Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Huwa najaribu kumuelewa IGP Sirro katika suala la kesi ya ugaidi dhidi ya Mbowe, hadi najiuliza hivi kweli uwezo wa IGP Sirro katika kufikiria ndio umeishia hapo?
Suala liko hivi. Huyo askari Luteni wa JWTZ anaita askari anasema ameambiwa na Mbowe kwamba anataka kufanya ugaidi, na anataka amtafutie makomandoo wa kumsaidia kufanya ugaidi.
Askari wanaingia laini ya huyu Luteni (bila kujiuliza kama inawezekana Luteni ana ugomvi wake binafsi na Mbowe na anataka tu kuwatumia Polisi kulipiza kisasi)
Kisha Polisi, badala ya kumalizana na huyo mtu ili wachunguze wenyewe (take ownership of the investigation) kama kweli kuna ugaidi - yaani watafute supporting evidence, wanamuambia endelea kutafuta watu wa kumfanyia ugaidi Mbowe halafu uwe unatupa taarifa.
Sasa ukosefu wa umakini wa Polisi wa pili hapa ni kwamba walipaswa wao ndio watoe hao makomandoo (undercover police), sio kumwachia huyu Luteni fake, lakini IGP hadi hapo hajaona ukihiyo unaofanyika. Hao makomandoo walipaswa kuwa watu wa TISS au polisi ili iwe rahisi wao kuwa insiders, lakini kwa uwezo wa IGP hakuwaza mbali kiasi hicho.
Mfano, ukiwaambia Polisi kuna mtu kanipa kazi ya kutafuta mtu wa kuua mke wake (contract killer), Polisi wanapaswa kukupa askari ambaye atajifanya yeye ndie muuaji aliepatikana , sio wakuambie wewe mtafutie huyo muuaji halafu uwe unatupa taarifa! Hiyo sio tu ni unprofessional, bali ni the most stupid mistake a police force can make!
Baada ya muda Luteni anawaambia polisi haya nimeshampa Mbowe makomandoo magaidi wawili.
Sasa tena, badala ya Polisi kuanza kufuatilia hao watu wanakutanana na nani, wananunua vitu gani (kama milipuko kwa ajili ya kulipulia hivyo vituo) wao wanaamua kwenda moja kwa moja kuwakamata hao "makomandoo". Na sio labda wanawakamata wakiwa na Mbowe wanapanga kitu ili wakamate na evidence, hapana.
Sasa masuala ya kujiuliza;
Na by the way, mie sio Polisi, bali hapa ni common sense tu. Unfortunately, najua kwamba common sense is not common to everyone, even the supposedly professionals!

- Polisi walimchunguza huyu Luteni ni mtu wa namna gani, kwa mfano kama ana akili sawasawa au anaweza akawa ana matatizo ya kufikria vitu kichwani kutonakana na post war traumas labda katika mission za JWTZ alizohusika? (Yaani ana paranoia ya ugaidi)
- Zaidi ya maneno ya huyu Luteni fake wa JWTZ, Polisi hadi wanaamua kufanya arrests, walikuwa na ushahidi wotewote wa ku-support tuhuma za ugaidi - wanasema Mbowe alitoa fedha, kwani katika kutoa fedha kuna mahali Mbowe aliandika "haya ni malipo halali kwa ajili ya vitendo vya ugaidi nilivyopanga"?
- Mmoja wa hao makomandoo aliajiriwa na Mbowe kama mlinzi. Je IGP Sirro hakujiuliza kwamba huyu Luteni wa JWTZ anaweza kuwa yeye ndio alikuwa anawapa maagizo hawa Makomandoo kwamba nawapeleka kwa Mbowe ili mkamsaidie kufanya ugaidi bila Mbowe kuwa na habari kwamba watu aliomuomba Luteni amtafutie kama walinzi wanaambiwa kwamba wanaenda Chadema wakafanye ugaidi
- Kimsingi, Mbowe ana fursa nzuri ya kumgeuzia kibao IGP Sirro na huyu Luteni wa JWTZ kwamba wao ndio walipanga kutafuta makomandoo wa kufanya ugaidi kwa kumtumia yeye na Chadema, ili hao makomandoo wakifanya ugaidi, huyu Luteni aseme nilishawaambia Polisi ni Mbowe sio mimi - au kwamba Luteni alitaka kufanya Ugaidi, na ili kujilinda, akawahusisha Polisi ili ionekane ni Mbowe, lakini kimsingi yeye ndio aliwatuma makomandoo wakafanye ugaidi kupitia kivuli cha Mbowe na Chadema (ndio maana ilikuwa muhimu sana Polisi kutoa makomandoo wao fake kumpa Mbowe)
- Kimsingi, IGP Sirro alitakiwa pia aelewe philosophy ya kupambana na serikali kwa ugaidi. Matukio ya ugaidi mara nyingi yanaendana na mtu au kikundi kujitambulisha kwamba sisi ndio tunahusika na kulipua kitu fulani ili haki zetu zitambuliwe. Hivi IGP Sirro alijiuliza kama Mbowe angefanyaje ugaidi bila kusema sisi Chadema ndio tumehusika? Wanadai Mbowe angelipua vituo vya mafuta - kwani vituo vya mafuta vinamilikiwa na Polisi au CCM hadi Mbowe awe na ugomvi navyo? Hakuna wanachama wa Chadema wanaomiliki vituo vya mafuta - sasa iweje Mbowe afanye ugaidi dhidi ya wanachama wake wa Chadema?