Operesheni ya Chadema ni Msingi na vuguvugu la Movement for Change jimboni Ukonga imeonekana kukisimika vyema chama hicho jimboni humo.
Wanachama wa Chadema jimboni Ukonga hawasiti kuupongeza uongozi wa jimbo hilo chini ya Mwenyekiti Thomas Nyahende maarufu kama Mwita Maranya kwa kazi kubwa waliyofanya tangu waingie madarakani.
Jimbo la Ukonga lenye ubovu mkubwa wa barabara limekuwa ngome kuu ya CCM kwa miaka mingi.
Hata hivyo katika uchaguzi uliofanyika wa Serikali za Mitaa wiki iliyopita Chadema wamejipatia ushindi mkubwa katika mitaa 10 huku washirika wao CUF chini ya mwavuli wa Ukawa wakijipatia mitaa 2.
Kikubwa zaidi ni kwa chama hicho kuweza kujipatia mitaa miwili muhimu.Mitaa hiyo ni ule anaokaa Meya wa Ilala Jerry Silaa wa Guluka Kwalala Gongolamboto na Mtaa wa Kivule unaoaminika kuwa na wakazi wengi zaidi kuliko mtaa wowote DSM.Kwa mfano katika mtaa huo wa Kivule mshindi alikuwa ni Afisa wa Chadema makao makuu Kamanda Mwita Mwikabe Waitara aliyepata ushindi wa kimbunga wa kura 1262 huku CCM wakiambulia kura 663
Kabla ya uchaguzi huu upinzani kwa ujumla walikuwa wanaongoza mitaa 2 tu kwa jimbo zima.
Jumapili wiki hii kutakuwa na marudio ya uchaguzi kwa mitaa 23 ambayo haikufanya uchaguzi wiki iliyopita.
Katika mahojiano na wanachama na baadhi ya viongozi wa misingi wamepongeza uongozi bora wa Mwita Maranya unaoshirikisha viongozi wote wa ngazi za chini na uwajibikaji uliotukuka.
Pia wanachama wameutaka uongozi wa Jimbo kutokubweteka kwa matokeo haya mazuri bali waendelee kukijenga chama bila kuchoka ili mwakani waweze kupata mbunge na madiwani wengi kwa lengo la kuongoza Manispaa ili walau wasimamie fedha za wananchi na hatimaye barabara za Ukonga zijengwe.
Haa haa, hongereni, mwita mwikabe amegombea uenyekiti wa mtaa? Ama..
Mkuu kama atagombea Ukonga itakuwa njema maana ataepusha mgongano na Heche kule Tatime! Huo mkakati nimeupenda nchi lazima tuigawane! Kama Kishapu nako hatuna mgombea ni bora Mpendazoe akarudi ili Segerea tuliachie jembe jingine la UKAWA!
kazi nzuri sana hii. hongera mkuu Mwita Maranya! mkuu Molemo kamanda waitara hagombei tarime mwakani? naona ameanza kukita mizizi jimbo la ukonga.
Bila kusahau wale wanaopisha mradi wa gesi mwaka wa tatu huu awajui malipo yao yatakuwaje. Wengine wasitisha ujenzi wa nyumba ili hali bado azijakamilika wakihofia kupat hasara! Makamanda wa ukonga walifatilie hili linaweza likawa janga lengine laupigaji hela...
Ninafarijika mongola ndege wamedelete CCM. ..
Mkuu Mwita Maranya kumbe ukiona kobe ameinama ujue anatunga sheria; umekaa kimya sana kumbe unajiandalia ushindi. Hongera kwa kupata ushindi huko kivule. Sasa yule ndugu yako Diwani wa Kivule una mpango gani naye, unataka kumuondoa?
Sinza ubishoo mwingi.Sinza tatizo nini hongera makamanda wotee ukonga
Let's get rid of this CCM all over our country.
Bora ya wewe umegundua hizi habari za Mleta mada ni kujipiga Chapuo na maPro mengi tu ya CHADEMAMbona huyu mama afisa uhusiano wa manispaa ya ilala ameitaja kivule kuwa uchaguzi unarudiwa?
Mkuu Kimbunga upo?
Nilikusoma mahali ukikiomba CCM kimpitishe John Magufuli kugombea Urais vinginevyo Ukawa watachukua nchi!
Nilicheka sana!!
Mawazo ya kitoto kabisa hayoPopote ulipo Habinder Singh Seth hakikisha unakwamisha maazimio ya Bunge letu TUKUFU ili mziki huu uwe mnene mwaka mzima mpaka uchaguzi MKUU utasaidia sana na watanzania wengi watakuwa wameamka juu ya wizi wa kutisha uliofanywa.JK na wewe kaa kimya ili watu wawe na akili maana uvivu wa kufikiri kwa watanzania ni mkubwa ili wajue kama wameibiwa wanatakiwa hata wakienda hospitali Wafie milangoni maana Dawa hakuna,UMEME upande ikiwezekana watu walipe laki mbili na nusu kwa mwez.maana hili TAIFA ni la Vilaza.kikwete oyeeeeeeee,Harbinder Singh Seth oyeeeeeeeee,maisha magumu kwa kila MTANZANIA safiiiiiiiiiiiiiii.