CHADEMA wasaliti - CUF

CHADEMA wasaliti - CUF

hii inadhihirisha ubinafsi na uchoyo wa baadhi ya viongozi wa cuf
 
Bora tuwe wakweli Vyama vya siasa havitafika mbali kama havitokuwa na tabia ya kuachiana majimbo. Kama kweli CUF ina nguvu zaidi ya CDM basi CDM waiachie CUF Igunga vinginevyo ni kuwapa CCM ubwete wa kushinda.
Acha ushamba,we hujui siasa.CUF wakishinda chadema itanufaika vipi,au chadema wakishinda CUF itanufaika vipi,Wote wasimamishe wagombea mshindi apatikane,Kumbuka kila chama kinahitaji kujinadi ili kikue kichukue dola.
 
Huyu Mtaa tiro mbona haeleweki? kinachoonekana hapa naye anajitahidi kutafuta umaarufu kwa kuishambulia Chadema ili naye asikike. Hivi kwa capacity yake kama naibu katibu mkuu wa chama bara anashindwa kuelewa fomula ndogo tu kwamba Chadema ni chama kilichosajiliwa na ni chama kikuu cha upinzani na kina haki zote za kugombea nafasi yoyote ya uchaguzi kama ilivyo cuf na vyama vingine vyenye usajili wa kudumu? Hivi ameshindwa kutambua kwamba vyama vya upinzani havijaungana na havijawahi kufanya hivyo katika uchaguzi wowote? hivi hakumbuki cuf walifanya nini katika uchaguzi mdogo wa Mbeya vijijini miaka ile? hivi hajui ni nini kilitokea Tarime katika uchaguzi mkuu uliopita? Mtatiro acha unafiki!!!
 
Sioni ubaya wa Mtatiro kwenye siasa hasa za Tanzania maneno aliyotumia ni ya kawaida hasa kipindi cha kampeni.Tatizo la JF hawataki vyama vingine vya upinzani zaidi ya CDM.

 
Pamoja na kuwa siipendi cuf na ccm yake,lakini maneno ya Mtatiro yamenigusa kihisia....yaani nimejua upande mwingine wa shillingi.
Kitu ambacho ningemshauri Mtatiro ni kuwa hapo CUF siyo mahala pake kabisa! yaani hapo unapoteza mda tu kaka anguu! njoo ujiunge na
jeshi la ukweli na ukombozi (CDM) kwani si siri kijana umesoma na una mtazamo mpana sana wa siasa za bongo. Hivi unategemea nini kwa
chama kama cuf kuwa na mbunge mmoja tu wa kuchaguliwa huku bara? Karibu kwenye jeshi la ukweli mkuu ili tuikomboe nchi yetu kwa mara
ya pili
 
hili nalo jipya
huyu ndo mtatiro au fotocopy?
jamani jamani
nafuu kauli hii ingetolewa na nape
sasa mtatiro???
kweli cuf ni ccm B
 
Mbona na hao ma cuf hawakutuachia Tarime? iweje leo tuwaachie igunga?
 
CUF wameenda igunga kuisaidia CCM ishinde siyo yenyewe kushinda,wao CUF wanamuafaka na CCM huko Zanzibar sasa ndoa yao si bado haijavunjika wananchi tusiwaskilize hao ni ccm ya pili.
Mi nafikiri kila chama katika uchaguzi kina haki ya kushiriki kugombea kiti chochote kilicho wazi,sioni haja ya kuona eti chama fulani kinakwenda kuharibia chama kingine hii hapana shindana ukishinda jipongeze si wakati wa kusaka kisingizio.
 
KIJANA MWENZETU JULIUS MTATIRO KUMEZA NDOANO YA CCM
NA KADA WAKE MAALIM SEIF IGUNGA???


Julius Mtatiro, you are far better than that school of thinking. Kazi yako iwe ni kutafuta kukishawishi CHADEMA kuunga mkono azma yaako na wala si kuanza kupiga kufua kiasi hicho.

Tafadhali rafiki badilisha haraka mwenendo wako huo wa kuendeleza tu utamaduni wa kuchimbana wenyewe kwa wenyewe.


Otherwise Ndugu Julius Mtatiro, amini usiamini, si kipindi kirefu saaaana utaanza kuwafanya bila ha kujua watu wenye akili waanze kuona kwamba siku zote BWEKA ZA MBWA KOKO SIKU ZOTE HUELEKEZWA DHIDI YAKE YULE YULE MNYAMA NGUNGULI KWAKE mithili ya Simba vile (CDM) amuogopaye zaidi ili ikiwezekana basi mfugaji wake akajitokeze kumpiga taafu dhidi ya kiogofia chake hicho.

Mtatiro, ndani ya siasa ni kutongoza na kutongozana kwa lugha laini wala si vita hapo Igunga. Kwa jinsi ninavyokujua siku zote natumai itayafanyia kazi mapendekezo haayo na wala hizo Preconceptions za Maalim Seif za tangu mwaka wa kuanza kwa vyama vingi nchini.

Wewe ni kijana bwana na ni lazima uenende na kufikiri kihivo, we vipi mkuu????? Hebu jizuie kidogo kwenda huko kabla haujapoteza jumla CREDIBILITY mbele ya jamii ya Tanzania.


Mratibu wa kampeni wa cuf Julius Mtatiro ameishtumu vikali chadema kwamba kiimeenda Igunga kwa lengo la kugawa kura za Cuf.

Mtatiro amesema chadema wanajua wazi hawana nguvu yoyote Igunga lakini wameamua kwenda huko ili ccm ishinde.Mtatiro amemueleza mwandishi wa habari hizi kwamba chadema wasijidanganye kuambulia hata nafasi ya pili bali watakuwa namba 3 nyuma ya ccm na cuf.

Mtatiro amesema cuf wamejipanga kuwaeleza wananchi wa igunga ukweli wote kuhusu chadema ili waamue wenyewe.
 
Ombi langu rasmi Mhe Dokta Slaa, Prof Baregu, Dr Kitila Mkumbo, Freeman Mbowe, Mzee Ndesamburo, Kamanda Lema, Zitto Kabwe na wapiganaji wengine wengi wa ukweli CDM; kwa mara nyingine nawasihi kusahau yale yaliopita (kwenye wino mwekundu hapo chini) na mkatafute fomula ya kufanya kazi kwa pamoja.

Ila katika kutafuta kote kufanya hivyo, kamwekeni pembeni huyu KADA WA CCM, Maalim Seif, mwenye mawazo mgando na badala yake mkafanye kazi na the progressives walioko ndani ya CUF akiwamo Pro Lipumba na Julius Mtatiro.

Na wewe Mhe Mbatia usidhani kwamba wananchi hatuja-note ukomavu wako kutokuweka mgombea Igunga; tunasema hongera sana. Lakini bado kuna jukumu shingoni mwako kuwakalisha chini CUF na CHADEMA wakaelewe kimsingi nini ulichokua unatafuta kwa vyama vya upinzani kufanya kazi kwa pamoja Igunga na kwingineko nchini.

Mhe Mbatia Usipofanya hivyo basi hata kile kitendo cha kwanza kitaenda na maji nakwambia.

Huyu Mtaa tiro mbona haeleweki? kinachoonekana hapa naye anajitahidi kutafuta umaarufu kwa kuishambulia Chadema ili naye asikike.

Hivi kwa capacity yake kama naibu katibu mkuu wa chama bara anashindwa kuelewa fomula ndogo tu kwamba Chadema ni chama kilichosajiliwa na ni chama kikuu cha upinzani na kina haki zote za kugombea nafasi yoyote ya uchaguzi kama ilivyo cuf na vyama vingine vyenye usajili wa kudumu?

Hivi ameshindwa kutambua kwamba vyama vya upinzani havijaungana na havijawahi kufanya hivyo katika uchaguzi wowote? hivi hakumbuki cuf walifanya nini katika uchaguzi mdogo wa Mbeya vijijini miaka ile?

hivi hajui ni nini kilitokea Tarime katika uchaguzi mkuu uliopita?

Mtatiro acha unafiki!!!
 
huyo hana jipya labda kaongwa baada ya kuona hana jipya! hivi chadema kwenda igunga si haki yake kikatiba?
1.je ameenda kuwaeleza watu wa igunga habari za chadema au kumnadi mgombea wake ili ashinde,
2. je tunashindana kwa sera na hoja zenye mashiko au kwa kushambuliana bila hoja
3.yeye anamuwakilisha nani ssm au caf na kwa nini wawaogope chadema
4.wanaigunga wana matatizo mangapi? mda wa kumunadi mgombea na kuwaelezea matatizo yao yatasolviwa vp wewe unataka kuisema chadema? AMA KWELI MIAFRIKA NDIVYO ILIVYO!!!!!!!!!!!!!!HASIRA YA JOHN MNYIKA NA UBUNGE WA UBUNGO?????????????????ULISHINDWA KWA HOJA KAKA! HAMNA JIPYA!
 
Mratibu wa kampeni wa cuf Julius Mtatiro ameishtumu vikali chadema kwamba kiimeenda Igunga kwa lengo la kugawa kura za Cuf.Mtatiro amesema chadema wanajua wazi hawana nguvu yoyote Igunga lakini wameamua kwenda huko ili ccm ishinde.Mtatiro amemueleza mwandishi wa habari hizi kwamba chadema wasijidanganye kuambulia hata nafasi ya pili bali watakuwa namba 3 nyuma ya ccm na cuf.Mtatiro amesema cuf wamejipanga kuwaeleza wananchi wa igunga ukweli wote kuhusu chadema ili waamue wenyewe.

Ukisikia unafiki mwingine ndio huu. Igunga kuna chama kimoja tu cha upinzani kinashindana na wanandoa magamba na cuf. Huyu mtatiro hana lolote la kuwaambia watu wa Igunga kwa sababu uhalali wake kama chama ameshaupoteza alipokubali kuolewa na magamba. Kwa hiyo haishangazi kusikia anaifagilia magamba ishinde kwa sababu wanajua wao walishapoteza muelekeo kwa kukubali ndoa na magamba. Poleni cuf
 
DEMOKRASIA KWA MAANA YAKE HALISIA HAIWALAZIMISHI KITU WAPINZANI
NCHINI KUFUATA NJIA MOJA TU WAIPENDAYO CCM


CUF, NCCR-Mageuzi na CHADEMA, msisikilize maneno ya kipuuzi hapo juu; enyi Wah wetu Dr Slaa, Freeman Mbowe, Prof Lipumba, James Mbatia, Julius Mtatiro, Zitto Kabwe, Halima Mdee, Tundu Lissu, Mabere Marando na wengine wengi tu tafute; katafuteni haraka 'MKAKATI WA SIRI' wa kufanya kazi kwa pamoja Igunga na mwisho kutuletea mwakilishi wa wananchi kwa mara ya kwanza katika kipindi chote cha miaka 15 iliyopita.

Manene ya hapo juu tafsiri yake rasmi ni kwamba CCM imeanza kutetemeka matumbo ENDAPO WAPINZA WATAPATA BUSARA ya kufanya kazi kwa pamoja maana kwa strategy hiyo wanajua wazi maana yake itakua vipi huko Igunga na kwingineko nchini.

Hakika Demokrasia si lazima iende kwa mtindo mmoja tu bli ukweli ni kwamba kuna njia kibao za watu kufika Igunga pindi unapotokea katika pembe yoyote ya taifa hili. Kwa kuwa maana halisi ya neno demokrasia (ambayo kimsingi hatuifahamu nchini) ni UAMUZI WA WATU WENGI KATIKA NCHI, KWA MASLAHI YA WATU WENGI KATIKA NCHI NA YAKIONGO NA CHGUO LA WATU WENGI HAO ili malengo ya pamoja yaweze kukidhika ipasavyo.

Hivyo basi, bado inawezekana wapinzani wakafanya mchakato wa kila chama kufanya mchujo binafsi wa wagombe wake kisha wakawapambanisha wale wagombea bora waliobahatika kushinda katika kila chama cha upinzani kimojawapo ili mgombea bora zaidi akapatikane miongoni mwao wale washindi katika kila chama.

Baada ya hapo, yule atakayeonekana kuwashinda wenzaake wote katika kinyang'anyiro hicho cha kufa mtu mwishowe hukabidhiwa bendera ya vyama vyote vilivyoridhia mkakati huo na sasa mbio za kuwang'oa mafisadi kung'oa nanga rasmi jimbo baada ya jimbo.

Na wewe Mwita hapo juu, ni bora ukaanza kushiri mawazo kama haya tena bila mzaha wowote ili CCM kisije kikapata ugumu sana baada ya sisi wapiga kura kukigeuza chama cha upinzani miaka si mingi sana toka sasa.

NB: Na nyinyi Maxence Mello, Invisible pamoja na William Malecela; hili la KUCHOMOA BAADHI YA SHIREDISHI kali ubaoni bila taarifa yoyote kwa wanajamvini ndio tuseme ni demokrasia ya wapi???????

Tunaomba majibu hapa jukwaani haraka.
 
wajameni,
huyu mtatiro ameshaeleza mara mbili hapa ndani juu ya hali halisi na shutuma anazopewa, na ameomba tuhuma hizo zithibitishwe, mleta mada ameingia mitini, hataki kuthibitisha, kwa hiyo tutamshambulia mtatiro wa watu bila hatia. In fact nasisitiza kuwa ukweli utasimama daima, kwa mtu yeyote aliyesoma mlimani na vyio vikuu vingine enzi za uongozi wa mtatiro atashangaa kuona mtatiro anakejeliwa na kudhihakiwa. Mimi binafssi namtetea mtatiro unless otherwise ikiwa proved hapa kuwa kasema hiki na kile. Good enough yeye mwenyewe kafafanua nini alichowahi kusema hasa kuhusu chadema na ametoa msimamo bila uoga wala kificho juu ya hali halisi, na kwa mtizamo wangu ameilinda hoja na ushahidi wake vizuri, so sioni kosa lake, au mtoa mada ana kisasi tusichokijua na mtatiro? au ndiyo mambo yaleyale ya kuizamisha JF ionekane inajadili hoja ambazo hazina ukweli na msingi wowote?
 
Ndo sababu siwezi kuwa chadema, tlp, nccr mageuzi na mwali wetu (cuf) . Mimi siku zote ni ccm na tutashinda sababu ya mwali wetu. Bb pigana la sivyo hutakula wali wa nazi tena!
 
Mratibu wa kampeni wa cuf Julius Mtatiro ameishtumu vikali chadema kwamba kiimeenda Igunga kwa lengo la kugawa kura za Cuf.Mtatiro amesema chadema wanajua wazi hawana nguvu yoyote Igunga lakini wameamua kwenda huko ili ccm ishinde.Mtatiro amemueleza mwandishi wa habari hizi kwamba chadema wasijidanganye kuambulia hata nafasi ya pili bali watakuwa namba 3 nyuma ya ccm na cuf.Mtatiro amesema cuf wamejipanga kuwaeleza wananchi wa igunga ukweli wote kuhusu chadema ili waamue wenyewe.

SO HICHO NDICHO WATAKACHOKUWA WANAKIFANYA AU? Ina maana CUF hawatakuwa na sera katika kipindi chote cha kampeni? Vp kama CHADEMA itacjitoa ghafla...je CUF nao watajitoa kwa kukosa sera? koz sera ya ni kuipinga CHADEMA....
Hivi vyama mbona vinafanya masikhara katika matured time....Mungu wangu, this is so so scary......ina maana katika utafiti wao wote ambao CUF kama chama walioufanya kuhusiana na mahitaji ya wana-Igunga, walichogundua ni kuwa wana-Igunda wanahitaji kufahamu UKWELI kuhusu CHADEMA? Kama mlifanya research na mkaja na majibu ya aina hiyo, nina kila sababu ya kusema data zenu mmezipika.

Turudini katika mstari na tukabiliane na uhalisia, CUF kwa kauli hiyo wajitambue kuwa wao ndiyo wanastahili kujitoa na si CHADEMA, nafasi ya pili waliyoshika kipindi kile, haipo valid tena sasa hivi, walishindwa ku-maintain wajikague tu kauli zao na kufanya maamuzi mepesi ya kujitoa, nayaita mepesi kwasababu hawana cha kupoteza na hakuna mt atakeshangaa
 
@Mtatiro kwa sasa hapaswi kuonyesha woga wa namna hiyo, kwani kwa kufanya hivyo kunampa nguvu kubwa sana mpinzani wake(Chadema). Woga wa namna hiyo umewahi kufanywa uchaguzi mkuu wa 2010 na haujasaidia chochote, mfano: 1/Ubungo(CUF dhidi ya Chadema) 2/Kawe(NCCR dhidi ya Chadema) 3/Arusha(TLP dhidi ya Chadema) 4/Urais(Lipumba dhidi ya Slaa) @Kifupi CCM&CUF wanaogopa sana ujio wa Chadema kwenye uchaguzi wa Igunga, si kwa sababu tu ya mashaka ya jimbo hilo kwenda Chadema (Kutokana na kukua kwa kasi kwa Chadema), Bali uchaguzi huo utakuwa; 1/Kipimo cha nguvu(Nafasi) ya kisiasa baina ya vyama hivyo(Political rank) 2/Unaweza ukawa ndio mwanzo wa Chadema kujenga ngome kuu ya kisiasa mkoani Tabora. (Kihistoria Tabora ndio chimbuko la siasa za vyama vya CUF-Tanzania bara, CCM-Tanzania bara(TANU)
 
wajameni,<br />
huyu mtatiro ameshaeleza mara mbili hapa ndani juu ya hali halisi na shutuma anazopewa, na ameomba tuhuma hizo zithibitishwe, mleta mada ameingia mitini, hataki kuthibitisha, kwa hiyo tutamshambulia mtatiro wa watu bila hatia. In fact nasisitiza kuwa ukweli utasimama daima, kwa mtu yeyote aliyesoma mlimani na vyio vikuu vingine enzi za uongozi wa mtatiro atashangaa kuona mtatiro anakejeliwa na kudhihakiwa. Mimi binafssi namtetea mtatiro unless otherwise ikiwa proved hapa kuwa kasema hiki na kile. Good enough yeye mwenyewe kafafanua nini alichowahi kusema hasa kuhusu chadema na ametoa msimamo bila uoga wala kificho juu ya hali halisi, na kwa mtizamo wangu ameilinda hoja na ushahidi wake vizuri, so sioni kosa lake, au mtoa mada ana kisasi tusichokijua na mtatiro? au ndiyo mambo yaleyale ya kuizamisha JF ionekane inajadili hoja ambazo hazina ukweli na msingi wowote?
<br />
<br />
acha ushabiki usio na msingi wowote.Hujasoma vyombo vya habari leo kwamba jana katibu wa itikadi na uenezi ccm nape nnauye alikutana katika kikao cha siri na vijana wa cuf na ccm huko Igunga katika ukumbi wa Silver C ?.Kwanini iwe hivyo? Tena alikuwepo mpaka katibu wa cuf igunga bw. Michael Maganga.Ina maana mambo haya yote yanatokea kwa bahati mbaya na Mtatiro hajui??
 
Kweli Raisi wangu mstaafu wa udsm ameisha kabisa na ccm B yake jamani ckuzote kama una tawi sehemu na kuna viongozi watawi basi ni ruksa kuweka mgombea sasa vp MTATIRO PAKAVU ANATEREZA.

umesahau mtatiro hajawahi, kuwa rahis wa udsm, pamoja na harakati na kujifanya jasiri aliishia kuwa wazir wa mikopo, na wazir mkuu tu. na makali yake yalipungua baada ya kuhongwa na mkandala, na kuitwa kwenye vikao vingi vyenye posho.
 
Back
Top Bottom