CHADEMA tulieni huu sio wakati wa kuleta kokoro, Uongozi dhaifu wa Mwenyekiti kuishiwa mbinu na kuanza kutengeneza makundi tatizo lilianzia hapo

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
12,633
2,000
Wana JF

Kilichofanya vyama vya upinzani kupigwa chini, ni matokeo mabaya ya uongozi wa Mbowe na kundi lake tiifu. Ndani ya chama chao ilianza fukuzana fukuzana. Ikaja susia susia watu walioona mbali wakaanza kujiondoa kwa kuunga juhudi upande wa pili. Hayo pia yaliyokea CUF ya Lipumba. Uovu kwa wapenda madaraka ya kudumu ndio chanzo cha kukataliwa. Kiongozi ukiishiwa mbinu unatakiwa kujipiga chini hata kama unajiona una akili Sana kuzidi unaowahisi.

CHADEMA jifunze demecrasia ianzie kwenu ndipo wengine wafuatie.

CHADEMA uliwanyima wananchi demekrasia kwa kumleta Lowasa na Sumaye mafisadi wakubwa waliokuwa wanatukanwa usiku kucha. Vijana wenye ali walikata tamaa kwa kuondoa mwanasiasa mkali wa mbinu Dr. Alaa. Hata kama Dr. Slaa angeshindwa tena lakini tungeendelea kujipanga kuanzia ngazi za chini mpaka za juu.

CHADEMA msingeweza kushinda uchaguzi wakati mlisusa serikali za mitaa. Kwenye mitaa ndio kuna wapiganaji wadogo wadogo wanaoounda kata kuja mpaka wilaya. Hawa wangeweza kueneza siasa za chini kufikia juu. Vijana baada ya kuondokewa na ali ya kukombolewa wamebaki kusubiri kuwekewa mafuta ya elf ishirini kwenye bodaboda angalau wapate pa kuanzia kuliko kupiga kelele bure wakati hawapati kitu.
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
3,565
2,000
Yaani kwa usiku mmoja karibu viongozi wote wa CHADEMA wameokotwa na Polisi. Chama hakina Intelligence?
Ulitaka intelligence iwaambie wakimbie nchi?!

Mtego mdogo tu, mmeingia wote.

Jinga sana nyie.
 

Msanii

JF-Expert Member
Jul 4, 2007
8,285
2,000
Yaani kwa usiku mmoja karibu viongozi wote wa CHADEMA wameokotwa na Polisi. Chama hakina Intelligence?
Wanasema wanayo intelejensia kali kuliko ya serikali.

Yaani hawa waheshimiwa watulie na kujipanga upya
 

CHARMILTON

JF-Expert Member
May 30, 2015
7,055
2,000
Ulitaka intelligence iwaambie wakimbie nchi?!

Mtego mdogo tu, mmeingia wote.

Jinga sana nyie.
CDM hawapo serious hata kidogo.

Kwa hali ilivyo bado teketeke walitakiwa hata wawe kwenye mahandaki.

Wana maneno ya kishujaa ila matendo ya kikondoo.
 

CHARMILTON

JF-Expert Member
May 30, 2015
7,055
2,000
Wanasema wanayo intelejensia kali kuliko ya serikali.

Yaani hawa waheshimiwa watulie na kujipanga upya
Hata kama wangeshinda uchaguzi bado wangekuwa na kazi nzito.

Intelligence kali ilikuwa wapi wakati Polisi walipoteka chama chote na kukisweka Lockup?
 

rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
8,324
2,000
Vyama vya upinzani na viongozi wao waliopo wakubali hawawezi kuitoa CCM madarakani kwa mbinu wanazotumia.

Pamoja na kwamba tuna miaka 25 tangu vyama vingi virudishwe bado vyama hivyo vimeshindwa kujijenga toka chini.

Wako na matawi ambayo hayana impact yoyote , hawawajui wapiga kura wao ni wakina inawezekana asilimia kubwa ya wasioenda kupiga kura ninwatu wasioipenda CCM ila kwa sababu hawana mizizi chini wameshindwa kuwatambua na kuwashaeishi wakapige kura.

Wameshindwa kusimamia hoja za msingi zinazowagusa watanzania kama watu kukosa malipo ya pensheni na kukazania mambo ambayo wapiga kura hayamgusi kwa haraka.

Wameshabikia sana Marekani na nchi za Ulaya na kutoa kauli za vitisho huku wakisahau wapiga kura wapo Tanzania.

Ni watu wasiojali wanachama wao wanataka nini ndiyo maana walimtoa mgomea aliyepitishwa wakamweka mgombea wanayemtaka wao.
Kushabikia mambo ambayo ni kinyume na utamaduni wa mtanzania ili mradi wapate support toka Ulaya
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom