CHADEMA yaijibu JWTZ

CHADEMA yaijibu JWTZ

Hivi mnyika ameishia darasa la ngapi hasa kielimu?shimbo alivitaka vyama vya siasa visigomee matokeo yatalapotangazwa akimaanisha vyama vyote ikiwemo ccm,sasa mnyika alijuaje kwamba ccm ndio watashinda hivyo ushauri wa jeshi unakilenga chadema na cuf tu?halafu mkiambiwa mna miliki kadi mbili mbili mnatoa povu,unaingia kwenye uchaguzi ukijua unaenda kushindwa si bora usishiriki basi

Unakubaliana nasi kuwa shimbo alifanya siasa.
kwa kuwa tamko lilihusu uchaguzi na vyama vya siasa, mtoa tamko sahihi angekuwa kama si msajili wa vyama vya siasa basi angekuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi.
Ikiwa kwa kitisho cha mpaka na malawi mkuu wa majeshi yetu hatakiwi kusema kitu sembuse kwa kazi isiyomuhusu kabisa!!!
Hawa wajeshi wajiongeze kidogo, wanaposema wanakitii chama kinachounda serikali wamepaswa kujua kuwa utii wao kwa kipande hiki si utii wa kijeshi, kwani waamrishaji si wanajeshi, ama la sivyo hawa wastaafu wa jeshi wanasomeka kuwa ni wanajeshi.
 
Uwezo Tunao; Mkubwa,Nimeipenda post yako sana! Na ni juzi tu nilikuwa naliongelea hili na makamanda wa4 wa pale Monduli (TMA) wakasema hii serikali ya mafisadi wanacheza tu kwani hawajui ya kwamba mioyo ya Watanzania ipo katika chama pinzani,wakaendelea kuzungumza mengi sana! Kwa kweli wameendelea kubwabwaja haswa wale makamanda! Na kwa kweli wanaichukia ccm kweli kweli na wakaendelea kusema ya kwamba ni dhahiri ya kwamba bado tupo kwenye UKOLONI MWEUSI HAKIKA!

Na kama kuna kosa CCM na Jeshi wanaweza kulifanya ni kumtimua yule mjeshi wa Lema. Yatafumuka mengi huko Jeshini. Tatizo kuna wakubwa wamekula wakavimbiwa wanasahau kuna "nyoka" wanataabika mle.
 
kama ndivyo basi kuna mahali raisi wetu anakosea i dare to admit that.

Mkuu Rais wetu hana makosa. Makosa yako kwenye Katiba ya CCM ambayo inatamka wazi wazi kwamba wakuu wote wa wilaya na mikoa ni makada wa chama hicho. Huwa najiuliza, suppose Chadema, CUF, n.k. nao wakiamua kuingiza hicho kipengele kwenye katiba zao itakuwaje?

So, Mkuu tatizo wala sio Rais bali mfumo mbovu wa magamba uliotufikisha hapa watanzania. CCM ni watu wa ajabu hakuna mfano!
 
Hivi mnyika ameishia darasa la ngapi hasa kielimu?shimbo alivitaka vyama vya siasa visigomee matokeo yatalapotangazwa akimaanisha vyama vyote ikiwemo ccm,sasa mnyika alijuaje kwamba ccm ndio watashinda hivyo ushauri wa jeshi unakilenga chadema na cuf tu?halafu mkiambiwa mna miliki kadi mbili mbili mnatoa povu,unaingia kwenye uchaguzi ukijua unaenda kushindwa si bora usishiriki basi

We m.p.u.u.z.i!.. Unajuaje kwamba shimbo kama mwanajeshi hakuwa anatoa vitisho kuibeba CCM? CHADEMA imepiga kelele muda mrefu kuwa mjeshi huyu anashirikiana na CCM kufisidi nchi, unategemea angeilinda CDM? Kama hujui jambo uliza?!!!!.
 
zuzu mwenyewe na wote wenye akili kama wanajeshi. jeshi la mafisadi nalo waliita jeshi? utakuwa umevurugwa wewe. cdm haina cha kupoteza maana haitegemei jeshi ktk kuendesha siasa kama magamba.jeshi hopeless, nashangaa linaitwa la wananchi wakati ni jeshi la magamba.

Dugu jeshi ndo litafanya kazi na chama kitakachokuwa kimeshinda kuingia nalo mzozo mapema hii ni hatari sana.
 
Unachosema kinaweza kuwa na ukweli lakini hakihusu jeshi pekee. Hata hivyo wanjeshi hawakatazwi kupenda vyama, wanachokatazwa ni kuonyesha ushabiki wao hadharani hasahasa wakiwa wamevaa uniform.
Vile vile ikumbukwe kuwa jeshi lilikuwa na uhusiano wa karibu sana na CCM mpaka mwaka 1992. Ikumbukwe kuwa hata JKT ilianzishwa kwa mawazo ya TANU youth league katika mkutano wao kule Tabora. Kwahiyo ni kweli kuwa jeshi bado lina chembechembe za CCM lakini haimaanishi kuwa sasa wanajeshi wavae sare za CCM na kwenda kuishabikia. Ukitaka kufanya majaribio ingia na gari yenye picha za kushabikia CCM katika eneo rasmi la jeshi kama Lugalo utaona kitakachotokea. Hata watumishi raia jeshini hawaruhusiwi kuvaa fulana za vyama katika maeneo ya yao ya kazi jeshini. na hili linahusu watumishi wote wa umma...

kwenye rangi nyekundu una maana na wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya sio?
 
sasa hii ndio point ambayo mnyika litakiwa aibainishe na si kusema kwann jesh limetolea tamko hii ilihali aishu ya meremeta ikiwa silent.nafikiri kama inawezekana tabale this point. ila sasa usisahau kwamba amiri jesh mkuu ndio kiongzi wa jesh sasa sijui hili linaonekanaje ingawa hawez kulitumia jeshi kwenye kampeni za chama chake

Mnyika ameyataja matukio yote yaliyolihusisha jeshi na kashfa za kisiasa na za ufisadi. Kataja meremeta, shimbo kufanya siasa za ccm, wanajeshi kuteuliwa kuwa wakuu wa wilaya na mikoa na hivyo kuwa wajumbe wa kamati za siasa za ccm. Kataja kauli ya mwigulu juu ya jeshi kuwaapia kuwalinda na mambo mengine yote.
Kwakuwa skendo zote hizo JWTZ haijawahi kutoa kauli ndipo tunashangaa hii ya mjeda kupiga picha tu na mbunge wa Chadema wanaitolea macho. Hapo ndipo tunahoji kuna nini nyuma ya pazia? Au mwenyekiti wa chama ametumia kofia yake ya uamiri jeshi mkuu kulishinikiza jeshi kuitolea kauli picha ya mjeda na kamanda Lema?
JWTZ ni jeshi la wananchi wa Tanzania na si jeshi la wanachama wa ccm!
 
Hoja za mnyika ni DHAIFU mara 100000000000000000000000,

Kikanuni, kufanya kosa kwa kuwa wengine wanafanya kosa ni umbumbumbu wa hali ya juu. Mnyika alitakiwa aseme kama yaliyotokea ni sahihi katika chama chao ama la na hatua ambazo jeshi linataka kuzichukua ni za kisheria ama la sio kujitetea kwamba eti mbona mwigulu.......................

Kweli shule muhimu
 
tuacheni ushabiki kwanza kabisa nasifu JWTZ kwa kutolea tamko punde walipona hili. jeshi nichombo ambacho hakitakiwi kufungamana na chama chochote cha siasa na kama ikitokea dosari kama hiyo ni kubwa sana kwa jeshi letu.

binafsi namsihi mnyika aangalie upya kauli yake hivi swala la wanajeshi kusema anajiunga na CDM na swala la meremeta utayafananisha??

meremeta liko katka ngazi tofauti na hata impact yake ni tofauti hii ya mjeda nayo ni tofauti na impact yake ni tofauti. tukiruhusu haya yatakuja yake ya majesh ya m23 ya DRC (sijui) tuacheni ushabiki hapa umakin unahitajika.

itohoe yenye rangi nyekundu, mahita alipogombe ubungu nini kilimsibu, mboma aliambulia nini, hao viongozi waandamizi wa jeshi hawapendwi na jamii kwa tabia yao ya kukipendelea ccm walipokuwa kazini.
 
They learnt to be loyal to the existing government,that is the only fact to consider.We CHADEMA, there are many opportunities to deal with so we have to ignore everything spoken by Mgawe,Shimbo or Mwigulu Nchemba. The issue is "African soldiers are born to be silent"
 
Hoja za mnyika ni DHAIFU mara 100000000000000000000000,

Kikanuni, kufanya kosa kwa kuwa wengine wanafanya kosa ni umbumbumbu wa hali ya juu. Mnyika alitakiwa aseme kama yaliyotokea ni sahihi katika chama chao ama la na hatua ambazo jeshi linataka kuzichukua ni za kisheria ama la sio kujitetea kwamba eti mbona mwigulu.......................

Kweli shule muhimu

wewe ni first class economist, umeshindwa hata kubuni vyanzo vya mapato kwa chama chako, mmebaki kutegemea ruzuku, na rushwa. unatunajisia bendera yetu ya taifa unapoifunga shingoni mwako.
 
Hoja za mnyika ni DHAIFU mara 100000000000000000000000,

Kikanuni, kufanya kosa kwa kuwa wengine wanafanya kosa ni umbumbumbu wa hali ya juu. Mnyika alitakiwa aseme kama yaliyotokea ni sahihi katika chama chao ama la na hatua ambazo jeshi linataka kuzichukua ni za kisheria ama la sio kujitetea kwamba eti mbona mwigulu.......................

Kweli shule muhimu

Wewe ndiwe Mwigulu nchemba, umesababisha kifo cha mnyiramba mwenzio kwa kujaribu kupambana na wenye akili kukuzidi namaanisha John Mnyika.
Tunakumbuka ulisema jeshi limeapa kuitumikia ccm, sasa hiyo akiliii matope?
 
CDM kama mazuzu! Chama kuingia mzozo na Jeshi ni hatari kwa chama husika. Yangu masooo.

Wakifanya upuuzi waambiwe HEWALA BABA!... Wewe hata mumeo akichukuliwa na rafiki yako ambaye ni mjeshi utawalipia hata gharama za Nyumba ya kulala wageni!!!!!!!
 
itohoe yenye rangi nyekundu, mahita alipogombe ubungu nini kilimsibu, mboma aliambulia nini, hao viongozi waandamizi wa jeshi hawapendwi na jamii kwa tabia yao ya kukipendelea ccm walipokuwa kazini.

sasa hapa napata hisia na iko hivi,
tunalichukia jesh simply kwasababu wanaonekana wanaibeba ccm sio?? hivi jeshi lingekaa kimya mngesemaje? na j unafikir wamekosea?
 
Mnyika ameyataja matukio yote yaliyolihusisha jeshi na kashfa za kisiasa na za ufisadi. Kataja meremeta, shimbo kufanya siasa za ccm, wanajeshi kuteuliwa kuwa wakuu wa wilaya na mikoa na hivyo kuwa wajumbe wa kamati za siasa za ccm. Kataja kauli ya mwigulu juu ya jeshi kuwaapia kuwalinda na mambo mengine yote.
Kwakuwa skendo zote hizo JWTZ haijawahi kutoa kauli ndipo tunashangaa hii ya mjeda kupiga picha tu na mbunge wa Chadema wanaitolea macho. Hapo ndipo tunahoji kuna nini nyuma ya pazia? Au mwenyekiti wa chama ametumia kofia yake ya uamiri jeshi mkuu kulishinikiza jeshi kuitolea kauli picha ya mjeda na kamanda Lema?
JWTZ ni jeshi la wananchi wa Tanzania na si jeshi la wanachama wa ccm!
Mwita Maranya nimekupa like kwasababu nimefurah mno kwamba huyu mwanajesh akithibitika kwamba ni mjeda kweli atawajibishwa ipasavyo. ila furaha yangu imezd mara dufu kwamba jeshi limekumbuka wajibu wake ipasavyo na naamin hawatayarudia haya yanaypleta hisia mbaya machoni pa watu.
 
Last edited by a moderator:
sasa hapa napata hisia na iko hivi,
tunalichukia jesh simply kwasababu wanaonekana wanaibeba ccm sio?? hivi jeshi lingekaa kimya mngesemaje? na j unafikir wamekosea?

Kukaa kimya ndio busara yenyewe. Waswahili wanasema ukikaa kimya watu wanajua una busara lakini pindi unapofungua mdomo wako tu ndipo wanajua upumbavu wako.
Kadri wanavyozidi kuongea kauli zinazodhihirisha kwamba wamesahau wajibu wao wa msingi na kujikita kufanya siasa tena za kuibeba ccm kwa gharama yoyote ndipo wananchi wanazidi kuwachukia.
Kuna Mboma, Mahita, Tibaigana na Kombe kwa uchache walivyoingiza miguu kwenye vinyang'anyiro waliishia kupata aibu. Lakini pia walitusaidia kujua kwamba majeshi yetu yanazuiwa kufanya siasa za upinzani tu lakini kufanya siasa ccm ni ruksa.
 
sasa hapa napata hisia na iko hivi,
tunalichukia jesh simply kwasababu wanaonekana wanaibeba ccm sio?? hivi jeshi lingekaa kimya mngesemaje? na j unafikir wamekosea?

Mkuu hisia hiyo ielekee hivi,
wanajeshi wengi wa vyeo vya juu ni adui wa wananchi si kwa nadharia bali kwa vitendo. wapiganaji askari wa vyeo vya kati na wasio na vyeo wanapendwa na jamii nao wanaipenda jamii, kama una mashaka na ninachokuambia basi rejea "picha" ya general Imran Kombe RIP.
huyu aliwapenda wananchi akawahurumia wanavyoumizwa na ccm. na huyu chalii wa mererani yupo upande wa wananchi.
CCM IMESHINDWA KUSHUGHULIKA NA MATATIZO YA WANANCHI LAKINI INANG'ANG'ANIA KUSHIKA DOLA.
 
Mwita Maranya nimekupa like kwasababu nimefurah mno kwamba huyu mwanajesh akithibitika kwamba ni mjeda kweli atawajibishwa ipasavyo. ila furaha yangu imezd mara dufu kwamba jeshi limekumbuka wajibu wake ipasavyo na naamin hawatayarudia haya yanaypleta hisia mbaya machoni pa watu.

Ahsante. Na mimi kama wanamageuzi wengine tunachotaka ni uwajibikaji wa vyombo vyetu vya dola bila kuweka hisia za ubaguzi wowote wa kisiasa.
Kama jeshi haliruhusiwi kufanya siasa basi wananchi tuione hali hiyo kivitendo.
Kama ambavyo mjeda huyo atachukuliwa hatua za kinishamu kwa hisia za kushiriki siasa basi tunataka kuona na wengine tena wale wakubwa nao wakishughulikiwa kwa kujihusisha na kushiriki siasa kinyume cha sheria na kanuni za kijeshi.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom