CHADEMA: Tuna dhamira ya kushika dola 2025

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,355
8,043
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika amesema chama hicho kitahakikisha kinaimarisha majimbo yote ya Tanzania na Zanzibar ili kufikia dhamira ya kuiondoa CCM madarakani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

“Tuna dhamira ya kushika dola mwaka 2025, kutokana na dhamira hii kuu, hatuwezi kuliacha jimbo lolote nyuma lazima yote tusonge kwa nguvu kamili. Ujumbe huu sio kwa Geita au kanda ya Victoria bali kanda zote 10 za Tanzania na Zanzibar,” amesema Mnyika.

Mnyika ambaye ni mbunge wa zamani wa majimbo ya Ubungo na Kibamba mkoani Dar es Salaam, ameeleza hayo jana Jumanne Desemba 27, 2022 wakati akihutubia katika mkutano mkuu wa jimbo la Geita Vijijini mkoani Geita.

Katibu mkuu huyo, kwa nyakati tofauti amekuwa akifanya ziara katika majimbo mbalimbali yaliyopo katika kanda 10 za chama hicho, ameshafanya vikao na makongamano na wanachama wa Chadema katika mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara na Dar es Salaam.

Amedai Chadema ndiyo chama cha tumaini kuu la Watanzania, akisema kama kunahitijaka mabadiliko ya uongozi, demokrasia na maendeleo, uhuru, haki za watu lazima kazi ya kujiimarisha ifanyike mahali kote ili chama hicho kiibuke kidedea na kuongoza Serikali mwaka 2025.

“Nyie wa Bukombe na Geita, kama ambavyo sisi wa kitaifa tutakavyozunguka katika majimbo na kata zote, nanyinyi mna wajibu wa kwenda kila kata, kijiji na kitongoji msiache mahali Chadema iamke ili kuwakomboa Watanzania,” amesema Mnyika.

Katika hatua nyingine, Mnyika amewataka wanachama wa chama hicho, kuutumia mwaka 2023 kudai Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi, akisema ni jambo linalopaswa kuwa la Taifa.

MWANANCHI
 
Kwa akili kama hizi za Wana CCM zilipofikia,hawa ni wa kuwaondoa pasibakie hata alama yao
JamiiForums-1992616779.jpg
 
Ngoja sasa wafufuke huko watu "wabaya"
 
kichefu chefu kabisa.
bora chadema iliyo kuwa ya E.Lowasa kuliko chadema ya sasa chini ya mlamba asali.
 
JamiiForums753274111.jpg
 
Back
Top Bottom