CHADEMA yawapa raha watanzania: Taifa Lazizima

CHADEMA yawapa raha watanzania: Taifa Lazizima

That is good analysis, magamba na mipasho yao ziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Akina Anna Kilango wamejaribu kuipinga ila Mungu ameisimami na imepita. Saa tuombee sehemu iliyobaki nayo iende kwa amani na kwa mapenzi ya Mungu Mwenye enzi
 
bila kumsahau Shibuda pamoja na umbumbu wake ambao wabunge wa CDM wameamua kupampatiliza lakini akaongeza kiasi cha Ruzuku inayoliamsha Taifa Tanzania


Hahahahaa.., Nimeipenda hii.., hapa ndo naamini kila kitu duniani kinafaida, hata ki.ny..est kinaweza tumika kama mbolea..:lol::lol:
 
Wakati mwingine sio lazima uchangie, nnajifunza kwa kusoma maoni makini na hata yasiyo makini., Nawasilisha wakuu.
 
WanaJF,
Tutakuwa hatutendi haki kama hatutasimama kama Watanzania kutoa pongezi za dhati kabisa kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kwa kusimamia kidete suala la Katiba mpya mpaka sasa marekebisho ya sheria ya Katiba mpya yakapitishwa na bunge leo.Ni wazi watu mbalimbali akiwemo Rais Kikwete wamechangia hili lakini bila kumung’unya maneno niseme kama si CHADEMA kusingekuwa na hoja hii ya Katiba mpya leo.

Kwanini?

· CHADEMA iliweka suala la Katiba mpya kwenye ilani yake ya Uchaguzi mwaka 2010
· Wabunge wa CHADEMA walitoka nje ya bunge siku Rais alipolifungua bunge pamoja na mambo mengine kudai katiba mpya itakayotoa fursa ya kuwa na tume huru ya uchaguzi
· Mwaka mzima wa 2011 CHADEMA iliongoza maandamano nchi nzima kutoa elimu ya uraia na kutaka kuungwa mkono na UMMA juu ya kupata katiba mpya
· Wabunge wa CHADEMA walitoka nje ya bunge mwezi Novemba 2011 kupinga mswada wa Katiba mpya uliokuwa na Mapungufu mengi na ya kimsingi
· Kamati kuu ya CHADEMA ilinyoosha Mkono wa mapatano na serikali kwa kukutana na Rais Kikwete kupinga mswada uliokuwa mbovu uliopitishwa kiushabiki na wabubge wa CCM na CUF
· Rais aliridhia mapendeklezo yote ya CHADEMA na kuamuru mabadiliko ya sheria iliyokuwa imepitishwa kishabiki na wabubge wa CCM na CUF
· Hatimaye marekebisho ya sheria yakapitishwa na bunge na kufungua rasmi mlango wa kutengeneza katiba mpya ya Tanzania.

Ni wazi kwa yote yaliyotajwa hapo juu yanatufanya tuamini CHADEMA imesimama imara katika kupigania Katiba ya nchi.Watanzania wengi walikata tamaa na kudhani baada ya mswada mbovu kupitishwa mwaka jana CHADEMA ingesusia moja kwa moja zoezi zima.Lakini CHADEMA imejenga taswira tofauti kwa Watanzania kwa kupigana kwa hali yoyote kuhakikisha Katiba mpya inapatikana.

Wafuatao wanastahili heshima ya pekee:

Pamoja na CHADEMA kama taasisi kuonekana kukomaa na kusimamia agenda zake,ni lazima tuwatambue baadhi ya watu walioongoza mpambano huu kwa Amani na utulivu na siku moja wataingia katika vitabu vya historia

· Dr Wilbroad P. Slaa-Ni kiongozi makini,madhubuti na anayeweza kuyasimamia maneno yake kwa kuinadi ilani ya CHADEMA nchi nzima wakati wa kugombea urais mwaka 2010 na watu wakaamini na kuona umuhimu wa Katiba mpya.Lakini Pia ni Katibu mkuu ambaye ni mtendaji mkuu wa chama anayeongoza sekretariati ya chama inayopanga agenda za chama na kusimamia mikakati yote ya chama,suala la Katiba mpya likiwa mojawapo ya mkakati.
· Freeman A.Mbowe-Huyu ni kiongozi wa upinzani bungeni na muda wote ameiongoza vema kambi ya upinzani bungeni kusimamia agenda hii ya katiba mpya.Hakutetereka na amekuwa akisimamia uwajibikaji wa pamoja wa kambi yake bungeni.Kwa jinsi leo alivyohitimisha mswada huu wa katiba mpya hawezi kusahaulika kirahisi.Amewafanya watanzania sasa kutambua ni nini maana ya kambi ya upinzani bungeni.
· Zitto Z.Kabwe-Huyu ni Naibu kiongozi wa upinzani bungeni na siku zote amekuwa msaidizi muhimu na wa kuaminiwa wa kiongozi wa upinzani bungeni.Ni wazi amesaidia sana kuifanya kambi ya upinzani kuwa kama jinsi ilivyo na anastahili kufurahia matunda ya kupigania katiba mpya ndani ya bunge.
· Tundu A.Lissu-Ni mnadhimu mkuu wa upinzani bungeni.Huyu ukitaja jina lake kwa sasa hata mtoto mdogo anamjua.Hili ni jembe kweli kweli.Alipinga kwa nguvu zote mswada mbovu wa mwaka jana.Kutokana na upinzani wake kwa mswada wabunge wa CCM na CUF walimshambulia kwa kila neno baya ili kumchafua mbele ya jamii.Lakini alisimama kidete kupambana ndani na nje ya bunge mpaka leo hii walau watanzania wanafurahia mabadiliko ya sheria ile.
· Wabunge wote wa CHADEMA-Hawa kwa ujumla wao wamesimama kidete kwa umoja ndani na nje ya bunge kuhakikisha katiba mpya inapatikana.Kila walichokifanya kuhusu katiba ni msimamo wa chama chao.Wote walinena lugha moja.Hakika huu ni mfano wa kuigwa kwa vyama vingie pale kunapokuwa na jambo la msingi la kuwatetea watanzania.Iliwashangaza wengi pale hata mbunge wa Maswa John Shibuda alipoungana na wenzake mwaka jana kutoka nje ya bunge kususia mswada mbovu uliowasilishwa.

  • Rais Jakaya Kikwete-Kwa heshima ya Pekee anastahili pongezi za dhati kabisa kwa uamuzi wake wa kukubali mwito wa kukaa na CHADEMA.Ni wazi Rais alikubali kuweka pembeni itikadi ya chama chake na kuamua kuwasikiliza CHADEMA na hatimaye kuyakubali madai yao yote.Ilihitaji moyo mkuu kufanya hivi.Aliipuuza kelele za wana CCM wenzake waliokuwa hawataki akubaliane na CHADEMA.Aliwapuuza na kuwadharau wabunge wa chama chake waliotishia kupiga kura ya kutokuwa na Imani na Rais kisa eti amekubali mapendekezo ya CHADEMA ili kupata katiba bora kwa Taifa letu.Wana CCM wengine wakadiriki kusema Rais anafanya haya kwa vile anamaliza muda wake wa urais kwa hiyo anajiandalia mwisho mwema,lakini hata hawa pia Rais aliwapuuza kwa maslahi ya Katiba bora.Kwa hili hakika Jakaya Kikwete amejiandikia historia ambayo haitafutika kirahisi.
Kwa ufupi kabisa niseme waliyoyafanya CHADEMA yameingia kwenye historia mpya.Yatasimuliwa vizazi na vizazivijavyo na ni mfano kwa wanasiasa na vyama vingine vyote.Hakika wameonyesha ukomavu wa hali ya juu.Na labda niseme lakini msiniite mtabiri! Kwamba ikipatikana Katiba mpya ya watu,ambayo itatoa tume huru kabisa ya uchaguzi itakayotenda haki kwa vyama vyote mwaka 2015,basi watanzania msishangae kumuona Michael Satta wa Tanzania akimrithi Jakaya Kikwete.Na tusubiri tuone.

Mungu awatangulie watanzania katika kupata katiba bora mpya ya Tanzania.Alilolipanga Mungu mwanadamu kamwe hawezi kulipangua.

WanaJF,Nawasilisha kwenu!
Aisee! Unastahili kupanda ngazi kuwa Premium Member sasa.
 
Umemsahau kwenye Orodha Kamanda John Mrema Mkurugenzi wa Utafiti na Bunge wa CHADEMA hata Lissu ametambua mchango wake katika hotuba ya upinzani.

Pia Mnyika ambaye hoja yake binafsi ndio ilitaka jambo hili lianzie bungeni kwa kutungwa sheria badala ya Rais kuanza mchakato kwa kuunda tume yake mwenyewe kama Kikwete alivyotangaza awali. Mnyika ametajwa tajwa sana humu JF kuhusu masuala ya katiba ikiwemo juu ya mazungumzo na Rais.

Bila kuwasahau maprofesa Majembe Baregu na Safari na mzee wetu Arfi nao wametoa mchango mkubwa kwa kuwepo kwenye kamati maalum ya kamati kuu ya chama chetu.

Kwenye CCM anayestahili shukrani ni Kikwete pekee kwa kuepusha shinikizo la maandamano.

serayamajimbo
 
Hongera kwa viongozi wa ukweli!....... Mligundua kuwa Baba Mwanaasha kaingizwa choo cha kike mkamshtua naye akafuata maelekezo yenu......... Walaniwe Anna Kilango na timu yake iliyotaka kuingiza Taifa kwenye machafuko kama yaliyotokea Kenya......... Hongera kwa JF members wote kwa kufuatilia mchakato kwa makini!...... Big up kwa moderators kwa kuweka kizuizi kwa serikali ya Magamba ili tusifungiwe na kusababisha kukosa utamu wa kupashana habari!
 
Haujamtendea haki Baba Mwanaasha kwa ushirikiano aliouonyesha wa kufumba macho na masikio na kukubali kuonekana kigeugeu kwa kukubali kufanyia marekebisho kitu ambacho ametoka kukubalina nacho mia kwa mia masaa machache tu yaliyopita.

Kweli mkuu maana jamaa wanataka kumtenga lakini aliona taifa mbele !


Pamoja na kumpa pongezi Baba Mwanaasha, ila ukweli ni kuwa hakuwa na jinsi, joto lilikuwa limepanda sana. CHADEMA walna watu na yeye ana Ikulu. Hivyo kuitawala nchi bila CDM isingekuwa rahisi. Wewe jiulize katika vyama vyote vilivyoenda ikulu, ni CDM tu ndo iliyokwenda mara tatu. vingine vyote ni mara moja moja tu. CDM walikuwa na hoja nzito na zaidi sana walikuwa na nguvu ya umma
.
 
Good analysis by fmpiganaji, viva. Sina hata kimoja cha kuongezea hapo, yote umedhungumza.
R.I.P kamanda Regia Mtema, huku mapambano yanaendelea kamanda, hakuna kulala mpaka kinaeleweka.
2015 for changes.
 
Haujamtendea haki Baba Mwanaasha kwa ushirikiano aliouonyesha wa kufumba macho na masikio na kukubali kuonekana kigeugeu kwa kukubali kufanyia marekebisho kitu ambacho ametoka kukubalina nacho mia kwa mia masaa machache tu yaliyopita.

Du! - yaani nyie Waswahili kwa kuwapachika majina watu! - yaani naona sasa katoka kuwa baba Riz na kawa baba Mwanaasha!
 
kazi nzuri siku zote lazima ipate sifa, big up wabunge wote wa chadema kwa msimamo wenu katika hili, pongez pia zimfikie JK kwa kuweka itikadi zake pembeni na kuwasikiliza wadau wote waliofika kwake.
 
Watanzania wenzangu! mimi nimsomaji tu humu na sijawahi kuchangia sana ila naomba na mimi kwa hili niingie kwenye historia ya wawakilishi wachache wataopata fursa ya kupongeza viongozi wetu makini waliofanikisha marekebisho haya kupita kwa ajili tu ya masilahi ya Watanzania.. Kwanza kabisa napenda kwa dhati kumshukuru na kumpongeza RAIS wetu J M Kikwete kwa ujasiri na pengine moyo wa usaliti aliouonyesha kwa chama chake na kuweka maslahi na uzalendo mbele kuridhia mawazo na mapendekezo yaliyowasilishwa kweke na CHADEMA. Ni ukomavu wa hali ya juu sana katika ulimwengu wa waliostaarabika. ni dhahiri siasa za dunia ya tatu ni tete mbovu hasa kwenye masuala ya msingi kitaifa kama hili. Ni historia Rais na utaishi na raha hiyo milelePili Nachukua fursa hii kuwapongeza CHADEMA NA WANA CHADEMA kwa kazi nzuri inayofanywa kuinua taifa letu changa linaloelekea kupotoshwa na kuyumbishwa na walafi wachache! ni hatua ya hali ya juu iliyotukuka inayokifanya CHADEMA kuimarika kila kukicha pale inapokumbatia Utaifa na uzalendo wa kweli kwa kila wazo au jambo linalofanywa. Nawapongeza sana na ninawahakikishia historia itachukua mkondo wake pale muda utakapotimia.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
WanaJF,Tutakuwa hatutendi haki kama hatutasimama kama Watanzania kutoa pongezi za dhati kabisa kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kwa kusimamia kidete suala la Katiba mpya mpaka sasa marekebisho ya sheria ya Katiba mpya yakapitishwa na bunge leo.Ni wazi watu mbalimbali akiwemo Rais Kikwete wamechangia hili lakini bila kumung’unya maneno niseme kama si CHADEMA kusingekuwa na hoja hii ya Katiba mpya leo.Kwanini?· CHADEMA iliweka suala la Katiba mpya kwenye ilani yake ya Uchaguzi mwaka 2010· Wabunge wa CHADEMA walitoka nje ya bunge siku Rais alipolifungua bunge pamoja na mambo mengine kudai katiba mpya itakayotoa fursa ya kuwa na tume huru ya uchaguzi· Mwaka mzima wa 2011 CHADEMA iliongoza maandamano nchi nzima kutoa elimu ya uraia na kutaka kuungwa mkono na UMMA juu ya kupata katiba mpya· Wabunge wa CHADEMA walitoka nje ya bunge mwezi Novemba 2011 kupinga mswada wa Katiba mpya uliokuwa na Mapungufu mengi na ya kimsingi· Kamati kuu ya CHADEMA ilinyoosha Mkono wa mapatano na serikali kwa kukutana na Rais Kikwete kupinga mswada uliokuwa mbovu uliopitishwa kiushabiki na wabubge wa CCM na CUF· Rais aliridhia mapendeklezo yote ya CHADEMA na kuamuru mabadiliko ya sheria iliyokuwa imepitishwa kishabiki na wabubge wa CCM na CUF· Hatimaye marekebisho ya sheria yakapitishwa na bunge na kufungua rasmi mlango wa kutengeneza katiba mpya ya Tanzania.Ni wazi kwa yote yaliyotajwa hapo juu yanatufanya tuamini CHADEMA imesimama imara katika kupigania Katiba ya nchi.Watanzania wengi walikata tamaa na kudhani baada ya mswada mbovu kupitishwa mwaka jana CHADEMA ingesusia moja kwa moja zoezi zima.Lakini CHADEMA imejenga taswira tofauti kwa Watanzania kwa kupigana kwa hali yoyote kuhakikisha Katiba mpya inapatikana.Wafuatao wanastahili heshima ya pekee:Pamoja na CHADEMA kama taasisi kuonekana kukomaa na kusimamia agenda zake,ni lazima tuwatambue baadhi ya watu walioongoza mpambano huu kwa Amani na utulivu na siku moja wataingia katika vitabu vya historia· Dr Wilbroad P. Slaa-Ni kiongozi makini,madhubuti na anayeweza kuyasimamia maneno yake kwa kuinadi ilani ya CHADEMA nchi nzima wakati wa kugombea urais mwaka 2010 na watu wakaamini na kuona umuhimu wa Katiba mpya.Lakini Pia ni Katibu mkuu ambaye ni mtendaji mkuu wa chama anayeongoza sekretariati ya chama inayopanga agenda za chama na kusimamia mikakati yote ya chama,suala la Katiba mpya likiwa mojawapo ya mkakati.· Freeman A.Mbowe-Huyu ni kiongozi wa upinzani bungeni na muda wote ameiongoza vema kambi ya upinzani bungeni kusimamia agenda hii ya katiba mpya.Hakutetereka na amekuwa akisimamia uwajibikaji wa pamoja wa kambi yake bungeni.Kwa jinsi leo alivyohitimisha mswada huu wa katiba mpya hawezi kusahaulika kirahisi.Amewafanya watanzania sasa kutambua ni nini maana ya kambi ya upinzani bungeni.· Zitto Z.Kabwe-Huyu ni Naibu kiongozi wa upinzani bungeni na siku zote amekuwa msaidizi muhimu na wa kuaminiwa wa kiongozi wa upinzani bungeni.Ni wazi amesaidia sana kuifanya kambi ya upinzani kuwa kama jinsi ilivyo na anastahili kufurahia matunda ya kupigania katiba mpya ndani ya bunge.· Tundu A.Lissu-Ni mnadhimu mkuu wa upinzani bungeni.Huyu ukitaja jina lake kwa sasa hata mtoto mdogo anamjua.Hili ni jembe kweli kweli.Alipinga kwa nguvu zote mswada mbovu wa mwaka jana.Kutokana na upinzani wake kwa mswada wabunge wa CCM na CUF walimshambulia kwa kila neno baya ili kumchafua mbele ya jamii.Lakini alisimama kidete kupambana ndani na nje ya bunge mpaka leo hii walau watanzania wanafurahia mabadiliko ya sheria ile.· Wabunge wote wa CHADEMA-Hawa kwa ujumla wao wamesimama kidete kwa umoja ndani na nje ya bunge kuhakikisha katiba mpya inapatikana.Kila walichokifanya kuhusu katiba ni msimamo wa chama chao.Wote walinena lugha moja.Hakika huu ni mfano wa kuigwa kwa vyama vingie pale kunapokuwa na jambo la msingi la kuwatetea watanzania.Iliwashangaza wengi pale hata mbunge wa Maswa John Shibuda alipoungana na wenzake mwaka jana kutoka nje ya bunge kususia mswada mbovu uliowasilishwa.
  • Rais Jakaya Kikwete-Kwa heshima ya Pekee anastahili pongezi za dhati kabisa kwa uamuzi wake wa kukubali mwito wa kukaa na CHADEMA.Ni wazi Rais alikubali kuweka pembeni itikadi ya chama chake na kuamua kuwasikiliza CHADEMA na hatimaye kuyakubali madai yao yote.Ilihitaji moyo mkuu kufanya hivi.Aliipuuza kelele za wana CCM wenzake waliokuwa hawataki akubaliane na CHADEMA.Aliwapuuza na kuwadharau wabunge wa chama chake waliotishia kupiga kura ya kutokuwa na Imani na Rais kisa eti amekubali mapendekezo ya CHADEMA ili kupata katiba bora kwa Taifa letu.Wana CCM wengine wakadiriki kusema Rais anafanya haya kwa vile anamaliza muda wake wa urais kwa hiyo anajiandalia mwisho mwema,lakini hata hawa pia Rais aliwapuuza kwa maslahi ya Katiba bora.Kwa hili hakika Jakaya Kikwete amejiandikia historia ambayo haitafutika kirahisi.
Kwa ufupi kabisa niseme waliyoyafanya CHADEMA yameingia kwenye historia mpya.Yatasimuliwa vizazi na vizazivijavyo na ni mfano kwa wanasiasa na vyama vingine vyote.Hakika wameonyesha ukomavu wa hali ya juu.Na labda niseme lakini msiniite mtabiri! Kwamba ikipatikana Katiba mpya ya watu,ambayo itatoa tume huru kabisa ya uchaguzi itakayotenda haki kwa vyama vyote mwaka 2015,basi watanzania msishangae kumuona Michael Satta wa Tanzania akimrithi Jakaya Kikwete.Na tusubiri tuone.Mungu awatangulie watanzania katika kupata katiba bora mpya ya Tanzania.Alilolipanga Mungu mwanadamu kamwe hawezi kulipangua.WanaJF,Nawasilisha kwenu!
 
Haujamtendea haki Baba Mwanaasha kwa ushirikiano aliouonyesha wa kufumba macho na masikio na kukubali kuonekana kigeugeu kwa kukubali kufanyia marekebisho kitu ambacho ametoka kukubalina nacho mia kwa mia masaa machache tu yaliyopita.

duuuh..
 
Back
Top Bottom