Mlalahoi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2006
- 2,182
- 883
Mwenyekiti wa Chama cha DP,Mchungaji Christopher Mtikila amesema CHADEMA hakipaswi kuaminiwa na Watanzania kwa kuwa ni chama chenye mafisadi na Wafanyabiashara haramu.
Pia amefananisha maneno yanayotolewa na Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa kuwa ni sawa na yaliyokuwa yakitolewa na mmoja wa viongozi nchini Uganda.
Mtikila aliyasema hayo jana wakati akiongea na Wandishi wa habari Ukumbi wa Traventine, Mtikila aliongeza kuwa "ni unafiki kwa Viongozi wa CHADEMA kujifanya ni wapambanaji wa Ufisadi kwa kuwa chama chao chenyewe kimejaa ufisadi wa kutisha, ninakwenda kufungua kesi Mahakama Kuu dhidi ya kuwaonyesha ni jinsi gani walivyo hatari, kesi ninayo kwenda kufungua ina husiana na utata wa kifo cha Mwanasiasa Chacha Wange nina ushahidi juu ya baadhi ya viongozi wa juu wa Chadema kuhusika na mauaji hayo"alisema Mtikila.
Aidha alisema kesi hiyo itahusisha na baadhi ya Viongozi wa Chadema kujishughulisha na biashara haramu na jambo hilo ni Ufisadi. Kutokana na hali hiyo Mtikila aliwataka wananchi kutafakari kuhusu utajiri wa kupindukia wa Viongozi wawili wa chama hicho Philemon Ndesamburo na Freeman Mbowe.
Mtikila alihoji na kubeza hatua ya CCM kujivua gamba akisema CCM ina mafisadi wengi na sio hao watatu tu. Kama kweli CCM wanataka kupambana na Ufisadi wawatimuwe mafisadi wote ambao orodha yao ni ndefu!
Mbona una-cherry pick habari?Katika mkutano huo Mtikila alitumia sehemu kubwa kuelezea namna Rais Kikwete alivyotumia vibaya nafasi yake kumwezesha mwanaye Ridhiwani kuwa bilionea wa kutupa.
Ila kwa vile una makengeza ya ubongo,umesikia habari za Chadema tu!