CHADEMA wanajua kutengeneza ajenda, Katiba Mpya imekuwa ajenda kuu ya Taifa

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Baada ya uchaguzi mkuu uliovurugwa, think tank ya Chadema iliona njia nzuri ya kulazimisha hayo yasitokee tena ni kuanzisha vuguvugu la kudai katiba mpya. Leo kila chama ajenda kuu ni katiba mpya.

Kwa hali ilivyokuwa miaka 5 iliyopita nani alijua leo rais atahudhuria sherehe ya ‘Sugu’, nani alijua leo Lissu atalipwa stahiki zake zote, nani alijua leo Mbowe atakaribishwa ikulu, nani alijua leo rais atakubali kukutana na Chadema.

Tume zimeundwa vikao vimefanyika na wote wanakubali umuhimu wa kuwa na katiba mpya, tofauti iliyopo ni lini mchakato uanze, kuna wanaotaka uanze sasa kuna wanaotaka uanze baada ya uchaguzi, kuna wale wanaosema Tumehuru kuelekea Katiba mpya. Hawa wote ni wafuasi wa mawazo ya Chadema.

Credit kwa Chadema, fikiria ni chama gani kikuu cha upinzani kilichodumu kwa zaidi ya miaka 20 bila kufa, NCCR, CUF viliwahi kuwa vyama vikuu vya upinzani lkn kutokana na misukosuko ya chama tawala na usaliti wa ndani havikudumu muda mrefu vikafa. Think Tank ya Chadema ni ya hali ya juu sana tusiipuuze.
 
Inawezekana ikawa kweli japo sidhani kama BiM atawapa katiba mpya, yaani atasukuma muda bypass mpaka kipindi chake kipite!
 
Kinachotakiwa ni pressure na determination ya wananchi.
Wananchi washachoka saizi, wanapambana na maisha yao wapate ugali wa kila siku, wewe ukawaambie wapambanie katiba watakua na hayo mawazo kweli?
 
Wananchi washachoka saizi, wanapambana na maisha yao wapate ugali wa kila siku, wewe ukawaambie wapambanie katiba watakua na hayo mawazo kweli?
Sio lazima watanzania wote wahusike wakijitokeza wachache kama wanaharakati, vyama vya siasa, wanatosha.
 
Hili suala ni la watu wachache sana na siyo la wananchi kwa wingi wao na hao wachache tayari wapo mikononi mwa mama kesha waweka kiganjani hivyo hawafurukuti tena ona sasa hivi ni kugonga cheers tu hakuna cha vuguvugu tena mama kajuwa kucgheza na akili za wapinzani sana mama kongole sana

Miaka mitano tena na mama
 
Kinachotakiwa ni pressure na determination ya wananchi.
Wananchi wa wapi? Pita tu hata mtaani kwako ufanye katafiti kadogo tu, wahoji watu 200 (bibi+babu 100, Vijana ke+me 100) kuhusu umuhimu wa katiba mpya, utaishia kucheka

Huku chini Wananchi hili jambo hawana mda nalo, hili jambo lipo mtandaoni na linajadiliwa na watu wachache sana Kati ya watanzania M60.

Kinachopaswa kufanyika ni watanzania wapewe elimu kuhusu katiba mpya, wakiitaka wao utaona tu, ila hizi harakati za sasa naziona kama za kutafutia ulaji tu
 
HILI SUALA NI LA WATU WACHACHE SANA NA SIYO LA WANANCHI KWA WINGI WAO NA HAO WACHACHE TAYARI WAPO MIKONONI MWA MAMA KESHA WAWEKA KIGANJANI HIVYO HAWAFURUKUTI TENA ONA SASA HIVI NI KUGONGA CHEERS TU HAKUNA CHA VUGUVUGU TENA MAMA KAJUWA KUCGHEZA NA AKILI ZA WAPINZANI SANA MAMA KONGOLE SANA
MIAKA MITANO TENA NA MAMA
 
Wananchi wawapi???? pita tu hata mtaani kwako ufanye katafiti kadogo tu, wahoji watu 200 ( bibi+babu 100, Vijana ke+me 100) kuhusu umuhimu wa katiba mpya, utaishia kucheka...
hahaha yaani watu wa mitandaoni wanajionaga kama wapo wengi sana au kama wanawakilisha taifa kumbe kuna wengine hata jf hawijui hawajui kama kuna watu wanawajumuisha humu jf
 
Wananchi wawapi???? pita tu hata mtaani kwako ufanye katafiti kadogo tu, wahoji watu 200 ( bibi+babu 100, Vijana ke+me 100) kuhusu umuhimu wa katiba mpya...
Kwahiyo rais aliunda Kikosi Kazi cha mitandaoni.
 
hahaha yaani watu wa mitandaoni wanajionaga kama wapo wengi sana au kama wanawakilisha taifa kumbe kuna wengine hata jf hawijui hawajui kama kuna watu wanawajumuisha humu jf
Na rais ni mtu wa mitandaoni?

BB1B0BBC-AA17-4C3D-AC3C-EA5C60BB32A0.jpeg
 
Wananchi wawapi???? pita tu hata mtaani kwako ufanye katafiti kadogo tu, wahoji watu 200 ( bibi+babu 100, Vijana ke+me 100) kuhusu umuhimu wa katiba mpya, utaishia kucheka

Huku chini Wananchi hili jambo hawana mda nalo, hili jambo lipo mtandaoni na linajadiliwa na watu wachache sana Kati ya watanzania M60.

Kinachopaswa kufanyika ni watanzania wapewe elimu kuhusu katiba mpya, wakiitaka wao utaona tu, ila hizi harakati za sasa naziona kama za kutafutia ulaji tu
Kwani Kati ya hao mil 60 wenye elimu nzuri ya kuchanganua masuala ni wangapi.

We unataka hata wajinga waijadili katiba badala ya kupewa elimu ya uraia ndipo waijue katiba.
 
Wananchi wawapi???? pita tu hata mtaani kwako ufanye katafiti kadogo tu, wahoji watu 200 ( bibi+babu 100, Vijana ke+me 100) kuhusu umuhimu wa katiba mpya, utaishia kucheka

Huku chini Wananchi hili jambo hawana mda nalo, hili jambo lipo mtandaoni na linajadiliwa na watu wachache sana Kati ya watanzania M60.

Kinachopaswa kufanyika ni watanzania wapewe elimu kuhusu katiba mpya, wakiitaka wao utaona tu, ila hizi harakati za sasa naziona kama za kutafutia ulaji tu
Hata katiba wanaijua? Wanaihitaji?

Wanahitaji kupunguzwa kwa bei za bidhaa na huduma na kuboreshwa kwa huduma za jamii na miundombinu yake.

Mbowe na wachaga wenzie ndio wahiyaji wa hiyo katiba mpya
 
Hata katiba wanaijua? Wanaihitaji?

Wanahitaji kupunguzwa kwa bei za bidhaa na huduma na kuboreshwa kwa huduma za jamii na miundombinu yake.

Mbowe na wachaga wenzie ndio wahiyaji wa hiyo katiba mpya
Hujui katiba ndiyo sheria mama wa hizo kanuni ndogo ndogo unazotaka wananchi wafanyiwe.
 
Hawa wanasema wao ndiyo walikuwa wa kwanza kuanzisha ajenda ya katiba mpya
 
Attachments

  • 92092D50-B84B-4A14-8893-8035EA4D66F7.jpeg
    92092D50-B84B-4A14-8893-8035EA4D66F7.jpeg
    41.3 KB · Views: 6
Hili suala ni la watu wachache sana na siyo la wananchi kwa wingi wao na hao wachache tayari wapo mikononi mwa mama kesha waweka kiganjani hivyo hawafurukuti tena ona sasa hivi ni kugonga cheers tu hakuna cha vuguvugu tena mama kajuwa kucgheza na akili za wapinzani sana mama kongole sana

Miaka mitano tena na mama
Vita yoyote humalizwa kwa mazungumzo, hecco Mbowe
 
Back
Top Bottom