Chadema Yakubali Yaishe! Yamtambua Rais!, Yampongeza Rais!. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema Yakubali Yaishe! Yamtambua Rais!, Yampongeza Rais!.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Feb 11, 2011.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,546
  Likes Received: 18,196
  Trophy Points: 280
  Watch TBC Live toka Bungeni!
  Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amekubali yaishe, wanamtambua JK kama Rais, Wanampongeza!
  Mbowe ameomba reconciliation for the sake of Umoja wa Kitaifa.

  Big Up kwa Freeman Mbowe, sio siri mimi binafsi nilikuwa simuheshimu sana Mbowe nikimuona kama spoon fed leader.
  Kuanzia sasa ni heshima mbele! Huo ndio uanamume, kukubali kushindwa na kukubali yaishe!

  Mbowe amewashukuru wapiga kura kwa kura walizoipigia Chadema!.

  Hiki Mbowe alichokifanya Bungeni, ndicho Dr. Slaa alichotakiwa kukifanya ile siku ya kutangazwa matokeo!

  Nilisema that was a golden missed opportunity. Sasa Mbowe amerekebisha makosa ya Dr. Slaa. Chadema sasa inarudi juu!

  Kuna posti niliwahi kuiposti kuwa Chadema hawajajipanga, nilishambuliwa piga ua. Sasa nasema Chadema imeanza kujipanga. Big up!.

  Kwanza mlibanaaa... mwisho mmeachia... I'm glad I was damm right!

  Chadema sasa tusonge mbele, hata mimi nikirudi uraiani, naweza kufikiria kujiunga Chadema, kuimarisha nguvu!

  Asante sana Freeman Mbowe!.
  Jee Mbowe Amemtambuaje JK?.
  Ile kumtaja tuu rais JK bungeni na kumshukuru kuanzisha mchakato wa katiba mpya, ni kumtambua tosha.

  Kuna kitu kinaitwa expressly na impliedly!
  Expressly ni kwa Mbowe kutangaza kwamba sasa Chadema inamtambua Rais!
  Impliedly ni pale Mbowe alipompongeza rais, akamsifu, akamshukuru na bla bla bla nyingi za kusifu na kutukuza na kuonyesha spirit ya reconciliation.

  mkubali msikubali, Chadema imemtambua Rais JK impliedly na wamekubali yaishe zaidi ya hapo ni ubishi tuu, vinginevyo Mbowe afanya Press Conference afafanue na kukazia kutomtambua JK!

  Tume ya Uchaguzi Ikiishamtangaza Fulani Ndio Ameshinda Urais, Huyo Ndiye Rais, Umtambue au Usimtambue, It Doesn't Matter at all!.

  Rais wa JMT ni kitu kinachoitwa being, yaani uwepo wake, ni kitu ambacho kipo na kina exist, huwezi kusema hukitambui, ni kama lilivyo Jua, jua lipo, ulipende, usilipende, lakini lipo, ulitake au usilitake, lenyewe lipo, ukitoka tuu nje juani, litakuchoma, namna pakee ya kuliepuka jua ni 6ft under!.

  Hivyo rais wa JMT ni mtu ambaye yupo, uwe ulimchagua au hukumchagua, ndiye rais wako. Uwe unampanda au humpendi, ni rais wako, uwe unamtambua, au humtambui, yeye bado yupo tuu, ni rais wako, ndiye rais wa Mbowe, ndiye rais wa Dr. Slaa, ndiye rais wa Lipumba, ndiye rais wa Watanzania wote, umtambue usimtambue hakuna tofauti!.

  Unaweza usimkubali, au usimpende, that is optional, ila kumtambua ni lazima tuu umtambue hata kama unatoa kauli kuwa humtambui!.


  Paskali.

  [​IMG]
   
 2. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,372
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Pasco nafatilia asante
   
 3. S

  SUWI JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mh.. more news pls
   
 4. Josephine

  Josephine Verified User

  #4
  Feb 11, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 787
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Pasco,
  Naomba uelewe since he is a President by Law what do you expect? However what is really inour heart has been expressed.

  No matter what we can not change it Today.
   
 5. L

  LAT JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0

  Mbowe amemshukuru Rais kwa kutumia busara na kukubali katiba mpya kwa kutumia sera liyokuwa kwenye ilani ya uchaguzi ya chadema ... na kuiomba serikali kutokusita kuomba ushauri kwa CDM kwani sera za CHADEMA hazina intellectual property right
   
 6. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  huyu shekifu naona anazungumza pumba-kuwa mkuu wa mkoa wa manyara hakukusaidii kujua undani wa mambo yaliotokea arusha-asubir tar-14 ndo azungumze haya
   
 7. W

  WildCard JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Siasa ni hasa. Wamkubali na Meya wa Arusha.
   
 8. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #8
  Feb 11, 2011
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  <br />
  Muongo mkubwa,alichosema Mbowe ni kuwa anampongeza Rais kwa kukubali kuanza mchakato wa katiba mpya japokuwa haikuwa katika ilani ya CCM.Mh.Mbowe amewataka serikali kuitumia ilani ya Chadema na wabunge wa CCM na wa vyama vingine wasiwe na hofu na wabunge wa CHADEMA na wawaelewe na kushirikiana nao.
   
 9. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #9
  Feb 11, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  Nadhani taarifa yako si sahihi, alichompongeza JK ni kukubali suala la katiba mpya, na amesema wazi kabisa kuwa suala la katiba halikuwa kwenye ilani ya ccm wala kwenye hotuba ya rais lakni kutokana na preasure amekubali. Huo ni uungwana kwani katiba ndiyo itakayoleta mustakabali wa nchi. Nina imani mpaka kesho Mh Mbowe akiulizwa kama JK ni rais halali atasema hapana, isipokuwa ni rais kwa mujibu wa katiba na sheria tunazozilalamikia.
   
 10. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #10
  Feb 11, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Sasa ile kutoka bungeni siku ya kwanza ilikuwa ni nini?

  Kweli chama hichi kiko consistent!
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #11
  Feb 11, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,546
  Likes Received: 18,196
  Trophy Points: 280
  Mode: Samahani nilihamanika nikakosea.
  Naomba nirekebishie heading ya thread hii isomeke
  ile news alert iondoke ibaki breaking news!. Chadema yakubali yaishe, Wanamtambua JK!, Wampongeza!.
   
 12. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #12
  Feb 11, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hakuna kitu kama hicho..
  Pasco karudie kusikiliza..
  Amesema anamshukuru Rais kwa kuwa msikivu, na kwamba amechukua hoja ya Chadema ya Katiba na kuiweka hadharani.
  Lakini hakumaanisha kuwa ni rais aliyeshinda kwa kishindo...
  Kuwa makini mkuu, hii ni ishu kubwa sana usii-amplify in a wrong way...
   
 13. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #13
  Feb 11, 2011
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Pasco wewe ni MWONGO umeidanganya Jamii Forums na Great thinkers wote
   
 14. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #14
  Feb 11, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Jamani jitahidini kusikiliza kwa masikio yenu wenyewe...
  CDM hawajasema kuwa kuanzia leo wanamtambua rais...
  Pasco ameghafilika!
   
 15. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #15
  Feb 11, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Asante Mkuu Pasco kwa bandiko hili, wengi takubaliana nami kuwa Mh. Mbowe hajakurupuka katika hili.
  [​IMG]
   

  Attached Files:

 16. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #16
  Feb 11, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  nickname: uko sahii, na ktk swala la katiba naona ujumbe umefika: ilani ya CDM iko juu.
   
 17. L

  LAT JF-Expert Member

  #17
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  kwa walioangalia TBC......unapotosha na kichwa cha habari na content za post yako zinakinzana na hazina ukweli wowote ule kutokana na alichosema Mh. Mbowe
   
 18. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #18
  Feb 11, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Uwongo na jua kali la mchana!
  Acheni hizo bana!
   
 19. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #19
  Feb 11, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Labda useme amefanya kwa makusudi. Mwandishi wa habari akaghafilike kwenye kitu kama hicho?

   
 20. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #20
  Feb 11, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,630
  Likes Received: 1,385
  Trophy Points: 280
  Sasa walichokubali kiishe hapo ni kipi? mbona sababu za kutoka nje ya bunge zilielezewa vizuri na cdm au mlikua mmelala?

  cdm walitoka nje kuonyesha msimamo wao juu ya mamlaka iliyomweka JK madarakani na wala hawakuvunja sheeria yeyote kwani ni haki yao kisheria, hii thread sijajua lengo lake ni nini?
   
Loading...