ZeMarcopolo
JF-Expert Member
- May 11, 2008
- 14,011
- 7,192
Nimeguswa na aina mpya ya propaganda inayofanywa na Chadema ya kukiita chama cha wananchi CUF kuwa ni CCM-B. Hii ni kufumbia macho uhalisia wa hali ya kisiasa ya Zanzibar iliyopelekea kuwepo kwa muafaka. Hebu basi tupitie historia ili ituonyesha, ikiwa Chadema wangekuwa wamevaa viatu vya CUF wangefanya maamuzi gani?
Katika uchaguzi wa Madiwani uliofanyika tarehe 14 Desemba, 2006, Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji ilipata Madiwani sita toka Chama cha Mapinduzi (CCM) na Madiwani saba toka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Kwa vile CCM ilishinda pia kiti cha Ubunge cha Jimbo la Kigoma/Ujiji, Mbunge huyo aliongeza namba ya Wajumbe toka CCM kuwa saba na kufanya jumla ya wajumbe wa Halmashauri wa kuchaguliwa kuwa kumi na nne.
Baadaye Tume ya Uchaguzi kwa mujibu wa kifungu cha 19 (1)(c) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Na.8 ya 1984 iliwateua Wajumbe watatu (3) toka CCM na watatu toka CHADEMA kuwa Madiwani wa Viti Maalum vya Wanawake. Uteuzi huo wa Tume ya Uchaguzi ulifanya jumla ya Wajumbe wa Halmashauri ya Kigoma/Ujiji toka CCM kuwa kumi na wale wa kutoka CHADEMA kuwa kumi pia. Hivyo, idadi ya Wajumbe toka Vyama hivi ililingana na kufanya jumla ya Wajumbe wote wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma kuwa ishirini.
Hali ya Wajumbe toka Vyama vya CCM na CHADEMA kulingana ilifanya iwe vigumu kumpata Mwenyekiti wa Muda wa Kikao ambacho kingemchagua Meya na Naibu wa Meya. Kilichojitokeza ni kuwa pale Mjumbe toka CCM alipopendekeza jina la Mwenyekiti wa Muda, Wajumbe wote kumi toka CCM waliunga mkono na Wajumbe wote kumi wa CHADEMA walipinga. Vivyo hivyo hali hii ilijitokeza pale CHADEMA walipopendekeza jina na ndipo Viongozi wa Kitaifa wa Vyama walipoona umuhimu wa kuingilia kati suala hili.
Tarehe 26 Januari, 2006 Viongozi wa Kitaifa wa Vyama vya CCM na CHADEMA walifikia Makubaliano kuwa Uongozi katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji uwe wa kushirikiana.
Iliafikiwa kwamba, Awamu ya Kwanza kuanzia tarehe 9 Machi, 2006 hadi tarehe 30 Juni, 2008 Mheshimiwa Diwani Kitita Juma Magonjwa wa CHADEMA awe Meya na Mheshimiwa Diwani Yahya Liheye wa CCM awe Naibu wa Meya wa Manispaa. Aidha, Awamu ya Pili itakapoanza tarehe 1 Julai, 2008 hadi tarehe 28 Oktoba, 2008 Mheshimiwa Diwani Nashon Bidyanguze kutoka CCM aliteuliwa kuwa Meya na Mheshimiwa Diwani Shabaan Mambo kutoka CHADEMA awe Naibu wa Meya.
Labda niwakumbushe pia kuwa mgombea wa urais wa Chadema, Dr. Slaa, aliahidi kuunda serikali ya umoja wa kitaifa iwapo atashinda Urais. Alitoa ahadi hizo wakati muafaka na katiba mpya Zanzibar vilikuwa vimeshapitishwa. Swali ni je, alipanga kuunda serikali hiyo kwa ushirikiano na chama gani?
Je, Dr.Slaa alikuwa anaongelea kutengeneza CHADEMA-B, C etc.?
Je, Chadema ni chama kinachotekeleza yale kinachoyaongea?