Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,260
- 5,257
Hakuna changamoto kubwa katika maisha ya vijana wetu wanaomaliza kidato cha sita katika elimu kama uchaguzi wa taaluma gani wanatamani kwenda kusomea vyuo vikuu na vyuo vya kati.
Ingawa wengi hutazama suala hili kama ni sehemu ya vijana kuumiza vichwa vyao katika tafakuri zao ila bado linabakia kuwa tatizo la jamii yote, kuna kiwango kikubwa sana cha vijana wanaokosa taarifa sahihi za taaluma ambazo wanachaguliwa achilia mbali mazingira na maisha ya chuo husika. Guidebook pekee haitoshi kumpatia picha halisi kijana huyu.
Kitu pekee ambacho tumepata kukubaliana nacho kama jamii ni kuwa kijana ataelewa mazingira yote ya taaluma pamoja na maisha ya chuoni ndani ya Orientation week, serious!? Orientation week ambayo kwa kawaida inakuwa na mrundikano wa mambo mengi sana, mambo ambayo uongozi wa chuo unatilia mkazo kuwa yakamilike ndani ya wiki hiyo.
Kulipia ada ya chuo, kufuatilia harakati za malazi ya mwanafunzi husika, kumfahamu mshauri wa kitaaluma wako, kufahamu madarasa ambayo utakuwa ukienda na kuhudhuria vipindi, na mbaya ni kuwa kuna wengine inawabidi kusafiri umbali mrefu huku wakiwa hawajui kitawakuta nini huko mbeleni, ingawa wana matumaini kuwa nakwenda kusoma UDSM au UDOM basi ni bahati tosha kwao.
Ni rai yangu kupitia andiko hili, kushauri menejimenti husika za vyuo vikuu vya Tanzania kuandaa expo ili kuweza kuwapatia nafasi wahitimu wa kidato cha sita katika kufahamu na kupata taarifa sahihi na za mapema wakati wakitarajia kuanza kuanza kufanya maombi ya taaluma kadhaa katika vyuo vyenu.
Expo ambazo zitawafungulia mlango wa kuelewa kwa upana wanakwenda kuomba kwenye chuo ambacho kina taaluma zipi, zinahitaji sifa gani pamoja na idadi kamili ya wanafunzi kwa taaluma hiyo. Lakini pia waalikeni walimu wa masuala ya fedha wapate kuwashauri vijana namna bora za kutumia pesa bila kufuja haswa pesa za kujikimu.
Ni katika expo hizi ndipo vijana wanaweza kupata kuzungumza na wafanyakazi wa vyuo husika kutoka vitivo na ndaki mbalimbali na kufahamu kwa kina kuhusu yote yale ambayo ni ya msingi kuhusu chuo husika pamoja na taaluma ambazo hutolewa.
Wakuu wa vyuo vya UDSM, St. John, UDOM, Muhimbili, Mzumbe, SAUT, Nelson Mandela, Ardhi pamoja na vingine kwa kushirikiana na TCU niwasihi kuandaa watalaamu katika Mikoa ya Mwanza, Dodoma, Mbeya, Arusha, Zanzibar pamoja na Dar es Salaam, na kuweka watu walio tayari kuzungumza kwa kina na kuwashauri vijana kuhusu mambo ya msingi katika safari yao.
Hii kwanza itapunguza kwa kiasi kikubwa sitofahamu na mvurugano katika kipindi cha Orientation Week, na kuwafanya wanafunzi kufanya mambo wakiwa tayari wana uelewa na ufahamu wa mambo husika. Kijana asibakie kuamini posts ziliyopo Tiktok na Facebook.
Lakini kwa upande wa pili, expo zitapunguza kwa kiasi kikubwa namba ya wanafunzi ambao hawana sifa husika kupoteza muda na rasilimali fedha katika kuomba nafasi kwenye taaluma fulani kwenye chuo fulani ilihali ni wazi hana sifa za kudahiliwa kwenye taaluma fulani.
Lakini sote ni mashahidi baadhi ya wanafunzi hukutana na matapeli haswa wakiwa safarini wakielekea vyuoni, haswa katika majiji ya Dar es Salaam na Mwanza.
Rai yangu ni sehemu tu ndogo ya mchango wa mawazo ambapo mnaweza kutengeneza ratiba na kufanya expo mkiwa chini ya mwamvuli wa TCU kama mlezi wa vyuo vikuu Tanzania, punde tu baada ya matokeo ya kidato cha sita kutolewa basi mnaweza kuwapatia taarifa watanzania kuwa kutakuwa na expo mahususi kwa ajili ya wahitimu wa kidato cha sita.
Kwa Mwanza mnaweza kufanyia Rock City Mall. Kwa Dodoma mnaweza kufanyia pale Jakaya Kikwete Convention Centre ambapo mtakusanya vijana kutoka mikoa ya jirani. Arusha mnaweza kufanyia expo hii Arusha International Conference Centre. Kwa Mbeya mnaweza kufanyia expo pale Tughimbe Conference Centre, pamoja na Zanzibar ambao inakuwa ikitoa taarifa na msaada kwa vijana kutoka Pemba na Unguja.
Kwa Dar es Salaam mnaweza kufanyia Julius Nyerere International Conference Centre, ambapo mnaweza kuwakutanisha vijana kutokea mikoa ya jirani.
Lakini mnaweza kuzungumza na vituo vya habari ili waweze kuwa na vipindi mubashara pamoja na kuwa na online tv kama Millard Ayo, ITV pamoja na TBC ili kutoa nafasi kwa wale waliopo mikoa ya mbali waweze kupata taarifa, aidha iwe kutoka kwa TCU ama chuo husika.
Katika hili pia mnaweza kuunganisha nguvu na bodi ya Mikopo katika kuwasaidia vijana kupata taarifa sahihi kuhusu vigezo na namna ya kuomba mikopo pamoja na taarifa zingine ambazo mara kadhaa huwa zinatoka vijana wakiwa tayari wameanza masomo.
Prof. Charles Kihampa pamoja na timu yako nzima, kina Dr. Telemu Kassile, Dr. Fikira Kimbokota pamoja na CPA Buyamba Kassanja, fanyeni kukaa chini ya vyuo vikuu vilivyopo Tanzania pamoja na TCU kwa ujumla na kuzungumza kuhusu mpango wa kuwa na expo mahususi za kila mwaka wa masomo kwa ajili ya vijana wetu wapya wanaotarajiwa kuingia vyuoni.
Dr. Jakaya Kikwete ukiwa kama Mkuu wa chuo cha UDSM kwa nafasi hiyo ya kipekee ukiwa Rais mstaafu na mwenye ushawishi mkubwa pamoja na wakuu wenzako wa vyuo mbalimbali Tanzania.
Nina imani kuwa uwepo wa exposition hizi utafungua njia bora sana ya vijana kuongeza mahaba na mapenzi sio tu katika taaluma zao bali pia katika vyuo husika.

Tunaijenga Tanzania moja kwa manufaa ya watanzania!