CHADEMA wachezea kichapo cha haja uchaguzi wa mitaa DAR!

CHADEMA wachezea kichapo cha haja uchaguzi wa mitaa DAR!

Naona hapa pro CCM wanatawala uwanja. Wale Pro CHADEMA wanatamani thread hii itolewe.
Afadhali wengine ambao tumeamua kuwa non alliance...
 
WanaJF!

Jiji la Dar es salaa kama wengi wetu tunavyo fahamu kuwa ndio kitovu cha nchi kwa kuwa na jamii za watu kutoa maeneo mbalimbali na wengi wao kuwa na ushawishi mkubwa huko walikotoka.

Wakazi wengi waishio Dar ni watu makini, wenye fikra pevu na zaidi ya yote wana tafakuri yakinifu katika kufanya maamuzi juu ya jambo fulani, hivyo maamuzi yao uwa ni sahihi kwa kiasi kikubwa.

Kitendo cha wananchi KUIKATAA CHADEMA katika ngazi za mitaa ni ujumbe tosha kwa taifa zima kwani ni ukweli usiopingika kuwa, Tanzania ni Dar, Dar ni Tanzania, hivyo kwa msimamo huu wa wakazi wa Dar, uwe ni ujumbe tosha kuwa CHADEMA hawana lao hapa nchini.

Aidha, ni kweli kwamba jiji la Dar linao wabunge wawili kutoka CHADEMA nao ni John Mnyika wa jimbo la Ubungo pamoja na Mdee wa jimbo la Kawe, ila ni wazi kuwa kama CCM ingelikuwa makini katika mchakato wa kura za maoni, leo Mnyika angeendelea na shughuli zake za utapeli mjini na huyo Mdee kwa kuwa ni binti, angeendelea ni viti maalumu.

CHADEMA Dar sio 'SIZE' yenu, huu ni ujumbe tosha kwa taifa.

Unashusha Hadhi ya chama chetu kwa Hoja nyepesi kama hizi,kujadili jadili upinzani ambavyo vimeanza JUZI ni Kupunguza UZITO wa CCM,Wananchi wametoa ridhaa ya kuongozwa Je tunawapa mrejesho Chanya kwa mda wa miaka 52,au tunasubili uchaguzi tutumie nguvu kubwa KUSHINDA sipendi Wanafiki katika chama na nimekuwa nayasema HAYA
"Vox Popoli Vox dei"
 
Huna data wewe punguza kiherehere....
Subiri hesabu ziletwe hapa, kila mtaa mshindi alipata kura ngapi na aliyeshindwa alipata kura ngapi

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Mkuu usitake kunikumbusha mambo ya mwaka 1995 kule Zanzibar. Wakati wa uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vya siasa, Komandoo Salmin Amour Juma alishinda kwa tofauti ya kura chache sana ila yeye akasema hata ushindi wa kura moja ni ushindi tu. Hii ndiyo demokrasia ya sanduku la kura kwamba hata ukishinda kwa kura moja basi unachukua kila kitu. Nakumbuka pia kule Shinyanga mwaka 2010 mbunge aliposhinda kwa tofauti ya kura moja!
 
Naona hapa pro CCM wanatawala uwanja. Wale Pro CHADEMA wanatamani thread hii itolewe.
Afadhali wengine ambao tumeamua kuwa non alliance...
Mkuu naona wewe uliamua kujitoa kabisa hutaki presha sasa chadema wenzangu na mimi leo na wiki yote hii kwa ujumla vijiwe vya kahawa hapa dar havikaliki kabisa.
 
Usikute umehamia kutoka upinzani kazi yako kupiga piga porojo ili tupate IMANI kuwa ni mwenzetu,mimi silipiwi KADI na wagombea nalipa kwa kipato changu,sipendi watu wanaolipiwa KADI na wagombea maana mara nyingi wamekaa kimajungujungu
CC HAMY-D
"Vox popoli Vox dei"
 
Ahsante kwa taarifa mkuu,hivi apo awali kati ya hiyo mitaa ccm walikuwa na w/viti wangapi?nao chadema walikuwa nao wangapio? Nataka kujua
 
Mwenye akili mara zote anafanya tathimini alikotoka, alipo na anakokwenda. Mnatakiwa muangalie awali mlikuwa na mitaa mingapi, sasa kwa nini mumepoteza huo mmoja? Mjaribu kwenda mbali kidogo kuwaza idadi za kura mlizopata awali na sasa. Compare !!

Ukiwa na hesabu butu kama hiz bas n dhahir shahr CCM itakuwepo madarakan kwa miongo mitatu ijayo tena,amka ww watu wa Dar sio fata upepo kama walivo mikoan huko,Wajanja wote tupo Dar
 
Nimefurahi sana yale niliyokuwa nikiandika na kuyasema mtaani kwamba tulimpa mnyika ili kujaribu tu na sasa tumemuona hafai tena hatutarudia kosa,buriani mnyika ubungo kwa heri safi wana ubungo wenzangu nimeipenda sana iyoooo

Usiwe mbulula wewe... Kwani kwenye uchaguzi wa 2010 Mnyika alipata ushindi wa 100%? Si mlikuwepo Maboga wachache ambao hamkumchagua? Sasa mkiendelea kuwepo kuna tatizo gani?
 
hapa dar maisha ndo yanafanya watu wanashindwa kufuata mambo ya siasa wanaona kama ni muda wanapoteza hakika mie ni chadema damu kama kweli tumeshindwa hapa dar basi ni aibu sana na siwezi sema kuwa ukombozi wa nchi hii utaanzia dar bado sana
mtu ambaye Watanzania wengi wanapenda kumtumia kama reference hasa kwenye mambo yahusuyo siasa ni Mwalimu Nyerere.
Nami sasa naanza kupata picha kuwa ni kwa nini Mzee wetu huyu aliona haja ya kuhamisha mji mkuu wa nchi kuwa Dodoma kutoka Dar es Salaam! Mh. Tundu Lissu alitupa angalizo alipofanya mkutano siku moja kule Tabata Liwiti ni jinsi gani watu wa Dar es Salaam wilivyo resistant to change na huu ni mwendelezo wa ushahidi. Lakini hakuna kukata tamaa, watu hawa wanahitaji kujitambua kwa hakika.
 
Leo hawakuzilinda kura zao maana wao wakishindwa wameibiwa..mkome kujiita nguvu ya umma nyie ni nguvu ya wajinga na wavivu wa kufikiri na wapendao vitu rahisi..chama cha ukoo na ukabila..2015 ndo mnazikwa rasmi.
Kweli kabisa maana Baba mwenyekiti, mama mjumbe wa Halmashauri Kuu na mtoto mjumbe wa Halmashauri kuu, mtoto kiongozi wa chipukizi hiki Chama cha Ukoo wa Kikwete.
 
Kati ya chaguzi za kijinga kuliko zote ni hizi za serikali ya mitaa, siyo kwa sababu chama kimeshinda au kushindwa bali kwa sababu namna zinavyoendeshwa. Kanuni zinabadilika kila siku. Huu ni ujinga. CCM walishinda chaguzi za mitaa hapa hapa Dar kwa karibu asilimia zote mwaka 2009, lakini ilipofika uchaguzi wenye kanuni (japo na zenyewe dhaifu 2010) tuliwanyanganya kata kibao na majimbo mawili. Subiri 2015 uone kama mnyika na Mdee hawajaongeza gap ya ushindi na idadi ya madiwani. Mtu asijidanganye na uchaguzi huu ambao kanuni zinabadilika kila mwaka. Umeshawahi kujiuliza kwa nini hawataki kutumia daftari la kudumu la wapiga kura?
 
Kweli kabisa maana Baba mwenyekiti, mama mjumbe wa Halmashauri Kuu na mtoto mjumbe wa Halmashauri kuu, mtoto kiongozi wa chipukizi hiki Chama cha Ukoo wa Kikwete.

TUKUMBUSHANE

1. Matokeo rasmi ya uchaguzi mdogo wa mitaa Magu: CDM yaigaragaza CCM (Feb 2013)
Ulikuwa uchaguzi mdogo wa mitaa miwili, vijiji 6 na vitongoji 37 … pia nafasi 120 za wajumbe wa serikali za vijiji.
CDM ilizoa mitaa yote miwili, vijiji vine (viwili waligawana CCM na UDP), vitongoji 16 kati ya 20 walivyosimamisha wagombea (2 CCM, 1 UDP na 1 CUF), wajumbe wa serikali za mitaa 80.
2. Uchaguzi wa vijiji Kilosa – CDM yaisambaratisha CCM
Mkiti kijiji cha Kifinga- CDM kura 450 na CCM kura 150
Mkiti kitongoji cha Ruaha B – CDM kura 600 na CCM kura 250
3. Uchaguzi mdogo Mbozi – CDM yaigaragaza CCM
Kitongoji cha Mbugani huko Vwawa- Mbozi CDM kura 192 na CCM kura 96. Jimbo hili ndipo anapotoka Mtela Mwampamba aliyefukuzwa CDM hivi karibuni.
4. Uchaguzi mdogo kijiji cha Gedamar, kata ya Gunyoda wilaya ya Mbulu
CDM kura 168 na CCM kura 150
….. nk. Ni kichapo tu from Kagera to Nachingwea …. Wananchi wamechoka udhalimu
5. Exept DAR???!!!
 
Naona hapa pro CCM wanatawala uwanja. Wale Pro CHADEMA wanatamani thread hii itolewe.
Afadhali wengine ambao tumeamua kuwa non alliance...
Hata sisiemu kupiga risasi raia wasio na silaha kama Ponda huna upande, gud!
 
Kati ya chaguzi za kijinga kuliko zote ni hizi za serikali ya mitaa, siyo kwa sababu chama kimeshinda au kushindwa bali kwa sababu namna zinavyoendeshwa. Kanuni zinabadilika kila siku. Huu ni ujinga. CCM walishinda chaguzi za mitaa hapa hapa Dar kwa karibu asilimia zote mwaka 2009, lakini ilipofika uchaguzi wenye kanuni (japo na zenyewe dhaifu 2010) tuliwanyanganya kata kibao na majimbo mawili. Subiri 2015 uone kama mnyika na Mdee hawajaongeza gap ya ushindi na idadi ya madiwani. Mtu asijidanganye na uchaguzi huu ambao kanuni zinabadilika kila mwaka. Umeshawahi kujiuliza kwa nini hawataki kutumia daftari la kudumu la wapiga kura?
Mikael P Aweda

Ndugu matokeo ya JUmla yakoje?
tunaweza kuyapata?
 
Last edited by a moderator:
Mnyika hurudi bungeni 2015 mark my word.Unafaa uwe unambebea Mbowe begi huna unachojua zaidi ya kujipendekeza.
 
Last edited by a moderator:
we unachekesha sana kweli misukule mna kazi! Kwani, ponda na uchaguzi wa Dar vina uhusiano?
Lazima wewe mchumba ucheke kwa kuwa kipigo cha risasi alichopata Ponda ni maagizo ya viongozi wenu, si bahati mbaya. Ponda kapigwa ili concentration iwe kwenye kipigo alichopata.
 
Mkuu naona wewe uliamua kujitoa kabisa hutaki presha sasa chadema wenzangu na mimi leo na wiki yote hii kwa ujumla vijiwe vya kahawa hapa dar havikaliki kabisa.

Wewe ni chadema?......unajua mbinu walizozifanya ccm wakati wa uchaguzi?tuulize tuliosimamia huo uchaguzi tukwambie.
 
Back
Top Bottom