Sijaongelea suala tajwa hapo juu,

nadhani CHADEMA wamekuja Igunga kama chama cha siasa na CUF tupo Igunga kama chama cha siasa, so ni kiasi cha kusubiri kipenga kipulizwe ndio tutajua nani alikuja kugawa kura za mwingine, nani CCM B au C n.k.

Kwa sasa ni mapema mno kupeana shutuma hizo za uongo, mimi nawaheshimu chadema kama chama cha siasa na sina ugomvi na uwepo wao Igunga.

Jambo lingine muhimu ni kuwa hii forum inaheshimika sana, kuna baadhi ya wadau wanajiunga hapa kuja kupotosha umma au ku_dogoesha watu fulani, yote haya hayatusaidii ikiwa bado watanzania wanashughulikiwa na sera za CCM. Hii ni forum muhimu sana na ninaogopa ikiwa itageuzwa kuwa mahali pa propaganda za vyama na masuala yasiyo na tija kwa jamii na taifa. Hali hii ikiendelea kufurahiwa itaharibu sura halisi ya forum na malengo yake.

Mimi ni kiongozi wa juu wa CUF na niko CUF kwa akili na utashi wangu na wakati najiunga CUF vyama vingine vyote vilikuwepo na sikuamua kujiunga navyo. Nitasimama CUF na kuijenga CUF , sitakimbilia kwenye vyama ambavyo vinaonekana vina mafanikio, nitapambana hapahapa nilipo na kuyatafuta mafanikio ya watanzania hapa hapa CUF.

Nawashukuru wote wanaoniunga mkono, wanaonikosoa kwa makusudi, bahati mbaya , kwa malengo mazuri au mabaya, sote tu watanzania na hatuna cha kuchekana.

Wasalaam,

Julius Mtatiro,

Naibu Katibu Mkuu(CUF),

TANZANIA Bara.

03/09/2011