.
Ndugu zangu naomba nitumie fursa hii kujitambulisha kama msomaji wa magezeti na mfatiliaji wa maswala ya kisisasa ya nchi hii hasa Gazeti la MWANAHALISI.
Mara nyingi nimekua nikiaangalia makala nyingi ziznazo andikwa ktk gazeti hili la mwanahalis nakugunua kua waandishi kama KUBENEA wana tatizo la ufinyu wa fikra na mawazo au kutofahamu tafsiri sahihi ya uzalendo.
Tatumia makala ambazo Kubenea amekua akiziandika na kuzionyesha ktk jamii kua alivo mzalendo. Mfano makala aliotoa au uchambuzi aliofanya baada ya uteuzi wa sekretarieti ya ccm na kuendelea wiki hii ktk Gazeti la Mwana Halisi ktk kichwa cha habari KIKWETE AMETEKWA NA MTANDAO MASLAHI imenionyesha ni jinsi gain alivo na ufinyu wa mawazo.
Kuwepo kwa NGELEJA,KARAMAGI ktk wizara ya Nishati ni hoja ambayo ametumia kudai kua wizara imebinafsishwa hapa najifunza either hajui maana halisi ya ubinafsishaji au anaelewa bali anatafuta umaarufu kwa kutumia kalamu yake hovyo ili jamiii imuone amesema kitu.
Kubenea na Gazeti hili wameshindwa kuonyesha wapi kikwete ametekwa ukiangalia hoja kua ROSTAM,MAKAMBA,LOWASA kushinda na hoja kua Mtandaao wameshiriki ktk uteuzi wa kamati ya madini na peter machunde kua Mjumbe havionyeshi ni wapi JK ametekwa na mtandao maslahi hoja hizi zisizo kua na JUSTIFICATION,kwa statistics,au ushahidi wa aina yoyoyete ndo hoja za kuandikwa na MHARIRI wa Gazeti? Hoja hizi za kitoto ndo alizotumia TINDU LISU ktk mdahalo siku ya higher learning pale DCC kua machunde hafai ktk kamati bcs aliwahi kukaribishwa bungeni na karamagi only that ndo ilikua base ya hoja yake.
Leo 21st century tuna waandishi kama kubenea ambae anaandika mawazo yake na kufanya ndo mawazo ya watanzania,Ukiangalia yeye na mchangiaji mwezie YUSUPH BUGENZI wanadai kua KUNA MINONGONO KILA MAHALI KUA URAISI UMEBINAFSISHWA KWA MTANDAO MASLAHI, hoja haina mifano halisi ningemuelewa kua anaelalamika ni yeye anaposema kila mahali anawakilisha wingi wingi amabao anashindwa kujustify kwa mifano hai au kusema anaglau alifanya survey aina flani na kuhoji watu namaba flani wakasema hayo anayo taka sisi watanzania tuamini.
Kubenea katika makala hiyo anadai hajui VIGEZO vya kumteua DK Rashid TANESCO anatak tuamini kua Rashid ameteuliwa kwa urafiki wake na ROSTAM hapa inaonyesha hajui historia ya DK Rashid,uzoefu wake inaonyesha pia kubenea anatatizo la usahaulifu kua huyo mtu anaeuliza uzoefu wake alishakua GAVANA wa BOT,utendaji wa Dk Rashid unafahamika,FIKA NMB uliza uwezo FIKA BOT uliza lakini hakuna mfatiliaji wa mabo anaeweza kujiuliza anachjiuliza kubenea kwani HISTORIA ya DK Rashidi inafahamika,Anaetakiwa kuulizwa uwezo na vigezo ni kubenea UHARIRI ameupataje? ELIMU, UZOEFU,UELEWA,UWEZO WA KUCHAMBUA
MAMBO,KUMBUKUMBUvYOTE HIVI TUNAJIULIZA kama unavyo inatia shaka juu ya uwezo wako na si DK RASHIDI,hivi kweli taaluma yako inakufanya uhoji matangazo yaneenda wapi umefanya uchunguzi kiasi gain kuona kua matangazo ya Tanesco yanenda Habari Corporation zaidi kuliko magazeti mengine?Uwezo wako mdogo wa kuchambua mambo umekufanya ushindwe kutambua kua Mkurugenzi hahusiki na utoaji wa matangazo labda nikuambia kama unataka matangazo Tanesco nenda kamuone PR wa Tanesco DDk Rashidi hafanyi hiyo Kazi.
Labda nikusaidie kubenea na wenzio wanaodhani watanzania hatuwezi kufikiri, KIKWETE si JINI ni MTU ana marafiki na hoja zenu za ROSTAM LOWASA na wengine kua marafiki wa kikwete kama mnavodai haina maana kua RAISI wa NCHI basi anakosa haki ya kua na marafiki.
Hivi Kubenea tukuhukumu na wewe tuseme kua umetekwa na Marafiki zako inawezekana unacho andika si mawazo yako thats why unaamini kua maamuzi ya RAIS ni maamuzi ya marafiki zake,naamini kua hivo sivo alivo kama angekua aametekwa na Mtandao Maslahi ambao unaowataja mara kwa mara kama ulivoandika ktk makala zako basi leo asingemchagua MSEKWA,MKUCHIKA,asingemteua SALIM, asinge mpendekeza KIGODA,SUMAYE inawezekana ukawa ni wale wenye macho hawaoni,Wenye masikio hawsikii,UWEZO WAKO umeudhihirishia UMMA wa kitanzania kua u mtu wa aina gain.
Ufike wakati Hoja iwe na justification nachokiona ni either kutufanya wote tunaosoma magazeti hatuna akili kwa kutuletea taarifa,makala uchambuzi usiokua na kichwa wal miguu mistake mawazo yenu yawe mawazo ya watanzania.
Imekua ni agenda yako binafsi kila ukiandika bila kutaja KIKWETE LOWASA ROSTAM MAKAMBA gazeti halijaenda kiwandani Tazama Kichwa cha HABARI KUA IKULU KWAFUKUTA MOTO.ukisoma kilichoandikwa hakina kitu cha msingi huo moto unaongelewa humo ni upi? Kilichovuja kutufikia wanachi ni kipi? IFIKE MAHALI VYOMBO VYA HABARI NCHI HII VIKEMEE waandishi kama KUBENEA nachojiuliza kubenea na UZALENDO WAKE anafanya kazi ya nani?ni vizuri kufaham hilo ili tuweze kumuelewa je anachofany ni kile tunachokiona ktk siasa za JAMBO FORUM? Kama ndicho ambacho tunakiona huko basi sishangai ila nawasikitikia wenye TAALUMA ya uandishi wa habari kwamba kuna mtu anawachafulia taaluma yao kwa kuandika mawazo yake binafsi na kutaka kufanya haya ndio mawazo yetu wanachi,kwa kutaka yeye afikri kwa niaba yetu watanzania.
Labda nikuambie watanzania tungeona ww ni mzalendo kama hoja zako zingekua zinalenga kutusaidia wengi 80% ya watanzania kwasas ni wakulima tembelea kwetu vijijimi andika kuhusu matatizo yetu wakuliama usilifanye gazeti lako kua plate form ya wanasiasa walioshindwa kuja kwetu wananchi kutueleza wantaka kutufanyia nini badala yake wamebaki na hoja za mtu na si issues.
Tazama za watu kama STEPHEN RAMADHANI na makala NGOMBALE WAMPOTOSHA JK Mtazame NDIMARA TEGAMBWAGE na Makala SEREKALI INAFICHA UKWELI mtu kama huyu anafikia mahali anasema RAISI wa ni mjinga kwa hoja kua alihoji anashangaaa why nchi masikini hilo nilitegemea yeye nae ajiulize na kama anajua why nchi yetu ni maskini anagetoa reasons,Hivi watu kama hawa STEPHEN anaesema mzee NGOMBALE anafanya Biashara amefanya utafiti wapi kugundua hilo au bcs gazeti muhariri na team yao hawajali juu ya aina ya maoni yanayotolewa basi huandika tu? Stephen jenga hoja yenye substance iwe na vigezo si kukurupuka na kuvunjia watu heshima zao FIKA BRELA ujifunze nani anmiliki hisa ktk kampuni unayo dai kua ya kingunge.
Nachojifunza ni kwamba NDIMARA hajui LOWASA alipokua anaongea aliongea kama WAZIRI MKUU na si LOWASA bali TAASISI kwahiyo namna ya kufanyia kazi jambo alilosema kuna utaratibu na si KAULI za watu kama kiana SLAA na MWANAHALISI NDO kusema kua taarifa wanazo ifike mahali watu kama NDIMARA wamesahau walishindwa kuendesha TAASISI ( NCCR) leo haipo ni kivuli.
Ndugu zangu fikieni mahali uzalendo usitafsiriwe vibaya nashauri KUBENEA na watu kama STEPHEN RAMADHANI,NDIMARA kueni more objective kujenga TAIFA hili na specifically kubenea nakua na shaka na elimu au uwezo wa kufikiri na kama unatumiwa angalia usije kuharibu UTU wako .
Watanzania tunaona,tunasikia,tunaelewa,tunafahamu,na tunaweza kuchambua thats why nimekaa muda mrefu kuangalia trend ya gazeti lako na uandishi wako ulivo na kunifanya nijiulize maswali, JE ELIMU NDOGO?,UFAHAMU MDOGO?,UWEZO WAKUELEWA MDOGO?,HUJUI MAJUKUMU YA MUHARIR?I,JE HII NI TAALUMA YAKO?,UNA AJENDA GANI?,UMETUDHARAU WATANZANIA KIASI HIKI KUTUFANYA TUAMINI UNACHOFIKIRI?UNATUMIWA NA NANI NA KWA MASLAHI YA NANI?