CHADEMA yawapa raha watanzania: Taifa Lazizima

CHADEMA yawapa raha watanzania: Taifa Lazizima

Pamoja na pongezi kwa CDM, binafsi naanza kumpopngeza JK, mambo mengi nimekuwa nikimuona JK anapotoka sana lakini katika hili, naweza kukiri kuwa akilisimamia vizuri basi naye atajiandikia historia katika siasa za Tanzania. Tulikotaka kwenda kama si busara za CDM na uungwana wa JK katika hili naamini tungefika pabaya. Ninachomhurumia tu JK asipokuwa makini na ndumilakuwili kama A. Kilango itakula kwake, big up JK kwa kuwa mbayuwayu(naamini walikushauri wahafidhina lakini ukatumia na zako).
:A S 465::A S 465:

Nilimsikiliza sana mama Kilango leo nikamuona wazi ni muasi anayetaka Kikwete asifanikiwe chochote katika uongozi wake.Huyu mama ni mnafiki mkubwa sana.Rais awe naye macho sana.
 
...KWA KWELI WANASTAHILI PONGEZI KUBWA SANA....Na hii inanifanya niamini kuwa kila jambo linalofanyika kwa taabu mwisho wake huwa ni mzuri...wamekuwa wakiitwa vichaa,wendawazimu,wapumbavu,wabishi,wapenda fujo...lakini hata wakati wa kupigania uhuru Nyerere na wenziye walipitia ugumu wa aina hiyo wa kutokuaminiwa hadi mafanikio yalipopatikana...CHADEMA NI CHAMA MAKINI,IMARA NA MADHUBUTI...KINA VIONGOZI WENYE UPEO WA KUONA MBALI NA UTAALAM WA HALI YA JUU,WENYE KUTHUBUTU KUDHALILIKA KWA AJILI YA UKOMBOZI WA TANZANIA....MUNGU AWABARIKI SANA!

Hakika Slaa Mbowe na Lissu hawatasahaulika katika ramani ya Taifa hili
 
Mkuu fmpiganaji u made an outstanding analysis and fabulous observation. Kwann baba Mwanahawa hakuoni akupe ajira pale magogoni? Big up cdm, big up baba mwanahawa and big up jf members, only those who are not leftists i mean riz, rejao, madam foxy and their company. Mkuu u made my day. 😛oa :focus:

Fmpiganaji is geneous
 
fmpiganaji, tunashukuru kwa kutupa mwelekeo mzima wa mambo yanavyokwenda mpaka sasa, lkn kama mkereketwa wa vuguvugu la mabadiliko ya kisiasa yanayoendela kutokea nchini Tanzania, naomba ufafanuzi kuhusu tukio la wabunge wa CDM kutoka nje ya bunge siku ambayo Rais Kikwete alipozindua bunge. Ninachokumbuka ni kwamba kitendo kile kilifanyika kama ishara ya kuonyesha kwamba wana-CDM hawakukubaliana na matokeo ya uchaguzi wa Rais, na kwa maana hii walitoka nje ya bunge kwa sababu ya kutomtambua Rais ambaye aliandaliwa kwa ajili ya uzinduzi wa bunge hllo. Kinachonichanganya zaidi ni kitendo cha viongozi wa CDM kuomba kukutana na Rais, ambae hapo mwanzo walitangaza kutomtambua, kwa ajili ya kumshauri kuhusu mambo ya katiba. Swali langu, au ufafanuzi ninaohitaji kuupata toka kwenu wanaJF, hasa wana-CDM, ni huu: Je, vuguvugu la wana-CDM kutomtambua Rais kikwete limeishia wapi?, na hivi nini tamko rasmi la CDM kuhusu kutomtambua Rais Kikwete

...Mimi ninavyokumbuka ni kwamba CDM walitoka bungeni kwa kutokumtambua rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wakatoa sharti kwamba,kwa vile katiba ya sasa hairuhusu kisheria kurudia uchaguzi wa rais,basi watamtambua rais iwapo tu KATIBA ILIYOPO AMBAYO CCM WANAITUMIA KUCHAKACHUA CHAGUZI ZA RAIS NA WABUNGE ITABADILISHWA...
 
ni hatua nzuri, asante mchambuzi kwa thread nzuri, nategemea kumuona PASCO wa JF kwenye hii thread, nakumbuka alivyomponda Lissu na kifungu chake cha kanuni ya 57.

Hakika alimaye juani hulia kivulini.Big up Lissu
 
fmpiganaji, tunashukuru kwa kutupa mwelekeo mzima wa mambo yanavyokwenda mpaka sasa, lkn kama mkereketwa wa vuguvugu la mabadiliko ya kisiasa yanayoendela kutokea nchini Tanzania, naomba ufafanuzi kuhusu tukio la wabunge wa CDM kutoka nje ya bunge siku ambayo Rais Kikwete alipozindua bunge. Ninachokumbuka ni kwamba kitendo kile kilifanyika kama ishara ya kuonyesha kwamba wana-CDM hawakukubaliana na matokeo ya uchaguzi wa Rais, na kwa maana hii walitoka nje ya bunge kwa sababu ya kutomtambua Rais ambaye aliandaliwa kwa ajili ya uzinduzi wa bunge hllo. Kinachonichanganya zaidi ni kitendo cha viongozi wa CDM kuomba kukutana na Rais, ambae hapo mwanzo walitangaza kutomtambua, kwa ajili ya kumshauri kuhusu mambo ya katiba. Swali langu, au ufafanuzi ninaohitaji kuupata toka kwenu wanaJF, hasa wana-CDM, ni huu: Je, vuguvugu la wana-CDM kutomtambua Rais kikwete limeishia wapi?, na hivi nini tamko rasmi la CDM kuhusu kutomtambua Rais Kikwete

Mkuu Kipeperushi, CDM walitoka nje kupinga mchakato uliomuweka Rais madarakani.Mchakato huo ulitokana na katiba mbovu iliyopo na wakatoa masharti ya kuandikwa kwa Katiba mpya.Suala ambalo wamelisimamia mpaka kimeeleweka.
 

Mkuu sina cha kuongeza! Tusipokuwa makini hadi UDINI utatumika ili kufanikisha malengo ya wapuuzi fulani. Kimsingi, ndio vita ya Katiba imeanza na ni vita ngumu ajabu.

Naamini chini ya uongozi madhubuti wa CDM hili litafanikiwa.
 
leo kwa machozi ya furaha nampongeza dr slaa,lissu,mbowe,mama nkya,jukwaa la katibu,deus kiwanga,wanaCDM wote duniani,mh col.jakaya m kikwete,katibu mkuu mpya,regia mtema/RIP,mwisho watz wote kwa kuipa mamlaka cdm itupiganie wanyonge..tulisema watawale toka ikulu,cdm itawale toka mioyoni mwa watu...namlaani selina,AG,na mama kilango waliokuwa wamepanga kutupeleka kwenye vita ya kijinga...mama kilango ulisema..hata cdm ikitoka bungen,wanaccm wanatosha kujenga katibu...yako wapi sasa?CHALIII! ASANTE CDM,ASA

Thankyou.You made my day .
 
Hilo ndilo kundi gani?
Hongereni CDM kwa kushindwa kufanya SWOT dhidi ya chama tawala ili muweze kuwashawishi wananchi vizuri 2015!
Suala la katiba limeshafanyiwa kazi na CCM...2015 mtakuja na sera gani????
Kwa taarifa yako walioshindwa kufanya SWOT ni magamba ndio maana hata agenda ya katiba ilitokea cdm, na mabadiliko ya muswada pia yametokea cdm.. unafikiri kwanini..? kwasababu magamba na timu yao (wabunge) walidandia treni kwa mbele. Kwa kukusaidia Bw Rejao wewe ni victim wa tabia hiyo ya magamba na sasa inakusumbua, ukweli ni kwamba sio 2015 tu bali hata sasa magamba hawana agenda yoyote ya kuingia nayo kwa wananchi, wewe ni shahidi kila waliyobuni ilikufa kabla ya utekelezaji mfano ni hii ya gamba!
 
Naunga mkono hoja iliyotolewa kama ilivyo without major reservations!
Tatizo la Chadema yetu kuna wazungumzaji watatafuta sifa out of this! Lakini wabunge wote wameonesha weledi ulioandika historia kwakweli! From my heart siwezi kuzuia pongezi za pekee kwa Tundu Lisu! Najua kwanini! Tundu Lisu is very smart! Mengine ya kibinadamu hakuna aliyekamili jamani!
 
Wengi mmetoa pongezi hapa, ili nisirudie rudie pongezi, ni bora kuchukua fursa hii kuwataka wote wenye mapenzi mema na taifa hili mshiriki kikamilifu katika kutoa maoni na mapendekezo ambayo yatajumuishwa katika kuunda katiba mpya. Msiwaachie wanasiasa kuifanya kazi hiyo.
Mh! Ila siridhiki bila kusema 'hongera chadema'.
 
Akina Anna Kilango wamejaribu kuipinga ila Mungu ameisimami na imepita. Saa tuombee sehemu iliyobaki nayo iende kwa amani na kwa mapenzi ya Mungu Mwenye enzi

mama mdogo wa watoto wa mzee wetu malecela anaboa sana.Si lazima kila kitu aseme.Swala la katiba si size yake ni bora angenyamaza kuliko alivyofanya jana.
 
Kwanza naomba nichukue nafasi hii kukushukuru sana wewe ndugu mtoa mada kwa kutuletea mada hii katika mtiririko unaostahili. Kwa faida yangu na watanzania wengine ambao labda kwa sababu ya shughuli za mchana kutwa tumejikuta kuwa tumekosa kufauatilia bunge kwa leo hata jana, sasa nilikuwa naomba mtudokezee kidogo tu au kwa kina, ni vifungu gani katika sheria ile vilivyofanyiwa marekebisho? kwa mfano ile sheria ya mtu atakayekwamisha tume kufanya kazi yake atafungwa kifungo kisichopungua miaka mitano na faini isiyopungua milioni tano imerekebishwa? na kama imerekebishwa imekuwaje? je mamlaka ya raisi katika mchakato huu yamewekwaje? Wajumbe wa tume ya kukusanya maoni watapatikanaje?Mwisho na mimi nitakuwa si muungwana kama sitautmbua mchango wa rais wetu wa wananchi(aliyechaguliwa japo hana nguvu ya kidola) Dkt. Wilbrod P. Slaa kwa kuliongoza jahazi hili la wapigania haki na kusimama suala hili mpaka hatua lilipofikia. Pia niwashukuru wabunge na viongozi wote wa chadema kwa kazi hii nzuri. Najua bado hatujafika lakini mpaka hapo tumeonyesha kujitahidi.Nashukuru kwa majibu mtakayo nipa.
 
walisema ooh wameenda kufunga ndoa na ccm...ooh cdm wameenda kunywa kahawa ikulu nafikiri sasa ni aibu kwao cdm ina watu makini sana......umakini huu udumu

cjilo!!ndugu yangu siku zote usipende kubishana na mtu anaengalia karibu! hafikirii mbali, kwa vyovyote vile viongozi wa CDM walienda ikulu wakiwa na matumaini kabisa kuwa kuna kitu watavuna!!lakini kwa watu waliokosa upeo humu JF ndio waliokuwa wanapiga kelele oooh wameenda kunywa chai,ooh juice haya kiko wapi sasa???
 
Uchambuzi mzuri kwa kuwa umebeba yafuatayo:-

i, Historia fupi ya harakati za upatikanaji wa katiba mpya.
ii, Maudhui ya madai na kiu ya watanzania wote juu ya katiba yao, na CDM wametenda haki kwaajili yao.
iii, Imetoa nafasi ya pongezi kwa wahusika wote bila upendeleo.
iv, Inatoa hamasa na uzalendo kwa wapiganiaji wa haki na uzalendo wa kweli ktk ngazi zote, yaani viongozi, wadau wa mtandao, wanaharakati n.k

Mungu akubariki sana mtoa mada, na hongereni kwa wanaCDM na uongozi wao wote, JK, wazee wetu Warioba, Dr. Salimu kwa kuwa na moyo na taifa hili.
 
chadema daima!sote tunakiri na kuunga mkono kazi nzuri iliyofanywa na viongozi wetu wote na popote walipo,wanajf pia wamefanya kazi nzuri na muhim kuelimisha watz,watz kwa kuukubali ukweli huu ndio utz,mungu ibariki tz na watz!
 
CHADEMA Imeonesha ukomavu mkubwa sana wa kisiasa,imeonesha uwezo wa kufanya mass mobilization na imeonesha uwezo mkubwa wa kushindana kwa hoja.Mtu yeyote akiwa kwenye mizani sawa anaweza kuliona hili.Inanikumbusha alivyotamka Dr Slaa kwamba sasa Chama kinabadilisha approach yake ya kufanya mambo na kuwa scientific zaidi pia chama kinaangalia namna ya kuwasaidia wananchi directly katika changamoto za kila siku.CHADEMA Imeonesha uwezo mkubwa kusimamia suala la katiba.

Ni mchawi tu anayeweza kuona CDM haistahili pongezi.Nawapongeza sana makamanda wote wakiongozwa na kamanda wa kikosi cha anga Freeman Aikaeli Mbowe.From the bottom point of my heart nimefurahishwa sana na CDM .KUSIMAMIA INACHOKIAMINI
 
Back
Top Bottom