CHADEMA yakubali yaishe! yamtambua Rais, yampongeza Rais

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amekubali yaishe, wanamtambua Rais, Wanampongeza!
Mbowe ameomba reconciliation for the sake of Umoja wa Kitaifa.

Big Up kwa Freeman Mbowe, sio siri mimi binafsi nilikuwa simuheshimu sana Mbowe nikimuona kama spoon fed leader.
Kuanzia sasa ni heshima mbele! Huo ndio uanamume, kukubali kushindwa na kukubali yaishe!

Kuna kitu kinaitwa expressly na impliedly!
Expressly ni kwa Mbowe kutangaza kwamba sasa Chadema inamtambua Rais!
Impliedly ni pale Mbowe alipompongeza rais, akamsifu, akamshukuru na bla bla bla nyingi za kusifu na kutukuza na kuonyesha spirit ya reconciliation.

mkubali msikubali, Chadema imemtambua Rais impliedly na wamekubali yaishe zaidi ya hapo ni ubishi tuu, vinginevyo Mbowe afanya Press Conference afafanue na kukazia kutomtambua

Tume ya Uchaguzi Ikiishamtangaza Fulani Ndio Ameshinda Urais, Huyo Ndiye Rais, Umtambue au Usimtambue, It Doesn't Matter at all!.

Rais wa JMT ni kitu kinachoitwa being, yaani uwepo wake, ni kitu ambacho kipo na kina exist, huwezi kusema hukitambui, ni kama lilivyo Jua, jua lipo, ulipende, usilipende, lakini lipo, ulitake au usilitake, lenyewe lipo, ukitoka tuu nje juani, litakuchoma, namna pakee ya kuliepuka jua ni 6ft under!.

Hivyo rais wa JMT ni mtu ambaye yupo, uwe ulimchagua au hukumchagua, ndiye rais wako. Uwe unampanda au humpendi, ni rais wako, uwe unamtambua, au humtambui, yeye bado yupo tuu, ni rais wako, ndiye rais wa Mbowe, ndiye rais wa Dr. Slaa, ndiye rais wa Lipumba, ndiye rais wa Watanzania wote, umtambue usimtambue hakuna tofauti!.

Unaweza usimkubali, au usimpende, that is optional, ila kumtambua ni lazima tuu umtambue hata kama unatoa kauli kuwa humtambui!.

Paskali.
Hili jambo liliwahi kutokea nyuma kwa Chadema kutangaza hawatambui matokeo na hawamtambui rais. Keshokutwa tarehe 8 Machi Chadema wanakwenda kutangaza kutambua matokeo, kumtambua rais Samia na kufungua ukurasa mpya!.
Update
Hatimaye Chadema wameacha kushupaza shingo na wamekubali matokeo!, kwa kuufuata ushauri wa bandiko hili CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao

Nimepokea taarifa, hii kutokea twitwani
Kisha nikasoma na bandiko hili humu JF Tundu Lissu: CHADEMA tumeanza kupokea Ruzuku

Chadema wameufuata ushauri wa bandiko hili, waneacha ujinga wa kujifanya hawayatambui matokeo ya uchaguzi wa 2020!, sasa wameacha kushupaza shingo, wameyatambua matokeo kimya kimya!, wamewasamehe mashujaa hawa kimya kimya msamaha ambao utatangazwa rasmi siku ya Jumatano tarehe 8 Machi na Mwenyekiti wa Chadema, mbele ya Rais Samia!.

Iliwa kusemwa kuwa hakuna mkate mgumu wowote mbele ya chai!, tayari Chadema imeisha anza kupokea ruzuku hivyo sasa ita survive!. Na ile kesi ya kina Halima Mdee na wale 19 iliyopo mahakamani itafutwa!.

Hongera sana Chadema, for doing the right thing!, mtabarikiwa, viongozi wenu watabarikiwa, chama chenu kitabarikiwa na Tanzania Itabarikiwa!.
Mungu ibariki Chadema
Mungu ibariki CCM kwa kukubali reconciliation
Mungu ibariki Tanzania
Paskali
 
Back
Top Bottom