Kiongozi anapostafu Jina la Cheo chake halifi kama unavyofikilia, mfano hata Rais wa Nchi anapostafu lazima aitwe Rais mustafu. Neno Rais hata kuwa ameondolewa ila Cheo cha Urais hatakuwa nacho tendo, ndicho kinachotokea hata kwa hao uliowataja. Naamini utakuwa umeelewa sasa, na Mwanajeshi anayesemekana kuhudhuria kwenye kikao cha chama cha siasa akiwa amevalia vazi la Jeshi kosa lake ni kushabikia Chama na wala si kupiga picha kama vyofikilia. Wote tuungane kukemea hili na wala si kutete uovu kwa kupaste historia ya siku zilizopita, na ndo maana ya kuhitaji katiba mpya ili iyafute hayo yote yaliyokuwa na mlengo wa Chama kimoja. Sijajua ni kwanini kosa litumika kutatua kosa!.
Siku zote ili sheria ziangaliwe upya, kupitiwa upya na kufanyiwa marekebisho basi ni lazima ajitokeze mtu nakuivunja hiyo sheria au kanuni husika (chanzo)!
1. Siku zote na mara ningi tumewaona wanajeshi kwenye sherehe za mwenge,tena wakiwa na sare je ni sahihi?
2. Wanajeshi pia tunawaona kwenye mikutano ya siasa, je ni sahihi?
3. Ni kweli wanajeshi hawana kadi za vyama vya siasa?
4. Je mpaka sasa ni wanajeshi wangapi wastaafu wako kwenye siasa na chama gani?
5. Naanza kupata mashaka huko jeshini wenye vyeo vya juu, wako chama fulani, na wale wa chini chama fulani au wamegawana kwa stahili fulani.
6. Uchaguzi uliopita yaani 2010, je kwenye sehemu ambazo wanajeshi ni wengi, ni chama gani kilishinda hayo maeneo?
Angalizo
1. Ili tusing'ang'anie katiba hairuhusu bila kuangalia wayforward, hebu waanze kwa kura ya siri bila malipizo wajue mioyoni hawa wanajeshi wanawaza nini. Uasi uko moyoni hauko kwenye gwanda!
2. Tume ya katiba je imewasikiliza wanajeshi, hasa wa kati na chini? Je wana maoni gani?
3. Jambo hili lichukliwe kama challenge kwa jeshi na lisitumie nguvu kubwa na hofu kwani, Kama nilivyosema uasi huanzia moyoni.
4. Mwisho tukumbuke hawa ni wanadamu kama sisi, tofauti ni aina ya kazi tu. kupenda si dhambi. Wakumbukeni mapolisi kwenye mechi za simba na yanga, pale ndio utajua kilichomjaa mtu. Mbona wale polisi uanjani hawakamatwi?
Boxing Day njema wana JF
Queen Esther