CHADEMA yakubali yaishe! yamtambua Rais, yampongeza Rais

Watch TBC Live toka Bungeni!
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amekubali yaishe, wanamtambua JK kama Rais, Wanampongeza!
Mbowe ameomba reconciliation for the sake of Umoja wa Kitaifa.

Big Up kwa Freeman Mbowe, sio siri mimi binafsi nilikuwa simuheshimu sana Mbowe nikimuona kama spoon fed leader.
Kuanzia sasa ni heshima mbele! Huo ndio uanamume, kukubali kushindwa na kukubali yaishe!

Mbowe amewashukuru wapiga kura kwa kura walizoipigia Chadema!.

Hiki Mbowe alichokifanya Bungeni, ndicho Dr. Slaa alichotakiwa kukifanya ile siku ya kutangazwa matokeo!

Nilisema that was a golden missed opportunity. Sasa Mbowe amerekebisha makosa ya Dr. Slaa. Chadema sasa inarudi juu!

Kuna posti niliwahi kuiposti kuwa Chadema hawajajipanga, nilishambuliwa piga ua. Sasa nasema Chadema imeanza kujipanga. Big up!.

Kwanza mlibanaaa... mwisho mmeachia... I'm glad I was damm right!

Chadema sasa tusonge mbele, hata mimi nikirudi uraiani, naweza kufikiria kujiunga Chadema, kuimarisha nguvu!

Asante sana Freeman Mbowe!.

Update 1: Angalizo!.
Kuna kitu kinaitwa expressly na impliedly!
Expressly ni kwa Mbowe kutangaza kwamba sasa Chadema inamtambua Rais!
Impliedly ni pale Mbowe alipompongeza rais, akamsifu, akamshukuru na bla bla bla nyingi za kusifu na kutukuza na kuonyesha spirit ya reconciliation.

mkubali msikubali, Chadema imemtambua Rais JK impliedly na wamekubali yaishe zaidi ya hapo ni ubishi tuu, vinginevyo Mbowe afanya Press Conference afafanue na kukazia kutomtambua JK!

Pasco.

attachment.php

Haha... mkuu umeanza kuipre-empty heading ya kesho ya Uhuru, Mtanzania , Habarileo na Dily News!!
 
Habari kama hizi za uongo tunaanza kuzizoe na kuzilea hapa JF jana ilikuja habari ya uongo wenye makusudi inayosema HR na Kafulila wameshindwa kwenye kura za kugombea uenyekiti wa kamati za bunge ilhali hawakugomebea hata ukileta habari sahihi bado watu hawaamini wanaamini ile iliyobeba kichwa cha habari. Tunakoelekea siko ila nadhani hii itafutwa kwasbabu ina maslahi na wengi!
 
Halafu Pasco, pamoja na umahiri wake kwenye mabandiko mengineyo anazidi kuiedit original thread kule juu, na kuiwekea na picha ili kushawishi watu kuwa alichoongea kinaendana....Nadhani si mantiki nzuri hii, maana after-all watu washakuquote original post yako, so ni kama vile unafanya utoto!
Pasco jitokeze tu uwaambie wanajamvi kuwa umeghafilika...hatuna adhabu yoyote tutakayokupa..
Uungwana ni pamoja na kutambua na kukiri makosa yako.

Vinginevyo labda nikupe siri kuwa unaheshimika sana majamvini hapa Mkuu, hivyo jambo hili dogo lisikurudishe MISRI!
 
Kitendo cha kutoa pongezi na kumtaja rais tayari kinathibithisha kuwa unatambua cheo chake na ndiyo maana ukampongeza, kwa mantiki hiyo ni kwamba CHADEMA wameonesha kumtambua rais ingawa hawakutumia neno "kumtambua"....
 
Hichi ndo PASCO alichokusudia. :)

Kitendo cha kutoa pongezi na kumtaja rais tayari kinathibithisha kuwa unatambua cheo chake na ndiyo maana ukampongeza, kwa mantiki hiyo ni kwamba CHADEMA wameonesha kumtambua rais ingawa hawakutumia neno "kumtambua"....
 
Pasco nina wasiwasi na akili zako. Kwa msimamo wako huo ina maana unaridhika kabisa na uongozi wa JK jinsi unavyoendesha nchi au?? Mwenzio Mbowe kashagundua kuwa nchi ilivyochoka kwa sasa ni heri umuachie Mkwere ahangaike peke yake, sawa na mtu anayeng'ang'ania kubeba gunia la Mavi... Muachie JK peke yake alibebe
 
Kama maneno yaliyo andikwa na huyu comrade ni, namnukuu, "chadema sasa tusonge mbele na mimi nikirudi uraiani, mwisho wa kunukuu". Hivi hii lugha ya uraiani inatumiwa na watu waliopitia au wenye taaluma gani hasa? halfa tafakari alichoandika. Katika kuchangia bunge, kila akiongea mb wa cdm lazima afuatiwe na wa ccm ambaye atakuwa ananeutralize kilichongongwewa na wa cdm, cuf wao wakiongea wataongozana wao. Kwa jinsi alivyoongea Mbowe leo lazima kuna kilichoendelea huko nyuma ya pazia. Sinahakika kama nchi hii wananchi watafikia kile wanachotaka kwa manufaa yao kirahi kazi bado ni mbichi sana.

Sasa hili la kumkubali rais linatatizo gani? wakati alishakubaliwa na sheria hata kabla ya uchaguzi mwenye tatizo labda ni yule anayejua kilicho ujaza moyo wake na nafsi inamsuta. Bahati mbaya hiyo haina dawa atasutwa mpaka atakapo ingia kaburini atleast kila atakapo kuwa anakumbuka (alichofanya) walichofanya .

Kubwa alilotuonyesha ni hata yeye huko aliko ambako siu uraiani hapendi haya yanayo endelea lakini analazimika.
 
Mode: Samahani nilihamanika nikakosea.
Naomba nirekebishie heading ya thread hii isomeke
ile news alert iondoke ibaki breaking news!. Chadema yakubali yaishe, Wanamtambua JK!, Wampongeza!.

Pasco kwa nilivyuomsikiliza Mbowe, nilitarajia uripoti habari hii kama tafsiri yako,kwa alichokiongea Mbowe, na sio kuitoa kama taarifa ya moja kwa moja. Mtu kama wewe kutoa taarifa ambayo inaweza kupotosha ukweli kama hii,ina athari kubwa sana kwa sababu zifuatazo;
- Kwenye JF Unatumia jina linalotambulika katika jamii
- Kama mwandishi wa habari,watu wanaheshimu taaluma yako
- Sehemu fulani ya heshima unayopata kutoka kwa watu mbalimbali, inatokana na uaminifu katika kazi yako (Pengine hata sehemu fulani ya kipato chako)

Wewe ulikuwa mojawapo ya wanaJF humu ambao nikiona post yao, hata niwe na haraka kiasi gani, nililazimika kuifungua, nikasoma nikitegemea kupata taarifa au uchambuzi fulani makini. Mwingine katika hilo kundi ni pamoja na Mwanakijiji, Maxence n.k.
Kutokana na taarifa yako hii, Nahisi kuwa nitajiuliza mara mbili kama utastahili kubaki katika hilo kundi...
 
Kabla sijamjua Pasco niliheshimu sana mabandiko yake.
Nakumbuka wakati wa uchaguzi mdogo wa Biharamulo na Busanda aliandika sana kwa uungwana.
Nimefikia hatua sasa nikiona bandiko lake, nasubiri nimalize kazi zangu ndipo nione kama nina muda.

Pole sana Pasco, umeambukizwa Malaria sugu na Haluu hazipo madukani.
 
Peoples power .........mtoa taarifa ameitoa utanzani ni mtangazaji wa TBC aka wazee wa kuchakachua habari sikiliza kitu kwa umakini na usifanye upotoshaji hapa....
 
ama kwel Pasco ana moyo mgumu! Ushaur wote bdo tu hajitokezi na kusema Samahan wana Jf nlipitiwa kdogo nikaupotosha umma kwa makusudi .
 
Pasco kama Pinda
Kifupi ni9 kwamba CHADEMA walisema hawan atatizo na Raisi wana tatizo na mfumo uliomuweka JK madarakani so chadema wanamtambua raisi na wakisema hawamtambui wana kesi ya kujibu na ndio maana mpaka leo wana dunda uraiani.
 
Back
Top Bottom