CHADEMA yasambaratika mkoani Kigoma

CHADEMA yasambaratika mkoani Kigoma

quote_icon.png
By Mwanaukweli

Kitaendelea? Kwani kimeshaanza?

Kimeanzia wapi mkuu? Kwa ushahidi gani?
unapaswa kusaidiwa na hiyo akili yako kwani hii post unayochangia inakwambia nini.
Ni propaganda tu, na mnalipwa kwa kazi hiyo. Mimi niko Kigoma, nakaa Mwanga mtaa wa Shaurimoyo.

Mimi akili yangu ni nzuri sana, hainunuliwi kwa propaganda nyepesi kama hizi.

Nathibitisha kuwa hayo yanayosemwa ni uongo mtupu! Anahitaji alete ushahidi hapa nami ntaleta ushahidi dhidi ya ushahidi wake.
 
Kwa hiyo unashauri nini Mkigoma,au ndo walewale wa kutaka kila mnachotaka mnakipata hata kwa........Arusha.
 
Hujajibu swali langu narudia:

Hivi Zitto ana tofauti gani na Slaa kiitikadi? Je wanampinga Slaa kwa itikadi gani na wanamuunga mkono Zitto kwa itikadi gani tofauti?

Natumaini unaelewa maana ya itikadi.

Wenye itikadi kamwe mmoja hawezi kuajiri kikundi cha watu kumdhuru mwingine. Kumshushia credibility, uaminifu wake kwa mambo ya kutunga. Slaa itikadi yake sio iliyokatika makaratasi ya chadema ambayo zito ndio anasimamia itikadi hiyo. Zitto amekuwa mtu wa busara na asiemnafiki. Umesahau kuwa slaa amemuunga mkono kagame dhidi ya nchi?
Umesahau jinsi anavyopinga kila jambo linaloanzishwa au kufanywa na ccm hata ikitokea nila muhimu kiasi gani kwa taifa?
 
Wenye itikadi kamwe mmoja hawezi kuajiri kikundi cha watu kumdhuru mwingine. Kumshushia credibility, uaminifu wake kwa mambo ya kutunga. Slaa itikadi yake sio iliyokatika makaratasi ya chadema ambayo zito ndio anasimamia itikadi hiyo. Zitto amekuwa mtu wa busara na asiemnafiki. Umesahau kuwa slaa amemuunga mkono kagame dhidi ya nchi?
Umesahau jinsi anavyopinga kila jambo linaloanzishwa au kufanywa na ccm hata ikitokea nila muhimu kiasi gani kwa taifa?
Hayo ni ya uongo na zitto mwenyewe alishayakanusha hata humu JF. Tamko la Zitto hili hapa:

Au unataka kutwambia kuwa Zitto ni muongo pamoja na sifa zote ulizotuwekea hapa za Zitto, ambazo mimi pia nazikubali?

Katika gazeti la Mtanzania toleo na. 7269 la Jumatano Machi 27, 2013 kuna habari yenye kichwa chenye maneno ‘SIRI YA KUUWAWA ZITTO YAFICHUKA' na vichwa vidogo ‘yadaiwa ilipangwa anyweshwe sumu hotelini' dk. Slaa atajwa kumtuma Saanane kummaliza'. Habari hii imeniletea usumbufu mkubwa kwani ndugu, jamaa, marafiki na wapiga kura wangu, wamejazwa na wasiwasi mkubwa sana kwamba ninaweza kuuwawa.

Napenda kusema yafuatayo:

Moja, sijawahi katika maisha yangu yote kukutana na mtu anayeitwa Ben Saanane na hivyo hicho kikao ambacho inasemekana nilikuwa naye na akajaribu kunipa sumu hakijawahi kutokea. Imetajwa Hoteli ya Lunch Time ambayo sio tu sijawahi kufika, pia hata siijui ipo wapi. Haijawahi kutokea mimi kufanya kikao cha pamoja na Ben Saanane, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba. Hivyo habari iliyoandikwa ni ya kufikirika na hivyo naomba mwandishi ahakikishe kuwa vyanzo vyake vya habari vimempa habari sahihi.

Pili, Siamini kamwe kuwa Katibu Mkuu wa chama changu anaweza kupanga kuniua maana hana sababu ya kufanya hivyo. Napenda kurudia kusema kwamba mimi ninaamini kuwa kila nafsi itaonja mauti. Kila mtu atakufa. Kama nitakufa kwa kuuwawa na mtu mwingine ndio itakuwa nimeandikiwa hivyo na Mungu. Ndio maana hata siku moja silalamiki kuhusu vitisho vya kuuwawa nk. Kama kuna mtu anafikiria kuwa kumuua Zitto ndio furaha ya maisha yake atakuwa anajidanganya tu maana Zitto anaweza kufa kimwili lakini mawazo, fikra na maono ya Zitto yataishi tu. Siogopi kufa maana maisha niliyoyachagua ndio haya ambayo yamejaa vitisho. Muhimu kwangu ni kufanya kazi zangu kwa bidii, uhodari na uaminifu. Siku zote nitasimamia ukweli bila kujali uchungu wa ukweli huo.

Tatu, nawashauri watu ambao wamehama CHADEMA na kuhamia vyama vingine watumie muda wao kujenga vyama vyao badala ya kila siku kuzungumzia masuala ya chama ambacho wao sio wanachama tena. Kama mtu kaamua kuhama CHADEMA anapoteza haki ya kujadili masuala ya CHADEMA maana kama angekuwa anapenda kuyajadili asingehama. Naonya mtu yeyote ambaye anatumia jina langu ili kufanikisha malengo yake ya kisiasa. CHADEMA sio pango la watesaji wala wauaji. Kama kuna mwanachama wa chama kingine cha siasa anayedhani kuna mtu ndani ya CHADEMA anapanga mipango ovu aende kwenye vyombo vya sheria kumshtaki. Matendo ya mtu mmoja yasifanyiwe propaganda kama ni malengo ya taasisi.

Nne, Nawashauri viongozi wenzangu wa CHADEMA na hasa wanachama tutumie muda wetu kujenga mshikamano ndani ya chama. Fitna, majungu, uongo, uzandiki nk kamwe havijengi chama. Chama chetu lazima kiwe mfano bora wa kuheshimu demokrasia na haki za binaadamu. Wananchi hawawezi kutoa dola kwa chama chenye mifarakano. Tusiruhusu kugawanywa kwa matakwa ya watu wachache. Tusimamie misingi ya kuanzishwa chama chetu.


=============


Thread inayoongelea kilichoandikwa na Mtanzania hii hapa - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ajwa-kumtuma-ben-saanane-kummaliza-zitto.html
Si kweli kuwa anapinga kila kitu. Slaa anapiga vita rushwa, na ufisadi, na hili ni jambo la kitaifa. Slaa anapigania matumizi mazuri ya rasilimali zetu.

Slaa anachukiwa kwa sababu nyingine tu ambazo mnaona aibu kuzitaja kwa kuwa ni za kibaguzi.

Lete propaganda nyingine.
 
:A S 2152::A S 2152:Tehe tehe tehe....! wakati chadema wanatumia nguvu nyingi kuitafuta nafasi ya kuingia Ikulu basi CCM wanacheza na Pychology na kutumia akili kuwa maliza

kwa utoto kama huu wa mkigoma huwezi kuimaliza cdm .
 
mkigoma wewe unajulikana kuwa ni mnazi wa chama cha cuf kwahiyo kuleta habari kama hii sio jambo la ajabu. Chama chenu kinapumulia mrija kwa sasahivi na mwaka 2015 mnazikwa na kusahaulika kabisa.
Nimepita ofisi zenu za makao makuu mtaa wa mtendeni inaonyesha dhahiri mlivyochokwa hata huku visiwani mlukokuwa mnajipatia uungwaji mkono kidogo nao wamewachoka hadi wanataka kuwatapika!!
 
Last edited by a moderator:
Kutokana na mvutano unaoendelea ndani ya Chama cha demokrasia na maendeleo na Chadema imesababisha Chama hicho kusambaratika na kupoteza mvuto mkoani kigoma, sababu hasa inaonekana ni kutengwa kwa kijana wao zitto kabwe ndani ya chama hicho, na hata tetesi zinazoongelewa katika vijiwe vya siasa mkoani kigoma, aliye kuwa mgombea wa chama cha chadema Mwaka 2010 Ally mlee akakihama Chama muda wowote kuanzia sasa. Hali ni mbaya mkoani hapa, kila kijiwe kinaongelea ubaguzi ndani ya chama hicho.
Habari yako tutaendelea kuichukua kama ulivyoeleza kwenye red hapo juu.
 
Dhambi ya ubaguzi inawaandama hawa chadema, na kila siku wanashauriwa hawasikii, sikio la kufa halisikii dawa.
Huku mtaani hilo linawatafuna taratibu, mwisho wa siku kwenye sanduku kura 10 wasingizie wameibiwa.
 
Sasa kama mpendwa wako ZITTO ameshindwa kuijenga CHADEMA mkoani kwake tu vipi angekabidhiwa CHADEMA TAIFA? Alipotaka kugombea uenyekiti taifa ilikuwa ni mpango wa kuisambaratisha CHADEMA bahati mbaya kwake na wapambe wake wakashitukiwa mapema!! CHADEMA mkoani Kigoma inasambaratishwa na ZITTO mwenyewe kwa sababu ya UJUAJI NA TAMAA ZAKE!! The guy has got self interests na hakuna aliyemtenga bali amejitenga yeye mwenyewe!! Pamoja na elimu yake lakini anasumbuliwa na USWAHILI!!!

Ni kipi alichofanya kuindeleza CHADEMA mkoani Kigoma na mikoa jirani? Tueleze mafanikio yake kisiasa mkoani humo: Je tangu awe mbunge na hizo sifa mnazompa amefanikiwa kuongeza madiwani na wabunge wangapi? Kama wewe siyo MGANGA NJAA natumaini utakuja na majibu ya maswali yangu!!



safi sana mkuu,umemjibu vema sana,majibu sahihi,kwa mtu sahihi na mda mwafaka,
kimsingi bwana Zitto kabwe amekuwa sawa na kansa inayoitafuna CDM Kigoma,ameshindwa kukijenga na kukiimarisha chama mkoani kigoma na wilaya zake,kama anadai anatengwa na kubaguliwa na viongozi wa kitaifa angerudi na kuimarisha ngome mkoani kwake kama anavyofanya Wenje,Sugu na Lema badala ya kulialia,me nipo kigoma na napta vijiwe na kuongea na watu wa makundi na rika mbalimbali,ukifanya mahojiano nae wengi watakwambia hawamwelewi na wanahisi atawasaliti watanzania mda c mrefu na ukisikia mtu anamtetea ujue anamtetea kwasababu wapo nae dini moja hawa wengi huwa ni wanachama wa CUF na wengine wanaomtetea ni wanachama wa CCM katika ile kutaka tumsimamishe mtu dhaifu,na mkumbuke Zitto hakubaliki kivile mkoani humu na ushahidi ni katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ambapo alishinda kwa tofauti ya kura 3000 tu can imagine ,wilaya zote mkoani Kigoma CDM ipo hoi kiuongozi japo wanachama ni wengi huku kuna wilaya tangu 2010 Zitto hajatia mguu kuimarisha chama ,shame on Zitto na waha tunasema hatumkubali na tunamwona kama mamluki ajirekebishe haraka na asitishe watu kwani hata cc tunajua jinsi ya kuzuia mpanya wetu wa ndani wasife.
 
vijiwe mbali mbali vya kigoma .
Kigoma ninayoijua mimi, ni Kigoma ambayo CCM ndicho chama kisichopendwa.

Sababu za Kutopendwa CCM Kigoma

Kuthamini Wenye fedha.

Hili lilijitokeza tangu mwanzo kabisa wa siasa za vyama vingi. Wakati huo Kigoma kulikuwa na watu wanaopendwa, waungwana na walio na karama za uongozi. Mfano ni Amaan Walid Kabourou na Rajab Kakolwa Mbano, ambaye kaka yake Marehemu Rajab Omar Mbano aliwahi kuwa mbunge kabla ya vyama vingi. CCM kwa kuthamini wenye fedha iliwaweka kando hawa na kumteua Azim Suleiman Premji kuwa mgombea wa CCM Kigoma mjini. Huyu hakuwa na mvuto kwa watu zaidi ya kuwa alikuwa tajiri. Alikuwa anamiliki Gereji ya Magari (Kigoma Auto Garage) na alikuwa anaendesha kwa kukodi Hotel ya kitalii iliyokuwa inamilikiwa na Railways (Kigoma Railways Hotel - Kwa sasa Lake Tanganyika Beach Hotel). Yaani alikuwa na uwezo wa kununua maamuzi ya vigogo wa CCM. Matokeo yake ni kuwa watu wa Kigoma wakasema EKAYEEE! (=NO). Wakamwambia Kabourou ajiunge na CHADEMA na wakamchagua Kabourou miongoni mbunge wa kwanza wa CHADEMA, na kati ya wabunge wachache sana wa upinzani 1995. Premji baadaye alikuwa Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Kigoma.

Kama hiyo haitoshi akajitokeza tajiri mwingine Kigoma. Huyu ni mmiliki wa Kigoma Hilltop Hotel, na Sheni's Commercial Ltd inayojishugulisha na uwindaji wa kitalii (tembo wetu). Huyu habari zake zimeandikwa sana mitandaoni na kwinginepo.
Muhsin Abdullah (Shen) Ameinunua This Country?


MOHSIN "SHENI" ABDALLAH AT IT AGAIN ; Where Have All the Elephants Gone?


Huyu Kada anaitwa Mohsin Abdallah, kuna yeyote mwana JF atupe Background yake ?


Mjue Kada wa CCM Mohsin Abdallah

Tanzania/Kenya - Where Have All the Elephants Gone? - Foreign Correspondent - ABC

Huyu pia alitaka kuingia kwenye siasa. Japo alikuwa hakubaliki kwa wanachama alikingiwa kifua na makao makuu, na kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa. Huyu Kada yumo katika list ya matajiri wahusika wa madawa ya kulevya. Kwa sasa amemaliza muda wake wa ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa. Analalamika kuwa yeye na Premji wamebaguliwa kwa rangi yao.

Kuna kada mwingine wa CCM wilayani kibondo kwa jina la Jamal Tamim. Huyu anatoka kijiji cha Mabamba wilayani Kibondo katika jimbo la uchaguzi la Muhambwe. Pale Mabamba shughuli anazofanya Jamal hazijulikani, lakini Jamal ni tajiri kupindukia. Mwaka 2007 walipafanya kura za maoni za kufichua wanaofanya biashara za viungo vya albino, Jamal aliongoza kwa kutajwa na wengi wilaya ya Kibondo. Licha ya hayo, Jamal anatuhumiwa kuwa na kikundi cha ujambazi ambacho pamoja na mambo mengine, huteka mabasi, na kufanya matukio mengine ya wizi wa kutumia nguvu. Pamoja na shutuma zote hizi kuwa wazi, CCM ilimpitisha Jamal kuwa mgombea ubunge kiti cha Muhambwe. Pingamizi la kwanza lilitoka mkoani Kigoma kwenye kamati ya Maadili ya CCM. Simbakalia na Kastico walionyesha wazi kuwa huyu Jamal hauziki, lakini kwa influence ya Rostam Aziz na JK, alipitishwa. Kastico (Katibu wa CCM Mkoa wakati huo) aliondolewa Kigoma Oktoba 2010 wakati wa kampeni kwa sababu aliweka pingamizi, na aliondolewa na JK mwenyewe alipofanya ziara ya dharura Kigoma Oktoba 2010.

Matokeo yake wana CCM wengi Kigoma walivunjika nguvu hata kupiga debe kwa wagombea wao. Uchaguzi uliopita, CCM ilishinda kiti cha Kigoma Mjini (kwa kuchakachua), Manyovu na Buyungu. Kati ya viti hivyo vyote Buyungu tu ndio wanaweza kusema kuwa waliwekewa mgombea wanayemtaka (Waziri Christopher Chiza) - ambaye hata mimi namkubali. Ni viti vitatu kati ya vinane. Ni mkoa wa bara ambao asilimia ya wawakilishi (wabunge) wa CCM ni ndogo kuliko popote Tanzania.

mkigoma, Shelui, Simiyu yetu, CHAMVIGA, utaifakwanza, Lizaboni, SONGEA ONE, njoni na hoja zinazoonesha mnaijua vizuri Kigoma na siasa zake.

Sisi watu wa Kigoma tuna mpango wa kuendelea kuikataa CCM na hatujali anayeingiea ni CHADEMA, CUF au NCCR, sisi hatuitaki CCM.

Muha akishasema NTIBHISHOBHOKA, harudi nyuma. Nyie endeleeni kupiga propaganda.
 
mleta mada pamoja na wale wanaoishabikia mada hii ya kijinga kwa tafsiri ya haraka na ya mtu muona mbali mtakuwa mnasumbuliwa na nyeg* mshindo za kidini,
nawashauri tafuteni mabasha ya kuwatimizia haja zenu maana wao waweza kuwa na akili za kufanana nanyi.

kwa fikra zenu hizo za kibaguzi ambazo mmekuwa mkizitumia na mkiwapumbaza baadhi ya watu wenye upeo mdogo hapo jimboni kwenu manispaa kigoma ujiji kumepelekea kubwagwa vibaya kwa aliyekuwa mgombea ubunge kupitia cdm ndg ally mleh na kuruhusu gamba kushinda.

kumbukeni kwa unafiki na fitina zenu za udini kulipelekea watu wenu kujikita ktk harakati za kumchagua bwana dhaifu kwa misingi ya imani zenu."ushahidi sanduku la kura 2010" vituo vyote vya ujiji ambako ndiko ngome ya wale akina yakhee wenzako na bhana kubwa kupitia gambaz aliongoza kwa kupata kura kwa misingi na mitazamo munayoijua ninyi tofauti na ilivyokuwa ktk matokeo ya ubunge "ally mle wa cdm" ambaye alipata kura nyingi tu kumshinda gambaz kwa misingi hiyo hiyo.

Labda tu mi niseme kitu kimoja, misingi ya ubaguzi haipo ktk cdm isipokuwa ipo miongoni mwa wapiga kura kama wewe na jamaa zako ktk manispaa hiyo ambayo mwisho wake iliwagharimu kwa kumkosa muwakilishi mliyemtaka kwani mlisababisha hata wale wenye mapenzi ya dhati na cdm kukisariti ktk kipindi hicho cha uchaguzi kwa mitazamo yenu ya kibaguzi.

Nikushauri tu kabla hujafungua kinywa chako ambacho sina uhakika na usafi wake kwa kuwasema vibaya chadema juu ya zitto hebu zitazame kasoro mlizonazo ninyi wakazi wa manispaa ya ujiji kwa ubaguzi wa maeneo "kiongozi yeyote lazima atoke ujiji", ukabila wa vijikabila vidogo vidogo dhidi ya waha ambao hapo manispaa ni mnawaita ni watu wa kuja "hawastahili kuongoza" na itikadi za kidini mlizonazo na kisha uiangazie taasisi hiyo ya kisiasa unayoisema.

utakumbuka kwa kuendekeza mambo yenu hayo ya kifedhuli,ubaguzi na dharau mlimsababishia dr. aman warid kubwagwa vibaya na serukamba na mwisho wake amekuwa akitafsiriwa kuwa ni msomi na siasa za kuganga njaa na hivyo kupoteza mvuto kabisa ktk medani za siasa nchini.

Wanajamvi, huyu jamaa kakurupuka na ama hangover za gongo au mihadarati kutoka lumumba kwa kupost pumba anazoziwazia yeye kwa ufinyu wake wa mawazo aliyonayo akifikiri na wengine ni wanamna yake.

Niijuavyo kg si hivyo unavyoipambanua kuwa cdm imesambaritika, sio wenyeji mkoani humo lkn siasa za kasulu,kibondo,kigoma vijijini,kakonko na buhigwe tunazifahamu sana si za misingi mliyonayo hapo manispaa kwa waswahili juha kila kukicha majungu,fitina na ubaguzi na mwisho wa siku mnayakosa yale yote mnayoyataka.
acha kupost upuuzi!!!!
#juha .

acha kupandikiza chuki zisizokuwa na tija na ikumbukwe kuwa siasa sio fitina ni ushindani wa hoja na kwa taarifa yako cdm hapo mjini Ipo sana tu kinyume na jinsi unavyotaka kuuaminisha umma.
 
Kutokana na mvutano unaoendelea ndani ya Chama cha demokrasia na maendeleo na Chadema imesababisha Chama hicho kusambaratika na kupoteza mvuto mkoani kigoma, sababu hasa inaonekana ni kutengwa kwa kijana wao zitto kabwe ndani ya chama hicho, na hata tetesi zinazoongelewa katika vijiwe vya siasa mkoani kigoma, aliye kuwa mgombea wa chama cha chadema Mwaka 2010 Ally mlee akakihama Chama muda wowote kuanzia sasa. Hali ni mbaya mkoani hapa, kila kijiwe kinaongelea ubaguzi ndani ya chama hicho.
Ukweli kuondoka baadhi ya wanachama kwa sababu binafsi kama hizo ni afya kwa chama!! UBAGUZI UBAGUZI UBAGUZI ukweli wote wenye matakwa binafsi wanatakiwa waondoke!! ni hasara si faida! wale wote wanaozikubali sera na ujinga wa CCM waondoke wakaangalie kwa nje! labda wataona tofauti!!
 
Ni propaganda tu, na mnalipwa kwa kazi hiyo. Mimi niko Kigoma, nakaa Mwanga mtaa wa Shaurimoyo.

Mimi akili yangu ni nzuri sana, hainunuliwi kwa propaganda nyepesi kama hizi.

Nathibitisha kuwa hayo yanayosemwa ni uongo mtupu! Anahitaji alete ushahidi hapa nami ntaleta ushahidi dhidi ya ushahidi wake.

tuambie kabila lako kwanza. kukaa mwanga sio sababu.
 
Kutokana na mvutano unaoendelea ndani ya Chama cha demokrasia na maendeleo na Chadema imesababisha Chama hicho kusambaratika na kupoteza mvuto mkoani kigoma, sababu hasa inaonekana ni kutengwa kwa kijana wao zitto kabwe ndani ya chama hicho, na hata tetesi zinazoongelewa katika vijiwe vya siasa mkoani kigoma, aliye kuwa mgombea wa chama cha chadema Mwaka 2010 Ally mlee akakihama Chama muda wowote kuanzia sasa. Hali ni mbaya mkoani hapa, kila kijiwe kinaongelea ubaguzi ndani ya chama hicho.

Unaishi sehemu gani ya Kigoma we kilaza. Hacha uchawi wa mchana ni vijiwe gani hivyo umeenda? Labda kama ni vijiwe vya CCM
 
Duu kweli Chadema moto chini hadi hamtulii. Lakini pia ni kama maisha ya ndoa wapo wanaoingia na wapo wanaotoka. Hivyo maisha yanaendelea.
 
Back
Top Bottom