CHADEMA yaijibu JWTZ

CHADEMA yaijibu JWTZ

Angekuwa kapiga picha na Nape isingekuwa ishu kabisa au ndo ule msemo"Kunya anye kuku akinya Bata kaharisha"

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Ahsante. Na mimi kama wanamageuzi wengine tunachotaka ni uwajibikaji wa vyombo vyetu vya dola bila kuweka hisia za ubaguzi wowote wa kisiasa.
Kama jeshi haliruhusiwi kufanya siasa basi wananchi tuione hali hiyo kivitendo.
Kama ambavyo mjeda huyo atachukuliwa hatua za kinishamu kwa hisia za kushiriki siasa basi tunataka kuona na wengine tena wale wakubwa nao wakishughulikiwa kwa kujihusisha na kushiriki siasa kinyume cha sheria na kanuni za kijeshi.

na nafikiri kwamba ni busara zaid kwa mambo ambayo yanagusa taifa kwa umoja wake basi sote tukaungana kusema hapa panamakosa ili kuweka nchi yetu pazuri zadi kuliko kusimamia itikadi zetu hali tunaiyumbisha nchi yetu. ufike wakati sasa serikali isikilize hoja za watu na kuzitafaari kwa kina isione mtu atasema nn ama ana hoja ya msingi la hasha itafakari kila hoja hata kama ni ya kipuuzi kuliko kudharau jambo.
 
Jeshi linapoteza heshima kama likiendelea kuwakumbatia magamba.
 
ifike mahali tukubaliane kuwa, hii kitu ya kupga siasa kwa vyombo vya usalama ni hatari than anything u cn imagine of, si kwa ccm wala cdm... kuna sabb nying zikiwemo za kimaslah....! tuwe na vyombo imara vya ulinz na usalama visivyofungamana na upande wowote na vinavyowajibika kwa hak na usawa kwa umma bx inatosha.. .! tuache ushabik
 
ifike mahali tukubaliane kuwa, hii kitu ya kupga siasa kwa vyombo vya usalama ni hatari than anything u cn imagine of, si kwa ccm wala cdm... kuna sabb nying zikiwemo za kimaslah....! tuwe na vyombo imara vya ulinz na usalama visivyofungamana na upande wowote na vinavyowajibika kwa hak na usawa kwa umma bx inatosha.. .! tuache ushabik
 
Nakuona mkuu unahoja tena nzito wakitoka jeshini wanahamia ukada wa ccm mikowa na wilaya, je huko ndo kutenganisha Jeshi

na siasa? watawala watuweke sawa hapa.

CCM ni ndumila kuwili
 
Kosa lipo pale alipotumia jezi za jeshi kupiga picha na viongozi wa vyama vya siasa,nadhani ndipo tatizo lilipo,lakini kama angepiga picha bila jezi tusingesikia matamko toka jwtz,ni kweli wanajeshi wajiweke pembeni,wasifungamane na chama chochote kile na kijana huyu dawa sio kumfukuza kazi ni kumpa onyo na kumweleza asome vyema sheria za kazi yake.maana kila kazi ina taratibu zake,yeye kazivunja taratibu hizo,hilo lipo wazi aombe msamaha yaishe na ajikite kusoma zaidi juu ya maadili ya kazi yake.
 
Ahsante. Na mimi kama wanamageuzi wengine tunachotaka ni uwajibikaji wa vyombo vyetu vya dola bila kuweka hisia za ubaguzi wowote wa kisiasa.
Kama jeshi haliruhusiwi kufanya siasa basi wananchi tuione hali hiyo kivitendo.
Kama ambavyo mjeda huyo atachukuliwa hatua za kinishamu kwa hisia za kushiriki siasa basi tunataka kuona na wengine tena wale wakubwa nao wakishughulikiwa kwa kujihusisha na kushiriki siasa kinyume cha sheria na kanuni za kijeshi.

Na tutegemee mgawanyiko mkubwa ndani ya vyombo vetu vya ulinzi kwa muda si mrefu.

Endapo huyu askari atakapochukuliwa adhabu kali, huku wakubwa wao wanajiingiza direct kwenye siasa. Na tena za kimaslai zaidi na wao wanakufa na njaa?!

Tutarajie mapya zaidi ya haya! Sababu hili si jambo la huyo mpiganaji mmoja tu? Na ninahis wapo wengi nyuma ya huyo, waliochoka kwa tabia za wakubwa zao..
 
sasa hapa napata hisia na iko hivi,
tunalichukia jesh simply kwasababu wanaonekana wanaibeba ccm sio?? hivi jeshi lingekaa kimya mngesemaje? na j unafikir
wamekosea?


mkuu umeliweka sawa wala halina ubishi.

1. kwasababu wanatumia mamlaka yao kuibeba ccm na zaid katika kuiminya haki, ccm ikineemeka kwa matendo ya maafisa wa

majeshi yote moja kwa moja wakiwa kazin, au wakitegemea kupata hisan ya mwenyekiti wa chama (ccm) watakapo staafu.

JWT, JKT, POLIS, MAGEREZA NK.


2. Ndiyo wanakosea sana, tukisema kila chama kifanye wanayofanya ccm, taifa la tanzania tutakuwa mashakan, wala amani hata kuwa rafiki kwetu tena.


3. Wakikaa kimya na jamii ikaamin hivyo (sio kinadharia-majukwaan), kila chama kitatii sheria, taratibu na kanuni, hata raia wataridhika sana maana kodi zao zitakuwa kwa manufaa ya wote na si kwa ccm peke yake kuhodhi matumizi ya jeshi hasa katika siasa ndiyo penye matatizo.
 
Kosa lipo pale alipotumia jezi za jeshi kupiga picha na viongozi wa vyama vya siasa,nadhani ndipo tatizo lilipo,lakini kama angepiga picha bila jezi tusingesikia matamko toka jwtz,ni kweli wanajeshi wajiweke pembeni,wasifungamane na chama chochote kile na kijana huyu dawa sio kumfukuza kazi ni kumpa onyo na kumweleza asome vyema sheria za kazi yake.maana kila kazi ina taratibu zake,yeye kazivunja taratibu hizo,hilo lipo wazi aombe msamaha yaishe na ajikite kusoma zaidi juu ya maadili ya kazi yake.


Mkuu nakukubali hasa kwenye hitimisho lako.

Usisahau mkuu kila jambo lisababu zake.

Kila jambo huenda na wakati wake, hii ni flash temperature - joto ambalo kwa mafuta ni kubipu cheche ya moto unausikia umelipuka.

-Wale wote wanaovaa kofia, kombati, buti za jeshi na vyeo vyao kichwani na mabegani kusimamia utekelezaji wa majukumu ya ccm na ilania zake huko tuendako wapo mashakani kama sio CCM kuingia kaburin bila ngazi ya kutokea. (flash point imefikia sasa tunasubiri ignition kufanyika)
 
Hivi mnyika ameishia darasa la ngapi hasa kielimu?shimbo alivitaka vyama vya siasa visigomee matokeo yatalapotangazwa akimaanisha vyama vyote ikiwemo ccm,sasa mnyika alijuaje kwamba ccm ndio watashinda hivyo ushauri wa jeshi unakilenga chadema na cuf tu?halafu mkiambiwa mna miliki kadi mbili mbili mnatoa povu,unaingia kwenye uchaguzi ukijua unaenda kushindwa si bora usishiriki basi

ww ngoja tukukumbushe kidogo,wananchi walitoa dhamana kwa cdm kwa kura nyingi za urais,na ccm walijua wazi kwamba wameshindwa urais,so plan B ilitumika kuchakachua na ili kuepusha mpango wowote ule wa kupinga matokeo hayo,jwtz kupitia shimbo walitoa kauli ya kuwaogopesha watanzania ili kuheshimu matokeo ya Nec ccm,
 
Mwita Maranya nimekupa like kwasababu nimefurah mno kwamba huyu mwanajesh akithibitika kwamba ni mjeda kweli atawajibishwa ipasavyo. ila furaha yangu imezd mara dufu kwamba jeshi limekumbuka wajibu wake ipasavyo na naamin hawatayarudia haya yanaypleta hisia mbaya machoni pa watu.


Naamini mnyika na wengine katika chadema wanacholalamikia ni tatizo la jeshi kutafuta sifa za eti kuchukua hatua katika dogo ili mradi mambo makubwa wameyanyamazia... sijui unaelewa?
 
Hivi mnyika ameishia darasa la ngapi hasa kielimu?shimbo alivitaka vyama vya siasa visigomee matokeo yatalapotangazwa akimaanisha vyama vyote ikiwemo ccm,sasa mnyika alijuaje kwamba ccm ndio watashinda hivyo ushauri wa jeshi unakilenga chadema na cuf tu?halafu mkiambiwa mna miliki kadi mbili mbili mnatoa povu,unaingia kwenye uchaguzi ukijua unaenda kushindwa si bora usishiriki basi
sio Mnyika aliishia darasa la ngapi bali wewe uliishia darasa la ngapi hata hujui hesabu za LOGIC! chama kimoja kupitia manyanga yake na support ya serikali na vyombo vya dola kina uhakika wa ushindi katika uchaguzi dhidi ya vyama vingine. msemaji mmoja wa chombo kimoja cha serikali ya chama hicho akatoa tamko vyama visipinge matokeo ya ushindi kwa sababu za kiusalama. kwa HESABU ZA LOGIC ambazo wewe hukusoma ni nani anaambiwa asipinge matokeo. sio vyama pinzani vya siasa! think logically sio kutoa comments za kishabiki!
 
[TABLE="width: 879"]
[TR]
[TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD]
Mwanajeshi anapojitokeza wazi kushabikia upinzani na wale wanaojificha kushabiki CCM

M. M. Mwanakijiji
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD]MOJAWAPO ya picha ambazo zimevutia hisia za watu wengi sana siku chache zilizopita ni ya mtu ambaye ameonekana akiwa amevaa fatigi ya kijeshi huku akiwa amesimama na kuzungukwa na wabunge wa CHADEMA Godbless Leman na Joshua Nassari.
Katika picha nyingine ‘askari' huyo ameonekana akiwa amesimama kama mmoja wa walinzi wa umati tena kikakamavu mbele ya jukwaa.
Kama picha hii ni ya kweli na kuwa mtu aliyepigwa picha hii ni mpiganaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ambayo yuko katika utumishi (active duty), basi siasa zetu zimefikia katika kiwango kingine kabisa.
Naomba kwa ajili ya hoja yangu hii tudhanie tu kuwa picha ni ya mpiganaji wa JWTZ na kuwa amejitokeza wazi kuiunga mkono CHADEMA na sera zake bila kujali matokeo yake katika ajira yake jeshini.
Baadhi ya wachangiaji mbalimbali kwenye mitandao ya jamii wameonyesha kuguswa na kitendo cha askari huyo kujitokeza na hasa pale ilipodaiwa kuwa amedai yeye mwenyewe kuwa hajali wakubwa wake watamfanya nini kwani amekizimia CDM.
Wapo ambao wameona kitendo hiko kuwa ni cha kishujaa na kinahitaji kuungwa mkono.
Wapo wengine ambao wameona kitendo hicho ni zaidi ya kishujaa kwani kinaonesha hali ya wananchi wetu wanavyopigika chini ya utawala wa CCM.
Kwamba hadi wanajeshi wamechoka ‘ile mbaya' kiasi kwamba hawajali tena kujificha kwenye kivuli cha "jeshi" na sasa kama huyo mmoja alivyoweza kujitokeza basi wengine wataanza kujitokeza vile vile kwani wao nao wanaonekana mitaani wanavyo hangaika na maisha.
Wapo wengine ambao pia ni wengi kidogo kwa maoni yangu ambao wanadai wakati umefika kwa wana jeshi wanaounga mkono upinzani wajitokeze wazi kwani kwa muda mrefu wanajeshi wenye kuunga mkono CCM wamekuwa wakitumia nafasi zao kuitetea CCM bila kukemewa na uongozi wa juu wajeshi.
Mfano mzuri ambao unatolewa mara moja ni jinsi alivyofanya aliyekuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Gen. Abdulrahaman Shimbo wakatit unaelekea uchaguzi mkuu wa 2010.
Gen. Shimbo alijitokeza na kuzungumza na waandishi wa habari na kupiga mkwara ambao ulionekana kuipigia debe serikali na hasa kumlinda Rais Kikwete badala ya kubakia bila upande.
Gen. Shimbo alizungumza maneno ambayo sehemu nyingine yangeonekana kuingilia mchakato wa upigaji kura.
Kwa wanaokumbuka niliandika katika gazeti hili wakati ule kulaani kitendo hicho. Nakumbuka niliandika wakati ule (Octoba 3, 2010) kuhusu jambo hili na kusema kuwa nijukumu la Jeshi kumpigia Saluti Rais anayechaguliwa na wananchi.
Hawawezi kuamua ni rais gani wanamtaka au hawamtaki.
Niliandika katika makala ile ya Kiingereza kulaani kitendo cha Shimbo kutoa vitisho na nikasema kuwa "It is for this reason, I condemn in all possible strongest terms any plan or arrangement that would not let the election process be free, fair and transparent for all to see. I call for an immediate statement from our military leadership to assure the country that they would remain neutral in this political and democratic process and will be willing and ready to ensure that the election will be peaceful and the results will be respected by all parties including the incumbent." Sikuamini kuwa Shimbo alifanya vile kwa sababu Polisi walishindwa kusimamia uchaguzi.
Lakini siyo hivyo tu wapo wanaotolea mfano kuwa wakati Mwigulu Nchemba amedai kuwa Jeshi limeapa kuilinda CCM mpaka kufa hakuna kauli yoyote iliyotolewa ama na uongozi wa jeshi au na mtu mwingine yeyote serikalini, hivyo kuonesha kuwa ni kweli uongozi wa juu wa jeshi letu uko tayari kufanya lolote kuilinda CCM madarakani.
Haikutolewa kauli yoyote kukanusha wala kujaribu kuuliza jeshi hilo liliahidi hayo lini? Lakini huyu bwana mdogo asiye na nguvu kujitokeza kupiga picha na kiongozi anayemhusudu au wa chama anacho kihusudu imekuwa nongwa?
Lakini wapo wengine kama mimi ambao tunachukulia yote mawili ni makosa. Ni lazima mstari uliochorwa wa wanajeshi kutokuingiza siasa uheshimiwe.
Katika demokrasia jeshi lazima liwe nje ya siasa na mwanajeshi yeyote anayetaka kushabikia siasa au kushabikia chama cha siasa ni lazima ama afanye hivyo nje ya sare zake na kama anataka kushika nafasi ya kisiasa ni lazima atoke jeshini kwanza.
Bahati mbaya sana mstari huu haujaheshimiwa na CCM yenyewe na matokeo yake wameendelea kutenda kana kwamba mstari huu haupo.
Kuna mifano ya watendaji kadhaa ambao wameendelea kuwa katika siasa licha ya kwamba ni wanajeshi na wengine haijawahi kuelezwa vizuri kama walistaafu jeshini rasmi.
Na wengine wameonekana wakifanya utumishi jeshini na mara moja wanapotoka wanapewa nafasi za kisiasa. Kwa mfano aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Adadi Rajabu ambaye baadaya kutoka Polisi akapewa Ubalozi na hayuko peke yake.
Na wengine hatutashangaa kusikia Gen. Shimbo akizawadiwa nafasi fulani. Yote haya ni mambo ya hatari kwa ukuaji wa demokrasia kwani watendaji wa vyombo vya majeshi wanaanza kutenda wakipigia mahesabu kuwa wata kuja kukumbukwa na watawala.
Haya yote yanachangiwa na kukosekana kwa sheria na kanuni wazi inayoweka kikomo kwa watumishi wakuu wa jeshi kushika nafasi za kisiasa. Kwa mfano sheria ikikataza mtu yeyote aliyeshika cheo cha kuanzia Kanali kwenda juu kuteuliwa nafasi yoyote yakisiasa hadi ipite miaka mitano tangu atoke jeshini inaweza kusaidia. Lakini kwa huku chini itakuwaje?
Kama wakubwa wanaweza kujihusisha na siasa baadaya ajira hawa wa chini wafanye nini? Je tuweke utaratibu gani ili wanajeshi wa ngazi za chini wasijisikie wanaonewa.
Naamini hakuna namna isipokuwa kuendelea kuhakikisha huu mstari unaheshimiwa. Wanajeshi wakiwa na sare zao wasishiriki kuunga mkono chama chochote cha siasa kwani hatutaki ilete hisia ya sehemu ya jeshi kugawanyika kisiasa.
Nje ya sare na nje ya muda wakazi wanajeshi waendelee kuruhusiwa kushiriki shughuli mbalimbali za kisiasa isipokuwa kuwa na kadi rasmi ya chama cha siasa.
Lakini kuwakatalia kuwa na kadi ya chama cha siasa nako siyo kuwanyima haki yao?
Hapa basi inabidi wanajeshi nao waruhusiwe kuwa na kadi za vyama vya siasa kitu pekee ambacho labda wasiruhusiwe kushika uongozi wowote ndani ya chama cha siasa hadi anapotoka jeshini.
Kwa kufanya hili la pili itasaidia pia kwa baadhi ya wapiganaji ambao watataka kushika nafasi za uongozi kwenye chama hasa zile zinazohitaji mgombea awe na muda fulani ndani ya chama.
Mtindo huu ndio unatumiwa sana na Marekani labda na baadhi ya nchi nyingine ambapo suala la uanachama linabakia na askari hadi anapotoka japo anajulikana kama ni "registered member" wa chama fulani.
Na wao wenyewe wanaheshimu mipaka hiyo ya kutokuingiza siasa katika utumishi wao na wanapofanya hivyo kuna kanuni kali kabisa – wanapoomba waondolewe jeshini au kuteremshwa vyeo kwa kuwa wana siasa badala ya wapiganaji.
Hivyo, basi wakati JWTZ linaendelea kuchunguza habari za mwanajeshi huyu uongozi wake pia ukae chini na kujiuliza kama kanuni zake zinawafanya watendaji wa juu wa JWTZ kuonekana wanakipendelea chama tawala na kuweka mipaka ya jeshi kujihusisha na siasa au na mambo ya kisiasa.
Kwa mfano, tayari tumeona dalili za jeshi kuingizwa kwenye harakati za kisiasa na kutishia maandamano ya kisiasa.
Ni lazima kanuni ziwekwe wazi ili jeshi libakie na heshima najukumu lake kuu la kulinda uwepo wa nchi yetu. Vinginevyo, itabidi iamuliwe kama jeshi ni la CCM.

Source: Tanzania Daima Jumatano,26,12,2012
blank.gif

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: left"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
blank.gif
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: #ffffff, colspan: 3"]

[TD="colspan: 3"]
blank.gif
[/TD]

[TD="colspan: 3, align: right"][/TD]

[TD="align: center"][/TD]
[TD="width: 506, align: center"]
[/TD]
[TD="width: 130, align: center"][/TD]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
blank.gif
 
Kosa mnalo lifanya nikuto ku jadili hoja badala yake mnajadili mtu binafsi!

Mkuu,

Mnyika hana point tatu A-level, ni UWONGO.

Hata yeye yuko hapa na anajua ukweli kwamba hana A tatu kwa A-level.
 
Mungi this is a bit serious ila kwan mkuu wa mkoa ni mwanasiasa??nikimaanisha kwamba ni lazima awe mwana-ccm??

nimeuliza haya kwan ninaye mtu wangu wa karibu namjua nje ndani si mwanasiasa kabisa lkn aliteuliwa na rais kushika wadhifa wa mkuu wa wilaya.

Wakuu wa Mikoa na wilaya wote ni makada wa chama tawala........................ hapo ndo ujiulize mwenyewe kama makada wa chama cha siasa ni wanasiasa
 
Mtu wa Shamba Hivi ni kwa nini ChHADEMA hata uovu wanautetea na kuhalalisha kuwa wema, amu ndo miungu watu kwamba wao hawakosei?. Penye ukweli tuseme, kama ni kweli yule alikuwa ni askari Jeshi basi aliandaliwa na wala si bure. Hata alivyokuwa amesimama kama greenguard wa CCM na wapambe wa CHADEMA mbele ya mkutanano!.

Ukipenda sifa sana madhara yake huwa ni makubwa sana, kwa hali hii Mnyika mnatuhadaa wananchi ili tuamini uongo kuwa ukweli.
 
Last edited by a moderator:
mbona kuna wanajeshi bado ni wanachama wa vyama vya siasa mfano wa wazi ni Capt, John Komba bado ni mwanajeshi na mwanachama wa CCM maana hajastaafu jeshi mbona jeshi halijamtoa kazini au halijamtimua
 
Mtu wa Shamba Hivi ni kwa nini ChHADEMA hata uovu wanautetea na kuhalalisha kuwa wema, amu ndo miungu watu kwamba wao hawakosei?. Penye ukweli tuseme, kama ni kweli yule alikuwa ni askari Jeshi basi aliandaliwa na wala si bure. Hata alivyokuwa amesimama kama greenguard wa CCM na wapambe wa CHADEMA mbele ya mkutanano!.

Ukipenda sifa sana madhara yake huwa ni makubwa sana, kwa hali hii Mnyika mnatuhadaa wananchi ili tuamini uongo kuwa ukweli.
Jeshi linapaswa kuwa na standard moja kwa vyama vyote. Je Mwigulu Nchemba aliposema Jeshi limeapa kuilinda CCM mpaka kufa kulitolewa tamko lolote la kijeshi?

Je Kanali Mzurikwao alipokuwa DC na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wa Wilaya ya Kibondo kwa miaka mingi wakati akiwa askari kamili wa jeshi, mbona hatukuona tamko lolote na CCM au jeshi kukosoa hali hiyo? Je viongozi wakuu wa CCM ambao bado wanapambwa na vyeo vya kijeshi: Kapt. Mkuchika, Kanali Abrahman Kinana, mbona jeshi halijatoa tamko lolote? Hata kama ni wastaafu, mbona JK pia ni mwanajeshi mstaafu lakini ameshaacha title ya kijeshi?

Mifano ipo mingi tu ya akina Shimbo, Kalembo, John Komba Mbunge kwa tiketi ya CCM n.k. ambao wamekuwa na vyeo ambavyo vinaambatana na ukada wa CCM bila kujitoa jeshini.

Double standard ya jeshi ndio issue kubwa hapa.
 
Mkuu tata mura, kumbuka hata cheo cha u captain wa jeshi John Komba alikipataje, ni kwa ajili ya kuimba nyimbo za ku promote CCM. Je kuna tamko lolote kutoka jeshini, je na wewe una tamko lolote?
 
Back
Top Bottom