CHADEMA wamtolea uvivu Gwajima

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
121,918
95,201
Kamati tendaji viongozi wa matawi wanachama wapenzi na mashabiki wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kata ya Somangila

Kwa pamoja tunalaani kitendo cha mchungaji Gwajima cha kuwashambulia viongozi wa CHADEMA katika madhabahu ya kanisa lake la ufufuo na uzima Jumapili iliyopita!

Aidha tunapenda kumjulisha Gwajima kwamba viongozi wetu wa CHADEMA wanamwamini Mungu na kumtumaini pia!
Pamoja na hayo viongozi wetu hawana desturi ya kuangamizwa kisa kukosa maarifa!

CHADEMA tunaamini kwamba kama tunaweza kulala katika vyandarua vyenye dawa ili kujilinda na malaria vivyo hivyo kuna haja ya kujikinga na vyanzo vya corona! Kama malaria haizungushiwi uzio wa moto kadhalika na corona haitazungushiwa!

Viongozi wa CHADEMA kwakujua umhimu wa kuchukua tahadhari walipendekeza wabunge wote wapimwe corona lakini hakuna utekelezaji uliofanyika kisa chuki binafsi dhidi ya upinzani hususani CHADEMA!

Mchungaji Gwajima wewe kinacho kukera ni kukosa moyo wa huruma kwa watanzania ambao wako wanakufa kwa corona nanyi mkisingizia mapenzi ya Mungu!

Uliposikia kwamba makanisa yafungwe kwa muda wewe akili yako ikawazia sadaka na mafungu ya kumi kuliko uhai wa waumini wake!

Dhana ya Gwajima ya kuwahadaa waumini wake kwamba amewazungushia uzio wa moto ili wasipatwe na corona nyumayake kuna roho ya Kibwetele!

Sisi kama CHADEMA kata ya Somangila tunamtaka Gwajima azungushie uzio huo wa moto katika shule na vyuo ili watoto wetu waendelee na masomo!

Aidha CHADEMA kata ya Somangila tuna mashaka na uchungaji wa Gwajima kwamba maana hata kauli mbiuyake ya WAPIGWE EE! Sio ya kichungaji!

Mbaya zaidi ni kwamba inashabihiana na matamko ya viongozi wa serikali ya chama cha Mapinduzi kuliagiza jeshi la polisi kuwapiga wapinzani hususani CHADEMA

Gwajima tangu watanzania walipo anza kupotea kutekwa kupigwa risasi kupewa kesi kuzuia shughuli halali za kisiasa ikiwa ni pamoja na mikutano mbona hukusimama na kukemea wakati unajua kabisa kwamba hiyo ni dhuluma??
Hakika Gwajima wewe ni mchungaji wa mshahara kondoo unawakamua lakini hujali maisha yao dhidi ya corona! Yoh 10:12

Mwisho kabisa CHADEMA kata ya Somangila tuna wasihi waumini wa kanisa la ufufuo na uzima mwe macho corona ipo na ina ua chukueni hadhari hakuna uzio wa moto mlio zungushiwa mtakufa kizembe kwa kukosa maarifa!

By Afisa habari Somangila

Screenshot_20200510-205025.jpeg


In God we Trust
 
Duh...!.
Kama hata Kamati tendaji ya tawi tuu inaweza kulaani, then Chadema kila mtu ni kambale ana sharubu.

Askofu Gwajima kaomba kibali kwa PM, anakwenda kumaliza tatizo la Corona kwa kuponyesha wagonjwa wote mahospitalini waliolazwa kwa Corona.
P
Ngwajima siyo mchungaji halisi, ni muhuni fulani tu.
Hata akiwa anahubiri utaona uhuni fulani tu ivi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu ni miongoni mwa watu ambao huwa siwamiini katika kazi zao. Maana nilishashiriki kazi na mchungaji wake mmoja. Ni shida tu.
 
Nikikumbuka wkt Gwajima anashangiliwa humu akiwa na ugomvi na Makonda haaaa haaaa kweli binadamu hatari sana! Ilikuwa mpaka watu wanapanga jpili flani wataenda kusali kwa Gwajima washangilie akimpolomoshea matusi Makonda Leo naona iko upande wao sasa!

Wale tusio na upande wa kushangilia tunawaangalia tu!

Sent using kidole gumba
 
Duh...!.
Kama hata Kamati tendaji ya tawi tuu inaweza kulaani, then Chadema kila mtu ni kambale ana sharubu.

Askofu Gwajima kaomba kibali kwa PM, anakwenda kumaliza tatizo la Corona kwa kuponyesha wagonjwa wote mahospitalini waliolazwa kwa Corona.
P
Kwa maombi au vipi.

Hebu ikiwa haimpati mwambie asichukue tahadhari/asijilinde au akae na mwenye nayo.

Lakin kusema hainipati kwasababu yupo mbali nayo asijidanganye na uwezo huwo hana hana na hatakuwa nao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnisaidie tu wadau, hivi wanaosali kwa gwajima wote ni wanachama wa CCM?

Sent using Jamii Forums mobile app
Uanachama wao huwa unategemea Gwajima kipindi hicho anashabikia chama gani. Wakati Bob Gwaji yuko chadema nao wote walisapoti mageuzi ila baada ya Bob kunyooshwa na kurudi chama kubwa ccm nao wamerudi mazima. Wao wanaangalia mpakwa mafuta anasemaje. Kesho akiwa TLP wao watasapoti TLP hata KANU au FRELIMO hawana tatizo kusapoti ilimradi tu baba mchungaji yuko wapi.
 
Back
Top Bottom