CHADEMA yaanzisha Harambee ya kuchangia familia za walioshitakiwa kwa ugaidi

Mungu akuzidishie
Nami nitachangia. Wanayopitia ni udhalimu wa hali ya juu. Kumsaidia yeye aliyepo matesoni, ni ibada iliyo njema mbele za Mungu. Tujiweke karibu na kumkaribia Mungu wetu kwa kushikamana na wenye kudhulumiwa.

Nitachangia kila mwezi mpaka watakapokuwa huru. Shetani hajawahi kumshinda Mungu. Mungu atawashindia dhidi ya mabaradhuli wenye kufurahia mateso ya wanadamu wenzao.

Tunaweza kupata taarifa kwa uhakika hatima ya Lijenje?
 
Mungu akubariki
Inasononesha sana

Changia_Familia_za_Makomandoo_wetu_wazalendo_na_watiifu_kwa_Taifa_la_Tanzania_waliobambikiwa_k...jpg
 
Amina , Mungu akuzidishie
Erythro, fanya hivi.
1. Kuna muda maalum

2. Kuna mrejesho baada ya muda maalum?

Hii yote inaweza kuwa ni kichocheo kwa wengine zaidi kujitokeza na kuendeleza mchango.

Hata kama haya hayawezekani kwa sababu maalum, BAVICHA watumie nafasi hii ya kuwashirikisha wananchi kwa lengo/malengo mahsusi.
 
Mimi sichangii chochote, ila nawasisitiza CHADEMA hebu wajiamini hizi issue za kujishusha na kuanza kuchangiana zimepitwa na wakati sana. Inaonesha jinsi msivyoweza kujiendesha. Mimi nashauri hivi vitu mwaachane navyo mfocus na agenda kubwa za kuwatoa hao watu. Chadema sio VICOBA.
 
Taarifa ya sasa inaeleza kwamba Chadema kupitia BAWACHA inawaomba wananchi wote kuchangia Familia za Makomandoo Adamoo na wenzake , walioshitakiwa kwa tuhuma za ugaidi , ambao inadawa ulifadhiliwa na mshitakiwa mwenzao Freeman Mbowe kwa kitita cha Tsh Laki 6.

View attachment 1966057

Tayari mchakato wa kampeni hiyo umekamilika kwa kufungua akaunti Maalum katika benki ya NMB , yenye namba 22601605514 kwa jina la BAWACHA TAIFA , ambapo yeyote atakayeguswa anaruhusiwa kuweka pesa ili ziweze kusaidia familia za wahanga .

KUTOA NI MOYO

Habari njema inayo kuja sasa japo kwa kuchelewa sana:

CHADEMA: Bila kuwapa Makavu hakuna Katiba Mpya

Ni muhimu kuupanua uwanja huu. Kutafuta namna endelevu ya kuwa karibu na wahanga wote wa misukosuko ya namna hii wakiwamo makomando hawa.

Wahanga mikononi mwao, hao ndiyo walio mashujaa wetu #1 wa mapambano.

Mungu ibariki Chadema.
 
Back
Top Bottom