wa taifa lako Tanganyika. ewe Mola mtukufu,nakuomba uendelee kuiongoza na kuilinda CDM na watu wa taifa lako wakionewa na watesi weusi ama weupe na wakaunganisha nguvu zao kupitia chama CDM,e Mungu wangu naomba uwasikie na kuwakomboa,ikiwa watu wako watapigwa na kujeruhiwa na mabeberu ama mabepari uchwara weusi ama weupe na wakakimbilia kakita ngome ya CDM,ewe Mtukufu nakusihi uwape faraja,uponyaji na zaidi ujasiri wa kujipanga upya na kurudi mapambanoni mpaka kieleweke,ewe Maanani nakuomba ikiwa watu wako watatoka kwenda vitani kupambana na mafashisti ama weupe, wa kijivu au weusi na kunyoosha vidole viwili juu na kiatana wao kwa wao " peopleeeeeeeeeeeeeeeee's.......poweeeeeeeeeeeeeeeeer", naomba Mola wangu uwape mori,hasira na nguvu ya kupambana na hawa mafashisti, naomba yote haya kwa unyenyekevu mkubwa na kuamini kuwa yatakuwa,amina
 
fikra pevu sana,huu uzi umekuja muda mwafaka na pongezi kwa mleta uzi huu ulijipanga vema bravo hii ni world of great thinkers na ukweli mtupu.
 
fikra pevu sana,huu uzi umekuja muda mwafaka na pongezi kwa mleta uzi huu ulijipanga vema bravo hii ni world of great thinkers na ukweli mtupu.

Nakushukuru mkuu.JF ni chuo changu cha mafunzo.Nitazidi kujitahidi kuleta habari zisizo na upendeleo wowote.
 
Ewe Mwenyezi Mungu mtukufu,twakushukuru kwa wema na upendo wako kwa kuilinda na kuiongoza CDM ili iwe mwanga wakati wa giza,maji wakati wa kiu,mana wakati wa njaa,ngome imara wakati wa dhoruba,kimbilio wakati wa unyanyasaji,faraja wakati wa uonevu,kinga wakati wa hatari na zaidi ya yote sauti na nguvu ya umma ya watu wa taifa lako Tanganyika. ewe Mola mtukufu,nakuomba uendelee kuiongoza na kuilinda CDM na watu wa taifa lako wakionewa na watesi weusi ama weupe na wakaunganisha nguvu zao kupitia chama CDM,e Mungu wangu naomba uwasikie na kuwakomboa,ikiwa watu wako watapigwa na kujeruhiwa na mabeberu ama mabepari uchwara weusi ama weupe na wakakimbilia kakita ngome ya CDM,ewe Mtukufu nakusihi uwape faraja,uponyaji na zaidi ujasiri wa kujipanga upya na kurudi mapambanoni mpaka kieleweke,ewe Maanani nakuomba ikiwa watu wako watatoka kwenda vitani kupambana na mafashisti ama weupe, wa kijivu au weusi na kunyoosha vidole viwili juu na kiatana wao kwa wao " peopleeeeeeeeeeeeeeeee's.......poweeeeeeeeeeeeeeeeer", naomba Mola wangu uwape mori,hasira na nguvu ya kupambana na hawa mafashisti, naomba yote haya kwa unyenyekevu mkubwa na kuamini kuwa yatakuwa,amina

Mkuu lazima wewe ni mtumishi.Umepiga sala ya nguvu kuombea katiba mpya.Kwa pamoja tutashinda.
 
Ni kweli CDM wanastaili pongezi kubwa kwa mambo ambayo wanatufanyia watanzania mungu awabariki waendelee kuwa na afya njema ikiwezekana waje waongoze nchi 2015 haya ndiyo mabadiliko ya kweli tunayotaka watanzania ahsanteni sana CDM

Mkuu Mungu mtukufu ni mwema atasikia sala yako.
 
CHADEMA ndio chama cha watanzania wazalendo,
daima haki husimama na dhuluma taratibu hufa
 
Hadi nitakapoyasoma mabadiliko yenyewe ndipo nitakapoweza kuchangia lolote. Kwa habari nilizozipata ni kwamba wajumbe wetu wamekubali kupokea hata kile kidogo tulichopewa maana haikuwezekana kushindana na CCM wakubali mapendekezo yetu, hivyo mapendekezo mengi ya sheria ya katiba bado yanawalinda CCM na viongozi wake. Kama ndivyo, hatujashinda kitu, vita bado kabisa inaendelea, kilichotokea ni kuweka uwanja safi kwa mapambano..
 
WanaJF,
Tutakuwa hatutendi haki kama hatutasimama kama Watanzania kutoa pongezi za dhati kabisa kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kwa kusimamia kidete suala la Katiba mpya mpaka sasa marekebisho ya sheria ya Katiba mpya yakapitishwa na bunge leo.Ni wazi watu mbalimbali akiwemo Rais Kikwete wamechangia hili lakini bila kumung’unya maneno niseme kama si CHADEMA kusingekuwa na hoja hii ya Katiba mpya leo.

Kwanini?

· CHADEMA iliweka suala la Katiba mpya kwenye ilani yake ya Uchaguzi mwaka 2010
· Wabunge wa CHADEMA walitoka nje ya bunge siku Rais alipolifungua bunge pamoja na mambo mengine kudai katiba mpya itakayotoa fursa ya kuwa na tume huru ya uchaguzi
· Mwaka mzima wa 2011 CHADEMA iliongoza maandamano nchi nzima kutoa elimu ya uraia na kutaka kuungwa mkono na UMMA juu ya kupata katiba mpya
· Wabunge wa CHADEMA walitoka nje ya bunge mwezi Novemba 2011 kupinga mswada wa Katiba mpya uliokuwa na Mapungufu mengi na ya kimsingi
· Kamati kuu ya CHADEMA ilinyoosha Mkono wa mapatano na serikali kwa kukutana na Rais Kikwete kupinga mswada uliokuwa mbovu uliopitishwa kiushabiki na wabubge wa CCM na CUF
· Rais aliridhia mapendeklezo yote ya CHADEMA na kuamuru mabadiliko ya sheria iliyokuwa imepitishwa kishabiki na wabubge wa CCM na CUF
· Hatimaye marekebisho ya sheria yakapitishwa na bunge na kufungua rasmi mlango wa kutengeneza katiba mpya ya Tanzania.

Ni wazi kwa yote yaliyotajwa hapo juu yanatufanya tuamini CHADEMA imesimama imara katika kupigania Katiba ya nchi.Watanzania wengi walikata tamaa na kudhani baada ya mswada mbovu kupitishwa mwaka jana CHADEMA ingesusia moja kwa moja zoezi zima.Lakini CHADEMA imejenga taswira tofauti kwa Watanzania kwa kupigana kwa hali yoyote kuhakikisha Katiba mpya inapatikana.

Wafuatao wanastahili heshima ya pekee:

Pamoja na CHADEMA kama taasisi kuonekana kukomaa na kusimamia agenda zake,ni lazima tuwatambue baadhi ya watu walioongoza mpambano huu kwa Amani na utulivu na siku moja wataingia katika vitabu vya historia

· Dr Wilbroad P. Slaa-Ni kiongozi makini,madhubuti na anayeweza kuyasimamia maneno yake kwa kuinadi ilani ya CHADEMA nchi nzima wakati wa kugombea urais mwaka 2010 na watu wakaamini na kuona umuhimu wa Katiba mpya.Lakini Pia ni Katibu mkuu ambaye ni mtendaji mkuu wa chama anayeongoza sekretariati ya chama inayopanga agenda za chama na kusimamia mikakati yote ya chama,suala la Katiba mpya likiwa mojawapo ya mkakati.
· Freeman A.Mbowe-Huyu ni kiongozi wa upinzani bungeni na muda wote ameiongoza vema kambi ya upinzani bungeni kusimamia agenda hii ya katiba mpya.Hakutetereka na amekuwa akisimamia uwajibikaji wa pamoja wa kambi yake bungeni.Kwa jinsi leo alivyohitimisha mswada huu wa katiba mpya hawezi kusahaulika kirahisi.Amewafanya watanzania sasa kutambua ni nini maana ya kambi ya upinzani bungeni.
· Zitto Z.Kabwe-Huyu ni Naibu kiongozi wa upinzani bungeni na siku zote amekuwa msaidizi muhimu na wa kuaminiwa wa kiongozi wa upinzani bungeni.Ni wazi amesaidia sana kuifanya kambi ya upinzani kuwa kama jinsi ilivyo na anastahili kufurahia matunda ya kupigania katiba mpya ndani ya bunge.
· Tundu A.Lissu-Ni mnadhimu mkuu wa upinzani bungeni.Huyu ukitaja jina lake kwa sasa hata mtoto mdogo anamjua.Hili ni jembe kweli kweli.Alipinga kwa nguvu zote mswada mbovu wa mwaka jana.Kutokana na upinzani wake kwa mswada wabunge wa CCM na CUF walimshambulia kwa kila neno baya ili kumchafua mbele ya jamii.Lakini alisimama kidete kupambana ndani na nje ya bunge mpaka leo hii walau watanzania wanafurahia mabadiliko ya sheria ile.
· Wabunge wote wa CHADEMA-Hawa kwa ujumla wao wamesimama kidete kwa umoja ndani na nje ya bunge kuhakikisha katiba mpya inapatikana.Kila walichokifanya kuhusu katiba ni msimamo wa chama chao.Wote walinena lugha moja.Hakika huu ni mfano wa kuigwa kwa vyama vingie pale kunapokuwa na jambo la msingi la kuwatetea watanzania.Iliwashangaza wengi pale hata mbunge wa Maswa John Shibuda alipoungana na wenzake mwaka jana kutoka nje ya bunge kususia mswada mbovu uliowasilishwa.

  • Rais Jakaya Kikwete-Kwa heshima ya Pekee anastahili pongezi za dhati kabisa kwa uamuzi wake wa kukubali mwito wa kukaa na CHADEMA.Ni wazi Rais alikubali kuweka pembeni itikadi ya chama chake na kuamua kuwasikiliza CHADEMA na hatimaye kuyakubali madai yao yote.Ilihitaji moyo mkuu kufanya hivi.Aliipuuza kelele za wana CCM wenzake waliokuwa hawataki akubaliane na CHADEMA.Aliwapuuza na kuwadharau wabunge wa chama chake waliotishia kupiga kura ya kutokuwa na Imani na Rais kisa eti amekubali mapendekezo ya CHADEMA ili kupata katiba bora kwa Taifa letu.Wana CCM wengine wakadiriki kusema Rais anafanya haya kwa vile anamaliza muda wake wa urais kwa hiyo anajiandalia mwisho mwema,lakini hata hawa pia Rais aliwapuuza kwa maslahi ya Katiba bora.Kwa hili hakika Jakaya Kikwete amejiandikia historia ambayo haitafutika kirahisi.
Kwa ufupi kabisa niseme waliyoyafanya CHADEMA yameingia kwenye historia mpya.Yatasimuliwa vizazi na vizazivijavyo na ni mfano kwa wanasiasa na vyama vingine vyote.Hakika wameonyesha ukomavu wa hali ya juu.Na labda niseme lakini msiniite mtabiri! Kwamba ikipatikana Katiba mpya ya watu,ambayo itatoa tume huru kabisa ya uchaguzi itakayotenda haki kwa vyama vyote mwaka 2015,basi watanzania msishangae kumuona Michael Satta wa Tanzania akimrithi Jakaya Kikwete.Na tusubiri tuone.

Mungu awatangulie watanzania katika kupata katiba bora mpya ya Tanzania.Alilolipanga Mungu mwanadamu kamwe hawezi kulipangua.

WanaJF,Nawasilisha kwenu!

Katika pongezi ni vyema kutambua mchango wa
1. Regia Mtema
2. Kamati kuu ya CHADEMA
 
Hadi nitakapoyasoma mabadiliko yenyewe ndipo nitakapoweza kuchangia lolote. Kwa habari nilizozipata ni kwamba wajumbe wetu wamekubali kupokea hata kile kidogo tulichopewa maana haikuwezekana kushindana na CCM wakubali mapendekezo yetu, hivyo mapendekezo mengi ya sheria ya katiba bado yanawalinda CCM na viongozi wake. Kama ndivyo, hatujashinda kitu, vita bado kabisa inaendelea, kilichotokea ni kuweka uwanja safi kwa mapambano..

Asante kwa mchango wako Mkandara.Hakika huu ni uwanja safi kwa mapambano..
 
Back
Top Bottom