Chadema wampa Kikwete 'siku tisa'

Lakini yote tisa wana JF hakuna kitu kinachi niuma MOYO kama nikiwaona wanafunzi wa vyuo vikuu wakiandamana, HAWA MIMI NAENDELEA KUWAITA WAPUMBAVU kila kukicha heti waongezewe Posho, watu wanaumiza vichwa ifanyike nini kuokoa taifa na inflation tena CDM na wananchi walio unga mkono maandamano kule mwanza ni mfano mzuri sana, na matamko waliyo yatoa, yakionyesha hawa watu wako kwa ajili ya kutetea Taifa letu, na si wabinafsi kwani bidhaa zikishuka bei helfu 2000 itatosha matumizi, gharama za maisha zitapungua, haya ambayo yangepaswa kuangaliwa na HETI WASOMI A.K.A MI NAWAITA MBUMBUMBU wanahangaika kuliongezea taifa mzigo, kuna swali huwa najiuliza.....! ina maana kuna siku wanaweza kuja kudai posho inayo lingana na mishahara ya wabunge kwa namna mambo yanavyo kwenda? maana mbunge na viongozi au matajiri ndo watu pekee wanayaweza maisha kwasasa, bei zikipanda wako nazo, sikisogea wako nazo, zicheze vipi wako nazo, maana pesa imejaa, regardless costs ya maisha, EMBU SERIKALI IWAULIZE WATAFANYA NINI KAMA IKIWAONGOZEA 120,000/- KWA SIKU? WATALETA MCHANGO GANI??? PUMBAVU HAWA ikiwa hata sasa wameshindwa hata kuleta mchango wowote wangali tunadhani wana akili,
 
CDM imekosa sera wanadakia matukio yanayojitokeza. DOWANS ilivyoibuka wamedakia-maandamano, umeme umepanda bei wanadakia-maandamano, sukari imepanda bei-tayari maandamano, Gongo la Mbota-maandamano..lingine likiibuka kesho utasiki maandamano. Wataandamana mpaka miguu itaingia ndani. Nendeni mkafanye kazi mtalala njaa...!!!

Let say wewe ndo una busara kuliko woooote!!! na CDM wanakusikia na wanaenda kufanya kazi, KODI inayo katwa inapelekwa wapi? baada ya wao kufanya kazi? unajua nini sababu za kupanda kwa gharama za maisha nchini? ina maanisha kila litakalo tokea utakaa kimya? Am afraid you are one of the elites who cut up the cate and eat in the dark.
 
Kutoa autimutum kwa chama cha siasa ni jambo la kawaida mkuu!unahisi wamevunja sheria gani ya nchi?inawezekana wewe ukawa umechoka kabisa kufikri ndiyo maana unatoa hoja dhaifu!kapumzike mkuu!!

Tena Kaka, mimi nina wasiwasi na Akilia ya huyu anaye jiita Majimshindo, hivi unajua unayowaza ndiyo yanayo ujaza moyo wako? ukiwaza maji maji nawe akili inakuwa maji maji, na moyo unakuwa maji maji, ujakosea mimi si CDM lkn hakika napenda kuchukua muda walau kulitafakari jambo nimekuwa natamani vyama visivyo vya serikali na mashirika ya kiraia wawe wahanga wa uanzishwaji wa haya maandamano labda italeta mantiki zaidi isiwe kwasababu CDM basi, mwana CCM hata kama anapukutishwa mpaka akili na anajua anapukutishwa basi hataki kushiriki kwakuwa yeye ni mwana CCM, NOOO!!!!!!!!! Embu amka ndg
 
CDM imekosa sera wanadakia matukio yanayojitokeza. DOWANS ilivyoibuka wamedakia-maandamano, umeme umepanda bei wanadakia-maandamano, sukari imepanda bei-tayari maandamano, Gongo la Mbota-maandamano..lingine likiibuka kesho utasiki maandamano. Wataandamana mpaka miguu itaingia ndani. Nendeni mkafanye kazi mtalala njaa...!!!

Ila ukiangalia vizuri Mzee LAPA, wewe ni MZEE LAPA KWELI!!!!!!! MAANA USEMI CDM WAMEKOSA SERA WE ZAKO NI ZIPI, MAANA MIMI NINAVYO JUA palipo kosekekana mtoa SERA basi akitokea mtu hata akaropoka na kutetea kauli yake inakuwa sera, embu chunguza mkuu ulichoandika, AU WEW NDO UMEKOSA LA KUANDIKA? maana we mtoto wa Rostam mbona nakujua sana...!! am sorr sio kusudio langu kukuweka wazi humu....!
 
Toka Dr Slaa toka ashindwe uraisi na nafasi ya kuwa mbunge kama zamani njia pekee ya yy kupata umaarufu ni kwenye maandamano,mbona wakati akiwa mbunge hakukuwa na maandamano?Dr Slaa ni mchu wa madaraka,na hata serikali ya Jk ikianguka sio yy ndiye atakayekuwa raisi,halafu kwann anawatoa sadaka mikoa mingie?angeanza kuwatoa sadaka mkoani kwake kwanza


He!!! We mfu kisiwani!! una kumbukumbu kweli wewe? hivi unajua huyu jamaa aliachia kiti chake cha ubunge kwa mtu asiye na umaarufu wowote? na bado wanachi wake walimpa mtu huyo? na kwa mtafiti mzuri utajua tu, alicho kifanya Dr, Slaa ni maandalizi ya kuichukua nchi 2015, na si kukosa uongozi, hivi mnatokea wapi nyinyi watoto wa vigogo humu ndani ya hii JF?
 
hAAAA!!!!!!!!!!! JAMANI MI NAHAMA HII MADA MAANA NIMESHAWAONA WATOTO WA VOGOGO WAMESHAINGIA TAYARI,:A S 13:

Maana wao ukiongolea maandamano tu basi wanajenga picha ya Baba kuachia ulaji, embu mtu mmoja awaeleweshe maandamano hayo si ya kuwaondoa Baba zao, NOoo!!!!!! ni kutetea ghrama za maisha kupanda, zinazo tokana na uzembe wa kutokuwajibika kwaviongozi wetu, wana mawazo mgando, wanuza nchi, ni bora Almasi tungechezea usolo na mdako, kuliko waingie ma mikataba ya kutuachia mashimo tupu, na madini huwa yanaisha,

Aha!! mi nahama
 
Siku 9 za kishindo zatangazwa
headline_bullet.jpg
Polisi wa Mwanza wafagiliwa

Main(65).jpg

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, akiwahutubia maelfu ya wananchi walioshiriki maandamano ya chama hicho ya kupinga mfumuko wa bei na malipo ya Dowans yaliyofanyika jijini Mwanza jana.



Maelfu ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Kidemokrasia na Maendeleo (Chadema), jana walifanya maandamano ya amani yaliyoongozwa na viongozi wa juu wa chama hicho, ambayo yalikuwa na msisimko mkubwa bila ya vurugu yoyote.
Maandamano hayo yalikuwa maalum kwa ajili ya kuishinikiza Serikali kutoilipa Kampuni ya Dowans, kupanda kwa bei ya umeme na kutokubali uchaguzi uliomweka madarakani meya wa Jiji la Arusha. Maandamano hayo yaliyoongozwa na
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Dk. Wilibrod Slaa na wabunge karibu wote wa chama hicho kutoka karibu majimbo yote Tanzania, yalianzia katika viwanja vya shule ya msingi Bugarika na kumalizikia katika viwanja vya Furahisha jijini hapa ikiwa ni karibu ya kilometa 10, ambapo viongozi hao wote walishiriki mwanzo hadi mwisho pamoja na maelfu ya wananchi wa Jiji la Mwanza, Baadhi yao wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali.
Akizungumza katika mkutano huo mkubwa kwenye viwanja vya Furahisha, Dk. Slaa alisema kuwa Chadema inamtaka Rais Jakaya Kikwete kuwachukulia hatua kali wale wote walioliingiza taifa katika matatizo ya kampuni ya Dowans.
Alisema kuwa anaamini kuwa kabla ya kumaliza maandamano hayo ya siku tisa katika mikoa tofauti, Kikwete atatangaza kuwachukulia watu hao waliosababisha taifa kutaka kuilipa Dowans wakati kampuni hiyo ni haramu kutokana na Kamati ya Bunge kutamka kuwa mkataba wa Kampuni ya Richmond uliorithiwa na Dowans haukuwa halali.
“Tunajua kabla hatumaliza maandamano yetu ya siku tisa tuna imani kubwa kuwa (Rais) Kikwete atangaza kuwachukulia hatua waliohusika la sivyo wananchi watatumia nguvu ya umma kama nchi za Kaskazini ya Afrika ambako kuna wimbi la nguvu ya umma ambalo linawatoa madarakani viongozi,” alisema Slaa.
Pia aliwaomba wananchi kuwazomea wabunge wote wa CCM watakapokuwa majukwaani kama walivyofanya wakati ule wa EPA, ambapo walikuwa wakiwazomea wabunge kila walipokuwa wakihutubia.
Naye Mbowe pamoja na mambo mengine ya kuishinikiza serikali kupunguza bei ya umeme na kutoilipa Dowans, aliwataka askari wote kuielewa Chadema na kulinda maslahi ya umma badala ya kuwalinda mafisadi wachache wanaoimaliza nchi kila uchao.
“Askari mgome kuwapiga watu, kama Misri askari waligoma kabisa kuwapiga watu, lakini Arusha askari walikubali kuwapiga ndugu zao risasi wakati hawakuwa na hatia,” alisema Mbowe.
Mbowe alimpongeza Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Simon Sirro, kwa kukubali maandamano hayo na kutowapiga mabomu watu wa Mwanza tofauti na Arusha ambako polisi wa huko kila mara wamekuwa wakiwapiga mabomu wananchi wa huko.
Mbunge wa Arusha Mjini, Godobless Lema, naye alikuwepo katika maandamano hayo alilaani polisi wa Arusha kuwapiga wananchi kila uchao, ambapo alisisitiza kuwa wananchi wa Arusha sasa hawaogopi mabomu ya machozi na wanayaona kama manukato tu.
 
Luteni said:
My take: Is a 9-day strategy a coincidence, planned?, na je baada ya siku hizo tisa nini kitafuata. This is a serious note, wasiwasi wangu wasije kuwa wamekurupuka kusema siku tisa.

why siku 9?
 
Chadema hawataitakii mema Tanzania yetu.

Kauli zao na vitendo vyao vyote vinaonesha kuashiria fujo, uvunjifu wa amani na uchu wa madaraka.

Hivi wana ubavu gani wa kuitisha Serikali?

Mini naiasa Serikali ya Tanzania. Usipoziba ufa, utajenga ukuta.

Hawa viongozi wa Chadema wachululiwe hatua kali za kisheria kwa kauli zao za uvunjifu wa amani ili wasituletee fujo na uvunjifu wa amani.

Siku tisa? Wana maana gani siku tisa? Na kwa sasa, Serikali iwapuuze kwa hayo maneno yao, na ione baada ya hizo siku tisa wamekusudia nini? Wakianzisha uvunjifu wa amani au chokochoko zinazoashiria uvunjifu wa amani baada ya siku hizo tisa, basi wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Wewe ni chizi sio kosa lako
 
wewe ni mpuuuzi ambaye huna tv wala redio kwako maana hatua zilizochukuliwa nchi zingine wewe hujaziona unabaki kushangaa. angalia umati wa jana then ndo uulize hatua ambazo wanaweza kuzichukua. bado uko kwenye TANU??

Mpashe huyo, naona anatufundisha uoga! nahisi anaishi kwa pesa za kifisadi ndo maana anahisi matanuzi yanafikia ukingoni! Amani....... amani bongo
 
Chadema hawataitakii mema Tanzania yetu.

Kauli zao na vitendo vyao vyote vinaonesha kuashiria fujo, uvunjifu wa amani na uchu wa madaraka.

Hivi wana ubavu gani wa kuitisha Serikali?

Mini naiasa Serikali ya Tanzania. Usipoziba ufa, utajenga ukuta.

Hawa viongozi wa Chadema wachululiwe hatua kali za kisheria kwa kauli zao za uvunjifu wa amani ili wasituletee fujo na uvunjifu wa amani.

Siku tisa? Wana maana gani siku tisa? Na kwa sasa, Serikali iwapuuze kwa hayo maneno yao, na ione baada ya hizo siku tisa wamekusudia nini? Wakianzisha uvunjifu wa amani au chokochoko zinazoashiria uvunjifu wa amani baada ya siku hizo tisa, basi wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Acha UKALE wako. Chadema na wananchi hawajatumia bunduki kulazimisha serikali ya JK kuzungumzia punguzo la bei ya sukari. Wameona maandamano ya Mwanza, wanaanza kujikosha kuwa ooh tutapunguza bei ya sukari, ooh deni la Tanesco limefutwa. Na bado, this is just an INTRO, DUCTION itafuata baadaye.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kitampa rais Kikwete siku tisa baada ya kumaliza mzunguko wake wa kwanza wa kuwahamasisha wananchi mikoani.

“Rais Kikwete tunakwenda naye kwa stepu, tutawasha moto wa maandamano nchi nzima, tukimaliza tutaangalia kama atakuwa amechukua hatua. Tutampa siku tisa,” alisema Mbowe na kushangiliwa.

Dk. Slaa aliyekuwa wa kwanza kuhutubia katika mkutano huo, alisisitiza sana msimamo wa chama hicho kumpa Rais Kikwete siku tisa za kuhakikisha anaondoa kodi kwenye maeneo yote yaliyosababisha bei za vyakula na bidhaa mbalimbali kupanda na kufanya maisha ya wananchi kuwa magumu.

My take: Is a 9-day strategy a coincidence, planned?, na je baada ya siku hizo tisa nini kitafuata. This is a serious note, wasiwasi wangu wasije kuwa wamekurupuka kusema siku tisa.

Slaa ana uroho wa madaraka ndiyo anataka eti nchi isitawalike ASUBIRI 2015 aache upuuzi wa vitisho
 
Chadema hawataitakii mema Tanzania yetu.

Kauli zao na vitendo vyao vyote vinaonesha kuashiria fujo, uvunjifu wa amani na uchu wa madaraka.

Hivi wana ubavu gani wa kuitisha Serikali?

Mini naiasa Serikali ya Tanzania. Usipoziba ufa, utajenga ukuta.

Hawa viongozi wa Chadema wachululiwe hatua kali za kisheria kwa kauli zao za uvunjifu wa amani ili wasituletee fujo na uvunjifu wa amani.

Siku tisa? Wana maana gani siku tisa? Na kwa sasa, Serikali iwapuuze kwa hayo maneno yao, na ione baada ya hizo siku tisa wamekusudia nini? Wakianzisha uvunjifu wa amani au chokochoko zinazoashiria uvunjifu wa amani baada ya siku hizo tisa, basi wachukuliwe hatua kali za kisheria.

wataakuwa wamesha chelewa.
Serikali ya jk haitawaliki kamwe,unaelewa nini hapo?
 
I believe Dr. Slaa(PhD) will make a Good President

luteni ni kweli,tunahaitaji viongozi jasiri na wanaoweza kuthubutu mfano wa Kagame
Wakati alipoanza kufanya mabadiliko hasa katika kuondoa matumizi yasiyo ya lazima serikalini wengi wa viongozi wa ngazi ya juu kwenye chama na serikali hawakupenda kwa dhati,kwa mfano ishu ya kusitisha kununua magari ya bei ghali serikalini
Kwa sasa Rwanda inafanya vizuri katika nyanja nyingi eg uchumi elimu na technolojia,wakati sisi tuna rasilimali nyingi wao hata nusu yetu hawafikii lakini wanatuzidi kwa mbali katika kusimamia rasilimali vizuri
Tuombe na tufanyie kazi ili kumpata kiongozi wa aina ya Kagame ili rasilimali tulizonazo ziwafaidishe watanzania wote badala ya watu wachache
 
Tatizo hapa ni kwamba baadhi ya wana JF hawakuelewa CHADEMA imesema nini: haikusema inampa JK siku tisa kuanzia leo. Kama alivyofafanua Quinine, ni siku tisa kuanzia kumalizika kwa hamasisho la nchi nzima kwa maandamano.

Ni wazi JK hatendi mpaka kuwe na pressure. Hamjaona jinsi wanafunzi wa vyuo vikuu walivyopata mahitaji yao kwa kuweka pressure? Hata wafanyakazi hawakuongezewa mshahara mpaka walipotoa vitisho.

Ni sawa kabisa CHADEMA kuweka pressure namna hii. Kama serikali itashindwa kushughulikia kero zinazotajwa baada ya muda kwisha, basi itatakiwa IJIUZULU. Hilo linawezekana sana. Bravo CHADEMA.
 
Waandishi Wetu, Mwanza
VIONGOZI wa juu na wabunge wa Chadema jana walitawanyika katika wilaya mbalimbali za mkoa wa Mwanza na kufanya mikutano ya hadhara kuendelea kupinga kupanda kwa gharama za maisha, malipo kwa Kampuni ya Dowans na kupanda kwa gharama za umeme.

Viongozi na wabunge hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe na Katibu wake mkuu Dk Willbrod Slaa aliyekuwa mgombea urais katika uchaguzi mkuu uliopita Oktoba 31 mwaka 2010 walichagiza katika mikutano hiyo ya mtawanyiko.

Mikutano hiyo ya hadhara ilikusanya maelfu ya wakazi wa mkoa wa Mwanza, huku mwenyekiti Mbowe akifanya mkutano wa hadhara wilayani Geita akiwa ameongozana na wabunge wanne wa chama hicho na Katibu wake Dk Slaa akiwa Kisiwani Ukerewe ambako naye aliambatana na mbunge wa Ukerewe, Salvatory Machemli na wabunge wa viti maalum, Rebecca Mngodo na Grace Kiwelu.

Freeman Mbowe
Mbowe alifuatana na Joseph Mbilinyi ambaye ni mbunge wa Mbeya Mjini, Halima Mdee (Kawe), Paulina Gekul na Anna Mallaki (viti maalum) pamoja na Profesa Kulikoyela Kahigi wa Bukombe.

Akihutubia katika mkutano huo Mbowe alisema wilaya ya Geita, ni masikini kupindukia kutokana na wananchi wake kuhujumiwa na viongozi wachache walioko serikali licha ya kuwa na mgodi mkubwa wa dhahabu.

Mbowe aliyasema hayo katika uwanja wa magereza nje kidogo na mji wa Geita, katika mkutano ambao ulitanguliwa na maandamano yaliyoaongozwa naye, huku wafuasi wa chama hicho wakibeba mabango mbalimbali, moja likilosomeka,’’Dowans ikilipwa, mimi nitajiua. Mtanzania halali’.’

Huku akikatishwa na kelele za wananchi Mbowe alisema kuwa mgodi huo ilikuwa umejitolea kutoa umeme katika mji wa Geita kwa kuunganisha kwenye gridi ya taifa, lakini viongozi wa CCM waligoma kwa vile wao hawana uchungu na mgao wa umeme na kwa vile wana majenereta nyumbani kwao.

Kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alirejea kauli yake kuwa kamwe Chadema hakitakubali ushirika na vyama vingine bungeni akidai kuwa vyama hivyo ni mawakala wa CCM, lakini akasema chama chake hakina ugomvi na wananchama wa vyama hivyo na kuwaomba radhi kuwa ugomvi uliopo ni kati ya chama hicho na viongozi wa vyama vingine vya upinzani hasa kile cha CUF.

Dk Wilbroad Slaa
Dk Slaa alifanya mkutano wake wilayani Ukerewe ambapo amemtaka Rais Jakaya Kikwete ajiuzulu kwa kile alichokiita uzembe wa serikali yake, kuendelea kusababisha maafa kwa wananchi pamoja na kauli yake ya kutowafaamu wamiliki wa kampuni ya kufua umeme ya Dowans.

Alisema haiingi akilini kuwa Rais Kikwete ambaye alikuwa mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri lililoidhinisha mkataba wa kampuni tata ya Richmond ambao umerisishwa kwa Dowans kudai kuwa hafahamu wamiliki wake ambapo aliongeza kuwa ikiwa ni kweli Kikwete hawafahamu wamiliki wa kampuni hiyo, basi huo ni uzembe na anatakiwa kujiuzulu pamoja na serikali yake.

Dk Slaa alisema pia kwamba Chadema haitakubali Tanesco kuingia mkataba na Dowans kama Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, January Makamba anavyoshauri, vinginevyo watatumia nguvu ya umma kupinga hilo .

Akifafanua alisema kimsingi mitambo hiyo inastahili kutaifishwa na kuonya kuwa kitendo cha kutaka kuingia mkataba na kampuni ya kifisadi ni ya kushangaza, kwani Serikali ilitambua tatizo la umeme wa kutegemea mabwawa ya maji tangu mwaka 2001 na baadaye tatizo hilo likajitokeza mwaka 2003.

"Serikali makini, ingenunua mitambo yake yenye uwezo wa kuzalisha nishati hiyo na siyo kuingia mikataba ya kifisadi kama ya Richmond na baadaye Dowans," alisema Dk Slaa.

Katibu Mkuu huyo wa Chadema alisema kwamba ameshangazwa na mtu aliyejitokeza kuwa ndiye mmiliki wa Dowans (Suleiman Al- Adawi) kujitokeza sasa akitoa madai tofauti ikiwemo na kutaka kusamehe deni hilo, baada ya kubaini mpango wa Chadema wa kutaka kutumia umma kupinga utapeli huo.

Mkutano wa Misungwi
Katika Wilaya ya Misungwi mkoani humo mkutano wa hadhara wa Chadema uliongozwa na mbunge wake wa Ilemela, Highness Kiwia huku ikielezwa kuwa mkutano huo ulisababisha kuvunjika kwa mkutano wa hadhara wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM, George Mkuchika uliokuwa ufanyike wilayani humo.

Katika mkutano huo Kiwia alifuatana na wabunge wa viti maalum wa Chadema Raya Ibrahim (Pemba) na Chiku Abwao (Iringa) ambapo alisema aliyekuwa mpinzani wake katika kuwania kiti cha ubunge Anthon Diallo amemfungulia kesi mahakamani akimtuhumu kwa kuiba kura katika uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2010.

Kiwia alisema pamoja na kumshitaki akidai aliiba kura kura zilizompa ushindi ametuhumiwa pia kufanya kampeni za vitisho na kusababisha wananchi kuogopa kujitokeza kwenda kupiga kura, lakini akasema ana uhakika kuwa waliomuweka madarakani ni wananchi kwa ridhaa yao na kudai kuwa atawapigania katika kuleta maendeleo.

Kuhusu Katiba Kiwia alisema Chadema haitapumzika hadi Serikali ifanye mabadiliko ya katiba ambayo itamuwezesha mtanzania kufanya uchaguzi wa haki na kweli bila ya kupigwa mabomu.
Katika mkutano huo wananchi waliohudhuria walipaza sauti wakisema kuwa Rais Kikwete hana budi kujiuzulu wakidai ameshindwa kuindesha nchi hii.

Mkutano wa Kwimba
Ezekia Wenje alifanya mkutano wake wa hadhara katika wilaya ya Kwimba huku akitoboa siri ya yaliyomsibu wakati wa kampeni za kuwania ubunge wa jimbo hilo.

Katika mkutano wake Wenje alifuatana na wabunge wenzake wa chama hicho ambao ni Rachel Mashishanga, Philip Maturano, Joyce Mukya pamoja na mkurugenzi wa fedha wa chama hicho Antony Komu.

Wenje alidai kuwa katika uchaguzi uliopita alihongwa Sh300 milioni ili ampishe aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na mgombea ubunge wa CCM katika jimbo hilo Lawrence Masha ambapo pia alidai moja ya chama siyo Chadema kilitenga Sh2.5 bilioni kwa ajili ya kuwagawia wapiga kura ili wachague chama hicho, lakini wananchi wa jimbo hilo waligoma na kulinda kura zao.

Viongozi hao wa Chadema na wabunge wao watafanya maandamo ya amani na baadaye mkutano wa hadhara leo katika mkoa wa Mara.

Kwa mujibu wa taarifa hizo maandamano hayo yataanza saa 5 asubuhi yakianzia eneo la Makutano na kuelekea katikati ya mji wa Musoma kwenye uwanja wa michezo wa Mkindo.

Habari zinaeleza kuwa ujumbe wa maandamano na mkutano wao wa hadhara ni sawa na ule walioutoa mkoani Mwanza, kupinga kupanda kwa gharama za maisha, malipo kwa Kampuni ya Dowans na kupanda kwa gharama za umeme.
Habari hii imeandaliwa na Sheila Sezzy, Misungwi, Frederick Katulanda, Kwimba na Jovita Kaijage, Ukerewe.

Source:Mwananchi 26/2/2011
 
Back
Top Bottom