Mkuu nadhani kukikosoa chama ni swala tofauti na kukejeri maamuzi ya chama. Sasa kwa mfano unapotoa hukumu ya kwamba Mbowe ni dikteta tayari umeshatoa hukumu ambayo sidhani hilo neno linatoa mwanya mzuri wa kujadili. Halafu nadhani tatizo mnalo nyie zaidi kwa sababu mnayapata majibu hapa hapa bila kuwasubiri wazee wa chama kama inavyotokea kwa CCM maanake hakuna kiongozi wala mwanaCCM JF mwenye habari za uhakika.
Haya unataka kuona CV ya Mbowe na viongozi wa CDM kwa nini? je hujui kwamba CV ya mtu haimfanyi kuwa kiongozi bora? Uongozi wa nchi hauna CV yaani hawatengenezwi bali kiongozi bora huzaliwa. Haya yalimkuta Prime minister wa Canada Paul Martin ambaye alikuwa waziri mzuri sana wa fedha, CV kubwa na pengine Canada haijawahi kupata mtendaji kazi kama yeye lakini siku alochukua Uongozi alichemsha, hivyo hivyo Gordon Brown wa UK kashindwa pamoja na kuwa na CV kubwa.
Mimi naweza kusema Mbowe is a better Politician (Leader) kuliko viongozi wengi sana na hakika CDM imeweza kufikia mafanikio haya ilokuwa nayo kwa sababu kasimama yeye. Tungeweza tu kumhukumu vibaya kama CDM ingeshuka daraja na binafsi nina kashalka makubwa kama CDM ingekuwa hapa ikiwa Zitto angechukua Uenyekiti...Kisha zaidi ya hapo kwa kitendo cha Mbowe kumwachia Dr.Slaa agombee Urais mwaka 2010 sijui kuna mwanasiasa gani Tanzania ktk nafasi ya Mbowe angekuwali kuachia hilo..Na zaidi ya yote kuna fahari gani kubwa kuwa mwenyekiti wa chama badala ya kuwa rais wa nchi..
Yes Mbowe anaweza kuwa na matatizo na pengine hata mimi kuna maswala hua tunapingana lakini mara zote hufikia maelewano tofauti kabisa na jinsi watu wanavyomzungumza hapa. Na nimeshawahi kukutana na watu tofauti lakini maturity ya Mbowe ktk siasa hakika imenishangaza hata mimi ambaye tumekuwa sote ktk ujana (ingawa mimi mkubwa kwake) na kama ujuavyo sii rahisi mtu kumpitisha mtu kisiasa ambaye mmekuwa pamoja na unayajua madudu ya ujana wenu.
Lakini nakwambia tu kwamba CDM inamhitaji mtu kama Mbowe kulingana na siasa za Tanzania na hakika kama ni dikteta basi huo Udikteta wake ndio unatakiwa ktk mazingira yetu maadam mafanikio yanapatikana hilo ndio muhimu zaidi..
Nami nitakujibu pia kwa kufuata mtiririko wako mwenyewe.Naomba nizungumzie sehemu nilizored:-
1. Hiyo umeiona ni hukumu? Ni mangapi yamesemwa na viongozi wa Chadema majukwaani juu ya ufisadi, kwa kuwataja watu kwa majina; sio hukumu ni ktazamo wangu kama ulivyo mtazamo wa hao wanaosimama majukwaani na kuwahukumu wengine kwa ufisadi.
2. Sipingani na wewe hata kwa chembe juu ya hili, ila najaribu kuonyesha ni kwa jinsi gani JF ilivyo bias kwa maswala yaihusuyo Chadema, kama hatukubali kukosolewa hatutajenga chama. Chadem, Chadema ni chama prospective kuchukua nchi, changamoto ni lazima ikutane nazo na ijue jinsi ya kuzitatua. Tumeona CV za wengi hapa na nilikuwa najaribu kukumbushia kuwa na zetu tuziweke hapa.
3. Mbowe ana akili kiasi, baada ya kugombea 2010 na kushindwa kwa kishindo alielewa, he is not popular na ndio maana anamwogopa hata Zitto hasa linapokuja swala la watu kupiga kura.
NB: JF tuwe watu wa hoja na tusiwe bias ili tuweze kujenga chama na tuifute dhana ya JF sio ya Chadema.
Atofautishe UFISADI wa RA, EL na utajiri wa Freeman Mbowe ambaye alirithi kwa baba yake mzee Aikaeli Mbowe . Ndesamburo ni mfanya biashara ambaye ame struggle mda mrefu sana na ndio maana ana ujasiri wa kuonyesha vitega uchumi vyake waziwazi. Hoteli za keys zinajulikana siku nyingi na siyo hela ya serikali aliiba. freeman na Ndesamburo hawajawahi kuwa waajiriwa wa Serikali wala taasisi zake ni watu wlioibuka kwa kujishughulisha . RA na EL wao wameibuka kwa kupitia nafasi zao na uhusiano wao wa karibu na viongozi wa serikali hasa kwa kupewa tenda zenye inflated prices ambazo zimewapatia mamilioni ya fedha haramu za watanzania. wameinyonya nchi na wananchi na kuipunguzia nchi kipato na hivyo kuongeza umaskini wa mtanzania wa kijijini.Hawa ndio MAFISADI wenye sifa zoote za kifisadi
Ahahaha!! leo ndio nimejua kumbe Pro-Chadema-JF wengi ni pumba, huyo Mtikila mmemsifia sana tena mmechukuwa maneno yake kama Reference kawambia Ridhiwan Kikwete Tajiri mkubwa tena mmechangia hiyo thread kwa kasi ya ajabu, saizi anawafahamisha ubaya wa Chadema mnakataa, Hongera Mtikila kwa kutujuza ukweli sisi wengine tulikuwa atujui
ahahaha!! Leo ndio nimejua kumbe pro-chadema-jf wengi ni pumba, huyo mtikila mmemsifia sana tena mmechukuwa maneno yake kama reference kawambia ridhiwan kikwete tajiri mkubwa tena mmechangia hiyo thread kwa kasi ya ajabu, saizi anawafahamisha ubaya wa chadema mnakataa, hongera mtikila kwa kutujuza ukweli sisi wengine tulikuwa atujui