CHADEMA wapunguze migogoro na serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA wapunguze migogoro na serikali

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Kisendi, Nov 2, 2011.

 1. K

  Kisendi JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 700
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Ndugu wana JF.
  Mimi kama Mtanzania mpenda maendeleo na nimwana CDM mwenye kadi. Napendekeza tuangalia kwa undani suala la maelendeleo na suala zima la kuwahimiza watanzania na kuwajengea uwezo wa kujiajiri badala ya kufanya malumbano kila mara. Mimi sipendezwi sana na hii hali. Sikatai kuwa Serikali inatumia nguvu sana kutatua migogoro ya Arusha lakini mpaka sasa Arusha maendeleo yamedororo sana. Je Sisi kama Watanzania tutoe mawazo ambayo yatasaidia chama chetu kiweze kusonga mbele.

  Pili tuwahamasishe watz kutopenda rushwa. Rushwa sio viongoziwa juu tu bali kuanzia kununua Sukari, Cementi, Mbao, Bati, kupata huduma maofisini ni Rushwa tu. Muuza bati mmoja alisema yeye hununua bati nyingi tu gauge 32 lakini usiku vijana hukesha wakikata bati na kuzigonga muhuri wa gauge 30. Je hii hali sisi kama wana CDM tunaionaje, Kweli Sukari imepanda kwa sababu ya Dola au kuna kitu nyuma yake.
  Tutafakari sana.


  Peoples Power
   
 2. Olengambunyi

  Olengambunyi Member

  #2
  Nov 2, 2011
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kweli mtazamo wako ni mzuri watanzania tupende kazi ila uiongozi wetu wana jukumu pia la kututengenezea njia. Kuh swala la sukari lazima kuna mchawi nyuma.
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Nov 2, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Tanzania kuna serikali au kuna wahuni tu waliojioganaizi na kujiita serekali ili waitafune inchi?
   
 4. K

  Kanyigo JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 959
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  naona ungeyaelekeza mawazo yako ccm kwani chadema si chama tawala.sikuelewi unasema chadema itengeneze nafasi za ajira ilihali ccm imeshindwa dawa ni kuiondoa ccm madarakani 2015 kwa amani ikishindikiana tutatumia kijiti kama ilivokua kwa Gaddafu.
   
 5. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #5
  Nov 2, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  mi nawashauri wabunge wa cdm waongeze juhudi ktk mchakato wa kulikomboa taifa wasiogope vitisho, jela, mabomu, Ma AKA 47 kwani ukombozi wa Taifa hili unahitaji roho ya ujasiri wa hali ya juu NGUU YA UMMA IKONYUMA YAO. peopless powerrrr
   
 6. j

  jigoku JF-Expert Member

  #6
  Nov 2, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Napaata mashaka na uanachama wako huenda wewe ni mamluki,kuna nini kinachoweza kufanyika ndani ya nchi inayoongozwa na CCM -mafisadi?wewe sio chadema,no mi napinga,hivi ya Arusha unaona Chadema wanamakosa?hivi unawezaji kusema CDM ipunguze mgogoro na serikali,hivi kwanza serikali iko wapi,wahuni hawa!
  Sijakuelewa mkuu
   
 7. W

  Wababa Senior Member

  #7
  Nov 2, 2011
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hujatulia wewe, serikali ndiyo inawachokoza cdm, tena nahic umetumwa wewe,
   
 8. M

  Molemo JF-Expert Member

  #8
  Nov 2, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  kuna mgogoro gani wa chadema na serikali? Mimi naona ubabe wa polisi dhidi ya wapinzani.Aliyekutuma mwambie akupe data vizuri
   
 9. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #9
  Nov 2, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni wananchi wenyewe, wanasahau kuwa kuamasishwa kuandamana au kugomea uongozi fulani pale mwanasiasa anakuwa yupo kazini lakini kwake kunaharibika.
   
 10. p

  politiki JF-Expert Member

  #10
  Nov 2, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  CHADEMA HATUKO KWENYE BIASHARA YA ROYAL OPPOSITION KWANI HAKUNA VIONGOZI WASTAHARABU UPANDE WA PILI .
  CCM haiwezi kwenda bila pressure my friend utakuwa unapoteza muda wako kwani kama ni kuambiwa wameshaambiwa sana na
  hawasikii dawa ya moto ni moto tu.
   
 11. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #11
  Nov 2, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  sijui malaika ganaani atumwe tena kutuambia kua tunepelekwa shimoni????????
   
 12. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #12
  Nov 2, 2011
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 0
  Acha unafiki we dada...sijui kaka..Hii nchi imefika ilipo kwa ajili ya watu kuwa waoga kudai haki zao. Mgogoro gani Chadema inauanzisha na serikali? serikali ndio inaanzisha mgogoro na CHADEMA. Kwa kumbukumbu zangu serikali ya CCM ndio imekuwa mstari wa mbele kuichokoza CHADEMA..Mf. kuingilia maandamano ya CDM na mikutano yake na kuua watu, kujichagulia meya bila kufuata kanuni na sheria..etc
  Na safari hii lazima wanafiki wote wa CCM mnaojifanya CDM lazima muaibike...Tunakwenda jino kwa jino. Kama mbaya na iwe mbaya! ku...m@maye!
   
 13. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #13
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Nayo serikali ijue majukumu yake iache kuvifuatilia vyama vya siasa hasa CDM! Kuhusu maendeleo alikuwepo Felix Mrema hapa Arusha yaani sijui alifanya nini katika miaka 10 ya amani na utulivu usio na maendeleo. Barabara Arusha hakuna hadi ikanyang'anywa hadhi ya jiji na kurejeshewa kwa masharti lakini leo Lema anaonyesha njia wajinga wanamkandia.
   
 14. k

  kulwa12 Senior Member

  #14
  Nov 2, 2011
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu iliezansha maada hii nakuunga mkono kabisa,japo kuna watu wametoa kejeli juu ya mawzo yako.lakini ukweli ni kwamba cdm ikiendelea na siasa ya namna hii haiwezi ikafika popote,kwani lazima kujua tamaduni za kitanzania ni zipi?? Watanzania wengi sana wanapenda amani,unapotumia nguvu na vurugu kudai haki,hata kama unachdai ni sahihi utaonekana hauko sahihi.naomba tujikite zaidi katika kuleta mabadfiliko ya kweli katika maisha na hali duni ya wanachi hasa katika majimbo amabayo yako chini ya cdm,kwani hiki ndio kipaumbele cha wananchi cha kwanza,sizani na siamini mtapewa kura na wananchi kuongoza taifa hili kwa kigezo cha kuonesha mnapingana kiasi gani na serikali bila hata kuonesha nyinyi mmetatua vipi matatizo ya wananchi??.mfano mzuri ni tyaliotokea leo arusha,watu sasa wanalalamika wamepigwa,vujiwa na kualibiwa mali zao,kisa tu wamekataa kushiriki maandamano ya kupinga kuwekwa ndani kwa mbunge wao.sasa hapa hii ni demokrasia gani??imeonesha mfano gani na tofauti yetu iko wapi na hao mnaowapinga?? Tuwe makini jamani,tufanye siasa za kutaka "cheap popularity" kamwe hazitafikisha chama popote!!na tuwe watu wa kukubali mawazo ya wengine,sio kila anaetoa mawazo mbadala wanaoneka katumwa au hakitakii chama mema,wengi wameshindwa harakati zao kwa kuwa na maono finyu kama haya.tupime nini kipaumbele cha watanzani kwa sasa?? Naomba tuchukue muda jinsi angel machel (kansela wa ujerumani) na chama chake walivyoweza kufanikiwa kucchukua dola,kifupi ni kwa kutoa msuluhisha mbadala kwa matatizo ya wanachi na sio kukicha kugombana na kulia kuonewa,"people's sympathy"(kulalamika kwa wananchi mnaonewa,ili mpate ghuluma yao na kupewa kura za huruma) kamwe haijawahi kukipa chama madara ila" people's confidence" (ianatokana na imani ya wananchi kwenu kwa kuonesha uwezo wa kutatua matatizo yao hata kwa madaraka madogo mlionayo)
   
 15. K

  Kanyigo JF-Expert Member

  #15
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 959
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  wewe ni ccm wa aina yake.
   
 16. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #16
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  mkuu umenena vema. mimi nafahamu kuwa chadema inakubalika ma imekubalika kwa watanzania wengi hasa mijini ila sasa haya masuala mengine ya ukorofi naona wana over do! Badala ya kwenda kuhamasisha watu vijijini wao wanang'ang'nia vurugu arusha mjini. Kwa vurugu zisizo na mwisho kuna siku watu wataichoka chadema
   
 17. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #17
  Nov 2, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni wazo zuri ila kulisisitizia kinyume chake pia ni muhimu sana......SERIKALI NA CCM YENU ACHENI KUICHOKONOA CHADEMA.......

  Ni kweli tunawanyima usingizi lakini mtakuwa mnafanya la maana kama mtaegemeza nguvu zenu kusimamia shilingi kukua na kuhakikisha wananchi wenu wanamudu maisha na kuhakikisha usalama wa wananchi wenu badala ya kutumia nguvu nyingi kuwafuatilia fuatilia wakina Lema na CDM kwa ujumla
   
 18. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #18
  Nov 2, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Sawa!Lakini na serikali pia wapunguze migogoro na CHADEMA!
   
 19. K

  Kisendi JF-Expert Member

  #19
  Nov 3, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 700
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Sio mamluki hata. Mawazo yangu ni kuwa hivi hatuwezi kufanya njia nyingine kuwadhbiti hawa mafisadi badala ya kutumia nguvu. Maana Arusha mpaka leo hakuna kinachoendelea. Lema nampenda na nimchapa kazi. kwa upande wa CCM wanamakosa makubwa sana kuhusu kumkamata lema maana hakuwa na kosa kuongea na Wapenzi wa CDM, Nasema tujaribu kutumia falsafa nyingine na Wakazi wa Arusha tupunguze kumzonga Lema ili mambo yake yaishe ajalibu kufanya ushawishi wa maendeleo katika Jimbo lake. Mawazo yangu lakini yanaweza kuwa na mapungufu.
   
 20. K

  Kisendi JF-Expert Member

  #20
  Nov 3, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 700
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Nashukuru ndugu, Maana mimi nimetoa mawazobaadhi ya Watz humu nao ni siasa tu kila kitu tufike mahali tujaribu kuangalia. Ili tuitoe CCM madarakani tuhitaji strategy na kupata katiba mpya. Mimi binafsi nasema umeniunga mkono nami niko nawe kabisa kimawazo. Mimi ni CDM kabisa na nina kadi yangu. So haya mawazo viongozi wetu wayafanyie Kazi. Mh Dr Slaa hebu tusaidie, Tutumie mbinu mbadala kutatua matatizo. Lini Arusha watafuatilia hata miradi ya Maendeleo kama Kila siku Lema yupo Polisi. Najua CCM wanatumia nguvu sana lakini kama wananchi tayari wanakipenda CDM kilichobaki ni kupata wana CDM wengi huko vijijini na mijini, Wasomi na wasiowasomi ili 2015 tushike nchi.

  Ni hayo.
   
Loading...