Chadema wampa Kikwete 'siku tisa'

Chadema wampa Kikwete 'siku tisa'

Chadema wanafanya usanii tu bana, sijaona mabadiliko yoyote wanatuletea zaidi ya wao kutafuta kusifiwa tu na kutupandisha jaziba.

Tarehe 12 Januari wakasema Mwema na Nahodha wajiuzulu. Wakaachia hapo, hadi leo kimya.

Tarehe 17 Febuari wakasema waziri wa ulinzi na mkuu wa majeshi wajiuzulu. Ndo imetoka.

Wiki iliyopita wakampa JK siku tisa. Hata hazijafika tayari wanasimamisha maandamano wanarudi Dar wakati ambapo watu ndo wamehamasika!

Mkuu ni wewe kweli na majibu haya au?? No comment
 
Chondechonde jamani,hayo maandamano yapite kwa heri
isiwe kama huko tunakosikia watu... Wame...
Hekaheka ya mabomu ya G'mboto ilinifanya nifikirie sana
huko kwa wenzetu inakuaje.
Siku 9 ndio hizi kikubwa amani!
 
Wanajf naombeni tusaidiane kudadavua hili jambo. Majuzi kati CDM wametoa tamko kali wakimtaka JK atoe ndani ya siku tisa awe ameshughulikia madai yao yote. Kwangu kutoa tamko sio tatizo. Bali kinachonisumbua ni hiki. Haya mamlaka ya kumpa JK siku 9 wametoa kwa mujibu wa nini. Katiba, Sheria, Kanuni au haki ya Kidemokrasia. Kama ni haki ya kidemokrasia, nadhani wako wrong kwa sababu hawakumchagua na hivyo hawana hawana haki katu ya kumtuma. Kwa hiyo wasidandie behewa lisilo la kwao.
 
Hapo hakuna cha sheria, katiba wala kanuni, wao wanatumia haki ya Nguvu ya Umma! (Peoples' Power!)
Kama ujuavyo, Katiba iliopo inalinda watawala, Mahakama ndo kabisaaa! Kanuni ndo unaona zinapindishwa na Bunge kwa maslahi ya watawala. Dawa ni Nguvu ya Umma ichukue mkondo wake kama Tunisia, Misri nk.
 
Tangu Chadema watoe tamko la kumtaka JK atekeleze matakwa yao ndani ya siku 9, nimekuwa nikijiuliza, hilo tamko limetolewa kwa mujibu wa sheria, katiba, kanuni au haki ya kidemokrasia. Baada ya kuperuzi rejea mbali2, ckufanikiwa any source of right, powers or duty inayowawezesha CDM kutoa matamko kama hayo. Labda kidogo kwenye haki ya kidemokrasia ambayo hata hivyo CDM wanatemwa kwa sababu hiyo haki, wajibu na uhuru wa kufanya hivyo wamepewa wale tu walioiweka serikali madarakani. Je CDM ndo kusema hawajui hilo au na wao pia waliisuport CCM? Kama hawajui hilo, nachelea kuona hatari inayolikabili Taifa kwa kuwa na viongozi mbumbumbu na ambao kutokana na hilo, wanatamani kuiingiza nchi kwenye machafuko. I stand 2b corrected not insulted.
 
Wakati wanahangaika kuwaaminisha watu kuwa wako sahihi, wenye akili wamesha washtukia kuwa wanataka kutumia maandamano kama shotcut ya kuingia ikulu.
 
Poa ndugu yangu, acha munkari, hiyo ndiyo siasa. Kazi ya chama chochote cha siasa ni kushika dola, CCM, CDM, CUF na wengineo lengo ni kuingia ikulu. Sasa ulitegemea CDM waitishe maandamano ya kumsifia jk na ccm yao? la hasha lengo ni kumng'oa ila kinachwasumbua ni kuwa mbona CDM wameanza mapema hivi? Hiyo ndiyo siasa ni mchezo kuviziana. Jambo ambalo sikubaliani nalo ni machafuko. Katika mikutano ya Mwanz, Musoma, Shinyanga na Kagera umesikia machafuko ama mapigano yoyote? hiyo ndiyo CDM, amani kwa kwenda mbele lakini ukweli usemwe.
 
Bahati mbaya nadhani hujanielewa. Mi nimeuliza hilo tamko la siku 9 wamelitoa kwa mujibu wa nini?
 
Tangu Chadema watoe tamko la kumtaka JK atekeleze matakwa yao ndani ya siku 9, nimekuwa nikijiuliza, hilo tamko limetolewa kwa mujibu wa sheria, katiba, kanuni au haki ya kidemokrasia. Baada ya kuperuzi rejea mbali2, ckufanikiwa any source of right, powers or duty inayowawezesha CDM kutoa matamko kama hayo. Labda kidogo kwenye haki ya kidemokrasia ambayo hata hivyo CDM wanatemwa kwa sababu hiyo haki, wajibu na uhuru wa kufanya hivyo wamepewa wale tu walioiweka serikali madarakani. Je CDM ndo kusema hawajui hilo au na wao pia waliisuport CCM? Kama hawajui hilo, nachelea kuona hatari inayolikabili Taifa kwa kuwa na viongozi mbumbumbu na ambao kutokana na hilo, wanatamani kuiingiza nchi kwenye machafuko. I stand 2b corrected not insulted.

Sababu ipi unajiuliza wakati majibu unayo. Je wasiwasi pia wa nini wakati CCM ilipata kura zaidi ya Milioni 5. Si zaidi ya Milioni 2 za Chadema au ni zile za kuchachua. Ingiwa sipindi kujihusisha na kinachoendelea, ila kwa taarifa kwa wasisi wasi wa wanaccm naanza kuamini kuwa watanzania hawakuiweka ccm madarakani. Tume ya Uchaguzi inajua ni chama gani kilishinda. Hii pia inajidhiirisha kwenye mikutano na maandamono ya Chadema yanayoendelea. Wote wanaoshiriki ndiyo wale waliokipigia chadema kura. Na kama Serikali inaanza kufikiria kutumia nguvu basi hakuungwa na watu milioni 5 . Ili kuhakikisha basi CCM yetu waitishe mkutano tuone wangapi watahudhuria.
 
Hapa tutabishana tu, aliyepewa hizo siku TISA alisema "Hayo si matatizo ya kumalizika ndani ya siku tisa"

Tafasiri ni kwamba anaomba kuongezewa muda zaidi ya aliopewa.
Muhusika anajua zimetolewa kwa mujibu wa nini ndio maana alijibu, so just relax.

Pamoja!!!
 
Hapa tutabishana tu, aliyepewa hizo siku TISA alisema "Hayo si matatizo ya kumalizika ndani ya siku tisa" Tafasiri ni kwamba anaomba kuongezewa muda zaidi ya aliopewa. Muhusika anajua zimetolewa kwa mujibu wa nini ndio maana alijibu, so just relax. Pamoja!!!
Lakini ni majibu yaliyolenga kutowapa CDM ushindi. So hakukusudia hicho unachokisema
 
Chadema wanafanya usanii tu bana, sijaona mabadiliko yoyote wanatuletea zaidi ya wao kutafuta kusifiwa tu na kutupandisha jaziba.

Tarehe 12 Januari wakasema Mwema na Nahodha wajiuzulu. Wakaachia hapo, hadi leo kimya.

Tarehe 17 Febuari wakasema waziri wa ulinzi na mkuu wa majeshi wajiuzulu. Ndo imetoka.

Wiki iliyopita wakampa JK siku tisa. Hata hazijafika tayari wanasimamisha maandamano wanarudi Dar wakati ambapo watu ndo wamehamasika!
Watu hamuelewi maana ya siku tisa, ilichofanya CDM ni kutimiza wajibu wa kumkumbusha Kikwete, Yesu aliposema atarudi mapema hakuwa na maana ya kesho ni kujiandaa hata CDM wamempa Kikwete hizo siku tisa za kujiandaa kutekeleza siyo kutimiza, mkihangaika na tarehe mtapotea.
 
Tangu Chadema watoe tamko la kumtaka JK atekeleze matakwa yao ndani ya siku 9, nimekuwa nikijiuliza, hilo tamko limetolewa kwa mujibu wa sheria, katiba, kanuni au haki ya kidemokrasia. Baada ya kuperuzi rejea mbali2, ckufanikiwa any source of right, powers or duty inayowawezesha CDM kutoa matamko kama hayo. Labda kidogo kwenye haki ya kidemokrasia ambayo hata hivyo CDM wanatemwa kwa sababu hiyo haki, wajibu na uhuru wa kufanya hivyo wamepewa wale tu walioiweka serikali madarakani. Je CDM ndo kusema hawajui hilo au na wao pia waliisuport CCM? Kama hawajui hilo, nachelea kuona hatari inayolikabili Taifa kwa kuwa na viongozi mbumbumbu na ambao kutokana na hilo, wanatamani kuiingiza nchi kwenye machafuko. I stand 2b corrected not insulted.

Ndugu
Fahamu kuwa upinzani siku zote si kuilamba miguu chama iliyoko madarakani wala kuiunga mkono chama iliyoko madarakani Bali ni kuikosoa. Na pale wapinzani wanapopata hoja nzuri za kuiondoa madarakani chama tawala katu hawawezi kukaa kimya eti kwa sababu uchaguzi haujafika"THATS NOT DEMOCRACY!!" Ndo sababu Japan, Israel, Italy, Marekani na kwingine kwenye demokrasia utasikia wanatafuta hata ushahidi wa hawala wa kiongozi wa miaka ileeee wakti kiongozi huska alikuwa chekechea [kumbuka jinsi walivyomuandama clinton, Kumbuka jinsi walivyomwandama netanyahu, kumbuka wanavyomwandama waziri mkuu wa italy, e.t.c].
Wanalofanya chadema ni sahihi kabisa!!! kinachotakiwa ni CCM kuondoa kero.
Angalizo Mkapa alikuwa mbunifu ndiyo sababu alimtengenezea ushindi mnono Kikwete. Ushindi wa 2005 wa kikwete umetokana na ubunifu wa Mkapa katika mambo haya:-
1. Wapinzani waliposhutumu kuwa jambo fulani ni kero yeye alilitatua [kumbuka jinsi CUF walivyopigia kelele suala la kodi ya kichwa na hatua alizochukua mkapa]
2. Hotuba za Mwisho wa Mwezi za Mkapa ziligusa moja kwa moja mambo yaliyokuwa yanajadiliwa mitaani kuhusu hali ya utendaji wa Serikali. ndiyo maana hotuba zake ziliacha wanasiasa wa upinzani wakijiuma midomo wasijue la kuongea.
3. Mkapa alianzisha utaratibu wa kukutana na Viongozi wa vyama vya upinzan. Hali hiyo iliongeza diplomasia na kuwapunguza nguvu wapinzani!!
4. Angetokea kiongozi wa kumrithi Mkapa aliye mbunifu kama yeye au zaidi basi upinzani ungekufa kabisa!!

JK kafanya nini cha ubunifu kupunguza pressure ya wapinzani????
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kitampa rais Kikwete siku tisa baada ya kumaliza mzunguko wake wa kwanza wa kuwahamasisha wananchi mikoani.

"Rais Kikwete tunakwenda naye kwa stepu, tutawasha moto wa maandamano nchi nzima, tukimaliza tutaangalia kama atakuwa amechukua hatua. Tutampa siku tisa," alisema Mbowe na kushangiliwa.

Dk. Slaa aliyekuwa wa kwanza kuhutubia katika mkutano huo, alisisitiza sana msimamo wa chama hicho kumpa Rais Kikwete siku tisa za kuhakikisha anaondoa kodi kwenye maeneo yote yaliyosababisha bei za vyakula na bidhaa mbalimbali kupanda na kufanya maisha ya wananchi kuwa magumu.

My take: Is a 9-day strategy a coincidence, planned?, na je baada ya siku hizo tisa nini kitafuata. This is a serious note, wasiwasi wangu wasije kuwa wamekurupuka kusema siku tisa.

Siku Tisa zimeisha sasa tutegemee nini ????????
 
Watu hamuelewi maana ya siku tisa, ilichofanya CDM ni kutimiza wajibu wa kumkumbusha Kikwete,
Yesu aliposema atarudi mapema hakuwa na maana ya kesho ni kujiandaa hata CDM wamempa Kikwete hizo siku tisa za kujiandaa kutekeleza siyo kutimiza, mkihangaika na tarehe mtapotea.
<br />
<br />
Acha umbea wewe,siku tisa zilizotajwa hazikuwa fumbo,wanapaswa kuzitekeleza kulingana na walichosema.Usipindishe hapa na kujifanya eti walinena kwa lugha.Washawasha na hamasa za mikutano husababisha wanasiasa kulopoka hata vile wasivyo na uwezo wao.Kama walivyodai,siku 9,tunaomba wafanye sasa walichotaka kufanya kwani hakuna jk alichotekeleza!
 
mkubwaaa acha kubwabwaja tu bila point,ebu soma kwa utuvu post zilizopita(hasa aliyonukuliwa kamanda Mbowe).Amesema watauwasha moto wa maandamano nchi nzima,wakimaliza WATAMPA mkwere SIKU 9.Je wameshafanya maandamano nchi nzima?
 
Back
Top Bottom