mbwigule
JF-Expert Member
- Jan 21, 2012
- 235
- 103
Kumbe sasa napata picha kwamba tatizo la Kikwete ni washauri wabovu, waliovimbiwa ufisadi na kupofushwa na tamaa zao binafsi yaani wao kwanza, taifa baadae. Nasema hivi kwa sababu baada ya Kikwete kukaa chini na kuwasikiliza CHADEMA vizuri aligundua mapungufu mengi yaliyochomekwa kwenye ule muswada aliousaini (Kwa hili anastahili pongezi) na kilichofuata ni kuchukua uamuzi mgumu kabisa dhidi ya mavuvuzela yake na kuurudisha muswada ule Bungeni bila kujali vitisho vya kupigiwa kura za kutokuwa na imani. Hebu sasa tujiulize, ni mara ngapi JK kapotoshwa na washauri wake na kufanya maamuzi yaliyompunguzia mvuto na heshima?fmpiganaji,
Bravo. Huo ni ukweli na ukweli mtupu. CHADEMA wanastahili pongezi za dhati kabisa. Frankly speaking CHADEMA ndiyo kioo cha Uongozi katika Taifa hili mabalo kwa sasa limepoteza mwelekeo kutokana na uongozi MBOVU wa Chama cha Magamba.
Kwa heshima na Taadhima napenda nami kuwapa pongezi nyingi Viongozi waandamizi wa CDM,Wabunge,Wanachama na Wapenzi wa CDM.
Sitakuwa nimetenda haki pasipo kumtaja Marehemu, dada yetu mpenzi Bi Regia Mtema(RIP) kwa mchango na mawazo yake kwenye mchakato huu kabla hajatutoka mapema mwezi uliopita.
My Take:
JK sasa amegundua kwamba ni salama zaidi kusimama upande wa umma kuliko wa mashabiki na walevi wa kifisadi. Namshauri asisite kushirikiana na wapinzani hata katika masuala tata kama hili linalolitesa taifa sasa la mgomo wa madaktari ili kuiepusha nchi na maafa yasiyo ya lazima.