CHADEMA wapinga muswada wa mchakato wa katiba mpya

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa amesema Chadema haitambui mswada wa mchakato wa katiba mpya kwani umechakachuliwa na bado umempa madaraka makubwa Rais kuingilia mchakato huo. Dr Slaa ameonya kama serikali haitasalimu amri na kubadilisha basi Chadema itawaongoza watanzania kuupinga kwa njia zote itakazoona zinafaa.

SOURCE-ITV SAA 2 HABARI
 
Imepokelewa mkuu na tuansubiri tu kuliunga mkono.na kwa kweli tusipoungana na kutoa sauti kali ya umma hawa watu wanatuangamiza
 
Nimevutiwa mno na huu mstari ..."itawaongoza watanzania kupinga kwa njia yeyote watakayoona inafaa " inaonyesha uwezo wa kufanya chochote dhidi ya serikali upo ila kilichopo ni uvumilivu
 
Naomba nieleweke, tusitegemee katiba mpya inayo kidhi hali ya sasa chini ya uongozi wa selikali ya ccm, ccm na selikali yao kama wataongoza upatikanaji wa katiba nzuri watakuwa wamejiondoa madarakani!
 
Hivi hawa watu wanaugua ugonjwa wa akili au wana mapepo?. Ni mara ngapi wananchi wamesema wanataka kupunguza madaraka ya rais? Kwa nini hawasikii? Draft ya kwanza imekataliwa kwa makosa haya haya ya sasa, wanataka wananchi wafanye nini? waingie barabarani?

Muda wa kufunika kombe mwanaharamu apite haupo, miaka 50 tuna uzoefu wa kutosha. Warekebishe huo mswada au wasubiri Tahriri Square.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Nami naunga mkono hoja.

............Tukumbushane lakini, hivi tumeshaandaa mswada mbadala ambao ndiyo utaongoza hoja kule mjengoni na baadae kwa wananchi (itakaposhindikana mjengoni)?

.......Je, tuna rasimu ya Katiba tuitakayo kwa ajili ya uamsho wa umma?
 
Hata kama ulikuwa hautaki kukasirika kwa kweli unakasirika. Kombani, why use Masaburi?
 
Nami naunga mkono hoja.

............Tukumbushane lakini, hivi tumeshaandaa mswada mbadala ambao ndiyo utaongoza hoja kule mjengoni na baadae kwa wananchi (itakaposhindikana mjengoni)?

.......Je, tuna rasimu ya Katiba tuitakayo kwa ajili ya uamsho wa umma?

UPO. Hatakama haupo utapatikana humohumo. Watu tunasoma na kuchuja maelezo.
 
Back
Top Bottom