CHADEMA wamtolea uvivu Gwajima

CHADEMA wamtolea uvivu Gwajima

Pole sana, hate ni ugonjwa mbaya sana utakusababishia kijeba cha roho, you may wish me dead ila kila ukiniona naendelea ku survive, utaumia roho, hivyo the best way kwao ni just ignore me, wish as if I don't exist, ukibonyeza ignore button huwezi tena kuona mabandiko yangu wala posts zangu. Uwe na amani na ubarikiwe sana.
P
NCV -next Corona victim
 
Ni kama watu wa somangila Walivyosema Hayo ndio aliyafanya KIBWETERE na Hakika watu Walikufa, na MUNGU muumbaji alishaonya na Kuacha Watu wakaangamia kwa ku kosa Maarifa, Hosea 4:6
Mpendwa Paschal Ukikosa maarifa MUNGU hashughuliki na wewe utaangamia bila msaada,yalishatokea na tukashuhudia kushabikia ujinga pia ni Kukosa MAARIFA.
Ushauri:-
Viongozi wa dini waache kuhadaa Waumini wao kwa kutaka SADAKA zao, Baadhi ya dini zimekuwa na VIBWEKA vinvyogharimu Maisha ya waumini Kijinga kabisa. Aliwahi kuibuka BABU akashangaza Dunia kwa kurundika Watu eti anatibu Ukimwi mpaka leo hakuna ushahidi wa mtu hata mmoja aliyepona na Ukimwi upo na unaua kila siku, Huyo Ghwajima mbona kashindwa kuweka uzio wa moto v/s ukimwi aje kuiweza CORONA?,
HITIMISHO;-
Tuwe makini na wachungaji /Viongozi wa Dini UCHWARA.
Ujinga wa mtu ni fursa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gwajima mtu wake ni lowasa, sasa lowasa karudi ccm hivyo na yeye hana budi kumfuata, ndio maana toka lowasa aondoke cdm uelekeo ya mashambulizi umegeukia upande mwingine, na hili sio kwa gwajima tu, ni wengi sana, kama ukichunguza kwa makini utaona wanaanza kuishambulia cdm tofauti na hapo awali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo ndiyo ukweli
Gwajima mtu wake ni lowasa, sasa lowasa karudi ccm hivyo na yeye hana budi kumfuata, ndio maana toka lowasa aondoke cdm uelekeo ya mashambulizi umegeukia upande mwingine, na hili sio kwa gwajima tu, ni wengi sana, kama ukichunguza kwa makini utaona wanaanza kuishambulia cdm tofauti na hapo awali.

Sent using Jamii Forums mobile app

In God we Trust
 
Duh...!.
Kama hata Kamati tendaji ya tawi tuu inaweza kulaani, then Chadema kila mtu ni kambale ana sharubu.

Askofu Gwajima kaomba kibali kwa PM, anakwenda kumaliza tatizo la Corona kwa kuponyesha wagonjwa wote mahospitalini waliolazwa kwa Corona.

Askofu Gwajima Atoa Kali, Aomba Kibali Serikalini Kuponya Wagonjwa wa Corona Mahospitalini, kwa Kutumia Miujiza ya Nguvu za Mungu!. - JamiiForums
P

Gwajima ni mfanya biashara mzuri sana wa kwenye idara ya dini. Anajua kuvutia watu na kuuza vitu lakini bahati mbaya sana hana kipaji chochote cha uponyaji. Nimemekutana na wachungaji wengi sana kutoka TZ na hata Gwajima nilikuwa naye wakati alipokuja kununua ndege yake ile bila walimzi wala wapambe ni mfanyabiashara mzuri sana sana. Ubaya kuna watu wanaamini anaweza kwenda mochwari na kufufua lakini si kweli. Mwalimu mwakasege yeye kweli ana maono ambayo hayaelezeki naye nilikutana naye Chicago kwenye mkutano wa DICOTA wa diaspora. Vilevile kuna manabii ambao ni kweli Mungu kawapa bahati ya unabii lakini sio uponyaji.

Huyu mtumishi anapenda kujiongeza kuliko uwezo wake lakini nasifia sana uwezo wa biashara zake.
 
Tena mkubwa tu
Mtu wa Mungu nani alimpa "utu wa Mungu"? Unajitangaza kuwa wewe ni mtu wa Mungu au watu wanakutangaza?
Hawezi kwenda maana anajua fika rohoni mwake kuwa ni utapeli!

In God we Trust
 
Chadema wapigweeee!!! Huyo ni Gwajima, ndio Maana Kwa sasa Chadema wameishiwa busala, wanaamua maamzi ya kitoto mengi
 
Kamati tendaji viongozi wa matawi wanachama wapenzi na mashabiki wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kata ya Somangila

Kwa pamoja tunalaani kitendo cha mchungaji Gwajima cha kuwashambulia viongozi wa CHADEMA katika madhabahu ya kanisa lake la ufufuo na uzima Jumapili iliyopita!

Aidha tunapenda kumjulisha Gwajima kwamba viongozi wetu wa CHADEMA wanamwamini Mungu na kumtumaini pia!
Pamoja na hayo viongozi wetu hawana desturi ya kuangamizwa kisa kukosa maarifa!

CHADEMA tunaamini kwamba kama tunaweza kulala katika vyandarua vyenye dawa ili kujilinda na malaria vivyo hivyo kuna haja ya kujikinga na vyanzo vya corona! Kama malaria haizungushiwi uzio wa moto kadhalika na corona haitazungushiwa!

Viongozi wa CHADEMA kwakujua umhimu wa kuchukua tahadhari walipendekeza wabunge wote wapimwe corona lakini hakuna utekelezaji uliofanyika kisa chuki binafsi dhidi ya upinzani hususani CHADEMA!

Mchungaji Gwajima wewe kinacho kukera ni kukosa moyo wa huruma kwa watanzania ambao wako wanakufa kwa corona nanyi mkisingizia mapenzi ya Mungu!

Uliposikia kwamba makanisa yafungwe kwa muda wewe akili yako ikawazia sadaka na mafungu ya kumi kuliko uhai wa waumini wake!

Dhana ya Gwajima ya kuwahadaa waumini wake kwamba amewazungushia uzio wa moto ili wasipatwe na corona nyumayake kuna roho ya Kibwetele!

Sisi kama CHADEMA kata ya Somangila tunamtaka Gwajima azungushie uzio huo wa moto katika shule na vyuo ili watoto wetu waendelee na masomo!

Aidha CHADEMA kata ya Somangila tuna mashaka na uchungaji wa Gwajima kwamba maana hata kauli mbiuyake ya WAPIGWE EE! Sio ya kichungaji!

Mbaya zaidi ni kwamba inashabihiana na matamko ya viongozi wa serikali ya chama cha Mapinduzi kuliagiza jeshi la polisi kuwapiga wapinzani hususani CHADEMA [emoji3577]

Gwajima tangu watanzania walipo anza kupotea kutekwa kupigwa risasi kupewa kesi kuzuia shughuli halali za kisiasa ikiwa ni pamoja na mikutano mbona hukusimama na kukemea wakati unajua kabisa kwamba hiyo ni dhuluma??
Hakika Gwajima wewe ni mchungaji wa mshahara kondoo unawakamua lakini hujali maisha yao dhidi ya corona! Yoh 10:12

Mwisho kabisa CHADEMA [emoji3577] kata ya Somangila tuna wasihi waumini wa kanisa la ufufuo na uzima mwe macho corona ipo na ina ua chukueni hadhari hakuna uzio wa moto mlio zungushiwa mtakufa kizembe kwa kukosa maarifa!

By Afisa habari Somangila

View attachment 1446180

In God we Trust
Hiyo picha kushoto ndivyo mnavyojikinga na Corona! Ahahahahahah! Kuwa nyumbu kuna raha yake!
 
Back
Top Bottom