Kasi ya Rais Samia yawapoteza CHADEMA katika ramani ya siasa, hakina tena ushawishi kwa Watanzania

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,024
9,442
Ndugu zangu Hivyo Ndivyo Hali Ilivyo kwa Sasa, Kasi ya Rais Samia kuwatumikia watanzania wa makundi yote,vyama vyote, Rika zote, jinsia zote, Kanda zote, Dini zote,makabila yote,maeneo yote na watu wa Hali zote bila ubaguzi wa aina yoyote kumeipoteza Chadema Katika Ramani ya siasa hapa nchini na kubakia chama Cha kurukia vimatukio vya kupita kama upepo.

Hii inatokana na kazi kubwa ya Rais Samia aliyoifanya ndani ya muda mfupi katika kuwatumikia watanzania, kila kundi na kila mtu kwa Sasa anamuona mama Samia kuwa Ni Rais wake, Ndio sababu ukienda secta binafsi utakuta anapongezwa kwa kuweka mazingira mazuri ya kiuwekezaji, ukienda kwa wafanyabiashara utakuta wanampongeza kwa kufanya mazingira ya biashara kuwa rafiki kwao.

Ukienda kwa wakulima utakuta anapongezwa kwa namna alivyo wasaidia wakulima kupungua kwa Bei ya mbolea na kupongezwa kwa bajeti ya Wizara ya kilimo kuongezeka, ukienda kwa wanafunzi wa vyuo vikuu utakuta wanampongeza kwa namna alivyowasaidia kupata Elimu baada ya kuwa wamepewa mkopo wa elimu ya juu, ukienda kwa wafugaji, wavuvi, wajasiriamali, bodaboda, machinga, watumishi wa umma, vijana, wazee,wakina mama wote utakuta wanampongeza Rais Samia kwa kuwasaidia katika shughuri zao na kuwawekea mazingira wezeshi.

Makundi haya ambayo yanamuunga mkono mama Samia Ndio yalikuwa Tegemeo la Chadema kuendeshea propaganda zake na kupandikiza chuki kwao ili waichukie CCM na serikali yake, Ndio maana ulikuwa ukiona makundi haya muda mwingi yanatupa lawama kwa serikali kuwa inayadidimiza kiuchumi, wafanyabiashara wakawa wanalia Sana kuwa wanakomolewa Sana katika suala Zima la ukadiliwaji wa kodi, hivyo wakawa wanawaunga mkono upinzani na hata kuwachangia fedha.

Lakini kwa Sasa baada ya Rais Samia kukaa na viongozi wa makundi Tofauti Tofauti ikiwemo viongozi wa machinga, kukaa na wachungaji, maaskofu, mashehe, vijana na wengine wengi na kuweza kuwasikiliza na kutatua kero zao na kutoa matumaini, Sasa makundi haya yamejenga Imani kubwa Sana kwa Rais mama Samia, yanamuunga mkono Rais kwa Sasa, yanamsikiliza na kumheshimu mh Rais kwa Sasa na yanajivunia Sana mama Samia kuwa Rais wao.

Hapa ndipo upweke wa chadema ulipoingilia maana kwa Sasa chadema imepuuzwa, haisikilizwi na mtu, haiungwi mkono na mtu, haifuatiliwi na watu Kama zamani, haina ushawishi kwa kundi lolote huku mitaani, Haina ngome ya kundi lolote au mkoa wowote, Haina mizizi yoyote kwa Sasa,imebaki Kama Tawi tu linaloelea na linalosubili kuangushwa na upepo mdogo tu, Chadema imekata Tamaa Sana, imejichokea,imepoteza mvuto kwa watanzania wa Rika zote.

Chadema kwa Sasa haina Sera Wala ajenda za kueleweka na wananchi, lakini kibaya zaidi Ni kuwa imekosa Dira na muelekeo hivyo kubaki inaenda tu Kama gari iliyokosa Taa usiku, Hii ni kutokana na kuwa mama Samia kabeba Sera na ajenda zote muhimu zenye kugusa maisha ya watanzania wa makundi yote na Rika zote na hivyo kuungwa mkono na makundi hayo yote.

Poleni Sana chadema, Ukurasa wenu ulishafungwa na watanzania, mizizi yenu ilishatupwa baharini,Huwezi kusimama Tena, wakati wenu ulishapita, Hamna namna zaidi ya kumuunga mkono Rais Samia kwa Sasa, msione aibu maana Wote Tupo na Samia, wote waliopoteza matumaini Sasa Wana matumaini na Imani na Rais Samia kuwavusha darajani, msishupaze shingo zenu maana mtaishia kuumia tu, watanzania hawana habari nanyi Tena ndio maana hawawasikilizi kwa lolote zaidi ya kuwapuuza tu na kuwaona wababaishaji, Huku Rais Samia akizidi kuchanja mbuga katika MIOYO ya mamillioni ya Watanzania.

Kazi iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti

Lucas Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
 
Chadema hawajui techniques za kisiasa , either hawako serious au ni washamba wa siasa , mwanasiasa Hana adui wa kudumu wala rafk wa kudumu , wakati Maghufuli yupo walikuwa na uadui naye , Jambo ambalo ni move nzuri kisiasa , Maghufuli alikuwa na maadui wengi pia ndani ya CCM , Jiwe amekufa walivyo hawajitambui wakaungana na CCM , wakaanza kumsifu Samia , bila kujua kuwa hyo inawaua kisiasa , kama unamsifia Leo kivip utakuja kumpinga kesho...

Badala ya kumtumia Jiwe kama ngazi , wanaenda kukumbatia kichaka cha mabua , watakula jeuri yao
 
Tatizo lako unadhani Chadema ndio tatizo la nchi. Chadema ni political competitor wa CCM. Halafu kuwa mzalendo sio kuwatukana Chadema kila siku.
Hapana mkuu wangu Mimi siwatukani chadema Ila nawaeleza ukweli naouona kwa kuiangalia chadema ya Sasa na Ile ya 2015 kurudi nyuma Hadi 2010 ambapo ndipo ilikuwa imepamba Moto na kuwavuta vijana wengi na watu wengi kuiunga mkono na kujiunga nayo
 
Chadema hawajui techniques za kisiasa , either hawako serious au ni washamba wa siasa , mwanasiasa Hana adui wa kudumu wala rafk wa kudumu , wakati Maghufuli yupo walikuwa na uadui naye , Jambo ambalo ni move nzuri kisiasa , Maghufuli alikuwa na maadui wengi pia ndani ya CCM , Jiwe amekufa walivyo hawajitambui wakaungana na CCM , wakaanza kumsifu Samia , bila kujua kuwa hyo inawaua kisiasa , kama unamsifia Leo kivip utakuja kumpinga kesho...

Badala ya kumtumia Jiwe kama ngazi , wanaenda kukumbatia kichaka cha mabua , watakula jeuri yao
Wanamuunga mkono mama yetu mpendwa mama Samia baada ya kugundua ukweli kuwa Rais Samia Ni zawadi kwetu watanzania na kwamba viongozi aina ya Rais Samia Hawazaliwi kila Siku Na hawapatikani kila nchi,
 
Chawa naona umeleta gazeti jingine leo ukijaribu kupima upepo. CCM ni chama cha wazee sio cha kizazi hiki.
Tindo rafiki yangu lazima ukubali ukweli kuwa CCM kwa Sasa ndio chama pekee katika Bara Hili la Afrika kilichofanikiwa kupata uungwaji mkono kutoka makundi yote kutokana na Sera zake na ajenda zake zinazogusa maisha ya makundi yote, lakini pia Ni chama kinachobadilika kulingana na wakati, Sasa chama Kama Chadema kitabadilikaje kifikira wakati Mwenyekiti Ni yule Yule miaka na miaka? Mwenye mitizamo na fikra zile zile uchaguzi Hadi uchaguzi?
 
Chadema akipotea wewe pangu pakavu unafaidika na nini? Tozo zinaondoka? Mgao wa umeme/maji unaisha?
Tozo Ni kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu, lazima tuijenge nchi yetu kwa mikono yetu wenyewe na tujivunie maendeleo na mafanikio yanayotokana na jasho letu wenyewe,
 
Tatizo lako unadhani Chadema ndio tatizo la nchi. Chadema ni political competitor wa CCM. Halafu kuwa mzalendo sio kuwatukana Chadema kila siku.
Wewe hata mama yako unamtukana. baba ndiyo kabisa mnagombea wanawake. kama huwezi kuwaheshimu wakubwa walioko Chadema, basi hata mama yako unaweza,,,,..;;'p[]=-0
 
Back
Top Bottom