CHADEMA yaijibu JWTZ

CHADEMA yaijibu JWTZ

Jeshi liache Uchama litumikie watanzania. Chama kuwa madarakani si sababu ya jeshi kulitumikia badala ya serikali. Ndio maana kwenye katiba mpya kuna haja ya kutenganisha vyeo vya kisiasa na vyeo vya kiserikali.
 
Mkuu,

Mnyika hana point tatu A-level, ni UWONGO.

Hata yeye yuko hapa na anajua ukweli kwamba hana A tatu kwa A-level.
kuwa na A 3 ama A7 si kigezo cha mtu/mwanafunzi kuwa anajua vitu vingi hasa kwa mfumo wa elimu tanzania ambao tunaupigia kelele! Kimsingi Sibishi ufahamu mzuri wa Mnyika.
 
Hoja za mnyika ni DHAIFU mara 100000000000000000000000,

Kikanuni, kufanya kosa kwa kuwa wengine wanafanya kosa ni umbumbumbu wa hali ya juu. Mnyika alitakiwa aseme kama yaliyotokea ni sahihi katika chama chao ama la na hatua ambazo jeshi linataka kuzichukua ni za kisheria ama la sio kujitetea kwamba eti mbona mwigulu.......................

Kweli shule muhimu

Mbumbumbu wewe picha nini bwana watu wanapiga picha na raisi siku zote hoja hapo ni kwanini lleo jeshi linashupalia isue hii ni chuki binfsi kwani hapo kafanya siasa nakuambia wapo wengi hawana mapenzi na watawala wa nchi hii tunao hawasemi huyo jamaa kaanza na anajua kuwa nini kitatokea we subiri afukuzwe kazi. ni woga na ujinga kukaa kimya wakati unaona mambo hayaendi sawa si nidhamu.
 
Hivi mnyika ameishia darasa la ngapi hasa kielimu?shimbo alivitaka vyama vya siasa visigomee matokeo yatalapotangazwa akimaanisha vyama vyote ikiwemo ccm,sasa mnyika alijuaje kwamba ccm ndio watashinda hivyo ushauri wa jeshi unakilenga chadema na cuf tu?halafu mkiambiwa mna miliki kadi mbili mbili mnatoa povu,unaingia kwenye uchaguzi ukijua unaenda kushindwa si bora usishiriki basi

hapana alisema vyama vya upinzani hakusema vyama vya siasa tunakumbukumbu vizuri
 
mnyika+ubungo.jpg

MBUNGE wa Ubungo na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika

SIKU moja baada ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kutangaza kumsaka mtu aliyepiga picha na Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema akiwa amevalia sare za jeshi hilo, chama hicho kimeibuka na kulijia juu jeshi hilo.

Hata hivyo, mbali na kauli hiyo, jeshi hilo limekijibu Chadema likisema kwamba halifanyi siasa na kwamba litaendelea kumsaka mtu huyo, kwa kuwa kanuni zake haziruhusu askari kushabikia siasa.

Jana, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alisema chama hicho kimeshangazwa na kasi ya jeshi hilo kuchunguza tukio hilo, huku akidai kwamba kuna masuala mazito ambayo hayajatolewa ufafanuzi kama lile la Meremeta.

“Serikali ilikataa kulifuatilia kwa madai ya kutokuingilia usiri wa jeshi hilo na halikutolewa ufafanuzi wala kufanyiwa uchunguzi mpaka sasa,” alisema Mnyika na kuendelea.

“Isitoshe Septemba, mwaka huu katika Mkutano Mkuu wa UVCCM Iramba, aliyekuwa Mweka Hazina wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu Bara wa chama hicho Mwigulu Nchemba (aliwahi kutoa matamko kuhusu JWTZ), lakini jeshi halikufikiria kuyatolea tamko.”

Mnyika alidai pia kuwa wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2010, aliyekuwa Mnadhimu wa Jeshi hilo Luteni Jenerali Abdulahman Shimbo aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kuvitaka vyama vya siasa kutokugomea matokeo ya uchaguzi kwa madai ya kulinda amani ya nchi.

“Kauli ile ya Shimbo ni ya kisiasa na ya kibaguzi ambayo ililenga kuvididimiza vyama vingine na kuibeba CCM. Mbona jeshi halichunguzi kauli hiyo hata baada ya Shimbo kustaafu?” alihoji Mnyika.

Mnyika alisema kwamba Chadema hakitaki kutumia tukio hilo la askari kuhalalisha makosa mengine, bali inataka sasa JWTZ iwajibike kwa kila jambo linalolihusu badala ya kukimbilia masuala yaliyofanywa na askari wadogo. Hata hivyo, Mnyika alisema chama hicho hakipo tayari kuingia katika mvutano na jeshi kuhusiana na tukio la askari huyo kujihusisha na siasa mpaka jeshi hilo litakapokamilisha uchunguzi na kutoa taarifa yake kwa umma.

Kwa upande wake, Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe alisema kuwa jeshi litaendelea kujiweka kando na shughuli za siasa na kusisitiza kuwa mtumishi wake yeyote anayetaka kujiingiza kwenye majukwaa ya kisasa anapaswa kujitoa jeshini. Akijibu hoja za Chadema kuhusiana na tamko lilitolewa na aliyekuwa Mnadhimu wa jeshi hilo Shimbo aliyewataka wanasiasa kutogomea matokeo wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita, Mgawe alisema: “Ebwa ehh! Na wewe sasa unataka kuniingiza kwenye siasa, mimi sitaki kuingia huko, lakini nikueleze kuwa sisi kama wanajeshi tuko royal (utii) kwa Serikali iliyoko madarakani,” alisema Mgawe.

Alisema kwa mujibu wa sheria, Jeshi halipaswi kufungamana na itikadi zozote za kisiasa kwani kwa kufanya hivyo kunaweza kulitumbukiza taifa kwenye hatari. “Leo huyu anaingia kwenye mkutano wa chama na sare za jeshi, kesho atakuja mwingine na silaha, huoni kwamba sasa tutakuwa tunakaribisha hatari ?” alihoji Mgawe.


Source: Mwananchi

Nasikia Mwanajeshi wetu amekamatwa, sasa tutafute CD gani tena?
 
Back
Top Bottom