Chadema yaipa polisi saa 24

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
Chadema imeipa polisi saa 24 kuwakamata watuhumiwa wote wanaotuhumiwa kuwashambulia viongozi wa Chadema kwenye kampeni za uchaguzi Arumeru Mashariki. Katibu wa chama hicho Dr. Slaa amesema kwa kushindwa kuwakamata watuhumiwa, yeye binafisi ataongoza maandamano yatakayowajumuisha maelfu ya wakazi wa Arumeru kwenda Ikulu kushinikiza kujiuzulu kwa maafisa wa ngazi za juu wa polisi.

Dr Slaa amedai kuwa viongozi wa Chadema wamekuwa wakishambuliwa na watu fulani kutoka CCM kwa muda wa siku tatu sasa, lakini pamoja na kuwaripoti watu hao polisi, hakuna hatua zozote ambazo zimechukuliwa. Alisema badala yake viongozi wa CCM ndio wanaodai kwenye vyombo vya habari kushambuliwa na Chadema huku wakitoa statements zao chini ya escort ya polisi.

Akiongea na wananchi wa sehemu ya Mgungani iliyoko kata ya Mbuguni, Dr Slaa amesema, maandamano hayo ambayo hayajawahi kufanyika Tanzania, yatawahusisha wananchi wa Meru na Arusha kwa kuandamana mpaka Ikulu, Dar Es Salaam. Wananchi waliokuwa kwenye mkutano walimjibu Dr Slaa kuwa wako tayari kuandamna hadi Ikulu baada tuu ya kumalizika kwa mkutano.

Dr. Slaa aliongeza kuwa wakati wakiandamana kutokea Meru watawasiliana na Watanzania wengine kutoka kona mbalimbali za nchi ili nao waandamane na kukutana jijini Dar Es Salaam.

Nikiripoti kutoka eneo hili la Migungani lililopo kwenye kata ya Mbuguni ni mimi EMT wa JF.
 
mmmh kama arusha ilikwezekana kukesha ile siku ya lema basi itawezekana kufika ikulu sisi tutawangoja njiani
 
Genuinely speaking.... Slaa anapenda kuandamana jamani. Haya best wishes....
 
Genuinely speaking.... Slaa anapenda kuandamana jamani. Haya best wishes....

AshaDii,
Bora aendelee kupenda kuandamana.
Akitangaza kuingia msituni sijui utasemaje?

Btw, wewe ungepewa nafasi ya kushauri alternative way, ungemshauri afanye nini?
 
hii habari iko kwenye gazeti la nipashe nitofauti kabisa na ulicho ripoti kwenye nipashe dr slaa kasema kama vyombo vya dola pamoja na nec vitaebeba ccm basi yeye dr slaa ataongoza maandamano mpaka ikulu...hayo maa 24 yako wapi
 
Nimesikia baada ua SLAA kutoa kauli hiyo Polisi wananoa zana za kazi.Ila sina hakika kama huyo DR anaweza kutembea kutoka Arumeru hadi Dar kwa mguu.Kila la heri DR.
 
Nani aandamane kutoka wapi!!!labda machizi kutoka mirembe na uwaambie wakifika dar wote wanageuka nyumba!
 
AshaDii,
Bora aendelee kupenda kuandamana.
Akitangaza kuingia msituni sijui utasemaje?

Btw, wewe ungepewa nafasi ya kushauri alternative way, ungemshauri afanye nini?


Dr. Slaa thrives on Vurugu (at least that is my IMO); Kuandamana mimi sioni kua ni tatizo sana... Kwa jinsi Serkali yetu ilivo na ilipofika huwezi pata kitu bila making noise. However Slaa ananiboa pale ambapo likitokea tatizo huweza li-manipulate in whatever way na kuwaambia na kuwashawishi wananchi kuandamana. Unfortunately yeye mradi wameandamana ndio raha yake; lakini hajaweka vigezo vya maandamano kua yawe yanakua vipi.... Kwamba walau hao vijana (maana ndio wengi); wanapo andamana basi kweli wastick kwenye kuandamana (si wamsikiliza sana) na sio katika kuwafanyia fujo fellow wananchi... In other cases watavamia maduka, haribu magari fanya fujo (as if ni genge la majambazi) badala ya kuandamana peacifully.....

Mimi naamini ana connections... na naamini lazima there is a better way of tackling the issue nje ya maandamano.
 
mkuu hebu tuweke wazi juu ya masaa 24...ni kweli kasema hivyo kama ulivyosema kwenye bandiko

Mimi nimesoma kwenye mwanachi.tena polisi wamemuonya kwa kauli hiyo kuwa ni ya kichochezi.. mimi ninachojiuliza hapa EMT hii habari kaipata leo? kwamba slaa karudia maneno hayo hata baada ya kuonywa??. otherwise, hii habari imeshachacha
 
Back
Top Bottom