Unakubaliana nasi kuwa shimbo alifanya siasa.
kwa kuwa tamko lilihusu uchaguzi na vyama vya siasa, mtoa tamko sahihi angekuwa kama si msajili wa vyama vya siasa basi angekuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi.
Ikiwa kwa kitisho cha mpaka na malawi mkuu wa majeshi yetu hatakiwi kusema kitu sembuse kwa kazi isiyomuhusu kabisa!!!
Hawa wajeshi wajiongeze kidogo, wanaposema wanakitii chama kinachounda serikali wamepaswa kujua kuwa utii wao kwa kipande hiki si utii wa kijeshi, kwani waamrishaji si wanajeshi, ama la sivyo hawa wastaafu wa jeshi wanasomeka kuwa ni wanajeshi.
Ndomba alipokuwa Mkuu wa Mkoa alikuwa amestaafu sio? Na Mkuu wa Mkoa ni mjumbe wa kamati ya mkoa ya CCM! Sasa hivi Ndomba ni nani jeshini!? Ndio maana Mboma na Mahita walipostaafu uCDF na uIGP wakaenda kugombea ubunge kupitia CCM, na Tubaigana pia!
I think its a blasphemy kusema jeshi is loyal au linatii chama kinacho ongoza serikali. I dont know about the laws za jeshi ila i think he should have said ´Jeshi linatii na kuheshimu kanuni na sheria za jamuhuri ya muungano bila kujali chama au mtu au taasisi´. Hawa viongozi wetu bana, they need more pressure ili wawezekujitambua.
hadi hapa maadili hakuna hata kidogo, yaliyopo mengine ni uovu uliohalalishwa.Ni rehema za Mungu tuu zinzoshikiliwa na wachache walio ktk wema na wasio hat ajua nini kinaendelea.Ipo siku nchi itakuja kupinduliwa,kama mmomonyoko wa maadili utaendelea kukuwa kwa kiasi hiki!
NI Kweli kuwa jeshi haliji halijihusishi na siasa lakini tunaona wengi wakistaafu utumishi hupewa nafasi za mkuu wa mkoa ,mkuu wa wilaya hawa ni wanasiasa kwa upande mwingine ,kwa sababu kama huna hata idea kidogo ya siasa hizi posti wengi wangezikataa na wengi wao hukubali bila shingo upande .
Ninaamini hawatakusikiliza haya mpaka yatakapowatokea kama yale ya Misri walipogoma kusikiliza amri zao. Kiburi na jeuri ya madaraka huwa ni mbaya sana.
Mkuu soma taarifa iliyotolewa wakati Ndomba anapandishwa cheo cha kijeshi.Hujui unachoakiongea!!!
Jifunze tofauti kati ya mwanajeshi na mwanajeshi mstaafu. Pia jifunze kuongea mambo kwa evidence...
So ametumikia jeshini, akawa Mkuu wa Mkoa na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM, tukadhani amestaafu jeshi, kisha akapandishwa cheo cha kijeshi na kurudi kwenye kazi za jeshi. Kwa hiyo huyu hakuwa askari mstaafu. Na bado alikuwa kiongozi wa CCM.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Meja Jenerali Samuel Albert Ndomba kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Aidha, Rais Kikwete amempandisha cheo Meja Jenerali Ndomba kuwa Luteni Jenerali.
Taarifa iliyotolewa leo, Ijumaa, Septemba 21, 2012, mjini Dar Es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais – Ikulu, imesema kuwa uteuzi huo unaanza leo.
Taarifa hiyo ya Balozi Sefue imesema kuwa kabla ya uteuzi wake, Meja Jenerali Ndomba alikuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Jenerali Ndomba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali Abdulrahman A. Shimbo ambaye amestaafu Jeshi kwa mujibu wa sheria baada ya kufikisha umri wa miaka 60.
​Taarifa ya Balozi Sefue pia imesema kuwa Rais Kikwete amemteua Brigedia Jenerali Raphael Mugoya Muhuga kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa kuanzia leo, Ijumaa, Septemba 21, 2012.
Aidha, Rais Kikwete amempandisha cheo Brigedia Jenerali Muhuga kuwa Meja Jenerali.
Kabla ya uteuzi wake, Brigedia Jenerali Muhuga alikuwa Mkuu wa Utawala na Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
21 Septemba, 2012
COL. NDOMBA ROAD
It starts near the railway crossing with Njiro road-through the former Maboxini settlement to breweries road. This is another bypass. The vehicles that are going to Esso/Unga ltd. Industrial area or Daraja Mbili instead of going to the city centre they will use this road. It will also reduce traffic congestion between RTD area and Kijenge round about and clock tower. It is named after the former Regional Commissioner for Arusha Col. Ndomba who convinced Arusha business community to contribute towards opening this important by pass. This by pass is 1.4 km.
Source; Arusha Times.
tatizo linaweza kuwa kipato kama haifikii kiasi cha kumaliza matatizo ya msingi +angalau kuweka akiba.Pia kuwe na tofauti za kifamilia za kijeshi na za raia wanaofanya kazi nyingine kwani wao wanakuwa exposed ktk mazingira ya hatari na kuwa mbali na familia zao bila mpangilio. Mara nyingi mambo ya msingi yakifikiwa kinachomshikiliwa mfanyakazi sehemu ni level ya satisfaction anayopata ktk hiyo ajira, na wengine ni kufanya kazi aipendayo ya ndoto yake.Wanajeshi wengi tuu wanaona raia wanaishi vizuri kuliko wao na kwa uhuru mkubwa.wengi wan amarafiki uraini kuliko kambini na wapo friendly ila bado hawajapata majibu ya maisha yao kam wanahitaji baki katika jeshi.Ni tafiti za jeshi tuu ndio zitakazowafungua hawa wakubwa-wababe akili na kujua hali halisi.Hata kama hawatapenda kuelewa ni kuwa huwezi danganya watu kwa muda wote na hasa kama huo uwongo unahusu maisha ya watu...Ebu niambie package formal na informal za hawa watu wanaojiita ma chief execautive na watumishi wengine wa umma una tofauti gani? Kuanzia majeshi, mashirika ya umma, na serikali zote kuu na za mitaa, njoo kwenye wabunge linganisha na wana siasa wengine, uje kwenye vyama vyenyewe vya siasa jinsi viongozi wa vyama hivyo vipatao vyao vinavyotofautiana na fursa..Je hapo nani akubali wengine wajipangie tu ukubwa wa keki wengine watazame kwa macho tu? How long can you fool people? Matokeo yake ndiyo haya sasa kila mtu kageuka mwizi tapeli ilimradi tu apate nafasi ya ku-fisadi kwa manufaa binafsi what kind of country are we building? Eti wanajitetea ni ubebari upi huo? Hata ubepari una miiko na msingi mkubwa wa ubepari ni kila mtu analipwa kwa jinsi awezavyo kuzalisha na ku accumulate capital sasa hii yetu ambapo mtu anatafuta sehemu ambapo public good zimekusanywa in terms of chash ndiyo anajigawia in the name of ubepari nani atakubali?
Mkuu soma wasifu wa Ndomba wakati anapandishwa cheo cha kijeshi.
So ametumikia jeshini, akawa Mkuu wa Mkoa na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM, tukadhani amestaafu jeshi, kisha akapandishwa cheo cha kijeshi na kurudi kwenye kazi za jeshi. Kwa hiyo huyu hakuwa askari mstaafu. Na bado alikuwa kiongozi wa CCM.
Arusha kuna barabara imeitwa kwa jina la Ndomba kukumbuka utumishi wake kama RC.
Hii sio shida, ila askari mdogo kupiga picha na chadema ni suala zito sana.
kuhusu ndomba kwa kweli sijaelewa maana mara anakuwa DC (Ngara) then RC (Arusha) baadae anarudishwa Jeshini hakika sijaelewa formula iliyotumika kumrusha rusha katika maeneo mawili tofauti (Jeshini) then SIASA then Jeshini au ni swahiba wa Mkulu?
Wale wale walioshindwa kujibu hili, leo wanakwazwa na mwanajeshi mdogo kupiga picha na Lema.Duuh! hapa lipo jambo, ninavyoelewa U DC ni cheo cha makada wale waliokosa nafasi zingine za wizarani na bungeni, hivyo hupewa U DC na RC wasikae kijiweni. na hii ni kwa washikaji wa karibu wa mkulu kwa namna moja ama nyingine.
DC ni mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM wilayani, kadahalika na RC mkoani. Sasa huyu jamaa atawezaje kutekelza ile dhana kuwa wanajeshi hawaruhusiwi kuwa wanasiasa, jee? atakuwa ameachana na Ukada!
Na ndio walioandaliwa ku risk zaidi.Wale wakubwa wanafundishwa kuwa hawastahili ku risk , na mara zote inabidi walindwe tena na hawa wadogo na wanaopigika.Mda utafika changes itatokea, askari wa chini ndio wapiganaji na ndio wenye hali ngumu.
Unakubaliana nasi kuwa shimbo alifanya siasa.
kwa kuwa tamko lilihusu uchaguzi na vyama vya siasa, mtoa tamko sahihi angekuwa kama si msajili wa vyama vya siasa basi angekuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi.
Ikiwa kwa kitisho cha mpaka na malawi mkuu wa majeshi yetu hatakiwi kusema kitu sembuse kwa kazi isiyomuhusu kabisa!!!
Hawa wajeshi wajiongeze kidogo, wanaposema wanakitii chama kinachounda serikali wamepaswa kujua kuwa utii wao kwa kipande hiki si utii wa kijeshi, kwani waamrishaji si wanajeshi, ama la sivyo hawa wastaafu wa jeshi wanasomeka kuwa ni wanajeshi.
huyu mnyika angekaa kimya tuu , jeshi na siasa ni vitu viwili tofauti , Amiri jeshi mkuu ni rais wa jamhuri ya muungano kwa hiyo ni sahii kwa msemaji wa jeshi kusema kwamba wanafuata serikali iliyo madarakani ,in this case ya ccm , wizara zote ,vyombo vyote vya usalama kuanzia polisi mpaka TISS ni lazima viheshimu sera za serikali iliyopo madarakani , kama wewe ni mwanajeshi ,polisi, usalama wa taifa unapenda sana sera za chadema au chama cha upinzani hutakiwi kujiingiza kwenye siasa labda utoke kwenye hiyo kazi . Dr slaa angekuwa rais si inamaa angekuwa amiri mkuu wa majeshi na vyombo vyote vya usalama vingefuata sera za chadema ...nini tatizo kufuata sera za ccm si ndo demokrasia ya vyama vingi ambayo tunaitaka
Ni sawa kuwa vyombo vya ulinzi na usalama hutekeleza majukumu yake chini ya amiri jeshi mkuu, ambaye ni rais wa nchi.huyu mnyika angekaa kimya tuu , jeshi na siasa ni vitu viwili tofauti , Amiri jeshi mkuu ni rais wa jamhuri ya muungano kwa hiyo ni sahii kwa msemaji wa jeshi kusema kwamba wanafuata serikali iliyo madarakani ,in this case ya ccm , wizara zote ,vyombo vyote vya usalama kuanzia polisi mpaka TISS ni lazima viheshimu sera za serikali iliyopo madarakani , kama wewe ni mwanajeshi ,polisi, usalama wa taifa unapenda sana sera za chadema au chama cha upinzani hutakiwi kujiingiza kwenye siasa labda utoke kwenye hiyo kazi . Dr slaa angekuwa rais si inamaa angekuwa amiri mkuu wa majeshi na vyombo vyote vya usalama vingefuata sera za chadema ...nini tatizo kufuata sera za ccm si ndo demokrasia ya vyama vingi ambayo tunaitaka
Ukiwa Mkuu wa Mkoa unakuwa mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM (M), ambao ni uongozi wa CCM, na bila shaka inathibitisha uanachama kwa kuwa huanza uanachama ndipo uongozi unafuata.ibara ya 147(3) ya Katiba inayosema,
"itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na chama chochote cha siasa...."
Ibara ya 147(4) inatafsiri ‘mwanajeshi' kuwa
"... ni askari aliyeajiriwa kwa masharti ya muda au ya kudumu katika Jeshi la Ulinzi, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza au Jeshi la Kujenga Taifa."