Kwa mujibu wa mwenyekiti wa CHADEMA kata Ndugu Paulo,amesema Kamanda Malisa ameshinda kwa kishindo katika uchaguzi huo na kumuangusha mgombea wa wa CCM ndugu Tom wa kitongoji cha Llima Sioni. Pamoja na utundu uliotumika wa CCM kuongeza madiwani watatu nao wapige kula lakini juhudi zao ziligonga mwamba na Ndugu Malisa kutoka kwenye ukumbi akiwa kidedea.Pia jopo hilo limemchagua makamu mwenyekiti nao ikaenda kwa CHADEMA na kuchaguliwa ndugu Richard Mkungu kwa kula nyingi na kumbwaga Richard wa CCM kitongoji cha Usa Madukani. Kwahiyo pia nafasi ya makamu wa mwenyekiti ikaenda CHADEMA.