CHADEMA
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 488
- 2,468
"Serikali inayoogopa watu, serikali inayoishi kwa uongo haiwezi kushinda kura. Na mimi niwaambie na hiyo meseji iwafikie, uchaguzi huu tunaenda hakuna wa kujitoa. Uchaguzi huu tunaenda, tunajua hakuna Tume Huru (ya Uchaguzi).
Tunajua wanatunga sheria zozote wanazotunga. Tumeamua tuache watunge sheria yoyote, kusiwe na Katiba, kusiwe na Tume Huru, uchaguzi tunakwenda kushindia kituoni. Wanataka hawataki, watatutangaza.
Nani anawadanganya kwamba hamtatangazwa? Toka lini CCM na serikali yake, toka lini walikuwa na mpango wa kuwatangaza wapinzani? Haijawahi kuwa nao, hawana, hawatakuwa nao. Tutawashida hivyo hivyo.
Ng'ombe huyu mara hii anachinjwa alivyolala, akilala kifudifudi, tunachinja kuanzia mgongoni. Akilala kiubavu, tunachinja kiubavu. Huyu tunachinja alivyolala. Tutawashinda wanapenda hawapendi."
Mhe. Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu Chadema, Bara.