CHADEMA yaizika CCM Ukonga

CHADEMA yaizika CCM Ukonga

Molemo bado hujanijibu swali langu kamanda,
mi sijapinga kuwepo mapingamizi,je kwa walivyopanga serekali yalipaswa kutolewa maamuzi lini?ili hata mgombea akilishinda pingamizi aweze kwenda kupigiwa kura???

Kamanda Marire kumbuka waliotunga kanuni hizi ni Tamisemi chini ya ofisi ya Waziri Mkuu.Lengo lao kubwa ni kuwatoa Ukawa nje ya uwanja kabla ya kura.

Kwa hiyo kwa kifupi tu elewa haya mapingamizi ni hujuma tu na hakukuwa na uhalali wowite kisheria na ndio maana hata kanuni zake hazikuwekwa wazi.
 
Last edited by a moderator:
Huu ni uhuni uliopitiliza yaani ukawa kwanini tusifungue kesi mahakamani kupiga hii rafu?

Hapo sasa tuko pamoja Kamanda.

Chadema wameshapanga kutumia jopo la wanasheria wake kupigania demokrasia mahakamani.

Kwa mfano tayari Chadema tumefungua kesi kule Shinyanga kwa sababu wagombea zaidi ya 2000 walienguliwa kule Meatu kwa hila za CCM na hivyo wagombea wote wa CCM wakatangazwa washindi.
 
Mbona Jimbo la segerea Chadema wameshinda mitaa mingi lakini siskii chochote?

Ni kweli Kamanda.Pamoja na hila nyingi zilizopangwa lakini Segerea nako CCM imefutwa Rasmi.
 
kama anakubalika ukonga si amwachie HECHE tarime na yeye awakongori magamba hapo dar?
Molemo?

wakati ukifika atapima upepo mkuu. na ujue jimbo la Ukonga litagawika mwaka ujao. ngoja tusubiri muda ukifika tutafanya tathmini kamanda Waitara agombee Dar na Heche agombee Tarime ili tuwakamue vizuri magamba.
 
Last edited by a moderator:
Km ni post za CHADEMA muwe mnasema hili Jukwaa ni lenu maPro na BAVICHA
WW POST za ajabu ajabu tuziache zipite
Dr. Slaa ailipua Ikulu
mara tunaletewa
'MBOWE KUPOKEWA KWA MAANDAMANO DAR'
CHADEMA Yaizika CCM Ukonga


km habari ni ya kutunga pelekeni Buguruni lakini sio matusi maana habari haijakamilika lakini habari inakuja km kweli imekamilika

sasa hapo ndio CCM kazikwa ukonga? Heading zinatisha nyau kwanini nisiziite za kitoto?

UKWAJU..Mkuu unafahamu kwa nini nilimuomba Molemo aache kuhangaika na wewe?.kama una akiri timamu unaweza kuniambia kwa nini Msalani Lizaboni na Lumumba buku 7 wote hawajaingia ktk uzi huu?.ni hivi tunavyo au wanavyozungumza kuwa ushindi wa kishindo Cdm yaizika ccm na mengine kama hayo ni kwamba kutoka kuwa huna mtaa hadi kuwa na mitaa kadhaa na hiyo mitaa umeichukua kutoka mikononi mwa ccm ambacho ni chama dola lazima uweke kila aina ya mbwebwe unapozungumzia huo ushindi.mkuu nakushauri sio kila uzi lazima ujitoe ufahamu.na ikitokea ukachangia changia kwa hoja sio kuleta viroja
 
Marire

Haya mambo yanazungumzika usihofu.Bahati njema Chadema ina hazina ya viongozi wenye hekima kubwa hususan majemadari wakuu Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa.

Mkuu Molemo huyu m/kiti aliyepigwa kimbunga na Kamanda Mwikabe alianza kuchonga hii barabara ya kivule sasa matokeo yalipotoka kasimamisha kuchonga i mean kasusa kumalizia! hebu ongea na Mwikabe afanye mchakato wa kumalizia ....
cc: Mwita Maranya
 
Last edited by a moderator:
Hawa CCM wana mgogoro mkubwa huko Ukonga.Jerry Silaa na Eugene Mwaiposa wanaparurana kila mtu anataka agombee ubunge Ukonga.

Wananchi wanaona wote hawafai na wanapalilia matumbo yao tu kwa sababu wote wameshindwa kuwasaidia wananchi wa Ukonga kuepuka dhahama ya ubovu wa barabara.

Jerry Silaa ambaye ni Meya wa Ilala na mjumbe wa Kamati Kuu CCM kushindwa vibaya kwenye mtaa wake ni rasharasha tu..za masika zinakuja!

Yaani hapo umenena its like a slap on his Face
 
Bora ya wewe umegundua hizi habari za Mleta mada ni kujipiga Chapuo na maPro mengi tu ya CHADEMA
Hivi wameshinda mitaa mingapi mpaka waitane majina ya Kikamanda?
kumbe uchaguzi unarudiwa
kumbe wameshinda mitaa miwili tu?
kweli mahali akikutana Mchagga na Mkurya ni vigumu kutawalika
yetu macho

Ni kwa vile hawatakii upuuzi na ujinga wanajitambuaaaa
 
wakati ukifika atapima upepo mkuu. na ujue jimbo la Ukonga litagawika mwaka ujao. ngoja tusubiri muda ukifika tutafanya tathmini kamanda Waitara agombee Dar na Heche agombee Tarime ili tuwakamue vizuri magamba.

Kamanda tpaul hivi Jimbo la Ukonga linagawanywa?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Molemo huyu m/kiti aliyepigwa kimbunga na Kamanda Mwikabe alianza kuchonga hii barabara ya kivule sasa matokeo yalipotoka kasimamisha kuchonga i mean kasusa kumalizia! hebu ongea na Mwikabe afanye mchakato wa kumalizia ....
cc: Mwita Maranya

Usijali Kamanda Wa Kwilondo.Mambo yote yatakwenda kama yatakavyopangwa.Kamanda Waitara ndiyo ameingia ofisini anapanga mikakati namna ya kuhakikisha mvua ijayo ya masika haitazuia wakazi wa Kivule kusafiri.
 
Last edited by a moderator:
Nilishawahi tuma post humu kuhusu huyu diwani wa chadema sinza Renatus Pamba mwana bongo fleva,kuwa huyu ni kilaza wa kutupwa na siajabu akaurudisha udiwani kwa ccm uchaguzi ujao,huyu napendekeza ashughulikiwe ASAP
 
Operesheni ya Chadema ni Msingi na vuguvugu la Movement for Change jimboni Ukonga imeonekana kukisimika vyema chama hicho jimboni humo.

Wanachama wa Chadema jimboni Ukonga hawasiti kuupongeza uongozi wa jimbo hilo chini ya Mwenyekiti Thomas Nyahende maarufu kama Mwita Maranya kwa kazi kubwa waliyofanya tangu waingie madarakani.

Jimbo la Ukonga lenye ubovu mkubwa wa barabara limekuwa ngome kuu ya CCM kwa miaka mingi.

Hata hivyo katika uchaguzi uliofanyika wa Serikali za Mitaa wiki iliyopita Chadema wamejipatia ushindi mkubwa katika mitaa 10 huku washirika wao CUF chini ya mwavuli wa Ukawa wakijipatia mitaa 2.

Kikubwa zaidi ni kwa chama hicho kuweza kujipatia mitaa miwili muhimu.Mitaa hiyo ni ule anaokaa Meya wa Ilala Jerry Silaa wa Guluka Kwalala Gongolamboto na Mtaa wa Kivule unaoaminika kuwa na wakazi wengi zaidi kuliko mtaa wowote DSM.Kwa mfano katika mtaa huo wa Kivule mshindi alikuwa ni Afisa wa Chadema makao makuu Kamanda Mwita Mwikabe Waitara aliyepata ushindi wa kimbunga wa kura 1262 huku CCM wakiambulia kura 663

Kabla ya uchaguzi huu upinzani kwa ujumla walikuwa wanaongoza mitaa 2 tu kwa jimbo zima.

Jumapili wiki hii kutakuwa na marudio ya uchaguzi kwa mitaa 23 ambayo haikufanya uchaguzi wiki iliyopita.

Katika mahojiano na wanachama na baadhi ya viongozi wa misingi wamepongeza uongozi bora wa Mwita Maranya unaoshirikisha viongozi wote wa ngazi za chini na uwajibikaji uliotukuka.

Pia wanachama wameutaka uongozi wa Jimbo kutokubweteka kwa matokeo haya mazuri bali waendelee kukijenga chama bila kuchoka ili mwakani waweze kupata mbunge na madiwani wengi kwa lengo la kuongoza Manispaa ili walau wasimamie fedha za wananchi na hatimaye barabara za Ukonga zijengwe.

Acha uongo mkuu yani mnajitekenya na kucheka wenyewe ebu tuambie jimbo la ukonga lina mitaa mingapi na nyie Chadema na Ukawa mmepata mitaa mingapi kwa ujumla wenu na utuambie CCM imechukua mitaa ipi ni vizuri ukataja kata zilizopo na mitaa yake kwa jimbo la ukonga fanya hivyo tutakuelewa vinginevyo mnajidanganya kwa kujitekenya na kucheka wenyewe
 
Last edited by a moderator:
Acha uongo mkuu yani mnajitekenya na kucheka wenyewe ebu tuambie jimbo la ukonga lina mitaa mingapi na nyie Chadema na Ukawa mmepata mitaa mingapi kwa ujumla wenu na utuambie CCM imechukua mitaa ipi ni vizuri ukataja kata zilizopo na mitaa yake kwa jimbo la ukonga fanya hivyo tutakuelewa vinginevyo mnajidanganya kwa kujitekenya na kucheka wenyewe

Nakushauri waambie mabwana zako wajenge barabara za Ukonga vinginevyo mtaangukia pua kila uchaguzi hapo Ukonga!
 
Hapo sasa tuko pamoja Kamanda.

Chadema wameshapanga kutumia jopo la wanasheria wake kupigania demokrasia mahakamani.

Kwa mfano tayari Chadema tumefungua kesi kule Shinyanga kwa sababu wagombea zaidi ya 2000 walienguliwa kule Meatu kwa hila za CCM na hivyo wagombea wote wa CCM wakatangazwa washindi.

Mahakama gani? Hii iliyopewa milion 800 na Rugamalila, ama nyingine. Labda UKAWA ianze lampaini nyingie kali ya watumishi kama majaji wa mahakama za wilaya, mikoa ili wawe neutral maana hata hizo za Ruge haziwafikii. Kuna haja ya kazi kubwa kuelemisha watumishi wa umma polisi,jeshi, mahakimu, waalimu nk wasaidie vita hii ya operationn delete CCM
 
TAARIFA YA MAAZIMIO YA CHADEMA KWA
VYOMBO VYA HABARI
LEO.

Baadhi ya maazimio ya CHADEMA kuhusu uchaguzi
serikali za mitaa
kama yalivyosomwa na Dr. Slaa
alipozungumza na
waandishi wa Habari.

¤ Suala la kupita bila kupingwa ni kinyume na
Demokrasia na haki
ya msingi ya raia ya kuchagua, hivyo utamaduni
huu ufe nakama
ikitokea basi zipigwe KURA za NDIO na HAPANA.

¤ Viongozi wa CHADEMA waliochaguliwa ikigokea
wanatuhumiwa
kwa vitendo vya rushwa kamwe chama
hakitawavumilia viongozi
hao na tutawachukulia hatua maramoja bila kusita
ikiwemo za ndani
ya chama na hata kuwashtaki mahakamani.

¤ Kamati kuu imezitaka mamlaka zinazohusika
kuwatambua
mabalozi wa CHADEMA katika masuala yote
ambayo yanahitaji wa
ngazi hiyo, ikiwemo utambulisho wa ukazi.
Wanachama wa
CHADEMA hawalazimiki kwenda kupata idhini ya
mabalozi
wanaotokana na CCM kama ambavyo serikali
inataka.

KUHUSU MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU 2015.

Kamati Kuu ya Chama imepokea kwa masikitiko
taarifa
zinazoonesha kuwa hadi sasa serikali kupitia Tume
ya Taifa ya
Uchaguzi haionekani kujipanga kuweza kufanikisha
uchaguzi mkuu
ujao.

Tayari kasoro nyingi ambazo kama hazitafanyiwa
kazi zitasababisha
vurugu huko tuendako zimeanza kuonekana kwenye
zoezi la
majaribio ya uandikishaji wapiga kura linaloendelea
hadi sasa
Kawe,Kilombero, na Mlele.

Akizungumzia vurugu na vifo na kasoro
zilizojitokeza katika
uchaguzi huo, Dr. Slaa amewalaumu Waziri mkuu
Mh. Pinda na
Waziri wa TAMISEMI Mh. Hawa Ghasia kuwa ndio
chanzo cha
matukio yote katika uchaguzi huo. Hasa kwa
kutunga kwao kanuni
mbovu na miongozo katika sheria ya uchaguzi
Serikali za mitaa
kanuni ambazo zimepelekea mauji katika baadhi ya
maeneo nchoni
hasa kule Nzega kutokea. Hivyo wote hawa
wanapaswa kujiuzulu
wenyewe ama wawajibishwe na Mh. Raisi mara
moja.

Akiyataja maeneo ya Miji midogo ambayo
CHADEMA imeshinda, Dr.
Slaa amesema:

"1. Nkasi - Namanyere
2. Hai - Bomang'ombe.
3.Karatu - Karatu.
4. Arumeru Mashariki - Usa river.
5.Vunjo - Ukawa.
6. Mbeya vijijini - Mbalizi.
7. Mbozi Maghari - Tunduma.
8. Mbozi Mashariki - Mlowo.
9. Kyela - Kyela.
10. Lupa - Makongorosi.
11. Busanda - Katoro.
12. Geita - Geita.
13. Chato - Chato.
14. Kwimba - Ngudu.
15. Karagwe - Kayanga.
16. Bukombe - Ushirombo.
17. Sengerema - Sengerema.
18. Tarime - Tarime.
19. Tarime - Sirari mji mdogo.
20. Rorya - Shirati ( 7/2).
21. Bunda - Bunda.
22. Serengeti - Mugumu 10/10 ( CUF 3).
23. Kahama - Kahama.
24. Bariadi - Bariadi ( 49/43).
25. Kilombero - Ifakara.
26. Magu - Magu.
27. Mbozi - Vwawa.

Sehemu zote hizo CCM ndio chama cha upinzani.
 
Mahakama gani? Hii iliyopewa milion 800 na Rugamalila, ama nyingine. Labda UKAWA ianze lampaini nyingie kali ya watumishi kama majaji wa mahakama za wilaya, mikoa ili wawe neutral maana hata hizo za Ruge haziwafikii. Kuna haja ya kazi kubwa kuelemisha watumishi wa umma polisi,jeshi, mahakimu, waalimu nk wasaidie vita hii ya operationn delete CCM

Umesomeka vizuri sana Kamanda PMM
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom