Panapostahili pongezi ni wajibu kupongeza,JK aliogopa historia kuja kumhukumu,hapo ndipo inapojidhihirisha aina ya watu walio mzunguka katika kabeneti yake.Wasaliti walio shindwa kujenga hoja za kutetea maamuzi ya serikali waliyokubaliana pamoja na kuagizwa kuyaingiza katika sheria iliyopitishwa na kusainiwa na rais ikiwa na mapungufu mengi yaliyojaa usimba na uyanga.
Hakika maneno yaliyotamkwa na kiongozi wa upinzani bunge yanadhihirisha think tank ya taifa ipo sehemu ganina think dump ya taifa ipo upande gani.kwanza kabisa Watanzania tuna bahati mmoja kubwa kwa kujifunza toka kwa majirani zetu.Imekuwa mara nyingi majirani zetu wanatangulia na sisi tunafuata,kwa kweli hilo ni jambo la kumshukuru Mungu kwa kutujalia nafasi hiyo ya kujifunza kutokana na matatizo yaliyowapata majirani zetu.
Tumekuwa tukitumika kama mediator na conciliator kwa matatizo ya wenzetu,si vizuri basi nasi tukaingia kwenye mkumbo huu,eti kisa maslahi binafsi ya vyama vyetu kama wenzetu waliojaribu kutaka kutuingiza huku kwa kuingiza wakuu wa wilaya katika mchakato huo wa kuandika katiba.Naupongeza uvumilivu wa CDM,kwa taadhari yao kuu tangu kutangazwa matokeo ya uchaguzi ulioaminika lkukumbwa na udanganyifu wa hali ya juu.uvumilivu huo leo hii unaonyesha njia muaafaka ya majadiliano kuelekea kuandika katiba ya kihistoria ya wananchi toka kusimikwa mizizi ya nchi hii.
Pongezi kwa wananchi kwa umoja wao kwa kuwa wavumilivu kipindi chote,kabla ya kuamua kuigeuza Tanzania kuwa Tahrir,katika kutafuta ukombozi wa kweli kwa kujiamulia mambo yetu wenyewe kwa jinsi tutakavyoona inafaa.Bila kuvisahau vyombo vya habari vilivyokubali kuutaadharisha umma juu ya muswada uliogeuzwa na kutekwa na makajanja wa demokrasia hapa nchini.mwisho pongezi kwa taasisi zote za kijamii zilizoguswa kwa namna moja ama nyingine katika kuhakikisha amani ya nchi yetu haichezewi kwa maslahi ya wachumia tumbo na walafi wa madaraka.