Usistajabu na hilo, wasomi wetu wa sasa hivi uwezo wao wa kufikiri ni mdogo kwasababu anguko la elimu ni la muda mrefu, hivyo wengi walio vyuoni ni wale ushindi wao ni wa kuungaunga.
Wameshindwa kutanabaisha maisha ya dhiki waliyonayo wazazi wao huko vijijini kwa sera mbovu za chama cha zamani, ufisadi uliokithiri kwa viongozi wetu kuanzia ngazi ya M/kiti wa mtaa/ vitongoji.
Sasa hivi kinachotakiwa si vyama bali Nchi yangu Tanzania,
Wasomi wakilijua hilo hawatayumba ktk haya yametekelezwa na ccm, Maisha bora kwa kila Mtanzania? Elimu inashuka kiasi cha huyu aliye chuoni hajui Nchi inaibiwa na viongozi kila uchao.
Ukiangalia kwa vyuo vikubwa kama UDSM NA UDOM Kasi ni kubwa sana.[/QUOTE]