CHADEMA walikuwa CCM-B kabla ya CUF.

Ni kama wewe uliyeandika tu habari kisha kuna mtu kakujibu na amekuelekeza kwamba tukio la CDM kupeana zamu ya mamlaka na CCM lilitokea baada ya madiwani kuwa sawa hivyo wakakaa chini na kukubaliana kuwa chadema wataanza kuwa na meya kisha CCM watamalizia ng'we.


Then amekuelekeza kuwa tofauti na CUF ambao walikalishwa chini kabla na kukubaliana kuwa baada ya matokeo ya uchaguzi kutakuwa na serikali ya mseto.


So ulitakiwa ukubali kuwa kwa matukio haya mawili CUF ndio walengwa haswa wa kuitwa CCM b.
Lakini wewe pointi ya jamaa umeiruka na kuikwepa matokeo yake umeendeleza zogo ili mradi tu watu wajue kuwa na leo umeandika thread...


Penye ukweli panakuja, mtaumbuka woote pmj na kiongozi wenu Maralia Sugu...
Ni hayo tu kwa sasa, ila kama unataka mengine utayapata, hata kupitia inbox yako.

Kumbe una matatizo binafsi. Sina haja ya kubishana, niko ki mjadala zaidi.
 
kama upo kimjadala well, tumia muda huu kukubali maelekezo uliyopewa kuwa CUF walikubaliana na CCM kuunda serikali ya umoja kabla ya uchaguzi kufanyika.


Then chadema walikaa na kujadili kufanya muundo wa kupeana zamu ya madaraka baadaya namba za madiwani wao kwenda karibu sawa.


Hivyo hizi ishu ni tofauti, kwani moja ilikuja baada ya uchaguzi na nyingine ilianza kabla ya uchaguzi...
 
kama upo kimjadala well, tumia muda huu kukubali maelekezo uliyopewa kuwa CUF walikubaliana na CCM kuunda serikali ya umoja kabla ya uchaguzi kufanyika.


Then chadema walikaa na kujadili kufanya muundo wa kupeana zamu ya madaraka baadaya namba za madiwani wao kwenda karibu sawa.


Hivyo hizi ishu ni tofauti, kwani moja ilikuja baada ya uchaguzi na nyingine ilianza kabla ya uchaguzi...

Unanikumbusha member mmoja anayeitwa JMushi.
hahahahahaha!
Soma vizuri article na michango yote, halafu utaelewa somo husika. Bado uko nje ya mstari. Sitakutafunia, jitahidi utaelewa tu.
 
Unanikumbusha member mmoja anayeitwa JMushi.
hahahahahaha!
Soma vizuri article na michango yote, halafu utaelewa somo husika. Bado uko nje ya mstari. Sitakutafunia, jitahidi utaelewa tu.

Kweli nimeamini mti ukipinda basi kivuli hakiwezi kunyooka...hye hye hyeeeee
 
Zemarc,

Nimekuwa nikifuatilia chaguzi za serikali za mitaa nchi tofauti duniani na nimegundua kuwa kuna miji mingi duniani, Serikali za mitaa ni watu hawana chama. Hii inakuwa rahisi sana kufanya kazi na wabunge wowote wale na bila kuwa na ushinikizi kutoka juu ya chama. Pia hata kwa chama, bado inakuwa kwao rahisi kwani hawahitaji kuchakachua uchaguzi kwa sababu wao haijalishi Mbunge au Rais ni nani.

Ukienda kwenye miji kama Califonia,Arnold Schwarzenneger alikuwa Republic na Mkewe ni Kennedy family ambao ni Democrat. Kitu ambacho kilitokea ni kuwa CA ni mji wa Democrat (na sasa wameuchukua tena), huyu Mr. Terminator, ilisemwa kabisa kuwa "panga pangua, itabidi ashirikiane na chama cha upinzani maana ndiyo wamejaa hapo CA. Hata kazi zake nyingi alifanya kwa kujiweka Neutral.

Ningelifurahi sana kama Tanzania itawekwa sheria ya watu kugombea bila vyama. Wakuu wa wilaya na Mikoa waondolewe na wawepo Mameya au Marais wa Mikoa/Wilaya. Viongozi kama hawa, hawatakuwa na heshima kwa Rais, PM au sijui nani maana wao wamechaguliwa kama Rais. Wanajibu moja kwa moja kwa Wananchi na siyo Rais aliyewachagua/au PM.

Kwenye serikali ya mitaa hilo jambo itabidi liwe linatokea sana. Kwenye Serikali kuu na bunge kwa sasa hali bado. Ikifika siku Chama tawala kina wabunge wanaozidi kigogo nusu na kwenye kura kunahitajika 2/3 ya idadi ya Wabunge, hapo ndiyo ujuwe kweli TUMEKOMAA na mtu hatalelewa kwa maovu yake maana upinzani watambeba na kwa sababu asilimia wamepisha kidogo sana, uchaguzi unaofuata wanaweza kuondolewa. Pia chama kingine kinaweza kuwaiba Wabunge wa chama fulani na hapo kukidhoofisha au kukifanya chama cha Upinzani. Ndiyo maana CCM wanapigana kwelikweli ili kulinda system ya "unagombea kwenye chama tu". Mtikila akishinda, atakuwa kaleta ukombozi mkubwa sana sana Tanzania.
 
I was going to type up a long response on the relationship between CCM and CUF, but instead, I'll just type the following: Ignorance is bliss.
 
Hivi huko Maulaya hakuna serikali za aina hii iliyopo Zanzibar ,na ikiwa zipo upinzani unakuwaje ? Hebu kaisikilizeni ile hotuba ya Maalim punde tu baada ya kutangazwa ushindi wa Sheni uliotungwa na Zec, kuna kipande alichomekea inahitaji mukielewe sana.
 
Joka Kuu,
Mwizi akiiba shilingi elfu kumi haimaanishi kuwa akipata nafasi ya kuiba milioni ataiacha. Swali lako ni sawa na kuuliza kwa nini mwizi wa elfu kumi na milioni wote ni wezi.
Msingi wa article hii ni kuweka bayana kuwa kushirikiana baina ya vyama siyo kukifanya chama fulani kuwa B,C etc.
Maamuzi yaliyofanywa na CUF bungeni wameyafanya kama chama, na kama wameamua kushirikiana na chama kingine siyo jambo la ajabu kama jinsi tunavyoona Chadema walivyoamua kushirikiana na CCM.

Zemarcopolo kuwa objective ndg yangu, ni kweli kwamba CUF ni ccm-b, hawapo kama wapinzani. Mfano mzuri ni wakati wa uchaguzi wa spika na naibu wake, na wakati wa uteuzi wa waziri mkuu. Mifano hii imeonyesha ukweli kuwa CUF siyo chama cha upinzani, bali sehemu ya chama tawala. CHADEMA ni chama cha kweli na makini cha upinzani Tanzania mtu asikudanganye.
 
subiri uone baada yamiaka 2 ndio utajua chadema ni chama cha upinzani au chakugombania ruzuku,we nahic huijui ccm ila ngoja utajionea na utakumbuka maneno yangu.

Usifananishe CHADEMA na hako katabia kako chafu cha kuhama chama baada ya kukosa soko, aibu uliiona mwenyewe. Acha kuongea ushabiki ukweli unaujua wewe.
 
Ngoja nikutafutie video ya mdahalo wa Moven pick. Amesema hilo bayana kabisa, wala halina ubishi.

Ukweli ni kwamba CHADEMA na Wakristo hawapendi kuona ZANZIBAR kuna amani.Watu hawa wanahoji kila rehma inayowapata wazanzibar.Walipenda Zanzibar mwaka huu pia wauwane hii ni roho ya kinyama iliyomo ndani ya nafsi zao. Utasikia wakisema chungu ya mambo mabaya tu.Kwa sasa mawaziri wanne tu toka Zanzibar imekua mjadala,badala ya kuangalia mustakabali wa taifa na muungano. Ninyi mnavyoleta udini na kuwatenga waislam basi dhambi hiyohiyo itawatafuna wenyewe kwa kuangalia huyu msabato,mkatoliki,mlokole nk,Na hakika dhambi hii ni mbaya sana.
 
subiri uone baada yamiaka 2 ndio utajua chadema ni chama cha upinzani au chakugombania ruzuku,we nahic huijui ccm ila ngoja utajionea na utakumbuka maneno yangu.

Mkuu,
Huyu ni mwera yule mbunge machachari kutoka tarime bunge lililopita au siye??

Very sad kama ndiye, eti CDM ni chama cha kugombea ruzuku, duh!
mkuu umesahau jinsi makamanda wa chadema walivyopambana kuhakikisha unachaguliwa kule tarime, wangekuwa wagombea ruzuku ile ruzuku si ingekuwa imekwisha hadi fedha za kampeni zingekosekana??


Hoja hapa ni aina ya muungano ambayo cuf wameukubali na ccm kule visiwani. Kosa kubwa la cuf ni kukubali kuwepo kwa non-executive VP.

Labda Zemarc. anisaidie kuelewa nini hasa ni majukumu ya Seif kwenye serikali na what if anything happen to Shein, cuf watatawala au itakuwaje? Tofauti ya makubaliano ya ccm na cdm kule kigoma na haya makubaliano ya ccm na cuf znzbr ni kuwa kule kgm cdm walikuwa na mandate ya kuaply sera zao kwa 100% katika ile nusu yao tofauti ya hii ya cuf amabo watatekeleza ilani ya ccm for next five yrs.

Hakuna maana kuwa na serikali ya mseto, jambo la maana cufg walichotakiwa kufanya ni kupigania katiba huru, tume huru na mfumo huru na wazi wa uchaguzi ili yule atakayeshinda aongoze serikali na aliyeshindwa ampe challenge mwenzake na kumkosoa huku akiwaonyuesha wananchi ni kwa nn next election achaguliwe yeye kuliko huyu aliyeko madarakani kwa sasa huu ndo muafaka cuf walitakiwa kuupata na sio ule wa kuingia madarakani tu, isitoshe hao ccm wenyewe hawana nia njema na hata mwenyekiti wao ameshasema huo muafaka ni wa miaka mitano ya majaribio.
 
Ukweli ni kwamba CHADEMA na Wakristo hawapendi kuona ZANZIBAR kuna amani.Watu hawa wanahoji kila rehma inayowapata wazanzibar.Walipenda Zanzibar mwaka huu pia wauwane hii ni roho ya kinyama iliyomo ndani ya nafsi zao. Utasikia wakisema chungu ya mambo mabaya tu.Kwa sasa mawaziri wanne tu toka Zanzibar imekua mjadala,badala ya kuangalia mustakabali wa taifa na muungano. Ninyi mnavyoleta udini na kuwatenga waislam basi dhambi hiyohiyo itawatafuna wenyewe kwa kuangalia huyu msabato,mkatoliki,mlokole nk,Na hakika dhambi hii ni mbaya sana.

Full of stupi udini.....hivi madini yenu yanawapa kula na kuishi nini?? Dont you have any other thing to construct your argument zaidi ya udini??
 
Ze Marcoplo Issue yako ni nzuri sana na ina mantiki kwakweli. Lakini huu si muda muafaka wa kujadili maana watu bado wana hasira na uchungu wa uchaguzi. HAWAJATULIA. Hebu lets buy time until these people settle then we can discuss the very crucial issue.
 
Hivi huko Maulaya hakuna serikali za aina hii iliyopo Zanzibar ,na ikiwa zipo upinzani unakuwaje ? Hebu kaisikilizeni ile hotuba ya Maalim punde tu baada ya kutangazwa ushindi wa Sheni uliotungwa na Zec, kuna kipande alichomekea inahitaji mukielewe sana.


Mwiba huu mfumo serikali za mseto upo hata ulaya lakini si kwa muundo huu wa hii ya znzbr. Zile za ulaya hutokea baada ya uchaguzi na chama kimoja kikashindwa kupata majority ya kuunda serikali peke yake, kwa hiyo inahitaji kuungana na chama kingine ili kufikia wingi unaohitajiak kuunda serikali.

Hii ya zanzbr ni tofauti sababu chama kimoja kitakuwa serikali kutekeleza sera za mwenzake, tofauti na zile za ulaya ambazo kabla ya kuunda serikali wanakaa mezani na kukubaliana sera za kufata hasa kwa kuwa kila mtu anakuwa na zake, mwisho wa siku wanakuwa na sera za pamoja, na pale mmoja anapokiuka tumekuwa tukishuhudia miungano hii ikivunjika.

Huu wa znzbr cuf hawatakuwa na nafasi ya kutekeleza sera zao watafata zile za ccm, deputy president ni non-executive so hana maamuzi kweny serikali. Mawaziri wote wameapa kuwa watiifu kwa rais wa serikali ya ccm.
 
Ukweli ni kwamba CHADEMA na Wakristo hawapendi kuona ZANZIBAR kuna amani.Watu hawa wanahoji kila rehma inayowapata wazanzibar.Walipenda Zanzibar mwaka huu pia wauwane hii ni roho ya kinyama iliyomo ndani ya nafsi zao. Utasikia wakisema chungu ya mambo mabaya tu.Kwa sasa mawaziri wanne tu toka Zanzibar imekua mjadala,badala ya kuangalia mustakabali wa taifa na muungano. Ninyi mnavyoleta udini na kuwatenga waislam basi dhambi hiyohiyo itawatafuna wenyewe kwa kuangalia huyu msabato,mkatoliki,mlokole nk,Na hakika dhambi hii ni mbaya sana.

Udini? Stupid! Stupid! Stupid! & Shame on You! Kama huna hoja peleka hizo pumba kwa mamako!
 
Kawaulize wakubwa wako CHADEMA ni nini? Tanzania kuna vyama vitatu tu vya upinzani, chadema ikiwemo. Rudi kamwulize makamba akuonyeshe mipango yote ya uanzishaji wa vyama vya upinzani, na majukumu aliyopewa kila mtu kwa nafasi yake. Au muulize Marando anafahamu zaidi ni kwanini alianzisha NCCR Mageuzi. Muulize Chief Fundikra (RIP) ni kwa nini hasa alianzisha chama. Pia kamuulize Edwini Mtei ni kwa vipi alianzisha CHADEMA.

Kwa taarifa yako vyama vingi vya upinzani vilianzishwa na serikali ya CCM kuitikia mwito wa umoja wa mataifa wa kuboresha demoncrasia. Chama kilichoanzishwa kwa misingi ya upinzani wa dhati ni CHADEMA, ambayo Edwini aliianzisha kumpinga Nyerere. Na alikuwa anamatumaini makubwa sana ya kuchukua nchi na kumtimulia vumbi Nyerere. Na kama utafuatilia kwa makini utajua ni kwanini Nyerere alikisifia CHADEMA siku za uhai wake. Alijua katika vyama vya upinzani vya kweli vyenye nguvu na vyenye uwezo wa kuongoza nchi ni CHADEMA pekee yenye sifa za kutosha. Kumbuka Nyerere hakuwa mnafiki.

Usijidanganye ndugu yangu chadema ni chama cha upinzani cha kweli kabisa, tofauti na NCCR, CUF au TLP.

Nakuunga mkono mia kwa mia. Umenikumbusha rafiki yangu mpenzi Marehem Kassim Maguto mmoja wa viongozi wa vyama vya upinzani, katika uhai wake, mara kwa mara alikuwa akinihadithia kuwa hivi vyanma vyote vimeanzishwa Ikulu. Naye aliendelea kusema kuwa "hakuna chama kitakachoongoza Tanzania kama hakipo ndani ya "system". Na hata ikitokea chama kingine kushika madaraka, basi hiyo ni mipango ya "system".

Maneno hayo ni mazito sana, aliyokuwa akinieleza. Naamini hawa kina Mbowe, Slaa, Lipumba, Maalim Seif, Mrema na wengi wengine, wote wamo ndani ya system na hizo kazi za vyama wanazojidai kufanya ni majukumu waliokabidhiwa na system.
 
Hata hivi sasa wao Chadema bado ni CCM B kwani si unaona jamaa alivyowacha kugombea ubunge na kukimbilia Uraisi huku akielewa kuwa kuwa kushinda ni sawa na kukauka bahari ,leo yupo wapi ,nasikia amerudi kijijini !
 
ZeMarcopolo,

..yaani unalinganisha masuala ya halmashauri ya jiji na mambo yanayotokea bungeni?

..lini Chadema wakafanya vitimbi vya kitoto kama walivyofanya CUF walipokwenda kukaa sehemu wanayokaa wabunge wa Chadema wakati wa hotuba ya Kikwete bungeni?

..CUF wameshinda Pemba, huku Tanganyika wamepata majimbo mawili tu. kwanini CUF waanze kufanya vituko ndani ya bunge la muungano ambalo kwa kiasi kikubwa ndilo bunge la Tanganyika?

Hata huko bungeni 2005 -2010, CHADEMA walianza na LOYAL OPPOSITION mode. Nakumbuka CCM B ndio jina ambalo timu ya kina Mwakeyembe, Ole Sendeka, Seleli, Diallo waliwapa wabunge wa CHADEMA wakati huo

It took Zitto, Chacha Wangwe, Halima, Mama Komu kurebel na kutoka nje ya bunge kuwaunga mkono CUF siku ya uchaguzi wa wabunge wa bunge la afrika mashariki CHADEMA kuanza kuwa protest party.....Nakumbuka Prof Baregu (aliyekuwa akitegemea kuchaguliwa ingawa ukweli CCM walishakubaliana kuhusu Dr Masha) pamoja na Dr Slaa waliniona mimi kuwa ndiyo niliowashawishi kina Zitto eti kuwasaidia wazanzibari wenzangu na kuniona adui.....

Hatua ya pili ya hii transformation ya CHADEMA ilianza na tishio na hatimaye Zitto kusimamishwa ubunge. Zitto kwa busara kubwa na kwa faida ya kujenga upinzani madhubuti akaamua kuwaachia viongozi wote wa Upinzani kuibuka na kung'ara huku yeye akijiweka nyuma yao ili nao wapate kufaidika na platform aliyoijenga yeye kwa faida ya upinzani wote kwa jumla.....

Leo hii wale waliokuwa waoga hata wa kuhoji CCM kwa ukali na kufunika mambo mengine na wengine waliotumia miaka mitano kulobyy kuteuliwa wabunge na Rais eti ndio wapiganaji na kudare kuquestion mitazamo ya Zitto katika masuala nyeti yanayohusu mustakabali wa nchi yetu ambao wao wanayaona katika macho ya "kulinda" umaarufu wao hadi 2015.................
 
Back
Top Bottom