maulaga
JF-Expert Member
- Feb 22, 2009
- 472
- 120
Nakupongeza sana kwa kujitokeza kwako na kutoa msimamo wako kuhusu kujiunga kwako na CUF. Nakuomba sana ukipata nafasi fanya ziara wilayani Kilwa ambako CUF mna wanachama wengi sana na mmefaanikiwa kuwa na mbunge. Wanachama wenu kule kilwa inaonekana hawajazielewa sera za chama chenu kwani wanaamini kuwa mwana CUF ni kuwa adui wa watumishi wa serikali na kwamba hawatakiwi kufanya shughuri yoyote ya maendeleo hata kama nikusafisha mazingira yao. Ajabu hawataki hata kuchimba vyoo kwa ajili ya shule zao. Uungwana uko wapi walimu katika shule kutojengewa vyoo na hivyo kuchangia choo kimoja na wanafunzi wao? Maelezo yanayotolewa eti CUF mnatangaza kuwa jukumu la kujenga vyoo shuleni ni la serikali. Sasa mchango wa wananchi ni upi? kwani mlipuko wa maradhi ukitokea watakaoathirika ninani?Tafadharini waelimisheni wana chama wenu umhimu wa kuchangia maendeleo yao.Sijaongelea suala tajwa hapo juu,
nadhani CHADEMA wamekuja Igunga kama chama cha siasa na CUF tupo Igunga kama chama cha siasa, so ni kiasi cha kusubiri kipenga kipulizwe ndio tutajua nani alikuja kugawa kura za mwingine, nani CCM B au C n.k.
Kwa sasa ni mapema mno kupeana shutuma hizo za uongo, mimi nawaheshimu chadema kama chama cha siasa na sina ugomvi na uwepo wao Igunga.
Jambo lingine muhimu ni kuwa hii forum inaheshimika sana, kuna baadhi ya wadau wanajiunga hapa kuja kupotosha umma au ku_dogoesha watu fulani, yote haya hayatusaidii ikiwa bado watanzania wanashughulikiwa na sera za CCM. Hii ni forum muhimu sana na ninaogopa ikiwa itageuzwa kuwa mahali pa propaganda za vyama na masuala yasiyo na tija kwa jamii na taifa. Hali hii ikiendelea kufurahiwa itaharibu sura halisi ya forum na malengo yake.
Mimi ni kiongozi wa juu wa CUF na niko CUF kwa akili na utashi wangu na wakati najiunga CUF vyama vingine vyote vilikuwepo na sikuamua kujiunga navyo. Nitasimama CUF na kuijenga CUF , sitakimbilia kwenye vyama ambavyo vinaonekana vina mafanikio, nitapambana hapahapa nilipo na kuyatafuta mafanikio ya watanzania hapa hapa CUF.
Nawashukuru wote wanaoniunga mkono, wanaonikosoa kwa makusudi, bahati mbaya , kwa malengo mazuri au mabaya, sote tu watanzania na hatuna cha kuchekana.
Wasalaam,
Julius Mtatiro,
Naibu Katibu Mkuu(CUF),
TANZANIA Bara.
03/09/2011