CHADEMA vs CCM: Nani Mbabaishaji?

Chadema Vs Ccm Nani Mbabaishaji?

CCM ina miaka karibu 45 sasa, na Chadema ina miaka karibu 20 sasa, hivi kweli within miaka yote hiyo ya uhai wa Chadema, na CCM hili swali halijajibiwa? Kama ni mafisadi ni ishu ya sheria sio siasa it has nothing to do na CCM kwa ujumla"

Umejitahidi kujenga hoja juu ya Ushindi wa CCM lakini umesahau facts kuwa kuna baadhi ya "Watanzania vijijini wanaofikiri kuwa bado Mwl. Nyerere(R.I.P) ni Rais". Laiti watanzania hasa wa vijijini wangekuwa na mwanga juu ya siasa, uchumi na sera basi wasingekubali kumpa mtu ambaye "HAJUI KWA NINI TU MASKINI" CCM kutawala ni mchanganyiko wa mambo mengi kuanzia wizi wa kura, kutumia vyombo vya dola(VITISHO na hata KUTOA VIBANO), Tume ya Uchaguzi(wasimamizi wote wanachaguliwa na Rais), Rushwa, Ukosefu wa elimu ya Uraia miongoni mwa wadanganyika na mengine mengi tu. Ni kweli CCM kuna kuna zaidi ya timu tano za uongozi(Lakini zote hizo zimeshindwa kumshauri JK kuwa tunatembea kinyumenyume badala ya kwenda mbele. WanaJF, tuombe kwanza CCM watujibu kwanini sisi WADANGANYIKA ni maskini"
 
FMES,

Nakubaliana na wewe kabisa kwenye hili, huwaga kila nikijiuliza je CHADEMA kwa sasa ilivyo yaweza kupewa na kuongoza nchi? naanza na kuhesabu viongozi ambao iliyonayo sasa, kwa ajili at least kuunda baraza la mawaziri dogo kuliko yote hapa duniani lenye uwiano na nchi yetu... naona haiwezekani maana majina hayafiki kumi (vidole vya mikono yangu miwili) nikishafikiri hivyo narudi nyuma nikisema wajameni tujizatiti vijiji, tujizatiti kupata angau 30% ya wabunge hapa tutake sasa kuongoza nchi hii

Sisi watanzania ni moja kati ya jamii lazy hapa duniani.Wengi wetu tunapenda sana kufanyiwa mambo na tuyakute tayari yako ndani ya order.Hakuna anayependa kushiriki pamoja na wengine ili kuleta mabadiliko,wengi wetu tuko nyuma tukisubiri hao waliotangulia watafanya nini na kilichobaki ni kusema hakuna mtu.Nimahodari sana sisi wa kulalamika lakini inapofikia kutenda tunakimbia.
Kwa kuwa tumeshajijengea utando wa kutokuwakubali watu walioko upande zaidi ya CCM,tumekwisha jizuia kuwaamini kuwa wanaweza kutenda.Ila tuko tayari kuwakubali watu wasio na record nzuri ili mradi ni CCM.
Ndani ya upinzani kuna watu wazuri na makini sana.Hakuna aliyekuwa anamtambua Zitto kabla ya kuwa mbunge!!Leo kawa mbunge na kapata mahali pa kusemea ndo tunakubali kuwa anafaa na huyo si wamwisho liko genge kubwa lenye uwezo kama wake ila kwa uchafu wa siasa za Tanzania wanashindwa kupata nafasi ya kuingia katika medani kama ya akina Zito ili wapate onekana.
 
Kuna watu wanasema kuwa eti CHADEMA ni Dr.Slaa, Lissu na Zitto, huu ni upunguani kwani haiwezekani chjama kikawa ni watu watatu.

Kamati kuu yao katika kudodosa kwangu naambiwa kuwa ina watu kama;
1 PROF;BAREGU, ADVOCATE MBOGORO, BALOZI NGAIZA,ADVOCATE AKOONAY MUSTAPHER, SUZAN LYIMO MBUNGE, NK.

hapa kutowajua sio kwamba hawapo na pia kuunda serikali sio lazima kuweka wacahdema tuu kumbukeni hapa kuna CUF, NCCR NA TLP.

nASHAWISHIKA KUONA UBONGO WA HAWA WANAOTAKA KUJENGA DHANA POTOFU KWA WATU MAKINI KAMA WA HAPA jf KUWA chadema INA UKOSEFU WA WATU WA KUTAWALA.

WAMETOKA NA TAMKO LA KAMATI KUU AMBALO NI MOTO JE?LA CCM LIKO WAPI JAMANI?
 
Afadhali Mbowe alikuwa anajua chanzo cha umasikini wa watanzania kabla hata ya kwenda kusoma zaidi. Kikwete hata baada ya kusoma na kukulia serikalini bado haielewi kwa nini Tanzania ni masikini. Kuendelea kumuacha pale ikulu ni kuendelea kuwatukuna watu wote wenye akili Tanzania. Kila siku unapigia kelele ushindi wa asilimia 80 kuhalalisha uwepo wake pale ikulu, unachosahau ni kuwa ushindi ule umepatikana kwa mizengwe- hauendani kabisa na uwezo wake wa kiasiasa pale kikwete. Asilimia 80 si kipimo cha imani ya watanzania kuhusu uwezo wa Kikwete, labda matumaini waliyolishwa kwa ahadi hewa tu ambayo sasa yamesalitiwa na wameanza kumnyooshea vidole. Ukipiga kura za maoni huru sasa hata asilimia 20 atapata kwa tabu. Ushindi wa Kikwete=Propanda za Mtandao toka 1995(za kuwabomoa wakina Malecela, Salim, Mwandosya na za kuficha udhaifu wa JK)+ Udhaifu wa upinzani(mara baada ya 1995 hususani kupomoromoka kwa NCCR Mageuzi)+ Kampeni za Rushwa( yeye mwenyewe amekiri+ Mahakama imethibitisha kwa kufuta takrima)+chama Dola(Mkapa alitangaza hadharani+ Tume ya uchaguzi ikatekeleza maeneo mbalimbali). Sasa anza kutoa kimoja hadi kimoja utaona kwamba huyu jamaa kama alikuwa anakubalika kwa asilimia 80 au la.

Kikwete ni mzigo kwa taifa! period

Kama CCM mtaendelea kudhani ni tumaini lilirojea mtandelea kuwakatisha tamaa watanzania na hakika Kikwete ataondoka na kina Rostam na Lowasa wake lakini Tanzania itasimama milele.

FMES, kwani Kikwete na JSM au SAS nani bora?

Asha
NADHANI DADA YANGU UMEGUBIKWA NA MAWAZO FINYU YALIYO BARIKIWA NA KAULI ZA WAANDISHI WA MWANAHALISI ULICHO ONYESHA NI PURE MAWAZO -VE YA WALIOPOTEZA DIRA NA MUELEKEO.NANI KASEMA MBOWE ANAJUA HUO UMASKINI MNAONGELA NANI KASEMA JK HAJUI HUO UMASKINI WA WATANZANIA?KUENI OBJECTIVE ACHENI BLA BLA ZA WATU KAMA NDIMARA ALIEANDIKA MAKALA KTK MWANAHALISI LA 28TH NOV.
 
NANI KASEMA MBOWE ANAJUA HUO UMASKINI MNAONGELA NANI KASEMA JK HAJUI HUO UMASKINI WA WATANZANIA?KUENI OBJECTIVE ACHENI BLA BLA ZA WATU KAMA NDIMARA ALIEANDIKA MAKALA KTK MWANAHALISI LA 28TH NOV.

Wewe ulikuwa wapi wakati JK anasema kuwa hajui kwa nini Tanzania na watanzania ni masikini?

Naona somebody anahitaji kuwa objective hapa kabla ya kuanza kutoa lecture ya objectivity na kupondea gazeti la mwanahalisi.

Of all things, hizi pumba ndizo umesajili jina kama la Mtoto wa Mkulima ambaye ingawa ni mwanaccm lakini anamake sense kidogo!
 
NADHANI DADA YANGU UMEGUBIKWA NA MAWAZO FINYU YALIYO BARIKIWA NA KAULI ZA WAANDISHI WA MWANAHALISI ULICHO ONYESHA NI PURE MAWAZO -VE YA WALIOPOTEZA DIRA NA MUELEKEO.NANI KASEMA MBOWE ANAJUA HUO UMASKINI MNAONGELA NANI KASEMA JK HAJUI HUO UMASKINI WA WATANZANIA?KUENI OBJECTIVE ACHENI BLA BLA ZA WATU KAMA NDIMARA ALIEANDIKA MAKALA KTK MWANAHALISI LA 28TH NOV.

Wewe Mtot, unaishi dunia ya wapi? Hayo ni maneno ya JK mwenyewe tena kwa akili zake timamu bila kulazimishwa na mtu yeyote, akishangaa na kushangauka kwamba hajui kwanini watanzania ni masikini... ohhhhh... na huyo ndo muheshimiwa wa kuleta 'maisha bora' kwa kila Mtanzania!!! Upo?
 
Unawezaje kulinganisha Chama ambacho kimeshika dola na chama ambacho hakijiwahi kushika dola. Labda kama ikija tokea CHADEMA kushika dola siku za mbeleni then baada ya kuwa madarakani ndio tunaweza kuwalinganisha na yale wanayoyatenda. Until then .............
 
WAMETOKA NA TAMKO LA KAMATI KUU AMBALO NI MOTO JE?LA CCM LIKO WAPI JAMANI?

Nakubaliana nawe kwamba kamati kuu ya CHADEMA imetoka na TAMKO bomba sana, mawazo mazuri sana, Cha Kusikitisha sana ni kwamba maazimio yao yalikuwa kamaya mwanafunzi aliyeshindwa kujibu maswali kwenye mtihani akaamua kujitungia swali jingine na hilo swali jingine akalijibu kwa usahihi wa hali ya juu sana! Simply hawakuelewa dhamira ya Rais no wonder wakaifanya issue ya Zitto ni hoja.
 
NADHANI DADA YANGU UMEGUBIKWA NA MAWAZO FINYU YALIYO BARIKIWA NA KAULI ZA WAANDISHI WA MWANAHALISI ULICHO ONYESHA NI PURE MAWAZO -VE YA WALIOPOTEZA DIRA NA MUELEKEO.NANI KASEMA MBOWE ANAJUA HUO UMASKINI MNAONGELA NANI KASEMA JK HAJUI HUO UMASKINI WA WATANZANIA?KUENI OBJECTIVE ACHENI BLA BLA ZA WATU KAMA NDIMARA ALIEANDIKA MAKALA KTK MWANAHALISI LA 28TH NOV.

Jibaba ukweli umekukera mpaka umeanza kulialia kama katoto kanakolilia maziwa, na umeanza mipasho ya vidole juu kama 'mtoto sio rizki'. Kumbuka kwenye kampeni-Mbowe alikuwa anajenga hoja kwa muda mrefu kuhusu nini chanzo cha umaskini Tanzania, JK alikuwa akizungumza dakika chache na kusema ile ilani aliyonipa mkapa ndio ina majibu yote. Kumbuka alipoanguka jukwaani alikuwa anasema nini vile? Ur guy is empty headed. Sijui kwa nini hamkuchukua SAS, JSM au MM. Soma tena ujumbe wangu ujibu nilichohoji, sio kusema tu 'mawazo finyu'. Umeruka kama nimekufinya vile!

Acha bla bla mwanaume..

Asha
 
Kuna watu wanasema kuwa eti CHADEMA ni Dr.Slaa, Lissu na Zitto, huu ni upunguani kwani haiwezekani chama kikawa ni watu watatu.

Upunguani? are you serious Chadema ina watu zaidi ya hawa watatu ambao wako serious na taifa?

Hatuwezi kumuhesabu Freeman, maana yuko shule bado, sasa mkuu hebu wataje wengine? Tamko la kamati kuu ipi hiyo? Yaani ubongo wenu ndio mzima wa kupiga kelele hapa forum tu huku uchaguzi unaendelea na mnapigwa chini na wananchi ndio unasema ni ubongo safi huo?

Halafu mbona unaanza kuleta matusi badala ya hoja, au ndio yale yale aliyosema MMJ, mkishiondwa hoja mnaaanza viroja? Hivi unafikiri wananchi wanaweza kuwachagua watu wenye kuwatukana kuwa ni mapunguani na ubongo wao ni mbovu, just because wanauliza maswali ya kuikosoa Chadema? Are you suprised kwa nini mnaendelea kuwa kwenye sidelines na haya matusi, tena kwa mtu mzito wa Chadema kama wewe?

What a joke, hivi mnafikiri mtapewa utawala tu kama samaki sokoni?
 
Kuna watu wanasema kuwa eti CHADEMA ni Dr.Slaa, Lissu na Zitto, huu ni upunguani kwani haiwezekani chjama kikawa ni watu watatu.

Upunguani? are you serious Chadema ina watu zaidi ya hawa watatu ambao wako serious na taifa?

Hatuwezi kumuhesabu Freeman, maana yuko shule bado, sasa mkuu hebu wataje wengine? Tamko la kamati kuu ipi hiyo? Yaani ubongo wenu ndio mzima wa kupiga kelele hapa forum tu huku uchaguzi unaendelea na mnapigwa chini na wananchi ndio unasema ni ubongo safi huo?

Halafu mbona unaanza kuleta matusi badala ya hoja, au ndio yale yale aliyosema MMJ, mkishiondwa hoja mnaaanza viroja? Hivi unafikiri wananchi wanaweza kuwachagua watu wenye kuwatukana kuwa ni mapunguani na ubongo wao ni mbovu, just because wanauliza maswali ya kuikosoa Chadema? Are you suprised kwa nini mnaendelea kuwa kwenye sidelines na haya matusi, tena kwa mtu mzito wa Chadema kama wewe?

What a joke, hivi mnafikiri mtapewa utawala tu kama samaki sokoni?

Na wewe nawe. Hebu achana nao hao wanaokupuka. Wewe ni mtu makini FMES. Mbowe hayuko fratenity leave kama mlivyomuweka Makamba wala likizo ya kuugulia kama mlivyomweka Balali.

Naona mwenzetu anamjua Mpaka Kieleweke kuwa ni mtu mzito CHADEMA, tuambie ni nani huyo?

Kwa hiyo walioipa utawala CHADEMA Karatu, Tarime na kwingineko ni "samaki wa sokoni"?

WanaCCM mnapenda sana kutukana wananchi, mara muwaambie wale manyasi, mara muwambie 'go to hell'

Wewe mtu makini bwana, rekebisha mambo kwenye chama chenu

Wewe ni kati ya wanaume ninaowapenda

Asha
 
Usalama wa ccm au kama wengine tulivyozoea(usalama wa taifa) jukumu lao ni kuhakikisha kuwa chama tawala kinaendelea kuwepo, budjet ya kulinda ccm ni kubwa na kwa taarifa yako hakuna mamlaka yeyote wanaweza kuhoji matumizi ya fedha za watanzania jinsi zinavyotumika wakati wa kutunza uhai wa ccm. Jukumu kubwa ni kufuatialia mienendo na hujuma za huu usalama. Vingineyo hakuna chama chochote kitakachoweza kushinda uchaguzi na kuchukua na kuongoza dola ya Jamhuri ya watu wa Tanzania.
 
tatizo la ccm ni ulimbukeni wa viongozi wake.wanakurupuka kujibu hoja ambazo sio zao ili waonekane wanaitetea serikali yao.
 
FMES,

Nakubaliana na wewe kabisa kwenye hili, huwaga kila nikijiuliza je CHADEMA kwa sasa ilivyo yaweza kupewa na kuongoza nchi? naanza na kuhesabu viongozi ambao iliyonayo sasa, kwa ajili at least kuunda baraza la mawaziri dogo kuliko yote hapa duniani lenye uwiano na nchi yetu... naona haiwezekani maana majina hayafiki kumi (vidole vya mikono yangu miwili) nikishafikiri hivyo narudi nyuma nikisema wajameni tujizatiti vijiji, tujizatiti kupata angau 30% ya wabunge hapa tutake sasa kuongoza nchi hii...

Mawazo tu....

Hao CCM wenye majina ya viongozi yenye kutosheleza vidole vya miguu na mikono na mengine kubaki, je wameweza kuendesha nchi to the satisfaction of Tanzanians!? Jibu unalijua. Ni nia tu ya kuwa na mapenzi ya kweli na nchi yako na watu wake, siyo wingi wa viongozi. Kumbuka ukubwa wa pua sio wingi wa kamasi!
 
FMES
tafadhali usituyumbishe, muanzisha mada ameanza vizuri kwa kuorodhesha 1,2 etecetera kama matamko ya chadema CC na inatakiwa vivyo hivyo point zilitoka ccm zipambanuliwe pia.Why hit around the bush FEMS?!
 
Hao CCM wenye majina ya viongozi yenye kutosheleza vidole vya miguu na mikono na mengine kubaki, je wameweza kuendesha nchi to the satisfaction of Tanzanians!? Jibu unalijua. Ni nia tu ya kuwa na mapenzi ya kweli na nchi yako na watu wake, siyo wingi wa viongozi. Kumbuka ukubwa wa pua sio wingi wa kamasi!

Na extrapolate "KIDOLE KIMOJA HAKIVUNJI CHAWA" au PENYE WENGI HALIHARIBIKI NENO.
 
Lakini matokeo ya udiwani wote tuliyaona na kilicho nikatisha tamaa ni jinsi viongozi wote wakuu wa vyama walivyokuwa kwenye mkutano wa kutoa "forensic evidence" za Ufisadi badala ya kwenda vijijini kuwa nadi wagombea wao.
 
Hatuwezi kumuhesabu Freeman, maana yuko shule bado, sasa mkuu hebu wataje wengine? Tamko la kamati kuu ipi hiyo? Yaani ubongo wenu ndio mzima wa kupiga kelele hapa forum tu huku uchaguzi unaendelea na mnapigwa chini na wananchi ndio unasema ni ubongo safi huo
?

Ubongo wa wananchi wengi wa Tanzania ni sawa nawa Rais,ambaye hajui nini matizo la umasikini wao. Watanzania wanajua wao ni masikini lakini hawajui kwanini wao ni masikini, hivyo hawajui dawa ya kuuondoa huo umasikini.Siku watakapojua kuwa wao ni masikini kwa sababu ya kuwa na vingozi wabinafsi,wezi waliokithiri,wala rushwa waliokithiri na wasiowajibika,CCM haitakuwa na chake. Kushindwa katika uchaguzi haimaanishi kuwa CCM si chama kilichosheheni kila aina ya ubadhilifu unaoiletea nchi hii umasikini.Wanashindwa kwa kuwa watanzania hawaendi kupiga kura ili kuleta mabadiliko ila kutimiza tu wajibu na haki yao ya kupiga kura.It is the matter of time
 
Lakini matokeo ya udiwani wote tuliyaona na kilicho nikatisha tamaa ni jinsi viongozi wote wakuu wa vyama walivyokuwa kwenye mkutano wa kutoa "forensic evidence" za Ufisadi badala ya kwenda vijijini kuwa nadi wagombea wao.

Mhh Icadon,

Inawezekana labda hujui sheria za uchaguzi wa Tanzania au umeamua kufanya ya Kikwete kujifanya hajui chanzo cha umaskini wa Tanzania.

Sheria za uchaguzi zinakataza kufanya kampeni siku ya uchaguzi. viongozi wa vyama vya upinzani wasingefanya kampeni siku ya uchaguzi kama unavyoandika hapa.

Wewe na wenzako wengi sana kimekuuma sana kuona kuwa at last watu wameweka hadharani wizi wa pesa BOT ulivyofanikisha ushindi wa CCM. WEWE na wenzako hapa mnataka ku-shift blame kuwa ccm inashinda kwa vile wapinzani hawakubaliki au hawapigi kampeni siku ya uchaguzi?

Mhh nimeshangaa sana kusoma hili toka kwako maana mara nyingi huwa uko makini kiaina katika mambo mengine. AU ni panic umepata kuona kuwa taratibu wizi serikalini unawekwa wazi?
 
Back
Top Bottom