CHADEMA vs CCM: Nani Mbabaishaji?

"mbowe lazima aongee muda mrefu na kuvaa magwanda ya mgambo ili apate muda wa kujieleza JK alikua na MANEFESTO mbowe hana,JK alikua anaendeleza manefesto na dira ya ccm mbowe hana na jk aliamini anawaelewesha wenye kuelewa hakujua wapo wanaopenda aongee muda mrefu ili uweze kuelewa"

JK mwenyewe alikuwa amekariri ILANI au alikuwa haelewi anasema nini. Mojawapo ya ushahidi ni kushindwa kuelewa kuwa yeye ndiye alikuwa kinara wa kunadi hoja ya Kadhi ambayo leo anakanusha kuhusika nayo. Nashindwa kumuelewa kwanini alikuwa makini kunadi ilani asiyoimani '

"ASHA GO TO SCHOOL pia inawezekana walioandika kua JK anshangaa umaskini walichukua kipengele cha maneno yake ili kiweze kuwafurahisha wapenda mipasho kama ww thats why my first comment ulifananisha na mipasho inawezekana ikaw ni intrest yako"

Tafadhali tujenge hoja kuliko kushambuliana, huwezi kumwambia mwenzako arudi shule, wakati hata wewe huna uhakika na unachokiandika. Nini maana ya neno inawezekana? Inaonyesha hata wewe umesukumwa na hisia tu.

"Jiulize rai linafikaje kwetu KANTARAMBE,au SHIRATI,MASIKE,NYAKARERE,INGRI,KIROGO etc ambako ilani ya ccm imefika through ofisi za matawi au through mabalozi wa nyumba kumi."

Ni kweli ilani ya CCM imefika maeneo yote hayo, hata mimi naongezea Ushokola, Chakabwimba, Vudee, Mugumu na maeneo mengine mengi tu kupitia "fedha" za walalahoi zinazopatikana kupitia mikataba ya kisanii. Mtoa hoja hii najua umeisoma vizuri sana ILANI hiyo, sasa naomba uniambie ni asilimia ngapi ya mambo yamekwishatekelezwa ndani ya hii miaka miwili.

"Imekua ni agenda yako binafsi kila ukiandika bila kutaja KIKWETE LOWASA ROSTAM MAKAMBA gazeti halijaenda kiwandani"

Ni kweli hili unalolisema, lakini kumbuka kuwa waandishi wanajua wananchi wamepigika sana hivyo wananunua habari yoyote ambayo wanadhani itawaonyesha kwanini wananendelea kupigika wakati wanaona kuwa Viongozi wao wanaishi maisha ya kusadikika. Lazima JK,EL na timu waulizwe kwa sababu waliapa kufanya kazi kwa maslahi ya Watanzania wote.

"Ndugu zangu fikieni mahali uzalendo usitafsiriwe vibaya nashauri KUBENEA na watu kama STEPHEN RAMADHANI,NDIMARA kueni more objective kujenga TAIFA hili na specifically kubenea nakua na shaka na elimu au uwezo wa kufikiri na kama unatumiwa angalia usije kuharibu UTU wako"

Hapa tusidanganyane, magazeti ya Uhuru, Mzalendo, Rai, Mtanzania n.k. sasa hivi hayana tofauti na Mwanahalisi. Yamekuwa yanaendekeza proganda za CCM kiasi kuwa hata issue ndogo tu, utasoma "JK avunja rekodi, kuileta Real Madrid n.k Tutafika kweli?
 
Mugo,
umechangia vizuri lakini niruhusu kuchangia mambo mawli.
1.Kuhusu Kadhi, ukisoma ahadi ya CCM kwenye ilani utajua kwamba JK hakukosea kitu na issue yenyewe iko on track. Jaribu usome ile sentensi vizuri usiache ukaletewa yaliyohaririwa.
2. Kuhusu asilimia ya utekelezaji, siamini kwamba bila kufanya utafiti unawezapata asilimia ya kweli lakini binafsi kulingana na ilani yao ukiacha utashi wetu jamaa wanachanja mbuga ndio maana confidence wanayo sana. Suppport ya MCC itawapaisha.
 


Majigambo yako yote kumbe hewa. Hapa umedhihirisha u msomi asiyesoma. Hujui kama Rai walichapa ilani za vyama vikuu kwa ridhaa yao bila malipo toka kwa chama chochote? Hivi ndivyo walivyosema wakati wanazichapa ilani. Nimetumia mfano wa gazeti kama ushahidi tosha kuwa CHADEMA walikuwa na ilani tofauti na kauli yako kuwa CHADEMA haikuwa na ilani. Mimi nilipata ilani ya CHADEMA kijijini kwetu Jang'ombe, hivyo walisambaza.

Usitudanganye, wajumbe wa nyuma kumi wengi hawakupewa ilani ya CCM

Nijibu maswali yangu basi jamani weeeeh

Asha
 

Tuwekee nakala ya walichoandika ili tujadili vizuri. Usije ukapindisha ukweli bureeeeeeeeeeeeeee

Sijaliona, ni gazeti la tarehe ngapi hivi?

Kumbe mwanahalisi nalo gazeti lilowachoma eeeh, nilidhania ni Raia Mwema tu

Asha
 


Well sijui kama ndio ilikuwa ilani ya 2005 au sera za Jumla za Chadema lakini tazama hapa
Kwa hiyo na wewe asha unayetupeleka kwenye magazeti yaliyo-offline unaturudisha nyuma.
 
Tuwekee nakala ya walichoandika ili tujadili vizuri. Usije ukapindisha ukweli bureeeeeeeeeeeeeee

Sijaliona, ni gazeti la tarehe ngapi hivi?

Kumbe mwanahalisi nalo gazeti lilowachoma eeeh, nilidhania ni Raia Mwema tu

Asha
ASHA NI MWANAHALISI LA 28TH Pg Namba 8 to 9,inaonyesha hausomi magazeti.
 
Iwe mtoto wa mkulima watokea Kaisho Ama isingiro?
watokea Oumrushaka ama katerero?

Hoja hapa ilikuwa nani mbabaishaji kati ya CCM na CHADEMA, sasa nashangaa unatumia uwanja huu huu kuanza kulishambulia gazeti la mwana halisi na hapo hapo unamshauri dada Asha aende shule eti kwa wewe kufika chuo kikuu unaona kuwa Asha kutokwenda ndio kunamfanya anashindwa kujua mambo hukumbuki kuwa ni hao hao waliochangia elimu yako kwa kodi zao.

Unasahau kuwa hata wangekuwa wanaouwezo wa kufika chuo kikuu kama wewe CCM haikuwa imeandaa vyuo vya kutosha kwenda kusoma ,

Unashindwa kulinganisha matatizo ya CCM kiutawala na umasikini wa watanzania.

Unashindwa kusoma hoja za mwanahalisi na jnsi Ngeleja alivyojikuta yupo kwenye wizara hiyo unasahau kuwa huyu kijana alikuwa ni mwanasheria wa vodacom na vodacom na RA nafikiri unajua mahusiano yao.

Unashindwa kujiuliza kwa nini DR. Rashidi apewe kuwa MD wa VODACOM wa baada ya kutoka kuwa gavana wa kule BOT na sasa yupo TANESCO nako huko ni nishati na madini.
Una kumbukumbu kuwa pesa za EPA zinzofanyiwa auditing leo zilipotea lini?
Unalijua kampuni linaloitwa Kagoda Agricultural ltd ni mali ya nani?unajua linahusika na wizi wa pesa za EPA?

Nakumbuka kuna siku nilikuwa kwenye club moja jijini na baadhi ya viongozi wa serikali hii ya ccm na mmoja wapo alikuwa ni waziri akasema kuwa tatizo ni kukosekana wa kumfunga paka kengele kwani wanawajua ,tena kwa majina ila hakuna wa kumwajibisha mwenzake.

Kuna haja ya watanzania na haswa hao walosoma kama huyu anayejiita mtoto wa mkulima japo inawezekana ni wale wakulima wanaopewa mbembejeo kutoka BOT kwa kisingizio kuwa ni wajasiriamali kulionea huruma taifa hili, kama unaona kuwa wanaopiga kelele na kusema hawafai jua kuwa taifa hili haliwezi kupona kama hapatakuwepo na watu wa kusema na nilitarajia msomi kama wewe uwe wa kwanza kutuelimisha sisi ngumbaru wa elimu ya zamani na sio kumponda Asha ,ukweli kimeniuma sana .

Naomba tena mwenye tamko la Chiligati juu ya maazimio ya CHADEMA aweke hapa ili tuweze kjujua nani mbabaishaji kati ya vyama hivi viwili.
 

Naona wewe sio mfuatiliaji wa siasa kama unavyodai kwani kama unashindwa kuelewewa jambo dogo kama kuwa IGP, sio lazima uwe mtu wa chama cha siasa na jua kuwa hawa ni viongozi kutokana na proffession zao sio wanasiasa hawa ni watendaji.

Usifikiri eti siku wapinzani wanachukua nchi basi watabadilisha kila mtu huo sio uongozi na ndio kitu kinaifanya CCM leo wanashindwa kutawala ni kuwataka hawa watu ambao sio wanasiasa kufanya kazi kwa mashinikizo ya kisiasa na hilo linaondoa ufanisi wao .

Jua kuwa sio wote walioko CCM kuwa ni mafisadi na haiwezekanni eti wapinzani wakakosa watu waadilifu think beyond the box, usiwaangalie wale walioko mstari wa mbele tuu bali angalia kwenye NGOS, TASISIS ZA KIDINI,KITAALUMA N.K. then unaweza kuwaona viongozi wazuri tuu wa kulikomboa taifa hili.
 
Posted Date::2/18/2008
Viongozi sita Chadema wajeruhiwa vurugu za uchaguzi
Na Mussa Juma,Kiteto
Mwananchi

VIONGOZI sita waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoka makao makuu ya chama hicho, wamejeruhiwa vibaya mmoja akiwa mahututi baada ya kupigwa na kuchomwa visu na kundi la vijana wanaodhaniwa kuwa ni wa CCM na Polisi katika vurugu za uchaguzi Jimbo la Kiteto ambalo lipo wazi baada ya aliyekuwa mbunge wake, Benedict Lusulutya (CCM) kufariki dunia hivi karibuni.

Licha ya kupigwa viongozi hao pia walimwagiwa kemikali machoni ambayo bado haijafahamika na kusababisha kutoona kwa zaidi ya nusu saa na mmoja wao hadi jana macho yalikuwa yake hayaoni.

Vurugu hizo zilitokea katika kata ya Kijungu wilayani hapa juzi majira ya saa 12 jioni , baada ya kundi la vijana hao maarufu kama Green Guard kutoka jijini Dar es Salaam, kuvamia viongozi hao wa Chadema wakiwa katika ofisi yao ya kata ya Kijungu kwa tuhuma za kuwapigia kelele wakiwa katika eneo lao la mkutano.

Waliopigwa ambao hadi jana asubuhi hali zao zilikuwa mbaya na wengine kulazwa katika hospitali ya wilaya hiyo ni Hamadi Mussa Yusuph Naibu katibu mkuu wa Chadema Zanzibar, Juju Danda, Afisa mwandamizi kurugenzi ya bunge na halmashauri kuu Taifa.

Wengine ni Joseph Freme(43) Mwenyekiti wa Ruvuma Chadema na mjumbe wa kamati kuu,Msafiri Mtemelwa, Kaimu Mkurugenzi wa kampeni na Uchaguzi,Selemani Mohamed mjumbe wa uchaguzi Kiteto.

Katika sakata hilo, dereva wa gari la makao makuu Daudi Baraka ndiye alijeruhiwa vibaya kwa kuchomwa visu na kupigwa vibaya ambaye hadi jana hali yake ilikuwa mahututi akiwa anaongezewa maji na kushonwa nyuzi kadhaa.

Freme alisema licha ya kupigwa viongozi hao, pia walikamatwa na kupigwa na polisi wa kituo kidogo cha Kijungu ambao awali walikuwa pamoja na viongozi wa CCM, Katibu Mkuu Yusuph Makamba na Makamu Mwenyekiti Pius Mswkwa.

"Sisi hatukupigwa sana na green guard pale ofisini lakini tulipofikishwa kituo kidogo cha polisi kijungu ndipo tulipigwa sana japo kuwa tayari mwenzetu alikuwa amechomwa kisu ubavuni," alisema Freme ambaye alikuwa hajaweza kutembea hadi jana.

Hata hivyo alisema mara baada ya kuona wakipigwa ovyo, alipiga simu kwa IGP na baadaye aliambiwa awasiliane na mkuu wa polisi mkoa wa Manyara ambaye baadaye ndiye alituma polisi kuja katika kituo hicho kutoka makao makuu ya wilaya hiyo umbali wa takriban kilometa 70.

Viongozi hao, waliashiwa na polisi majira ya saa tano usiku baada ya juhudi kubwa zilizofanywa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa,Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na Mbunge wa viti maalum Grace Kiwelu.

Viongozi hao mara baada ya kuandikisha maelezo yao kwa mkuu wa polisi wa wilaya ya Kiteto,Archi Killo waliachiwa kwa dhamana na kupewa hati ya matibabu PF 3 na walitakiwa jana asubuhi kuripoti polisi.

Akizungumzia mgogoro huo, Msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Kijungu, Ibrahim Mdugo alisema vurugu hizo zilianza majira ya saa 12 jioni baada ya kundi la vijana hao wa CCM kuanza kulalamikia kelele kutoka kwa viongozi hao wa Chadema waliokuwa wakisimamia kwaya yao iliyokuwa inafanya mazoezi.

Mdugo alisema awali viongozi hao wa Chadema walikuwa na gari lao wakitangaza watu kujitokeza kupiga kura Februari 24 bila ya woga wakitumia vipaza sauti ambavyo CCM waliokuwa katika mkutano ulikuwa unahutubiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa,Pius Msekwa walikuwa wanalalamikia.
 
watu wamepigwa kweli labda wengine watauwawa kweli na ninani huyo atakuwa na muda wa kukuuwa hapa kwenye net?!
 
Date::8/5/2008
CCM imeanza lini kuisaidia Chadema?
Mwananchi

JANA katika safu hii tuliwaasa wanasiasa hasa viongozi wa kambi ya upinzani, kwamba si busara wala Uafrika kutumia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime (Chadema), Chacha Wangwe, kama mtaji wa kujiongezea umaarufu.

Kabla hata wino ulioandika tahariri hiyo haujakaula, Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho si tu kwamba ni chama tawala, ila kikongwe kwa maana ya kujua maadili na miiko ya kujitafutia umaarufu wa haraka miongoni mwa wananchi kwa vitu kama misiba, kimejitwalia dhima ya kusambaza waraka unaodaiwa kuwa ni wa marehemu Wangwe.

Habari za CCM kufanya kazi hiyo tulizichapisha jana katika toleo la gazeti hili ukurasa wa kwanza na inaonekana kwamba ni mpango ambao umeasisiwa ndani ya chama hicho kwa kuwa taarifa hizo zinasambazwa kupitia ofisi za chama za mikoa.

Tunafahamu vyama vya siasa vina kila sababu ya kujitafutia umaarufu na hivyo kuungwa mkono na wananchi ili, kama chama kipo madarakani, kiendelee kushika madaraka, na kwama ni cha upinzani, kikubalike na hivyo kupewa ridhaa na wananchi ya kuongoza dola.

Lakini sisi hatuwezi kuunga mkono kikundi au mtu yeyote anayetaka kutumia kifo cha raia mwingine ili kupata umaarufu wa kisiasa. Tunasema hivyo kwa sababu hadi sasa kinachojulikana ni kwamba chanzo cha kifo cha Wangwe ni ajali ya gari iliyotokea Julai 28, 2008 kijiji cha Pandambili, wilayani Kongwe, Mkoa wa Dodoma.

Kwa mantiki hiyo, tunaamini kwamba hadi sasa Wangwe alikufa kwa ajali. Kwa hiyo mengine yote ambayo yanasukumwa na wanasiasa kwa manufaa yao ya kisiasa tunaamini kuwa si haki, na kwa kweli tusipokuwa macho tutajenga utamaduni mbaya wa kuzushiana mambo na hivyo kuwa mwanzo wa kuporomoka kama taifa.
 
Chama Cha Mafisadi, kimejaa mafisadi wanaojali matumbo yao tu na maslahi ya chama chao. Hawana hata cembe ya ubinadamu kwa jinsi walivyokuwa manyang'au na kutaka kutumia msiba kujinufaisha. CCM kwa kifupi imeoza na hivyo pamoja na kuwa Watanzania wengi hatupendi wanavyotaka kutumia kifo na waraka huo unaosemekana uliandikwa na Wangwe. Mkuu wa Chama hicho msanii JK amekaa kimya wakati chama chake kinafanya mambo yasiyokubalika na Watanzania walio wengi. Kwa mara nyingine tena ameonyesha jinsi alivyo na uwezo finyu wa kuongoza chama hicho cha kifisadi. Kwa kifupi CCM imemshinda kuiongoza kama vile alivyoshindwa kuiongoza Tanzania
 
Heshima Mbele,

Kwa mujibu wa habari nilizozipata toka Nyumbani Tanzania,na zimeandikwa katika moja ya magazeti ya leo huko Nyumbani ni kwamba Marehemu Chacha Wangwe alikuwa na mpango wa kuiacha CHADEMA na kuhamia CCM,na kabla ya kuhama alikuwa amepanga kuanika wazi wazi yale ya CHADEMA na ugomvi wao.

na lengo la kusambazwa kwa waraka ule kwa viongozi wa CCM ilikuwa ni kujiandaa na kumpokea Marehemu chacha Wangwe.

Masikini Chacha wangwe umetutoka kabla ya kueleza ukweli
 
Last edited by a moderator:
MKuu hapa hawa CCM kwa taarifa yako CHADEMA wamekuja juu wanataka Makamba ahojiwe kutokana na CCM kusambaza waraka nchi nzima kuhusu ishu ya Chacha siku moja kabla ya kupata ajari.
 
Hizo ndo zile propaganda za Wanasiasa wa Bongo; kuhamia CCM ingemaanisha anapoteza Ubunge wake ambao aliupata kwa gharama kubwa ya watu kuwa tayari kupoteza maisha kwa ajili yake. Kama ni hivyo haingekuwa bure CCM wangemnunua kwa bei kubwa sana na kwa kuwa wana mapesa ya kifisadi hilo linawezekana.
 
MKuu hapa hawa CCM kwa taarifa yako CHADEMA wamekuja juu wanataka Makamba ahojiwe kutokana na CCM kusambaza waraka nchi nzima kuhusu ishu ya Chacha siku moja kabla ya kupata ajari.
Na ingekuwa ni vyema Makamba akajibu a kuhusu hili la Wangwe kutaka kuhamia CCM.Hii ni habari nene..

Nimeambiwa habari hii iko katika Gazeti la Raia mwema la leo,nimemwambia jamaa aliscan na anitumie..
 

Inavyoonekana walishamunua siku nyingi,Kuna yale maneno aliwahi kuyasema MP kwamba Chacha lishwahi kuongea na RA pale Kempski..mie namuomba aje hapa.

Alafu Mod,
inakuwaje mie naweza breaking News wewe unasema TETESI?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…