CHADEMA walikuwa CCM-B kabla ya CUF.

Nimeguswa na aina mpya ya propaganda inayofanywa na Chadema ya kukiita chama cha wananchi CUF kuwa ni CCM-B. Hii ni kufumbia macho uhalisia wa hali ya kisiasa ya Zanzibar iliyopelekea kuwepo kwa muafaka. Hebu basi tupitie historia ili ituonyesha, ikiwa Chadema wangekuwa wamevaa viatu vya CUF wangefanya maamuzi gani?

Katika uchaguzi wa Madiwani uliofanyika tarehe 14 Desemba, 2006, Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji ilipata Madiwani sita toka Chama cha Mapinduzi (CCM) na Madiwani saba toka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Kwa vile CCM ilishinda pia kiti cha Ubunge cha Jimbo la Kigoma/Ujiji, Mbunge huyo aliongeza namba ya Wajumbe toka CCM kuwa saba na kufanya jumla ya wajumbe wa Halmashauri wa kuchaguliwa kuwa kumi na nne.

Baadaye Tume ya Uchaguzi kwa mujibu wa kifungu cha 19 (1)(c) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Na.8 ya 1984 iliwateua Wajumbe watatu (3) toka CCM na watatu toka CHADEMA kuwa Madiwani wa Viti Maalum vya Wanawake. Uteuzi huo wa Tume ya Uchaguzi ulifanya jumla ya Wajumbe wa Halmashauri ya Kigoma/Ujiji toka CCM kuwa kumi na wale wa kutoka CHADEMA kuwa kumi pia. Hivyo, idadi ya Wajumbe toka Vyama hivi ililingana na kufanya jumla ya Wajumbe wote wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma kuwa ishirini.

Hali ya Wajumbe toka Vyama vya CCM na CHADEMA kulingana ilifanya iwe vigumu kumpata Mwenyekiti wa Muda wa Kikao ambacho kingemchagua Meya na Naibu wa Meya. Kilichojitokeza ni kuwa pale Mjumbe toka CCM alipopendekeza jina la Mwenyekiti wa Muda, Wajumbe wote kumi toka CCM waliunga mkono na Wajumbe wote kumi wa CHADEMA walipinga. Vivyo hivyo hali hii ilijitokeza pale CHADEMA walipopendekeza jina na ndipo Viongozi wa Kitaifa wa Vyama walipoona umuhimu wa kuingilia kati suala hili.

Tarehe 26 Januari, 2006 Viongozi wa Kitaifa wa Vyama vya CCM na CHADEMA walifikia Makubaliano kuwa Uongozi katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji uwe wa kushirikiana.

Iliafikiwa kwamba, Awamu ya Kwanza kuanzia tarehe 9 Machi, 2006 hadi tarehe 30 Juni, 2008 Mheshimiwa Diwani Kitita Juma Magonjwa wa CHADEMA awe Meya na Mheshimiwa Diwani Yahya Liheye wa CCM awe Naibu wa Meya wa Manispaa. Aidha, Awamu ya Pili itakapoanza tarehe 1 Julai, 2008 hadi tarehe 28 Oktoba, 2008 Mheshimiwa Diwani Nashon Bidyanguze kutoka CCM aliteuliwa kuwa Meya na Mheshimiwa Diwani Shabaan Mambo kutoka CHADEMA awe Naibu wa Meya.

Labda niwakumbushe pia kuwa mgombea wa urais wa Chadema, Dr. Slaa, aliahidi kuunda serikali ya umoja wa kitaifa iwapo atashinda Urais. Alitoa ahadi hizo wakati muafaka na katiba mpya Zanzibar vilikuwa vimeshapitishwa. Swali ni je, alipanga kuunda serikali hiyo kwa ushirikiano na chama gani?
Je, Dr.Slaa alikuwa anaongelea kutengeneza CHADEMA-B, C etc.?
Je, Chadema ni chama kinachotekeleza yale kinachoyaongea?

Pole sana.Utumbo mtupu.
 
Hata hivi sasa wao Chadema bado ni CCM B kwani si unaona jamaa alivyowacha kugombea ubunge na kukimbilia Uraisi huku akielewa kuwa kuwa kushinda ni sawa na kukauka bahari ,leo yupo wapi ,nasikia amerudi kijijini !

Pamoja na Dr. Slaa kuacha ubunge na kugombea urais bado jimbo lipo CHADEMA, hivyo kusema CHADEMA ni ccm-b ni kukosa maneno ya kuandika humu. Dr. Slaa hana tamaa ya madaraka kama unavyofikiri, kumbuka kuwa hakuwa hata na nia ya kugombea urais, isipokuwa baada ya kuombwa kufanya hivyo alikubali. Kuna watu humu wanataka kubadilisha hii topic kujadili ushabiki. Daima ukweli utabaki kuwa ukweli, CHADEMA itabaki kuwa the Strong oposition party in Tz, no doubt on this.
 
Chadema, hasa viongozi wa Chadema, namely Mbowe na Slaa ni ma time bomb, talipuka saa yoyote, kama mnabisha mtakuja yaona. Sababu ya kusema haya ni very simple, hawana uadilifu, mmoja anategemea biashara ya ukahaba na mwingine ni Padiri mstaafu mwenye kupora wake za watu. Sasa kama si mataim bom ni nini?
 
Punguza makali ya maneno! Hatuangalii biashara wanazofanya watu, bali tunaangalia wanawezaje kutukomboa katika utumwa huu wa karne ya 21. Kama nikuangalia tabia za watu kama unavyofanya wewe mpumbavu, hata JK asingefaa kuwa rais kwa tabia yake ya kumiliki vikundi vya uhalifu. Acha kuropoka hizo pumba zako.
 
Huangalii biashara wanayofanya na uadilifu wa unaowaita viongozi halafu unasema upo karne ya 21? Unanishangaza sana tena sana. Leo hii hata ukienda kuomba kazi tu, yeyote iwayo, unatakiwa upeleke cv, referees nk. Kwa nini? Ili ujulikane u mtu wa aina gani. Leo hawa watu wanajulina kabisa uozo wao halafu bado mnawatetea kuwa ni viongozi? Siwaelewi kabisa. Hayo ni mataim bom na hayafai kuongoza.
 
Ok. Nimekuelewa, na JK ni permanent Bom.
 
Chadema, hasa viongozi wa Chadema, namely Mbowe na Slaa ni ma time bomb, talipuka saa yoyote, kama mnabisha mtakuja yaona. Sababu ya kusema haya ni very simple, hawana uadilifu, mmoja anategemea biashara ya ukahaba na mwingine ni Padiri mstaafu mwenye kupora wake za watu. Sasa kama si mataim bom ni nini?
You wish wait and see
 
Mimi nakubali kuwa Chadema ni chama cha upinzani cha ukweli. Ila sikubaliani na wewe pamoja na wafuasi wengine wa Chadema mnaokipaka matope chama cha CUF kwa sababu ya muafaka wa Zanzibar, jambo ambalo hata Chadema wanatamani wangelipata. Na article hii ni ushahidi kuwa Chadema inatamani ingepata nafasi kama ya CUF.

MKUU nadhani bado hujaelewa malalamiko ya wananchi kuhusu CUF tatizo siyo Mwafaka wa Zanzibar Tatizo ni viongozi wa CUF kujikomba kwa CCM kiasi kwamba wamesahau kuwa mjibu wa chama cha Ushindani ni kuiondoa serikali iliyoko madarakani kwa mikakati thaditi.Mfano ni juzi tu ndugu yetu Hamadi Rashid alikuwa akiwakirisha kambi ya upinzani Bungeni na alionekana kuwa na msimamo lakini tangu wameahidiwa vyeo hata kama yeye hakupewa amekuwa mtu wa tofauti hata anavyochangia mada anaonekana amepoteza mwelekeo.Mfano aliponda kitendo cha wabunge wa CDM kususia hotuba ya JK huku akibeza uamzi kama huo uliowahi kuchukuliwa na wajumbe wa baraza la wakirishi wa CUF kususia vikao vya bunge kwa msimu mzima kwa maneno ya R.Hamadi ambaye hajui nini anapaswa kufanya kwa sasa kama mpinzani hasa ukizingatia katibu wake Maalimu Seif anatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi zanzibar ambapo miongoni mwa malengo ya ilani hiyo ni kuhakikisha CCM inashinda nafasi zote za kugombea kwa kupata ushindi wa kishindo ktk kila chaguzi na kutetea pamoja na kurejesha viti vyote vya ubunge walivyovipoteza.Hamadi alisema wabunge wa CUF walifanya maamzi yasiyo sahihi kwakuwa walikosa mshahara kwa mhula mzima(kauli hii ya Hamadi inaonekana yeye yuko after mshahara wakati wale wabunge wa CUF waliosusia vikao walikuwa after mabadiriko ambayo hivi leo yameishia kumnufaisha Katibu wao Mkuu na Viongozi wachache wa CUF kinyume na mtazamo wao wa mwanzo ambapo wapiganaji hao walilenga kuleta mabadiriko kwa ajili ya manufaa ya Wazanzibari wote.Hivyo nikweeli CUF sasa inatekereza sera za CCM na Kamwe hawatakaa wakanyage ikulu na huo uchaguzi wa 215 otaona idadi yao itakavyoshuka kama siyo kutoweka kabisa bungeni huku CDM ikivuna viti zaidi ya 250 vya ubunge na kupate Rais Makini.
 
Hata hivi sasa wao Chadema bado ni CCM B kwani si unaona jamaa alivyowacha kugombea ubunge na kukimbilia Uraisi huku akielewa kuwa kuwa kushinda ni sawa na kukauka bahari ,leo yupo wapi ,nasikia amerudi kijijini !

Kama umeshindwa kutambua kuwa kwa kugombea Urais, Dr. Slaa ametoa mchango mkubwa wa kihistoria si tu katika kuimarisha nafasi ya CHADEMA kisiasa bali hata kubadili dynamic ya siasa za vyama nchini, basi una uelewa wa taabu sana.
 
Ok. Nimekuelewa, na JK ni permanent Bom.

JK si unaona mambo yake swafi, CV yake jee? swaafi, kaanza uongozi toka shule. Sasa wewe unataka kufananisha vinyangarakata hivi na JMK?
 
Nimeguswa na aina mpya ya propaganda inayofanywa na Chadema ya kukiita chama cha wananchi CUF kuwa ni CCM-B. Hii ni kufumbia macho uhalisia wa hali ya kisiasa ya Zanzibar iliyopelekea kuwepo kwa muafaka. Hebu basi tupitie historia ili ituonyesha, ikiwa Chadema wangekuwa wamevaa viatu vya CUF wangefanya maamuzi gani?

Katika uchaguzi wa Madiwani uliofanyika tarehe 14 Desemba, 2006, Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji ilipata Madiwani sita toka Chama cha Mapinduzi (CCM) na Madiwani saba toka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Kwa vile CCM ilishinda pia kiti cha Ubunge cha Jimbo la Kigoma/Ujiji, Mbunge huyo aliongeza namba ya Wajumbe toka CCM kuwa saba na kufanya jumla ya wajumbe wa Halmashauri wa kuchaguliwa kuwa kumi na nneBaadaye Tume ya Uchaguzi kwa mujibu wa kifungu cha 19 (1)(c) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Na.8 ya 1984 iliwateua Wajumbe watatu (3) toka CCM na watatu toka CHADEMA kuwa Madiwani wa Viti Maalum vya Wanawake. Uteuzi huo wa Tume ya Uchaguzi ulifanya jumla ya Wajumbe wa Halmashauri ya Kigoma/Ujiji toka CCM kuwa kumi na wale wa kutoka CHADEMA kuwa kumi pia. Hivyo, idadi ya Wajumbe toka Vyama hivi ililingana na kufanya jumla ya Wajumbe wote wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma kuwa ishirini.

Hali ya Wajumbe toka Vyama vya CCM na CHADEMA kulingana ilifanya iwe vigumu kumpata Mwenyekiti wa Muda wa Kikao ambacho kingemchagua Meya na Naibu wa Meya. Kilichojitokeza ni kuwa pale Mjumbe toka CCM alipopendekeza jina la Mwenyekiti wa Muda, Wajumbe wote kumi toka CCM waliunga mkono na Wajumbe wote kumi wa CHADEMA walipinga. Vivyo hivyo hali hii ilijitokeza pale CHADEMA walipopendekeza jina na ndipo Viongozi wa Kitaifa wa Vyama walipoona umuhimu wa kuingilia kati suala hili.

Tarehe 26 Januari, 2006 Viongozi wa Kitaifa wa Vyama vya CCM na CHADEMA walifikia Makubaliano kuwa Uongozi katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji uwe wa kushirikiana.

Iliafikiwa kwamba, Awamu ya Kwanza kuanzia tarehe 9 Machi, 2006 hadi tarehe 30 Juni, 2008 Mheshimiwa Diwani Kitita Juma Magonjwa wa CHADEMA awe Meya na Mheshimiwa Diwani Yahya Liheye wa CCM awe Naibu wa Meya wa Manispaa. Aidha, Awamu ya Pili itakapoanza tarehe 1 Julai, 2008 hadi tarehe 28 Oktoba, 2008 Mheshimiwa Diwani Nashon Bidyanguze kutoka CCM aliteuliwa kuwa Meya na Mheshimiwa Diwani Shabaan Mambo kutoka CHADEMA awe Naibu wa Meya.

Labda niwakumbushe pia kuwa mgombea wa urais wa Chadema, Dr. Slaa, aliahidi kuunda serikali ya umoja wa kitaifa iwapo atashinda Urais. Alitoa ahadi hizo wakati muafaka na katiba mpya Zanzibar vilikuwa vimeshapitishwa. Swali ni je, alipanga kuunda serikali hiyo kwa ushirikiano na chama gani?
Je, Dr.Slaa alikuwa anaongelea kutengeneza CHADEMA-B, C etc.?
Je, Chadema ni chama kinachotekeleza yale kinachoyaongea?

Complete rubbish, Stupid and nonsense.Hivi huna kazi ya kufanya wewe mpumbavu unapoteza muda wako kuandika utumbo namna hii.Eti kapora mke wa mtu kwani unajua maana ya kupora wewe.Kupora ni kuchukuwa kitu pasipo ridhaa ya huyo mhusika.Kwani huyo aliporwa alilazimishwa kwenda kw slaa.Wewe ni mpumbavu na huna akili hata kidogo it just shows wanachama wa CUF wasivyo na dira wala akili.Si ndio maana mlikimbia kwenda mombasa mlivyo jidai eti hamtambui karume.CUF ni chama cha kidini na maanisha waislamu hamwangalii uwezo wa mtu alimradi tu siyo mwezenu basi.Kwani unafikiri angekuwa mkapa mngekubaliana naye kisa mkristo. Cuf ni chama cha kidini ndio maana top leaders wote ni waislamu.
 
Inawezekana si vyema kwa vyama vya upinzani kushambuliana hadharani ilhali kuna uozo mkubwa zaidi ndani ya chama tawala, lakini ukweli unabaki kwamba CUF HAWAJAJITENDEA HAKI kabisa. Ni kama vile wameamua kutupilia mbali malengo makuu ya chama chao na kuamua "usipoweza kuwashinda, jiunge nao"! Baada ya harakati zote zile, mhanga wote ule, wanakubali "serikali ya umoja wa kitaifa" ambayo hawana sauti nayo kabisa? Bila kuwa na nafasi katika kuchagua mawaziri na viongozi wengine wa taasisi nyeti kama Tume ya Uchaguzi, n.k. unaweza kweli kusema mko pamoja na CCM?

Hata wakati wa kampeni, Maalim alikuwa analalamika mwenzake hapigii chapuo serikali ya umoja wa kitaifa. Haya, Mkapa naye akasema (tena kwa jeuri) kuwa anaunga mkono serikali ya aina hiyo ilmuradi inaongozwa na CCM! Tetesi tunazosikia ni kwamba CUF ndio walioshinda uchaguzi wa Rais lakini ili isiwe taab, wamesalimu amri chapchap - ili kulinda "maridhiano" yaliyofikiwa. Kile kitendo cha "kujaza" viti vya wabunge wa CHADEMA walipotoka nje wakati wa hotuba ya Rais, kinaonyesha jinsi chama hicho kilivyo na mdadi wa kuonekana kinakiridhisha chama tawala katika kadhia zozote zinazotokea.

Swali gumu ambalo CUF hawawezi kukwepa kujiuliza na kutafuta jibu la uhakika ni: kipi hasa walichopata katika maridhiano hayo kulinganisha na gharama ya kukubali kuachia ushindi wao wa dhahiri ukichezewa na CCM huko visiwani? Nimesikia wajuzi wakisema CCM haijawahi kushinda visiwani na ndipo walipopata nia ya kukazania hoja ya "serikali ya umoja wa kitaifa" ili kuendelea kuchakachua bila kero toka kwa mshindani wao mkuu-CUF. Aidha, yapo maswali mengine. Baada ya maridhiano hayo visiwani, nini mustakabali wa CUF huku bara? Kitakuwa na jeuri tena ya kupambana na "mbia" wake huyo kwa upande huu au ndio kauli yake itakuwa ni katika kuikinga CCM dhidi ya mashambulizi ya vyama vingine? Kampeni ya Prof. Lipumba imeonyesha bado CCM ni chama kisichokuwa na uwezo wa kuwaletea Watanzania maendeleo. Prof. amefafanua kitaalamu mambo mengi ambayo CCM inakosea na kutoa mikakati mizuri sana kama ule wa kutoa elimu bure unaofanana na wa vyama vingine - tena yeye kwa ufasaha zaidi. Atapata wapi tena nguvu ya kuwabana CCM kisera katika mambo muhimu kwa taifa hili baada ya maridhiano hayo ya Z'bar yasiyotoa nafasi sawa kwa CUF.

Kwa kifupi, chama cha CUF na wafuasi wake ndio walioumizwa sana na vitendo vya serikali ya CCM hasa huko visiwani. Na CCM haijabadilika. It is still full of crude elements. Labda kama wana mkakati maalum wa kuhakikisha wanabakia kuwa nguvu ya uhakika (a force to reckon with) katika siasa za Z'bar na Tanzania kwa ujumla katika huo mwamvuli wa serikali ya umoja wa kitaifa. Sipendi waitwe CCM-B au chochote kinacholingana na hicho. Lakini bado naamini kwamba mpaka sasa hawajajitendea haki wala hawajawatendea haki wafuasi wao walioweka tumaini lao kwao hadi kujitoa mhanga kiasi kikubwa.
 
Back
Top Bottom