Una uhakika na ulichokiandika hapo? Point tatu form six? Hamuogopi hata kudanganya?
Mnyika ana uwezo na ayafanyayo hata kama elimu yake sio kubwa. Ila hakuna haja ya kudanganya kuweka elimu au matokeo ambayo hana.
hans kupiga picha na mwanajesh dhambiHujui ya kuwa mwanajeshi akistaafu bado ni mwanajeshi,pakitokea tatizo lolote huitwa kikosi.Kwa nini usitwe wewe!
Jeshi linapaswa kuwa na standard moja kwa vyama vyote. Je Mwigulu Nchemba aliposema Jeshi limeapa kuilinda CCM mpaka kufa kulitolewa tamko lolote la kijeshi?
Je Kanali Mzurikwao alipokuwa DC na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wa Wilaya ya Kibondo kwa miaka mingi wakati akiwa askari kamili wa jeshi, mbona hatukuona tamko lolote na CCM au jeshi kukosoa hali hiyo? Je viongozi wakuu wa CCM ambao bado wanapambwa na vyeo vya kijeshi: Kapt. Mkuchika, Kanali Abrahman Kinana, mbona jeshi halijatoa tamko lolote? Hata kama ni wastaafu, mbona JK pia ni mwanajeshi mstaafu lakini ameshaacha title ya kijeshi?
Mifano ipo mingi tu ya akina Shimbo, Kalembo, John Komba Mbunge kwa tiketi ya CCM n.k. ambao wamekuwa na vyeo ambavyo vinaambatana na ukada wa CCM bila kujitoa jeshini.
Double standard ya jeshi ndio issue kubwa hapa.
Hujui unachoakiongea!!!
Jifunze tofauti kati ya mwanajeshi na mwanajeshi mstaafu. Pia jifunze kuongea mambo kwa evidence...
Wanajeshi wasiostaafu wako wengi sana huko ccm kupitia hiyo milango ya ukuu wa mikoa na wilaya.
Namkumbuka pia Kanali Edmund Mjengwa alikuwa mkuu wa wilaya huku akiwa hajastaafu JWTZ.
Hawa watu wasipende kuropoka wakashani hatuna kumbukumbu kama wao.
Kiongozi anapostafu Jina la Cheo chake halifi kama unavyofikilia, mfano hata Rais wa Nchi anapostafu lazima aitwe Rais mustafu. Neno Rais hata kuwa ameondolewa ila Cheo cha Urais hatakuwa nacho tendo, ndicho kinachotokea hata kwa hao uliowataja. Naamini utakuwa umeelewa sasa, na Mwanajeshi anayesemekana kuhudhuria kwenye kikao cha chama cha siasa akiwa amevalia vazi la Jeshi kosa lake ni kushabikia Chama na wala si kupiga picha kama vyofikilia. Wote tuungane kukemea hili na wala si kutete uovu kwa kupaste historia ya siku zilizopita, na ndo maana ya kuhitaji katiba mpya ili iyafute hayo yote yaliyokuwa na mlengo wa Chama kimoja. Sijajua ni kwanini kosa litumika kutatua kosa!.
Hujui unachoakiongea!!!
Jifunze tofauti kati ya mwanajeshi na mwanajeshi mstaafu. Pia jifunze kuongea mambo kwa evidence...
Mkuu: Kanali John Antoni Mzurikwao hakuwa mstaafu wa jeshi wakati akiwa mkuu wa wilaya ya kibondo na baadaye kuhamishiwa Sumbawanga.Kiongozi anapostafu Jina la Cheo chake halifi kama unavyofikilia, mfano hata Rais wa Nchi anapostafu lazima aitwe Rais mustafu. Neno Rais hata kuwa ameondolewa ila Cheo cha Urais hatakuwa nacho tendo, ndicho kinachotokea hata kwa hao uliowataja. Naamini utakuwa umeelewa sasa, na Mwanajeshi anayesemekana kuhudhuria kwenye kikao cha chama cha siasa akiwa amevalia vazi la Jeshi kosa lake ni kushabikia Chama na wala si kupiga picha kama vyofikilia. Wote tuungane kukemea hili na wala si kutete uovu kwa kupaste historia ya siku zilizopita, na ndo maana ya kuhitaji katiba mpya ili iyafute hayo yote yaliyokuwa na mlengo wa Chama kimoja. Sijajua ni kwanini kosa litumika kutatua kosa!.
Mkuu,
Mnyika hana point tatu A-level, ni UWONGO.
Hata yeye yuko hapa na anajua ukweli kwamba hana A tatu kwa A-level.
[TABLE="width: 879"]
[TR]
[TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD]Mwanajeshi anapojitokeza wazi kushabikia upinzani na wale wanaojificha kushabiki CCM[/TD]
M. M. Mwanakijiji
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD]MOJAWAPO ya picha ambazo zimevutia hisia za watu wengi sana siku chache zilizopita ni ya mtu ambaye ameonekana akiwa amevaa fatigi ya kijeshi huku akiwa amesimama na kuzungukwa na wabunge wa CHADEMA Godbless Leman na Joshua Nassari.
Katika picha nyingine askari huyo ameonekana akiwa amesimama kama mmoja wa walinzi wa umati tena kikakamavu mbele ya jukwaa.
Kama picha hii ni ya kweli na kuwa mtu aliyepigwa picha hii ni mpiganaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ambayo yuko katika utumishi (active duty), basi siasa zetu zimefikia katika kiwango kingine kabisa.
Naomba kwa ajili ya hoja yangu hii tudhanie tu kuwa picha ni ya mpiganaji wa JWTZ na kuwa amejitokeza wazi kuiunga mkono CHADEMA na sera zake bila kujali matokeo yake katika ajira yake jeshini.
Baadhi ya wachangiaji mbalimbali kwenye mitandao ya jamii wameonyesha kuguswa na kitendo cha askari huyo kujitokeza na hasa pale ilipodaiwa kuwa amedai yeye mwenyewe kuwa hajali wakubwa wake watamfanya nini kwani amekizimia CDM.
Wapo ambao wameona kitendo hiko kuwa ni cha kishujaa na kinahitaji kuungwa mkono.
Wapo wengine ambao wameona kitendo hicho ni zaidi ya kishujaa kwani kinaonesha hali ya wananchi wetu wanavyopigika chini ya utawala wa CCM.
Kwamba hadi wanajeshi wamechoka ile mbaya kiasi kwamba hawajali tena kujificha kwenye kivuli cha jeshi na sasa kama huyo mmoja alivyoweza kujitokeza basi wengine wataanza kujitokeza vile vile kwani wao nao wanaonekana mitaani wanavyo hangaika na maisha.
Wapo wengine ambao pia ni wengi kidogo kwa maoni yangu ambao wanadai wakati umefika kwa wana jeshi wanaounga mkono upinzani wajitokeze wazi kwani kwa muda mrefu wanajeshi wenye kuunga mkono CCM wamekuwa wakitumia nafasi zao kuitetea CCM bila kukemewa na uongozi wa juu wajeshi.
Mfano mzuri ambao unatolewa mara moja ni jinsi alivyofanya aliyekuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Gen. Abdulrahaman Shimbo wakatit unaelekea uchaguzi mkuu wa 2010.
Gen. Shimbo alijitokeza na kuzungumza na waandishi wa habari na kupiga mkwara ambao ulionekana kuipigia debe serikali na hasa kumlinda Rais Kikwete badala ya kubakia bila upande.
Gen. Shimbo alizungumza maneno ambayo sehemu nyingine yangeonekana kuingilia mchakato wa upigaji kura.
Kwa wanaokumbuka niliandika katika gazeti hili wakati ule kulaani kitendo hicho. Nakumbuka niliandika wakati ule (Octoba 3, 2010) kuhusu jambo hili na kusema kuwa nijukumu la Jeshi kumpigia Saluti Rais anayechaguliwa na wananchi.
Hawawezi kuamua ni rais gani wanamtaka au hawamtaki.
Niliandika katika makala ile ya Kiingereza kulaani kitendo cha Shimbo kutoa vitisho na nikasema kuwa It is for this reason, I condemn in all possible strongest terms any plan or arrangement that would not let the election process be free, fair and transparent for all to see. I call for an immediate statement from our military leadership to assure the country that they would remain neutral in this political and democratic process and will be willing and ready to ensure that the election will be peaceful and the results will be respected by all parties including the incumbent. Sikuamini kuwa Shimbo alifanya vile kwa sababu Polisi walishindwa kusimamia uchaguzi.
Lakini siyo hivyo tu wapo wanaotolea mfano kuwa wakati Mwigulu Nchemba amedai kuwa Jeshi limeapa kuilinda CCM mpaka kufa hakuna kauli yoyote iliyotolewa ama na uongozi wa jeshi au na mtu mwingine yeyote serikalini, hivyo kuonesha kuwa ni kweli uongozi wa juu wa jeshi letu uko tayari kufanya lolote kuilinda CCM madarakani.
Haikutolewa kauli yoyote kukanusha wala kujaribu kuuliza jeshi hilo liliahidi hayo lini? Lakini huyu bwana mdogo asiye na nguvu kujitokeza kupiga picha na kiongozi anayemhusudu au wa chama anacho kihusudu imekuwa nongwa?
Lakini wapo wengine kama mimi ambao tunachukulia yote mawili ni makosa. Ni lazima mstari uliochorwa wa wanajeshi kutokuingiza siasa uheshimiwe.
Katika demokrasia jeshi lazima liwe nje ya siasa na mwanajeshi yeyote anayetaka kushabikia siasa au kushabikia chama cha siasa ni lazima ama afanye hivyo nje ya sare zake na kama anataka kushika nafasi ya kisiasa ni lazima atoke jeshini kwanza.
Bahati mbaya sana mstari huu haujaheshimiwa na CCM yenyewe na matokeo yake wameendelea kutenda kana kwamba mstari huu haupo.
Kuna mifano ya watendaji kadhaa ambao wameendelea kuwa katika siasa licha ya kwamba ni wanajeshi na wengine haijawahi kuelezwa vizuri kama walistaafu jeshini rasmi.
Na wengine wameonekana wakifanya utumishi jeshini na mara moja wanapotoka wanapewa nafasi za kisiasa. Kwa mfano aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Adadi Rajabu ambaye baadaya kutoka Polisi akapewa Ubalozi na hayuko peke yake.
Na wengine hatutashangaa kusikia Gen. Shimbo akizawadiwa nafasi fulani. Yote haya ni mambo ya hatari kwa ukuaji wa demokrasia kwani watendaji wa vyombo vya majeshi wanaanza kutenda wakipigia mahesabu kuwa wata kuja kukumbukwa na watawala.
Haya yote yanachangiwa na kukosekana kwa sheria na kanuni wazi inayoweka kikomo kwa watumishi wakuu wa jeshi kushika nafasi za kisiasa. Kwa mfano sheria ikikataza mtu yeyote aliyeshika cheo cha kuanzia Kanali kwenda juu kuteuliwa nafasi yoyote yakisiasa hadi ipite miaka mitano tangu atoke jeshini inaweza kusaidia. Lakini kwa huku chini itakuwaje?
Kama wakubwa wanaweza kujihusisha na siasa baadaya ajira hawa wa chini wafanye nini? Je tuweke utaratibu gani ili wanajeshi wa ngazi za chini wasijisikie wanaonewa.
Naamini hakuna namna isipokuwa kuendelea kuhakikisha huu mstari unaheshimiwa. Wanajeshi wakiwa na sare zao wasishiriki kuunga mkono chama chochote cha siasa kwani hatutaki ilete hisia ya sehemu ya jeshi kugawanyika kisiasa.
Nje ya sare na nje ya muda wakazi wanajeshi waendelee kuruhusiwa kushiriki shughuli mbalimbali za kisiasa isipokuwa kuwa na kadi rasmi ya chama cha siasa.
Lakini kuwakatalia kuwa na kadi ya chama cha siasa nako siyo kuwanyima haki yao?
Hapa basi inabidi wanajeshi nao waruhusiwe kuwa na kadi za vyama vya siasa kitu pekee ambacho labda wasiruhusiwe kushika uongozi wowote ndani ya chama cha siasa hadi anapotoka jeshini.
Kwa kufanya hili la pili itasaidia pia kwa baadhi ya wapiganaji ambao watataka kushika nafasi za uongozi kwenye chama hasa zile zinazohitaji mgombea awe na muda fulani ndani ya chama.
Mtindo huu ndio unatumiwa sana na Marekani labda na baadhi ya nchi nyingine ambapo suala la uanachama linabakia na askari hadi anapotoka japo anajulikana kama ni registered member wa chama fulani.
Na wao wenyewe wanaheshimu mipaka hiyo ya kutokuingiza siasa katika utumishi wao na wanapofanya hivyo kuna kanuni kali kabisa wanapoomba waondolewe jeshini au kuteremshwa vyeo kwa kuwa wana siasa badala ya wapiganaji.
Hivyo, basi wakati JWTZ linaendelea kuchunguza habari za mwanajeshi huyu uongozi wake pia ukae chini na kujiuliza kama kanuni zake zinawafanya watendaji wa juu wa JWTZ kuonekana wanakipendelea chama tawala na kuweka mipaka ya jeshi kujihusisha na siasa au na mambo ya kisiasa.
Kwa mfano, tayari tumeona dalili za jeshi kuingizwa kwenye harakati za kisiasa na kutishia maandamano ya kisiasa.
Ni lazima kanuni ziwekwe wazi ili jeshi libakie na heshima najukumu lake kuu la kulinda uwepo wa nchi yetu. Vinginevyo, itabidi iamuliwe kama jeshi ni la CCM.
Source: Tanzania Daima Jumatano,26,12,2012
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: left"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: #ffffff, colspan: 3"][/TD]
[TD="colspan: 3"][/TD]
[TD="colspan: 3, align: right"][/TD]
[TD="align: center"][/TD]
[TD="width: 506, align: center"]
[/TD]
[TD="width: 130, align: center"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Kiongozi anapostafu Jina la Cheo chake halifi kama unavyofikilia, mfano hata Rais wa Nchi anapostafu lazima aitwe Rais mustafu. Neno Rais hata kuwa ameondolewa ila Cheo cha Urais hatakuwa nacho tendo, ndicho kinachotokea hata kwa hao uliowataja. Naamini utakuwa umeelewa sasa, na Mwanajeshi anayesemekana kuhudhuria kwenye kikao cha chama cha siasa akiwa amevalia vazi la Jeshi kosa lake ni kushabikia Chama na wala si kupiga picha kama vyofikilia. Wote tuungane kukemea hili na wala si kutete uovu kwa kupaste historia ya siku zilizopita, na ndo maana ya kuhitaji katiba mpya ili iyafute hayo yote yaliyokuwa na mlengo wa Chama kimoja. Sijajua ni kwanini kosa litumika kutatua kosa!.
Ni kweli mkuu,chadema wasijivunie ile picha na kutaka publicity ya aina yoyote ile,lile lilikuwa ni kosa kwa lema na kwa askari,lema pale alichemsha, otherwise wasimamie kanuni kuwa wanajeshi wote ni no partisan,na ni marufuku kushiriki siasa.,,kesho na kesho kutwa itakuwa wao.Chonde chonde Mnyika siasa na Jeshi sio sahihi, CHADEMA kiangalie namna ya kuwa na mahusiano bora na jeshi, huyo mwanajeshi mmoja sio issue
Dada samahan sijakuelewa!Wakifanya upuuzi waambiwe HEWALA BABA!... Wewe hata mumeo akichukuliwa na rafiki yako ambaye ni mjeshi utawalipia hata gharama za Nyumba ya kulala wageni!!!!!!!
CHADEMA wako sahihi, JWTZ ni chombo cha wananchi na wala si chombo cha CCM hivyo kama vipi wale wakuu wa mikoa na wilaya na wengine wanaotumikia vyeo vya u-kada katika CCM wachukuliwe hatua haraka kabla hatujamtazama mwanajeshi wa Mh Lema Jijini Arusha hivi majuzi.
Ni wakati mwafaka jeshi letu pendwa likajikwamua na U-CCM wa enzi za chama kimoja katika kipindi hiki cha vyama vingi ili chombo hiki muhimu kiweze kuendana na wakati wa hivi sasa.
Roho ikipenda kitu wala hakuna haja kuewndelea kujificha; ukweli wa mambo ni kwamba zaidi ya asilimia 80 ya jeshi letu linapenda chama kile ambacho wananchi tulio wengi tunakipenda - CHADEMA!!!!!
Mkuu zeMaracopolo
Ukiona mwenzio kapewa ukuu wa mkowa nawewe ndo umekalia kiti chake baada ya yeye kustaaafu na kuwa kada, je
hutashawishika kutetea maslahi ya chama ili nawewe ujepewa ukuu wa mkoa hapo baadaye? imekaaje hii!!