Augustine Moshi
JF-Expert Member
- Apr 22, 2006
- 2,556
- 1,394
naona wameamua kupiga mande kila kona usukumani
Hukumsikia Dada Regia Mtema akisema watakaba hata penalti, ndani na nje ya bunge?
Hizi ni rasharasha, mvua zenyewe bado!
naona wameamua kupiga mande kila kona usukumani
Mkutano wa Misungwi
Katika Wilaya ya Misungwi mkoani humo mkutano wa hadhara wa Chadema uliongozwa na mbunge wake wa Ilemela, Highness Kiwia huku ikielezwa kuwa mkutano huo ulisababisha kuvunjika kwa mkutano wa hadhara wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM, George Mkuchika uliokuwa ufanyike wilayani humo.
Chadema hawataitakii mema Tanzania yetu.
Kauli zao na vitendo vyao vyote vinaonesha kuashiria fujo, uvunjifu wa amani na uchu wa madaraka.
Hivi wana ubavu gani wa kuitisha Serikali?
Mini naiasa Serikali ya Tanzania. Usipoziba ufa, utajenga ukuta.
Hawa viongozi wa Chadema wachululiwe hatua kali za kisheria kwa kauli zao za uvunjifu wa amani ili wasituletee fujo na uvunjifu wa amani.
Siku tisa? Wana maana gani siku tisa? Na kwa sasa, Serikali iwapuuze kwa hayo maneno yao, na ione baada ya hizo siku tisa wamekusudia nini? Wakianzisha uvunjifu wa amani au chokochoko zinazoashiria uvunjifu wa amani baada ya siku hizo tisa, basi wachukuliwe hatua kali za kisheria.
japo wanaashiria uvunjifu wa amani...serikali nayo iangalie madai kama ni ya msingi.....!
Chadema hawataitakii mema Tanzania yetu.
Kauli zao na vitendo vyao vyote vinaonesha kuashiria fujo, uvunjifu wa amani na uchu wa madaraka.
Hivi wana ubavu gani wa kuitisha Serikali?
Mini naiasa Serikali ya Tanzania. Usipoziba ufa, utajenga ukuta.
Hawa viongozi wa Chadema wachululiwe hatua kali za kisheria kwa kauli zao za uvunjifu wa amani ili wasituletee fujo na uvunjifu wa amani.
Siku tisa? Wana maana gani siku tisa? Na kwa sasa, Serikali iwapuuze kwa hayo maneno yao, na ione baada ya hizo siku tisa wamekusudia nini? Wakianzisha uvunjifu wa amani au chokochoko zinazoashiria uvunjifu wa amani baada ya siku hizo tisa, basi wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kitampa rais Kikwete siku tisa baada ya kumaliza mzunguko wake wa kwanza wa kuwahamasisha wananchi mikoani.
"Rais Kikwete tunakwenda naye kwa stepu, tutawasha moto wa maandamano nchi nzima, tukimaliza tutaangalia kama atakuwa amechukua hatua. Tutampa siku tisa," alisema Mbowe na kushangiliwa.
Dk. Slaa aliyekuwa wa kwanza kuhutubia katika mkutano huo, alisisitiza sana msimamo wa chama hicho kumpa Rais Kikwete siku tisa za kuhakikisha anaondoa kodi kwenye maeneo yote yaliyosababisha bei za vyakula na bidhaa mbalimbali kupanda na kufanya maisha ya wananchi kuwa magumu.
My take: Is a 9-day strategy a coincidence, planned?, na je baada ya siku hizo tisa nini kitafuata. This is a serious note, wasiwasi wangu wasije kuwa wamekurupuka kusema siku tisa.
Huu ni uhaini!!!
Inabidi CDM wajipange upya na wawe na maslahi ya Watanzania na siyo ya kwao binafsi. Ila naona sasa wanatimiza azma yao ya kuhakikisha kuwa wanashinda uchaguzi wa 2010 kwa njia yoyoyote. Uchaguzi si uliisha na wakashindwa kupata hata robo ya wabunge? Mimi nafikiri siasa za kistaarabu badala ya kudai uraisi barabarani wangejijenga kwa ajili ya 2015, kwa kutoa hoja ambazo zitaingia akilini mwa wananchi na siyo kwa kutumia majukwaa. Sasa hivi uchaguzi umeisha, CDM wawaachie wanachi wafanye kazi.
Ni kweli kuwa maisha ni magumu kwa sababu ya kupanda kwa bei za vyakula na bidhaa nyingine - Hivi kwa kuchukua wao nchi ndio wataleta mvua? Au CCM ndio wanaoficha sukari? Tangu kuingia bungeni wamekuwa ni watu wa kupiga makelele yasiyo na msingi na kususa kitototo (na baadaye kujirudi baada ya kuona wanachi wamewa-ignore. Si kweli kuwa wote ambao siyo wanachama wa CDM bsai ni wana-CCM. Kwa wakati huu, ni vizuri kuangalia nguvu ya hoja, badala ya hoja ya nguvu.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kitampa rais Kikwete siku tisa baada ya kumaliza mzunguko wake wa kwanza wa kuwahamasisha wananchi mikoani.
Rais Kikwete tunakwenda naye kwa stepu, tutawasha moto wa maandamano nchi nzima, tukimaliza tutaangalia kama atakuwa amechukua hatua. Tutampa siku tisa, alisema Mbowe na kushangiliwa.
Dk. Slaa aliyekuwa wa kwanza kuhutubia katika mkutano huo, alisisitiza sana msimamo wa chama hicho kumpa Rais Kikwete siku tisa za kuhakikisha anaondoa kodi kwenye maeneo yote yaliyosababisha bei za vyakula na bidhaa mbalimbali kupanda na kufanya maisha ya wananchi kuwa magumu.
My take: Is a 9-day strategy a coincidence, planned?, na je baada ya siku hizo tisa nini kitafuata. This is a serious note, wasiwasi wangu wasije kuwa wamekurupuka kusema siku tisa.
Kwani hukusikiliza hotuba ya mkulu? mara tumefuta ushuru wa sukari, mara tumetoa fedha za kuzalisha umeme wa dharura, mara CDM wanataka kunipindua, oooohhh naomba wananchi mnisaidia chadema wasije kuniondoa madarakani etc. Hayo ndio majibu ndani ya siku 9, mbona mkulu hakuthubutu kukaa kimya ili CDM watoe tamko? hawana haja ya kutoa tamko tena walitaka mkulu abwabwaje ameshafanya hivyo basi wanasonga mbele.
Hii ni mistake inayofanywa na Chadema ,siku tisa jamani siku tisa ni muda mdogo sana sana,kuwahi kujenga matumaini,ingawa sijaelewa nini kitafanywa na CDM,na siku ndio zinakaribia kwisha.
Huku ni kujikwamisha na kuonekana hakuna ukweli ikiwa siku tisa zitakwisha na hakutaonekana lolote lililo au litakalofanywa na CDM, wazalendo wa kawaida na hata wanachama watahoji na kumhoji mkuu.
Msimamo wa aina hii ni lazima uwe na ukweli vyenginevyo yatakuwa mazoea na mtazoeleka kuwa mna kauli za uwongo,hamuna msimamo.
Kutoa siku tisa kwa utawala ni kujenga matumaini ya juu kabisa kwa wananchi na kuwapa matarajio kuwa safari hii ni kitaeleweka.
That is all !! Na umeridhika kuwa jawabu lililohitajiwa na CDM ni hilo,kubwabwaja kwa Kikwete ,tuseme sawa hilo ndio lilitegemewa na CDM kujibiwa na Mkuu wa serikali,Kikwete amewajibu na kupanda ndege,kwa hiyo zile siku tisa hazipo tena ? Kama ni hivyo Kikwete na serikali yake nionavyo hubwabwaja kila siku. Nilitegemea atawajibu kuwa ataboresha hali ya maisha na kuyabadilisha maisha ya Mtz kwa kipindi kifupi kinachokuja.
Kikwete amesema baada ya miezi mitatu tu mnaanza purukushani ? Nafikiri CDM wanaweza kuijibu hiyo kwa kumwambia Kikwete kama hujui umeshapitisha miaka mitano kuwepo madarakani na huna jipya na sio miezi mitatu kwani hatuzungumzii miezi mitatu au miaka kumi tunasema tokea tupate uhuru badala ya kwenda mbele tunaporomoka na sasa hata miti inateleza ,muondoke madarakani wewe na chama chako miaka mliokaa madarakani imetosha ,how it sound yaani kabla hazijamalizika siku tisa mnatoa jawabu papo kwa papo.Mnatoa jawabu kipindapinda.