Kigoma ninayoijua mimi, ni Kigoma ambayo CCM ndicho chama kisichopendwa.
Sababu za Kutopendwa CCM Kigoma
Kuthamini Wenye fedha.
Hili lilijitokeza tangu mwanzo kabisa wa siasa za vyama vingi. Wakati huo Kigoma kulikuwa na watu wanaopendwa, waungwana na walio na karama za uongozi. Mfano ni Amaan Walid Kabourou na Rajab Kakolwa Mbano, ambaye kaka yake Marehemu Rajab Omar Mbano aliwahi kuwa mbunge kabla ya vyama vingi. CCM kwa kuthamini wenye fedha iliwaweka kando hawa na kumteua Azim Suleiman Premji kuwa mgombea wa CCM Kigoma mjini. Huyu hakuwa na mvuto kwa watu zaidi ya kuwa alikuwa tajiri. Alikuwa anamiliki Gereji ya Magari (Kigoma Auto Garage) na alikuwa anaendesha kwa kukodi Hotel ya kitalii iliyokuwa inamilikiwa na Railways (Kigoma Railways Hotel - Kwa sasa Lake Tanganyika Beach Hotel). Yaani alikuwa na uwezo wa kununua maamuzi ya vigogo wa CCM. Matokeo yake ni kuwa watu wa Kigoma wakasema EKAYEEE! (=NO). Wakamwambia Kabourou ajiunge na CHADEMA na wakamchagua Kabourou miongoni mbunge wa kwanza wa CHADEMA, na kati ya wabunge wachache sana wa upinzani 1995. Premji baadaye alikuwa Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Kigoma.
Kama hiyo haitoshi akajitokeza tajiri mwingine Kigoma. Huyu ni mmiliki wa Kigoma Hilltop Hotel, na Sheni's Commercial Ltd inayojishugulisha na uwindaji wa kitalii (tembo wetu). Huyu habari zake zimeandikwa sana mitandaoni na kwinginepo.
Muhsin Abdullah (Shen) Ameinunua This Country?
MOHSIN SHENI ABDALLAH AT IT AGAIN ; Where Have All the Elephants Gone?
Huyu Kada anaitwa Mohsin Abdallah, kuna yeyote mwana JF atupe Background yake ?
Mjue Kada wa CCM Mohsin Abdallah
Tanzania/Kenya - Where Have All the Elephants Gone? - Foreign Correspondent - ABC
Huyu pia alitaka kuingia kwenye siasa. Japo alikuwa hakubaliki kwa wanachama alikingiwa kifua na makao makuu, na kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa. Huyu Kada yumo katika list ya matajiri wahusika wa madawa ya kulevya. Kwa sasa amemaliza muda wake wa ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa. Analalamika kuwa yeye na Premji wamebaguliwa kwa rangi yao.
Kuna kada mwingine wa CCM wilayani kibondo kwa jina la Jamal Tamim. Huyu anatoka kijiji cha Mabamba wilayani Kibondo katika jimbo la uchaguzi la Muhambwe. Pale Mabamba shughuli anazofanya Jamal hazijulikani, lakini Jamal ni tajiri kupindukia. Mwaka 2007 walipafanya kura za maoni za kufichua wanaofanya biashara za viungo vya albino, Jamal aliongoza kwa kutajwa na wengi wilaya ya Kibondo. Licha ya hayo, Jamal anatuhumiwa kuwa na kikundi cha ujambazi ambacho pamoja na mambo mengine, huteka mabasi, na kufanya matukio mengine ya wizi wa kutumia nguvu. Pamoja na shutuma zote hizi kuwa wazi, CCM ilimpitisha Jamal kuwa mgombea ubunge kiti cha Muhambwe. Pingamizi la kwanza lilitoka mkoani Kigoma kwenye kamati ya Maadili ya CCM. Simbakalia na Kastico walionyesha wazi kuwa huyu Jamal hauziki, lakini kwa influence ya Rostam Aziz na JK, alipitishwa. Kastico (Katibu wa CCM Mkoa wakati huo) aliondolewa Kigoma Oktoba 2010 wakati wa kampeni kwa sababu aliweka pingamizi, na aliondolewa na JK mwenyewe alipofanya ziara ya dharura Kigoma Oktoba 2010.
Matokeo yake wana CCM wengi Kigoma walivunjika nguvu hata kupiga debe kwa wagombea wao. Uchaguzi uliopita, CCM ilishinda kiti cha Kigoma Mjini (kwa kuchakachua), Manyovu na Buyungu. Kati ya viti hivyo vyote Buyungu tu ndio wanaweza kusema kuwa waliwekewa mgombea wanayemtaka (Waziri Christopher Chiza) - ambaye hata mimi namkubali. Ni viti vitatu kati ya vinane. Ni mkoa wa bara ambao asilimia ya wawakilishi (wabunge) wa CCM ni ndogo kuliko popote Tanzania.
mkigoma,
Shelui,
Simiyu yetu,
CHAMVIGA,
utaifakwanza,
Lizaboni,
SONGEA ONE, njoni na hoja zinazoonesha mnaijua vizuri Kigoma na siasa zake.
Sisi watu wa Kigoma tuna mpango wa kuendelea kuikataa CCM na hatujali anayeingiea ni CHADEMA, CUF au NCCR, sisi hatuitaki CCM.
Muha akishasema NTIBHISHOBHOKA, harudi nyuma. Nyie endeleeni kupiga propaganda.