Watanzania wenzangu wana
CCM wenzangu leo hii napenda
kutoa ukweli mchungu ambao
wenzetu hawataki kuusema
aidha kwa makusudi ili liwalo
na liwe, au kwa woga wa
madaraka,au kuogopa
kuwaudhi wakubwa au kwa
faida ya matumbo yao
wasiharibu nafasi na vyeo vyao
hivyo wote tupo kimya kila mtu
anamtazame mwenzake asijue
lakufanya tupo katika
mwanguko mkubwa wa chama
chetu cha CCM.
Wana ccm wenzangu leo hii
chama chetu hakina mkubwa
wala mdogo wote tumekuwa
kambale huu ni mwanguko
mkubwa mfano ni bungeni
wabunge wetu ndiyo
wamekuwa wakijibu tuhuma
za serikali badala ya kuibana
serikali huu ni mwanguko ulio
dhahiri.
Wana ccm wenzangu leo
wabunge wetu wameamua
kuwaachia vijana mahiri wa
upinzani kuwasemea wananchi
na wao wamebaki kupiga
kelele za ndiyo na kutetea uovu
wa serikali huu ni mwanguko
mkubwa kwa chama chetu cha
ccm.
Chama chetu bungeni huwezi
kumtofautisha mbunge na
waziri wote wamekuwa
watetezi wa maovu ya serikali
hili ni mwanguko mkubwa
wana ccm wenzangu.
Vijana wetu mahiri wengine
kama wachumi nambari moja
kina Mwigulu mchemba yeye
akisimama ananza
kutukana ,CHADEMA, DR slaa
ambaye hata bungeni
hayupo ,MBOWE na wapinzani
wakati vijana wa upinzani
wanaogelea kwenye hoja na
matatizo makubwa ya
wananchi wana CCM wenzangu
hili ni anguko kubwa ni
mwanguko mkubwa
Wana CCM wenzangu mawaziri
wetu wamefikia hawana hata
uwezo wakujibu maswali
kuanzia waziri mkuu na
mawaziri wake hivi sasa
wanatumia asilimia 90 ya mda
wao kuwa attack wapinzani
badala ya kujibu hoja murua na
maridadi za wapinzani huu ni
mwanguko mkubwa wana ccm
wenzangu .
Wana CCM wenzangu spika na
naibu wake wanasaidia kukiua
chama chetu kwa kuwawekea
kinga wajibu maswali ya umma
hasa mawaziri kwa kuruhusu
majibu yasiyokidhi haja ya
wauliza maswali huu ni
mwanguko mkubwa kwa
chama chetu.
Wana ccm wenzangu spika
wetu kupendelea chama chetu
kwa wazi kabisa na naibu spika
kuonyesha waziwazi
hawapendi upinzani huko ni
kuwapa wapinzani nguvu na
mashabiki wengi nje ya uwanja
na kutudhoofisha chama chetu
huu ni mwanguko mkubwa
wana ccm wenzangu.
Wana ccm wenzangu wabunge
wetu hawawezi kujenga hoja
tena kazi yao ni kupiga makofi
na kuitikia ndiyoooooooooo....
HUU NI MWANGUKO MKUBWA
WANA CCM WENZANGU.
Hata pale spika anapopunguza
nguvu za upinzani kwa kuwapa
adhabu eti kwa kuomba
muongozo lakini wabunge
wetu na mawaziri wetu bado
hawawezi kukabili na kujibu
hoja za wapinzani wanne tu
kama ilivyokuwa alhamisi hoja
ya wizara ya utawala bora ya
waziri wassira na Kombani,
mawaziri karibu sita
mwanasheria mkuu na
wabunge wote wa CCM
walishindwa kujibu hoja za
msingi kabisa toka kwa vijana
mahiri wa upinzani
mh.Mkosamali, HAlima Mdee,
Mnyika na mzee wao professor
Kahigi kwa walioshuhudia
chama chetu kilishindwa kujibu
hoja za msingi wabunge wetu
na mawaziri wetu walishinda
hoja ile kwa kura za ndiyoooo
huo ni Mwanguko mkubwa
wana CCM.
Wana CCM wenzangu ninaona
mwanguko wa chama chetu ni
kama UNIP ya mzee wetu
KAUNDA au KANU ya mzee wetu
MOI Tupo katika mwanguko
mkubwa.
Wana ccm wenzangu chama
chetu kinapowatetea
watumishi waandamizi kabisa
wa UMMA wa vyombo vya
usalama wametuhumiwa katika
kashfa kubwa kabisa na
kuwaachia waendelee na kazi
wakiwa katika kashfa nzito
namna hiyo huo ni mwanguko
mkubwa wa chama chetu na
serkali yetu pia.
Wana ccm wenzangu inapofikia
chama hakiwezi kufanya
mkutano bila kuwahonga
wanachama wetu kwa kanga
kofia na kuwanunulia vyakula
huo ni mwanguko mkubwa
tena mwanguko mbaya sana.
Wana ccm wenzangu inapofikia
ili kufanya mikutano inabidi tu
import watu kwa maroli
kuwaleta sehemu ya mkutano
ili tujaze uwanja au ukumbi
huku ni kujidanganya na hili ni
anguko ni anguko kubwa sana
huu ni mwanaguko ulio
dhahiri.
Wana ccm wenzangu inapofikia
hoja ya mbunge mmoja wa
upinzani inajibiwa na mawaziri
na wabunge wote wa chama
chetu na bado haijitoshelezi
hilo ni anguko ni mwanguko
mkubwa.
Wana ccm wenzangu tupo
katika mwanguko mkubwa
mwanguko mkubwa
mwanguko mkubwa sana....
Wana ccm wenzangu hatuna
wabunge wawakilishi wa
wananchi na nchi tuna makada
ambao kazi yao ni kuwajibu
wapinzani hata katika zile hoja
za msingi kabisa na za wazi
wabunge wetu wao kazi ni
kuwajibia mawaziri huwezi
kujua mbunge wa chama chetu
ni yupi na waziri we serikali ni
yupi wote wamekuwa
wakiijibia serikali hili ni anguko
huu ni mwanguko mkubwa na
2015 utakuwa ni mwanguko
mkubwa sababu wananchi
watataka kupeleka wabunge
watetezi wao na si watetezi wa
dola.
Wana ccm wenzangu huu ni
mwanguko mkubwa chama
kubakia na wabunge wawili tu
wawakilishi wa wananchi
chama kuwakilishwa na Deo
filikunjombe na Kange lugola
pekee yao hili ni anguko ni
anguko kubwa huu ni
mwanguko wote tu mashahidi
wa mashujaa wetu hawa
wanavyotetea maslahi ya umma
na siyo watu wa nddiyooo .
Tupo katika mwanguko wana
ccm wenzangu chama chetu
kinaangushwa kwa maslahi ya
kwao tumekubali kuangushwa
huu ni mwanguko mkubwa.
wana CCM wenzangu wabunge
wetu wamechanganyikiwa
kabisa husimama kwa kuponda
hoja zilizotolewa na upinzani
tena zile zenye maslahi kwa
Taifa, hapo hapo anaunga
mkono hoja kwa asilimia mia
moja 100% lakini hapo hapo
huitoa kasoro na kuonyesha
mapungufu ya hoja hiyo wana
ccm wenzangu kama kitu kina
kasoro kinaweza kuungwa
mkono mia kwa mia huu ni
mwanguko mkubwa kwa
chama chetu.
Wana ccm wenzangu
kuwanyima wapinzani viwanja
vya kusemea kuwazuia
mikutano yao bila sababu huku
ni kuwaunganisha zaidi
wapinzani na wananchi na
huku ni kujihujumu wenyewe
wanaofanya hivyo wanasaidia
huu mwanguko na
wamedhamilia kutuangusha.
Wana ccm wenzangu huko
mawilayani kuwatumia ma
RPC,OCD ,RC's na maDCkuzuia
mikutano ya wapinzani
kunajaza sana mori wananchi
kuhisi wanahitaji ukombozi wa
kuwatimua hao wakoloni
weusi na kufanya chama chetu
kizidi kuchukiwa hawa watu
hawatusaidii ni sehemu ya
mwanguko wetu.
Wana ccm wenzangu viongozi
wetu wamekuwa ni kundi la
kulindana hata inapotakiwa
mmojawapo kuwajibika kwa
heshima ya chama na serikali
yetu hawako tayari kufanya na
watatea kwa nguvu zote huu ni
mwanguko tena mwanguko
mkubwa.
Inapofikia waziri mkuu
anatumia 90%ya mda wake
kumsema tu mbowe na
chadema badala yakueleza
serikali imefanya na itafanya
nini huo ni mwanguko tena ni
mwanguko mkubwa na kama
waziri mkuu ameanguka basi
ndiyo wote tumeanguka tupo
katika mwanguko.
Wana ccm wenzangu Kama
naibu katibu mkuu wetu
amekuwa akihusika kama
inavyosemekana kuhonga na
kununua wapinzani akifikiri
ndiyo silaha ya ushindi wetu
huko mbele hili ni anguko ni
anguko dhahiri ni anguko lililo
kubwa na kama tunataka
kujenga taswira ya chama
chetu kuepusha huu
mwanguko basi tumpatie kazi
nyingine sababu hana heshima
tena mbele ya wananchi huu ni
mwanguko.
Wana ccm viomgozi wetu hivi
sasa hawana uwezo wa
kushawishi wanachama wapya
badala ya kurudisha imanai na
kuendeleza misingi ya chama
wao sasa hivi ni kurubuni
wapinzani na kuwahonga
viongozi wa upinzani na
kitembea mbele uetu na makapi
ya viongozi waliofukukuzwa na
vyama vingine hii ni kuonyesha
tumefika mwisho tupo katika
mwanguko mwanguko ulio
dhahiri huu ni mwanguko.
Wana ccm wenzangu tupo
wengi tunaona mwanguko huu
lakini tunapotoa ushauri
hausikilizwi sababu chama
kimekuwa genge la watu fulani
hawataki mawazo nje huu ni
mwanguko mwanguko
uliodhahiri.
Wana ccm wenzangu tunajenga
chama saa ngapi tunajibu kero
za wananchi na kuzitatua saa
ngapi kama kila ziara za chama
utasikia inatajwa chadema na
viongozi wakati chama kina
mambo ya msingi
hayajatekelezwa kwa miaka 50
sasa na hayana majibu sisi kila
siku ni kuimba chadema, DR
slaa ,mbowe nk huu ni
mwanguko wana ccm
wenzangu.
Wana ccm wenzangu pimeni
wenyewe uelewa wa wabunge
wa upinzani hotuba zao, hoja
zao linganisha na wabunge
wetu na mawaziri wetu mtajua
kama kweli tupo katika
mwanguko.
Wana ccm wenzangu
wapinzani wana sema mbunge
wao mmoja ni sawa na
wabunge wa ccm 40 mimi ni
mwana ccm mwandamizi
nathubutu kusema wabunge
wetu 40 na mawaziri watano
ndiyo sawa na mbunge mmoja
wa upinzani mwenye kubisha
aangalie bunge kwa uangalifu
na apime hoja za pande mbili
atagundua tupo katika
mwanguko.
Wana ccm wenzangu Maneno
haya yatawakera wengi hasa
wale wenzetu wanafiki wenye
kuogopa ukweli kwa maslahi
yao huu ni mkweli mchungu na
lazima usemwe na wenye
uchungu sababu tupo katika
mwanguko mbaya.
Wana ccm wenzangu leo chama
chetu kinazunguka nchi nzima
kinasema CHADEMA ni chama
cha kidini na kikabila wakati
chama hiki kina wabunge toka
mbeya, iringa , biharamulo,
Mwanza, kigoma, maswa,dar es
salaam kina wabunge dini zote
kutuaminisha uongo wa
dhahiri na kutufanya
wanachama sisi ni ndondocha
huu ni mwanguko mwanguko
uliodhahiri.
Wana ccm wenzangu
mwanguko huu hautazuiwa na
polisi, wala vyombo vya
usalama kama hatutakubari
ukweli huu ni mwanguko
mwanguko ulio dhahiri.
Watanzania wenzangu
naombeni tujadili mwanguko
huu katika hali ya utulivu bila
kashfa sababu huu ni
mwanguko mkubwa
uliodhahiri namalizia kwa
kusema tupo katika
mwanguko.
Karibuni tujadili...kwahisani ya
Burigi